Lukuvi: Standardization ifanyike ili matokeo ya wanafunzi yalingane

Lukuvi: Standardization ifanyike ili matokeo ya wanafunzi yalingane

Matokeo kufutwa sio kitu cha ajabu,standardization pia sio kitu kipya,form 4 1998 kuna mitihani ilifutwa baada ya kuvuja hivi nyie form 4 wa mwaka huo msiajiriwe kwa kua ni wezi wa mitihani?au mnadhani hao watoto wa form 4 ya mwaka jana hawana nafasi tena kwenye nchi yao kisa wamefeli?nyie mnaoshinda kwenye facebook wakati wakazi hamuoni kua na nyie mmefeli kwenye kazi zenu?

Acha kutumiwa mkuu, inaonekana uwezo wako wa kufikiria hauna tofauti na wa Lukuvi na serikali yake; Yaani wewe kwa mtizamo wako kufutwa kwa mtihani wa mwaka 1998 kutokana na kuvuja kwake, na saga la vijana kufeli kwa kiasi cha kutisha mwaka 2012, unaona ni matukio yanayo fanana ?
 
Standardization ni kitu cha kawaida na kinafanyika duniani kote! Hivyo usione ajabu!

Niliwahi kuandika humu kuwa katika mwaka mmoja wa miaka ya 80 wanafunzi wa third year engineering UDSM karibu wote walifeli hesabu lakini alipokuja external examiner kutoka Makerere 90% ya wanafunzi walipasi!

Mkuu hakuna anaye pinga hoja ya standardization, possibly umekurupuka. Je standardization inafanyika wakati gani ni kabla au baada ya matokeo ? Je unataka kutuaminisha ya kuwa Mhadhiri wa hesabu kitivo cha Engineering alitangaza matokeo na ikaonekana wanachuo wote wamefeli, baadaye akaitwa external examiner kutoka Makerere ndo ku-standardise, kubatilisha na kutangaza matokeo upya ?

Mkuu, kwa uelewa wangu mdogo nilio nao, Standardization huwa ni siri ya Mwalimu wa somo na ofisi yake na siyo swala la kawaida kama unavyotaka kutuaminisha. Kwa mantiki hiyo basi Serikali kwa ushirika wa Dr. Joyce Ndalichako walitakiwa wafanye standardization kabla matokeo ya kidato cha nne - 2012 hayajatangazwa na waziri wenye dhamana. Na kulikuwa hakuna umuhimu wowote wa kututangazia ya kuwa matokeo haya ni baada ya standardization, kama nilivyosema awali ingebaki kuwa siri ya Dr. Ndalichako na NECTA yake na siyo vinginevyo.

Hivyo maamuzi yoyote ya ku-utangazia umma wa Watanzania juu ya hatua ya standardization baada ya matokeo ya kidato cha nne 2012 yamesha tangazwa, na baadhi yao wakiwa wamesha chukua result slip hayata kuwa na tija kwa taifa, sana sana ni muendelezo wa utekelezaji wa ilani ya CCM ya "Bora Elimu".
 
Naona mkuu master peace unavyo endeshwa na hisia na kuukwepa ukweli.

Suala la elimu hasa ili la kushuka kwa ufaulu limefanyiwa utafiti na tume ya Pinda, wajumbe wa hiyo tume ni wadau wakubwa wa elimu hapa nchini, na wala sio wanasiasa.

Lakini vilevile, maamuzi ya kusahisha upya na ku-standardize yametolewa na serikali kufuatia mapendekezo ya tume, sasa hapa siasa iko wapi?

Kinachofanyika hapa sio kibaya, ila ni katika jitihada ya kunusuru hawa watahiniwa, angalau waendelee na masomo ya kidato cha tano na sita, huku jitihada za kuboresha elimu zikiendelea.

Watakao nufaika na utaratibu wa standardization sio waliopata daraja sifuri, la hasha, ila serikali inataka wale wenye daraja la 4 na point 28-29 wafike angalau daraja la 3 na point 25.

Wewe kama mtanzania tena mzalendo utathubutu kukebehi na kukejeli maamuzi haya? hemu tuweke utaifa mbele na tuubariki huu mpango ili vijana waendelee na masomo, hizi dhihaka hazijengi chochote ndugu zangu.

