CHADEMA yatuma salamu za Rambirambi kwa Familia ya Lowassa, Mbowe asema amejifunza Hekima ya Uongozi kwa Lowassa!

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,990
142,007
Mwenyekiti wa Chadema mh Mbowe amesema hayati Lowasa alikuwa mtu mwenye Upendo, Muungwana na Kiongozi Mpenda Maendeleo asiyechoka

" Kwa niaba ya Chadema natuma salamu za pole kwa mama na familia nzima ya Mzee Lowassa" amesema Mbowe

Rip Edward Lowasa

======
Kwa niaba ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na Watanzania wenzangu, napenda kutoa salamu zangu za dhati, za Pole kwa familia, ndugu, jamaa, marafiki na wapenda demokrasia wote kwa kifo cha aliyekuwa Waziri Mkuu wa Tanzania, Mheshimiwa Edward Ngoyai Lowassa, kilichotokea leo tarehe 10 Februari 2024.Mheshimiwa Lowassa alikuwa kiongozi shupavu, mwanasiasa mahiri, mwanaharakati hodari na alikuwa mstari wa mbele katika kupigania mabadiliko ya kisiasa na kiuchumi nchini mwetu.

Alikuwa rafiki yangu na mshirika katika safari ya kuleta demokrasia ya kweli Tanzania. Alikuwa mtu mwenye hekima, busara, ujasiri, uzalendo, mtu mwenye huruma, upendo na msamaha kwa wote. Alikuwa mtu mwenye maono, mipango na mtekelezaji mzuri wa miradi mbalimbali ya maendeleo kwa manufaa ya wananchi.Nimepokea kwa mshtuko na majonzi makubwa taarifa za kifo chake.

Nimepoteza rafiki, ndugu na mshauri mzuri. Tanzania na Dunia imepoteza kiongozi shujaa, mwenye mchango mkubwa katika kujenga amani, ushirikiano na ustawi wa jamii.Namuomba Mwenyezi Mungu aiweke roho yake mahali pema peponi, amsamehe makosa yake na amjaalie rehema zake. Mungu aipe faraja, nguvu na subira familia yake, chama chake, wafuasi wake na wote walioguswa na msiba huu.Tutaendelea kuenzi kazi, mawazo na hekima alizotuachia Mheshimiwa Lowassa.

Tutaendelea kumuombea na kumkumbuka kwa mema aliyotutendea.Mungu ailaze roho ya Mheshimiwa Edward Ngoyai Lowassa mahali pema peponi. Amina.

Freeman Aikaeli MboweMwenyekiti wa CHADEMA
 
Mwenyekiti wa Chadema mh Mbowe amesema hayati Lowasa alikuwa mtu mwenye Upendo, Muungwana na Kiongozi Mpenda Maendeleo asiyechoka

" Kwa niaba ya Chadema natuma salamu za pole kwa mama na familia nzima ya Mzee Lowassa" amesema Mbowe

Rip Edward Lowasa
Wote wanafiki.

Walimtukana na kumdhalilisha sana huyu mzee, walimwita Fisadi, mgonjwa na kila aina ya matusi inashangaza leo wanakosa hata tone la aibu.
 
Back
Top Bottom