Maajabu ya bongo movie..

Kuna Hemed ananiboa sana, Hereni muda wote hata akienda kulala.
Ushawahi kuona mtu anaenda ofisini huku amevaa hereni?
Ofisi ya nani watakuruhusu uvae hereni?
Bongo movie alizikwa nayo Kanumba
 
Inasaidia mtu ukiwa tayari na jina, hivyo ukiigiza panakuwa na mvuto zaidi, imagine Mbowe akaamua kuigiza movie leo hii.., its likely ita vutia..
 
Huyu majuto ni moja ya waigizaji wapuuzi kupata kutokea dunian.angekuwa baba yangu ningemkana anaigiza movie za kipumbavu sana na hazina maadili. Ingawa yeye na watu wenye akili kama zake wanaamin ndo anachekesha.kiukwel sikuwah kuona anachochekesha ni nini zaid ya utoto utoto.

iv ile muvi ya majuto na wenzie inaitwa inye plus nayo sion kama ina maadili kabisa..wala haichekeshi cha zaid ipo kama ponograph..
 
Jamani, kama movie ya dk 15 wanaboa kiasi hiki, je ikitokea series ya kibongo [emoji15] [emoji15] [emoji15] [emoji15]
 
December 27. 2014. ........ nilikuwa nasoma uzi bila kujua ni kaburi la zamani..... kumbe game lilianza kuharibika kitambo hivi[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]

Wangejirekebisha siku hizo , wasingefika hapa leo.
 
Hongera RC kwa kuonyesha uzalendo japo ni maamuzi magumu kuzuia filamu za nje na si wote tulio furahia, twende kazi.
 
Bongo movie ni takataka na makelele tu,kitu bora hujiuza chenyewe na si kwa kushikiwa bango
 
Hongera RC kwa kuonyesha uzalendo japo ni maamuzi magumu kuzuia filamu za nje na si wote tulio furahia, twende kazi.
Tutaenda kuangalia mikoa mingine,kule Tunduma watu huvuka mpaka kwenda kunywa viroba huku wakiwapungia mikono polisi wa TZ na wakishalewa hurudi TZ.Kwa watu waliofika Tunduma nadhani wanujua huo mpaka ulivyo ,
 
king majuto yupo vizuri Sanaa tatzo ni production mbovu

jaribu kuangalia kipaji cha mtu si kukimbilia uvumi wa watu kisa bongo movie zinachukiwa na wengi
 
Nionavyo mimi Bongo Movie wanahitaji kufanya utafiti kwanza kabla ya kulalamika. Dunia ya sasa ni ya ushindani kwa kila kitu, suala la kutegemea kubebwa kwa uzalendo halipo. Wanatakiwa wajiulize tatizo lipo wapi? Ubora wa filamu? Maudhui? Waigizaji? Watanzania wanataka nini?

Kimsingi Bongo Movie kuna kundi ambalo siyo wabunifu kabisa na hawaijui film industry ikoje. Kwa mfano filamu nyingi za magharibi zinabase aidha kwenye vitabu vilivyotungwa na waandishi mahiri au matukio halisi kwenye jamii ( angalia sinema za James Bond zinabase kwenye novel za Ian Flemings au sinema iitwayo John Q ya Dezel Washington inayoakisi maisha ya tabaka fulani). Kwa kufuata hivyo mtu anahamasika kuangalia filamu.

Tulikuwa na tunao waandishi mahiri wa vitabu hapa nchini kwa mfano marehemu Elvis Musiba ( Njama, Kikosi cha Kisasi nk), Hammie Rajabu, Ben R Mtobwa ( Tutarudi na Roho Zetu?) na akina Eric Shigongo ( Rais anampenda mke wangu) na wengine wengi, lakini hakuna mwigizaji aliyethubutu kuigiza kutoka vitabu hivyo. Hivi ni nani hatoshawishika kuangalia filamu ya Willy Gamba?

Watazama filamu hushawishika na stori kwanza kisha kujua nani aliyeigiza (Angalia Bourne Identity, Bourne Ultimatum). Bongo movie wao wanang'ang'ania stori ambazo hazivutii, hivyo hata kama itaigizwa na gwiji JB itaonekana hovyo tu.

Teknolojia pia inawaangusha Bongo Movie. Wanatumia vifaa duni sana kutengeneza filamu. Camera, editing, production ni kama za kurekodi harusi, kweli jamani?

Ushauri wangu ni kuwa wasijipe umaarufu kama vile wameshafanya kazi kubwa sana kwenye film industry, wakae chini na kubuni vitu vitakavyosisimua watazamaji na siyo kutoa kitu kisicho na mashiko halafu kulazimisha watu waangalie. Wawashirikishe wasomi katika taaluma hii ili kuwakwamua hapa waliponasa.
 
Umeongea point mwanzo mwisho
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…