Daata
JF-Expert Member
- Dec 24, 2012
- 4,639
- 1,793
Mtaani ndo wanaitwa ma -super star
Hicho ndicho kiwanavimbisha vichwa wakati kamna kitu
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mtaani ndo wanaitwa ma -super star
Ingefaa hata hawa wenye Tv station kabla hawajazirusha hewani waziangalie kama ulivyosema dosari yoyote itskayoonekana wapewe wakarekebishe,ni wendawazimu watu wanaigiza vitu wasivyovijua then wanaita eti movie,movie my foot..kuna kale kakipande mama yuko jikoni anakaanga kuku,wanapoteza mda kuonyesha jinsi mpishi anavyogeuza vipande vya kuku,kutoa kuweka kwnye sinia kisha kurudia tena hivyo hivyo yan sehem isiyokuwa na mpango wwte inachukua dk4,kikawida tungeona tu mama yuko jikon akipika kisha sekunde 10 tungeona wako mezani wanakula,wanachosha wasanii wetu.
Kuna movie nilikua nikiangalia hapa EATV inaitwa CHOZI LA BABA duuuh yaaan kuna kipande kimenishangaza sana yan mtu ameshindwa ata kupiga ishara ya msalaba kweli duuuh kwa style hii kweli uigizaji gani huu...
Kwa atakayeipata angalia kipande kile mama mtu na mwanae wa kike walipo kwenda kaburini kuangalia kabur la baba yao kilicho tokea ni kwamba wote wawili izo ishara tu za msalaba zimekuwa tatizo...
Movie za bingo soko la kimataifa bado sana
Mkuu hata mimi niliona nikashangaa sana,kuwaje watake kufanya ishara ya msalaba ilhal hawakufundishwa hivyo ktk kile wanachokiamini,na kwanini wahusika wasingeruhusiwa kwamba wafanye maombi kwa kuzingatia walichofundishwa ktk imani zao,wasanii wetu badilikeni hizo movie zenu hawaangalii wa Tz tu jaribuni kuigiza hali halisi ya mnachoigiza sio mnakariri then mkikosea hamfanyi hata editing kuondoa au kurekebisha kile mlichokosea,sijui ni njaa inawasumbua maana mnataka kuachia movie 10 ndani ya mwezi mmoja but ubora ni sifuri yaani zero,badilikeni mna-bore.
ukichunguza vizuri utagundua hao si wakristo. ni waoslam ambao kwa 'bahati mbaya' wamekumbana na hiyo scene na walawa reluctant kuigiza uhalisia. sijaiona ila ni mtazamo wangu
wafuasi wa ccm hao na akili zinafanana hivyo hivyo
Kuna moja nilicheka miaka ya nyuma sana eti steringi alimfytulia mkuu wa maadui risasi na kioo kilikuwa kimewatenga mkuu wa maadui baada ya kufytulia risasi upande mwengine wa kioo akaanguka na kufa na damu kibao kuchuruzika lakin kioo hakikuvunjika.
Nyingine eti jini kuvuka barabara anaangalia kushoto kulia kushoto na kuhakikisha hamna magari anavuka
Nasikia the young billionaire ya kanumba the legindary (rip) waliekti masaa kumi na moja tu kwa anzia asubuhi had jion
inspekta seba nini?? Kwa upande flan alijitahid inspekta seba hasa ile last scene fight mkuu wa maadui alikuwa noma kweli nilimkubali alikuwa anaruka sarakas wewe anabwaka hapa na kuibukia upande wa pili anaweza pia kuzama hapa na kuchomoza kwengine. Ilimchukua muda mrefu sana inspekta seba kumzibit kwenye hule mjengo chakavu. Walijitahid sana kibongobongo kwenye hii movieMnakumbuka na zile za action et sterling na jambazi wanavyo pigana bac ni vituko tu akipiga teke mmoja nae nangoja mwenzie arudishe ndo anapiga tena na wlmwenzie anamngoje ivo ivo kweli bongo bwana