Mkuu, possibly wewe unaishi ughaibuni; Utafiti huo ulikuwa na lengo gani ? Yaani kuna Mtanzania asiye jua kwa nini wanafunzi wamefeli ?
Je una uhakika gani kuhusu uhuru wa tume iliyo undwa na Mizengo Pinda ? Je mie nikisema tume imetekeleza majukumu yake kwa maelekezo kutoka juu, yaani haikuwa huru, ntakuwa nimekosea ?

Is standardization a solution of that problem, or it is just a postponement of the problem ?
Tatizo lako wewe na serikali yenu mmezoea zima moto, Tuambie basi mtaendelea na mfumo wa standardization hadi lini ?
 
Tuacheni ushabiki muda mwingine, Lukuvi ana kosa gani hapo? Yeye katoa msimamo wa serkal kama muwakilishi,
Pia wengi tulikuwa tukitoa povu na kusema tume ya pinda haitakuja na lolopte jipya alafu leo hii tunaanza kulalama,
Wengi wenu mnaotoa povu either hamna uchungu na wadogo zenu waliofelishwa, watu wamezika huku mtaani hiv hiv kisa upumbavu wa NECTA alafu mnaanza kutetea upumbavu na wakati wengi humu JF tilifahulu kwa alama za zamani sasa kwanini tulazimishe hawa madogo wapimwe kwa kutumia alama mpya tena za juu sana.? Shit !!!

Mkuu punguza jazba, inaonekana na wewe ni miongoni mwa victim; sijakusoma vizuri hapo kwenye red, walifelishwa na nani ?
 
Imagine Lukuvi ndo kichwa cha CCM bungeni, serikali dhaifu mnoooo
 
Mleta mada inaelekea elimu yako ndogo sana, utambui mhe. Lukuvi ni nani kwenye ripoti ya tume ya Pinda?
Mhe. Lukuvi amekukera kwa lipi? maana alichopeleka bungeni ni maazimio ya serikali na wala sio yake binafsi.
Kuhusu standardization, watakokotoa kiwango ambacho kitaongezwa kwa kila mwanafunzi, mara nyingi kiwango hiko hakibadili sana matokeo, maana ni ongezeko dogo tu linaongezwa.

we mjanja, maana hata ban umeweza kuichakachua!! any way turudi kwenye uzi
Hii serikali haikupaswa kufanya hivyo, kwani huo mfumo uliotumika ulishajadiliwa vya kutosha na ukaonekana unafaa tena waziri akiwa mwenyekiti katika kikao cha kujadili huo mfumo, leo wanamtetea kwamba ulikuwa haufai. Maswali tunayoweza kujiuliza ni kuwa
- waliupitishaje mfumo ambao haukufanyiwa uchunguzi wa kutosha? je walienda kufanya nini kama walipitisha mfumo usiofaa.
- Je kwa huo wastani watakaoongeza, watatuhakikishiaje kutokuja tena na hoja za matokeo mabaya huko baadae kama tunavyoona sasa wanavyolalamika watoto wanaojiunga kidato cha kwanza hawajui kusoma wala kuandika huku ni wao viongozi ndio walioshusha wastani toka 30/50 chini ya miaka ya 2000 na kuwa masomo matano na wanafaulu kwa wastani hadi wa 15 kwa somo na baadhi ya wilaya kushusha hadi 10.
- Je hawatokuja na hoja kama zile tulizoona za kuchanganya masomo ya Chemistry na Physics na baada ya muda mfupi yakatenganishwa tena? Pia ya kufuta masomo ya Commace na Bookeeping kwa O-level na baada ya muda mfupi wakayarudisha tena.
- Je sababu iliyotajwa ndiyo sababu pekee ya kushuka kwa matokeo? na kama ndiyo mbona huko nyuma matokeo yaliendelea kushuka pamoja na kusisitiza mfumo huu mpya usitumiwe na badala yake watumie mfumo wa nyuma?
- Kwa trend hiyo fupi tu je serikali yetu iko makini katika maamuzi yake? na kama haiko makini leo tutaamini vipi kauli hiyo inayosemwa?
Hata hivyo kwa watu wachambuzi, wadadisi na wapenda maendeleo ya Tanzania kwa Quality sio Quantity kama tunavyoona sasa katika sekta hii ya elimu watakwambia serikali haiko makini. Umakini wa sasa ni kiongozi kuendelea na madaraka bila kujali utendaji na uwajibikaji wake kazini.
 
