Maalim Seif: Lowassa amerudi CCM kwa shinikizo la familia na Chadema kutotendea vyema

Kamanda Sefu ndio kasema sio mimi, mngejadili kama chama ili kutoa majibu ya hoja yake badala ya jazba.
Wewe ndio umeleta hapa, hivyo sema hoja yako ni ipi? Kuokota vi clip na kubandika hapa kisha kuwataka wajadili ni zaidi ya upumbavu na ukosefu wa akili.
Utakufa bure kwa sumu unayoitengeneza mwilini mwako dhidi ya Chadema.

Umeona wanawake wenzako walio BAWACHAa wanavyo zidi Ku shine? Na inshaalla octoba baada ya Tumehuru kuwepo ndio utajua ushawishi wao katika jamii na hivyo viti maalumu unavyo tambia hesabu maumivu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
9974f01c730ebafba67c88640f572f9c


Mwenyekiti wa Chama Cha ACT-Wazalendo, Maalim Seif Sharif Hamad ametoa mtazamo wake kuhusu uamuzi wa aliyekuwa mgombea urais kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) akiungwa mkono na vyama vya upinzani vilivyounda ‘Ukawa’, Edward Lowassa kurudi Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Maalim Seif ambaye mwaka 2015 alikuwa mgombea urais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kupitia Chama Cha Wananchi (CUF) kilichokuwa mshirika wa umoja huo, amesema yeye hawezi kumhukumu Lowassa kwa uamuzi wake ingawa anakiri amewaumiza na kuwaangusha wapinzani kwa uamuzi wake huo.

Amesema Waziri Mkuu huyo wa zamani alikuwa na sababu nyingi za kumfanya arudi CCM ikiwa ni pamoja na msukumo wa familia lakini pia kutotendewa vyema na chama hicho kikuu cha upinzani.

Amesema kuwa Lowassa ni tofauti na yeye kwakuwa yeye ameweza kuvumilia mikikimikiki na matokeo ya kuwa mpinzani.

“Yule [Lowassa] ujue alikuwa Waziri Mkuu, na malupulupu yake yote ya Uwaziri Mkuu, kwahiyo baada ya kuona lile ambalo alilitegemea kupata katika upinzani hakupata, na akaona kwamba Serikali inamsindikiza…,” alisema.

“Na ninavyosikia mimi familia yake ilimshinikiza, kwamba kuna mmoja kati ya wakwe zake alikuwa gerezani na watoto wake walikuwa wanamwambia ‘baba unaona… baba yetu sisi anapata shida kwa sababu wewe uko upinzani. Kwahiyo, ile presha ya familia ilikuwa kubwa sana. Lakini vilevile tunasikia pia kuwa na Chadema hawakumtendea vyema vilevile… kwahiyo ana sababu nyingi na mimi sitaki kumhukumu, lakini tulivunjika moyo sana [Lowassa kurudi CCM],” Maalim Seif aliiambia Global TV.

Mwanasiasa huyo alikiri kuwa ujio wa Lowassa ndani ya Ukawa ulisaidia na kuongeza nguvu kubwa ya umoja huo katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015, ingawa hawakufanikiwa.

Machi 1, 2019, Lowassa alirejea rasmi CCM aliyoihama mwaka 2015 baada ya kuondolewa kwenye kinyang’anyiro cha kupata nafasi ya kugombea urais kwa tiketi ya chama hicho.
 
😂 nilichoona kwenye maelezo yako nikuwa kumbe Eddo karudi ccm kwakuwa familia ilimtaka afanye hivyo na sio ulichotuamisha wewe hapo juu!!, Ungesema alichowalaumu maalim seif hawa chadema ungeeleweka vizuri ila unaonekana una-kimimba kichanga juu ya chadema ndio maana hutulizi miguu
 
Vijana wa Chadema watakuja kumtukana mzee wa watu aliyewapa wabunge zaidi ya ishirini

Mwaka huu lazima mrudi kwenye wabungu watatu

Sent using Jamii Forums mobile app
Kwani Lowasa kaondoka leo kwenda CCM? Mzee Lowasa aliondoka kistaarabu na alisema maneno mchache tu kuwa amerudi nyumbani na watu waliheshimu maamuzi yake wala hakuwa kutukanwa wala kukejeliwa. Mtu aliyeondoka kishamba ni Sumaye.

Sasa huyu Maalim naye sijui aliahidiwa nini huko Magogoni anajiropokea tu mbona hasemi ni jambo gani baya Chadema walimtendea Lowasa? Wote waliokwenda magogoni wametoka na maelekezo. Tutafahamiana tu mbele ya safari.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kamanda Sefu ndio kasema sio mimi, mngejadili kama chama ili kutoa majibu ya hoja yake badala ya jazba.
Seif anahusiana nini na Cdm ?!
Uliachwa lakini hawajakutoka moyoni !!.

Hivi unafikiri Maghufuli kutoka magogoni na kwenda kumpokea Lowassa kule Lumumba ilikuwa kazi ndogo na rahisi ?!. Hilo lilikuwa deal la system a k a wasiojulikana. Si swala Cdm

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom