Maajabu ya mjadala ITV, watu wote wana mawazo sawa

Maajabu ya mjadala ITV, watu wote wana mawazo sawa

Heheheheee jaman katika siku nmecheka nijana...nlipata hasira nikazima tv..kuna mzee mmoja anashangaa vijana kumtukana dikteta pale ndipo nlipochoka kabisa
 
Ma ndezi kweli wamepangwa,Wanaongea pumba tupu.
Jingine linasema wingereza kwa siku wanakufa watu elfu tano.
Aibu taifa linageuka la mandezi
Yule kenge anasema pia watoto wanatekwa laki moja plus kwa siku..nikajua kakosea ajabu likawa linasimamia hapohapo ndipo nlipojua mabashite yapo mengi
 
Ndio maana huwa najiuliza yule mzee yale mapengo aliyapata kwa usalama kweli!!
Wewe unafikiri Utachangia Vizuri huku Muna Maaskari wastaafu humo kweli..........Akiingia kwenye Daladala kaaaaaa anaongea yeye tu.......sijui ana Matatizo gani.........Naona alistaafu kabla ya Muda.............Nadhani anaishi KIWALANI kama sikosei.........
 
Hahaha machadema yamechachawa baada ya kuona yapo peke yao, na bado hiyo ITV mliyokua mnaisifia kwamba ipo balanced saivi tena mnaitukana?

Tatizo mkilishana pumba hapa jf na kuelewana mnafikiri watu wote wana akili finyu kama zenu anayempinga Magufuli ni taahira tu.
Ha ha ha ha.....mwanzo adui namba moja ilikuwa Clouds Media baadae Clouds ikawa ndio redio bora. ITV nayo ilikuwa inasifiwa kweli kweli mara hii nayo ni takataka. Ni wazi kwa baadhi ya watu TV/Redio bora ni ile inayoponda serikali.
 
Taaluma na ethics zake havifuatwi tena,bali upumbavu umechukuwa nafasi.
 
KIPINDI: Malumbano ya Hoja
MAADA: Miaka miwili ya serikali ya awamu ya tano, nini mafanikio na changamoto?

Wachangiaji wote wanamsifu Magufuli, hakuna anayemkosa raisi. Wakuu, mimi ni mfugaji wa ng'ombe, hata ng'ombe huwa hawafikiri sawa. Unaweza ukataka kuwasagwa waende mbele lakini utaona kuna wengine wanaenda pembeni na wengi wanarudi nyuma, hiki ni kiashiria kwamba ng'ombe pia hutofautiana fikra na maamuzi.

Nashangaa kuona hawa wachangiaji wote wana mawazo sawa, je? watu hawa wametolewa wapi na ITV?
Daah hii ni hatari na imetoa maana nzima ya MALUMBANO YA HOJA.
 
KIPINDI: Malumbano ya Hoja
MAADA: Miaka miwili ya serikali ya awamu ya tano, nini mafanikio na changamoto?

Wachangiaji wote wanamsifu Magufuli, hakuna anayemkosa raisi. Wakuu, mimi ni mfugaji wa ng'ombe, hata ng'ombe huwa hawafikiri sawa. Unaweza ukataka kuwasagwa waende mbele lakini utaona kuna wengine wanaenda pembeni na wengi wanarudi nyuma, hiki ni kiashiria kwamba ng'ombe pia hutofautiana fikra na maamuzi.

Nashangaa kuona hawa wachangiaji wote wana mawazo sawa, je? watu hawa wametolewa wapi na ITV?
Balile ndio alisifu na kukosoa. Huyu ni mhariri wa Jamahuri Media
 
Fanyeni kaz aisee,siasa tupen kule,maana tumechoka kelele za kupinga tuu kila siku hata kama watu wanafanya kaz..wa tz sjui wanatakaga nin yan.
 
Aibu yenu.

Mwenye sifa zake ni vizuri apewe sasa mlitaka wasimsifia wakati anastahili,mlitaka wampake matope ambayo hana kama nyie mnavyofanya.

Na bado mtaumbuka sana tu.

Akimaliza 10 tunamuongezea.
 
Idadi kubwa ya washiriki walikuwa wana- CCM, sasa hapo unategemea wamkosoe rais anayetoka chama chao? Mpaka mwanasheria wa CCM alikuwepo na aliweka sheria pembeni naye akaingia kwenye ushabiki wa kisiasa. Balile na mshiriki mmoja kutoka Morogoro ndiyo walionekana kukosoa. Mzee wa bao yeye alipongeza sana magazeti kufungiwa, yule kweli ni mcheza bao ndio maana hajui umuhimu wa magazeti.
 
Simple, huwezi kumkosoa Rais wazi wazi tena live katika TV ukabaki salama awamu hii.... Wengi hujificha nyumba ya keyboard na fake ID..... Siwalaumu
Mkuu mbona Balile alikosoa wazi wazi kabisa?
Alikosoa tabia ya kufungia gazeti kwa kosa lililofanywa na mtu mmoja. Na akatoa mfano wa wale madaktari wa Muhimbili waliomfanyia mgonjwa operation ya kichwa badala ya goti kwamba wao ndio waliadhibiwa na wala Muhimbili haikufungwa kwa sababu yao.

Pia alikosoa uamuzi wa raisi kupiga marufuku mikutano ya kisiasa ambayo iko kisheria na wakati yeye mwenyewe kama mwenyekiti wa CCM kuendelea kufanya mikutano.

Alikosoa pia raisi kuzuia bunge live wakati ziara na mikutano yake yote iko live. Kwa hiyo mkuu inategemea tu mtu anavyojiamini na kujenga hoja yake, kumkosoa mkulu wazi wazi hakuna kosa ni uoga tu ambao umeshajengeka kwenye awamu hii.
 
Ha ha ha ha.....mwanzo adui namba moja ilikuwa Clouds Media baadae Clouds ikawa ndio redio bora. ITV nayo ilikuwa inasifiwa kweli kweli mara hii nayo ni takataka. Ni wazi kwa baadhi ya watu TV/Redio bora ni ile inayoponda serikali.

Wakati huo hizo tv na redio zikisifiwa, wa upande wa pili na serekali walikuwa wakizisifu pia?
 
Back
Top Bottom