Mleta mada inaelekea elimu yako ndogo sana, utambui mhe. Lukuvi ni nani kwenye ripoti ya tume ya Pinda?

Mhe. Lukuvi amekukera kwa lipi? maana alichopeleka bungeni ni maazimio ya serikali na wala sio yake binafsi.

Kuhusu standardization, watakokotoa kiwango ambacho kitaongezwa kwa kila mwanafunzi, mara nyingi kiwango hiko hakibadili sana matokeo, maana ni ongezeko dogo tu linaongezwa.

mara ya kwanza nilijua wanasahihisha upya na kutoa matokeo katika viwango vinavyojulikana tu bt kama sababu ni standardization huo ni ufinyu wa mawazo......

Hii serikali imekopa hela imemaliza saivi wameanza kukopa marks za kuwaongezea wanafunzi pindi wanapofeli?
 
Tuacheni ushabiki muda mwingine, Lukuvi ana kosa gani hapo? Yeye katoa msimamo wa serkal kama muwakilishi,
Pia wengi tulikuwa tukitoa povu na kusema tume ya pinda haitakuja na lolopte jipya alafu leo hii tunaanza kulalama,
Wengi wenu mnaotoa povu either hamna uchungu na wadogo zenu waliofelishwa, watu wamezika huku mtaani hiv hiv kisa upumbavu wa NECTA alafu mnaanza kutetea upumbavu na wakati wengi humu JF tilifahulu kwa alama za zamani sasa kwanini tulazimishe hawa madogo wapimwe kwa kutumia alama mpya tena za juu sana.? Shit !!!

Mkuu.
Punguza jazba,pata Glass ya Maji kwanza then shusha Pumzi.
Hivi NECTA ndo wanatengeneza mitaala.
Hivi NECTA ndo wako responsible kuboresha Maslah ya Walimu ,kujenga Vyoo mashuleni,kupekeka Vitabu shulen etc etc.
Kama utakuwa umeshusha Jazba then sidhan kama utaendelea kuilaumu NECTA.
Hiv unafikir kuwa hawajui standardization??
Hivi Mkuu unaelewa Standardization zinafanyika katika Circumstance zipi.
Mwaka Jana Mwanaasha Kikwete alitambalia Magoti tukawa bigup NECTA.
Leo vp tena Mkuu
 
watoto watazidi kuvaa milegezo na kunyoa viduku mashuleni, kama mpango wenyewe ndio huu, wa standardization after matokeo...
 
Naweka Kumbukumbu sawa.
Mwaka jana,Mwanaasha JK alipata Division 4 pekee Feza Girls.
 
mambo ya double standard sijui yatatutoka lini tu ndg zangu; leo unasema hivi kwa huyu, na kesho unasema vingine kwa hoja ileile isipokuwa kwa mtu mwingine. nani anafahamu kama mwaka jana matokeo wali-standardize na kwa factor gani ikilinganisha na haya? form four wote waliopita nao wanaweza wakadai matokeo yao yachunguzwe.
 
Mkuu punguza jazba, inaonekana na wewe ni miongoni mwa victim; sijakusoma vizuri hapo kwenye red, walifelishwa na nani ?

Mkuu ndio mimi sio victim lakin ninaweza kuwa victim kama mtanzania mdau wa elimu maana kila mtanzania ni victim hata wewe pia, lakin kwakuwa umeshajiexclude kuwa ww sio victim so hakuna chochote utakachojenga zaidi ya kubomoa.

Swali kwako unaamini walimu wakilipwa by 100% ndo madogo watafahulu kwa ghafla? Pia una uhakika gan wanafunzi hawajafelishwa?
 
Nadhan na ya mwaka huu watastandardize pia, ninamdogo wangu yupo form 4 bonge ya kilaza akijitahid saana atapata division 4, lakin kwa matakwa ya Lukuvi na wenzake serikaln anaweza akapewa division 1.
 
