Mkuu nikuambie tu kwamba Kagame ana wapinzani lukuki toka jeshini kwake; Kumbuka akina Gen. Kayumba Nyamwasa, Col. Karegeya na Brig. Gen. Kazaura walishamkimbia na wanamfahamu vizuri na hilo Gen. Kagame analijua. Pia ana wapinzani wengi tu wa Kabila la Hutu wala si wa kutafuta japo hakuna haja ya kufanya hivyo. Kwa upande wa Museveni naye ukumbuke kwamba kuna watu wake wa ndani walishamkimbia. Hawa ni kama Gen. David Sejusa (Tinyefunza), akina Gen. Mugisha Muntu, Col. Basigye nk. Ukiona watu kama hao yaani high ranking army officers wanakumbia basi ujue upinzani ni mkubwa ndani ya jeshi kwani nao huwa wana wapiganaji ambao wanawaunga mkono kinachosubiriwa ni cheche tu na moto uwake! Tusiende huko. Gen. Kagame na propaganda zake zinakaribia kufikia mwisho.
Asante kwa kunijuza.