Maajabu ya mjadala ITV, watu wote wana mawazo sawa

Maajabu ya mjadala ITV, watu wote wana mawazo sawa

KIPINDI: Malumbano ya Hoja
MAADA: Miaka miwili ya serikali ya awamu ya tano, nini mafanikio na changamoto?

Wachangiaji wote wanamsifu Magufuli, hakuna anayemkosa raisi. Wakuu, mimi ni mfugaji wa ng'ombe, hata ng'ombe huwa hawafikiri sawa. Unaweza ukataka kuwasagwa waende mbele lakini utaona kuna wengine wanaenda pembeni na wengi wanarudi nyuma, hiki ni kiashiria kwamba ng'ombe pia hutofautiana fikra na maamuzi.

Nashangaa kuona hawa wachangiaji wote wana mawazo sawa, je? watu hawa wametolewa wapi na ITV?
Walipelekwa na mabasi ya uda?
 
Yale mamtu yalikua yameandaliwa, huskii makampeni yanayoendelea kuwa tumuunge mkono mkulu? huko tbc ndio usiseme!
 
Ha ha ha ha.....mwanzo adui namba moja ilikuwa Clouds Media baadae Clouds ikawa ndio redio bora. ITV nayo ilikuwa inasifiwa kweli kweli mara hii nayo ni takataka. Ni wazi kwa baadhi ya watu TV/Redio bora ni ile inayoponda serikali.
Acha upumbavu watu wanataka ukweli sio kujikomba
 
Jiulize kwanza, Chadema mlimtoa wapi Lowassa?
Umejitoa ufahamu hilo cii linaeleweka baada ya kumkata kwenye mchakato akatafuta chama cha kuhamia na chama ni wanachama hivyo chadema wakampokea kama kina shonza walivyopokelewa au mpendazoe na upande mwingine hivyo ni yeye aliyejipeleka
 
KIPINDI: Malumbano ya Hoja
MAADA: Miaka miwili ya serikali ya awamu ya tano, nini mafanikio na changamoto?

Wachangiaji wote wanamsifu Magufuli, hakuna anayemkosa raisi. Wakuu, mimi ni mfugaji wa ng'ombe, hata ng'ombe huwa hawafikiri sawa. Unaweza ukataka kuwasagwa waende mbele lakini utaona kuna wengine wanaenda pembeni na wengi wanarudi nyuma, hiki ni kiashiria kwamba ng'ombe pia hutofautiana fikra na maamuzi.

Nashangaa kuona hawa wachangiaji wote wana mawazo sawa, je? watu hawa wametolewa wapi na ITV?
Msigano wa fikra ni muhimu sana kwa afya ya taifa na akili.

Vv
 
Jamani alikuwepo mmoja tu alikuwa na mawazo tofauti,wengine majipu wanawinda ugali,halafu hawajitambui,au yoga wa watu.wasiojulikana
 
Kwahiyo wasio bavicha na huo upande wako wasichangie mjadala hapa jf?!?!?!
Wachangie tu hakuna ban yoyote mkuu. Sababu Habari nyingi Itv hivi sasa sehemu kubwa ni maendeleo na harakati zinazofanywa na mh. Magu inawaboa sana Bavicha ndo mana wanaiponda Itv hivi sasa. Wanapenda kusikia zaidi habari za mapungufu ya serikali tu
 
Iko hivi wazee. Kile kipindi kiliandaliwa maalum kusifia utawala wa Magu baada ya miska miwili. ITV walikiandaa kushirikiana ma polepole. Ndio maana uliona wawakilishi wa ccm ndio walijaa pale. Makatibu wa uvccm, mawakili na wsnasheria wa ccm ndio wamejaa pale.
Nani alimsikia Bahati Alex wakati wa kufunga kipindi? Alisoma messsge kutoka kwa rais kwamba naye alikuwa anafuatilia kipindi. Aha,! Hivyo mjiongeze.
Ila nimshauri mh rais hivi: kupongezwa na wanaccm wenzake is a non-issue. Si habari hiyo. Everybody expects that. Infact wengi wao wanatokwa mapovu ya kupongeza kwa sababu wameshaujua udhaifu wa Mh rais. Kwamba mpongeze na kumsifia sifia uule.
Namshauri mh rais aache kabisa huu utaratibu wa kuteuwa watu tu eti kwa sababu wanamwimbia mapambio! Arudi kwenye ule utararibu wa kuxingatia weledi na taratibu za utumushi wa umma katikauteuzi. Hawa watu wanakupasifa za uongo mh rais. Watakuponza!
 