Unataka kusema NECTA hawajui standardization.? Au magoli yanapanuliwa ili kila mtu afunge?. Maana magoli madogo wagungaji wachache hivyo serikali imeona ni vyema milingoti ya magoli kutanuliwa ili wafungaji wawe wengi, badala ya kuhangaika kuwafundisha wafunga magoli!.

Sent using wireless by wire
Hapana, magoli hayapaswi kupanuliwa bali kitakachofanyika ni kutumia marking scheme iliyokuwa ikitumika miaka ya nyuma na siyo hiyo mpya iliyobuniwa na Ndalichako!
 
Mkuu hakuna anaye pinga hoja ya standardization, possibly umekurupuka. Je standardization inafanyika wakati gani ni kabla au baada ya matokeo ? Je unataka kutuaminisha ya kuwa Mhadhiri wa hesabu kitivo cha Engineering alitangaza matokeo na ikaonekana wanachuo wote wamefeli, baadaye akaitwa external examiner kutoka Makerere ndo ku-standardise, kubatilisha na kutangaza matokeo upya ?

Mkuu, kwa uelewa wangu mdogo nilio nao, Standardization huwa ni siri ya Mwalimu wa somo na ofisi yake na siyo swala la kawaida kama unavyotaka kutuaminisha. Kwa mantiki hiyo basi Serikali kwa ushirika wa Dr. Joyce Ndalichako walitakiwa wafanye standardization kabla matokeo ya kidato cha nne - 2012 hayajatangazwa na waziri wenye dhamana. Na kulikuwa hakuna umuhimu wowote wa kututangazia ya kuwa matokeo haya ni baada ya standardization, kama nilivyosema awali ingebaki kuwa siri ya Dr. Ndalichako na NECTA yake na siyo vinginevyo.

Hivyo maamuzi yoyote ya ku-utangazia umma wa Watanzania juu ya hatua ya standardization baada ya matokeo ya kidato cha nne 2012 yamesha tangazwa, na baadhi yao wakiwa wamesha chukua result slip hayata kuwa na tija kwa taifa, sana sana ni muendelezo wa utekelezaji wa ilani ya CCM ya "Bora Elimu".

Kwanza napenda kukuhakikishia kuwa sijakurupuka bali ni nimetumia kanuni zinazotumika katika kusahihisha mitihani kote duniani!

Pili naungana na wewe kuwa standardization ilipaswa kufanywa mara baada ya matokeo halisi kufahamika na kabla ya kutangazwa rasmi kwa umma. Hivyo ni kweli wizara ya elimu ilifanya makosa kuharakisha kutangaza matokeo kwa hiyo serikali inapaswa kujilaumu yenyewe. Labda serikali ilifanya hivyo ili kupata sympathy ya wananchi na hivyo wananchi wawachukie waalimu, jambo ambalo halikutokea na badala yake wananchi wakaungana na waalimu kuishinikiza iboreshe maslahi ya waalimu!

Kifupi naweza kusema lilikuwa kosa kubwa la kiufundi lililofanywa na serikali!

Kuhusu kitivo cha engineering, external examiner aliitwa baada ya matokeo kufahamika lakini ilikuwa kabla ya kutangazwa kuwa matokeo rasmi!
 
Hivi kwanza Lukuvi alipeleka maazimio ya serikali kuhusu suala la elimu yeye ndie waziri wa elimu? Kawambwa na mwenzie F6 liver wako wapi?
 
Hapo tunapigwa changa la jicho, kama kweli Matokeo yanaweza kutangazwa bila Waziri kufahamu mchakato wa kuyaandaa basi amekosa sifa ya kukalia kiti hicho. Yeye ndiye anayechagua wajumbe wa Baraza na kwa taarifa nilizonazo kutoka vyanzo vya kuaminika Maafisa wa Wizara pamoja na Kamishna wa Elimu ni wajumbe wa Baraza la Mitihani, iweje serikali inadai kuwa haikujua kinachoendelea NECTA?? Gazeti la the Guardian on Sunday limeandika makala ndefu sana kuhusu saga hili uk 1,2,3 na 12 na katika uk wa 2 kuna sehemu anasema haya yote yanayosemwa kulaumu baraza yanaonesha kuwa "something fishy could have occured btn NECTA and the Ministry" Naunga mkono hoja it is really fishy
 
Lukuvi na ccm ni hewa chafu kwa taifa
 
Back
Top Bottom