Maalim Seif: Lowassa amerudi CCM kwa shinikizo la familia na Chadema kutotendea vyema

Wakudadavuwa

JF-Expert Member
Feb 17, 2016
17,506
15,997
Ndugu zangu,


Karma inafanya yale unayomfanyia mwenzio, taabu wanazopata Chadema huenda ni malipo ya mabaya waliyofanyia waliowainua.

========

Mwenyekiti wa Chama Cha ACT-Wazalendo, Maalim Seif Sharif Hamad ametoa mtazamo wake kuhusu uamuzi wa aliyekuwa mgombea urais kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) akiungwa mkono na vyama vya upinzani vilivyounda ‘Ukawa’, Edward Lowassa kurudi Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Maalim Seif ambaye mwaka 2015 alikuwa mgombea urais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kupitia Chama Cha Wananchi (CUF) kilichokuwa mshirika wa umoja huo, amesema yeye hawezi kumhukumu Lowassa kwa uamuzi wake ingawa anakiri amewaumiza na kuwaangusha wapinzani kwa uamuzi wake huo.

Amesema Waziri Mkuu huyo wa zamani alikuwa na sababu nyingi za kumfanya arudi CCM ikiwa ni pamoja na msukumo wa familia lakini pia kutotendewa vyema na chama hicho kikuu cha upinzani.

Amesema kuwa Lowassa ni tofauti na yeye kwakuwa yeye ameweza kuvumilia mikikimikiki na matokeo ya kuwa mpinzani.

“Yule [Lowassa] ujue alikuwa Waziri Mkuu, na malupulupu yake yote ya Uwaziri Mkuu, kwahiyo baada ya kuona lile ambalo alilitegemea kupata katika upinzani hakupata, na akaona kwamba Serikali inamsindikiza…,” alisema.

“Na ninavyosikia mimi familia yake ilimshinikiza, kwamba kuna mmoja kati ya wakwe zake alikuwa gerezani na watoto wake walikuwa wanamwambia ‘baba unaona… baba yetu sisi anapata shida kwa sababu wewe uko upinzani. Kwahiyo, ile presha ya familia ilikuwa kubwa sana. Lakini vilevile tunasikia pia kuwa na Chadema hawakumtendea vyema vilevile… kwahiyo ana sababu nyingi na mimi sitaki kumhukumu, lakini tulivunjika moyo sana [Lowassa kurudi CCM],” Maalim Seif aliiambia Global TV.

Mwanasiasa huyo alikiri kuwa ujio wa Lowassa ndani ya Ukawa ulisaidia na kuongeza nguvu kubwa ya umoja huo katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015, ingawa hawakufanikiwa.

Machi 1, 2019, Lowassa alirejea rasmi CCM aliyoihama mwaka 2015 baada ya kuondolewa kwenye kinyang’anyiro cha kupata nafasi ya kugombea urais kwa tiketi ya chama hicho.


Chanzo: Dar 24



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Seif anasema "anasikia" Chadema haikumtendea haki Lowassa akiwa Chadema, but hajui ni haki gani; lakini ana uhakika Lowassa alikuwa Waziri Mkuu hivyo marupurupu na mshahara wake vyote vilitoka serikalini, sasa hapo sababu ya Lowassa kurudi CCM mbona iko wazi tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
Huyu mdada mleta uzi ni mshilawadu adharauliwe tu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kumbe sababu ilikuwa malalamiko ya familia nanyingine ni marupurupu ya uwaziri mkuu, hapa chadema ilihusika vipi,nakama matarajio yake ilikuwa nikuwa Rais nani alizuia yeye kutokutimia ndoto zake, ubaya wa chadema niupi ilimpokea ikampa nafasi yakugombea wanachadema na waliompenda wakaungana wanampigia kura nyingi tu matokeo Kila mtu aliyasikia wapi ubaya wa chadema kwahuyu mzee?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Unaipenda sana CHADEMA, imekukaa moyoni, inakuwashawaha muda wote, ukilala unaiota CHADEMA, ukiamka unaiwaza CHADEMA.

Ushauri wa bure, nenda kawaombe msamaha urudi kundini.
 
Unaipenda sana CHADEMA, imekukaa moyoni, inakuwashawaha muda wote, ukilala unaiota CHADEMA, ukiamka unaiwaza CHADEMA.

Ushauri wa bure, nenda kawaombe msamaha urudi kundini.
Ni Sefu kasema kamanda sio mimi, ungemjibu hoja yake.
 
Back
Top Bottom