Nakubaliana na wewe. Wengine tumesema muda mrefu kwamba ITV na magazeti ya IPP ghafla yamebadilika. Kumbuka kulikuwa na mvutano fulani kati ya Bashite na vyombo vya habari vya Mengi. Hapo katikati pengine kuna jambo limefanyika ndipo yakatokea haya mabadiliko ya ghafla. Ma vendor wanadai gazeti la Nipashe limeanza ku drop kwenye mauzo (sina uhakika).Iko hivi wazee. Kile kipindi kiliandaliwa maalum kusifia utawala wa Magu baada ya miska miwili. ITV walikiandaa kushirikiana ma polepole. Ndio maana uliona wawakilishi wa ccm ndio walijaa pale. Makatibu wa uvccm, mawakili na wsnasheria wa ccm ndio wamejaa pale.
Nani alimsikia Bahati Alex wakati wa kufunga kipindi? Alisoma messsge kutoka kwa rais kwamba naye alikuwa anafuatilia kipindi. Aha,! Hivyo mjiongeze.
Ila nimshauri mh rais hivi: kupongezwa na wanaccm wenzake is a non-issue. Si habari hiyo. Everybody expects that. Infact wengi wao wanatokwa mapovu ya kupongeza kwa sababu wameshaujua udhaifu wa Mh rais. Kwamba mpongeze na kumsifia sifia uule.
Namshauri mh rais aache kabisa huu utaratibu wa kuteuwa watu tu eti kwa sababu wanamwimbia mapambio! Arudi kwenye ule utararibu wa kuxingatia weledi na taratibu za utumushi wa umma katikauteuzi. Hawa watu wanakupasifa za uongo mh rais. Watakuponza!
tafakuri yetu tunaweza kuipanua kidogo. Alialikwa mzee Simbeye kuzungumza kwa niaba ya wafanyabiashara (bila shaka). Huyu ni mtu ambaye yuko karibu na Mengi. Alivyokuwa akiongea, ukimtazama usoni ni kama wakati mwingine alikuwa akizungumza mambo ambayo hata yeye mwenyewe hayaamini! Sekta ya biashara ina changamoto nyingi mno, lakini mzee huyu alionyesha kama mambo ni barabara mno! Sasa ukija kwa wachangiaji ilikuwa aibu kabisa kwa kweli..Ni kushusha hadhi ya kituo cha tv na kipindi chenyewe. Na kwa mwendo huu labda iwe u super brand huwa unanunuliwa, vinginevyo kituo kinachungulia kaburi kwenye content. Ninaunga mkono hoja yako kwamba hawa watu walikuwa wameandaliwa!