Mpumbavu baba yako.
Acheni matusi babu zenu tupo humu, au tuweke picha zetu tunaheshimiane
fc4db289530a3890cfbd29665d1704cd.jpg
 
Inawezekana ikawa ni uwoga katika kulinda maslahi yao, kama nchi ilipofikia sasa uhuru wa kuongea umekua hadimu wachache ndio wenye uthubutu kama wa yule “panya wakijivu aliemfunga paka kengele” na kuwakomboa wenzie wote!!

Wengi wata endelea kusifia!! Ni nani wa kumlaumu!??
 
Umeonae? Mwenyewe Nilkuwa naangalia ilbidi nihamishe channel. Hataree
NIlijitahidi kuangalia mpaka pale Raisi wa bao alipoanza ngonjera zake nikazima kabisa tv Jamani kwani kuna nafasi iliyobaki haijajazwa maana ................................
 
Huenda washiriki wote walipewa semina elekezi kabla kipindi hakijarushwa hewani
Hawana cha semina wala nini, sio kila mtu anayeenda pale huruhusiwa kuingia bali huchaguliwa baadhi tu na wanaochaguliwa kwa sasa ni wale wanaojulikana ni mawakala wa CCM.

Mwanzoni hata CHADEMA walikuwa wanaruhusiwa kuingia lakini mle ndani walikuwa hawaruhusiwi kutoa maoni ya kuikosoa serikali, kuna lile litangazaji linene liliaza mpaka kuwa lisemaji la serikali kuanzia hapo wengi siku hizi hatuangalii kabisa ITV hata habari tunaangalia Azam 2.
 
KIPINDI: Malumbano ya Hoja
MAADA: Miaka miwili ya serikali ya awamu ya tano, nini mafanikio na changamoto?

Wachangiaji wote wanamsifu Magufuli, hakuna anayemkosa raisi. Wakuu, mimi ni mfugaji wa ng'ombe, hata ng'ombe huwa hawafikiri sawa. Unaweza ukataka kuwasagwa waende mbele lakini utaona kuna wengine wanaenda pembeni na wengi wanarudi nyuma, hiki ni kiashiria kwamba ng'ombe pia hutofautiana fikra na maamuzi.

Nashangaa kuona hawa wachangiaji wote wana mawazo sawa, je? watu hawa wametolewa wapi na ITV?
Kuna na ITV umeangukia kule kule kwenye kupanga matokeo.
Haiwezekana ukapanga kipindi ukakiita MALUMBANO YA HOJA alafu kisiwe na malumbano yoyote ya hoja bali kusifiana mwanzo mwisho.
Mzee Mengi vijana wako wanatunyima tunachostahili.
 
KIPINDI: Malumbano ya Hoja
MAADA: Miaka miwili ya serikali ya awamu ya tano, nini mafanikio na changamoto?

Wachangiaji wote wanamsifu Magufuli, hakuna anayemkosa raisi. Wakuu, mimi ni mfugaji wa ng'ombe, hata ng'ombe huwa hawafikiri sawa. Unaweza ukataka kuwasagwa waende mbele lakini utaona kuna wengine wanaenda pembeni na wengi wanarudi nyuma, hiki ni kiashiria kwamba ng'ombe pia hutofautiana fikra na maamuzi.

Nashangaa kuona hawa wachangiaji wote wana mawazo sawa, je? watu hawa wametolewa wapi na ITV?
Hiki kipindi kitakuwa kimeshanunuliwa. Kwanza kimeshakosa uelekeo
 
Back
Top Bottom