Wizara ya Elimu, njooni na mbadala wa kuwafutia matokeo Wanafunzi

NAMBA MOJA AJAYE NCHINI

JF-Expert Member
Oct 29, 2019
8,526
17,433
Ni hivi majuzi tu matokeo ya Darasa la Saba yametoka ya Shule mbalimbali nchini. Kuna baadhi ya Shule zimefutiwa matokeo kutokana na uzembe na ulaji rushwa wa wasimamizi, tuseme wanafunzi wameingizwa mkenge na waliowaamini kama wasimamizi na walimu wao.

Kuwafutia wanafunzi matokeo ni adhabu kali sana tena ya maisha na kuteketeza ndoto zao za kuwa wataalamu wa kada mbalimbali. Mi nadhani umefika wakati wa kufikiria mbadala wa janga hili napendekeza yafuatayo!

1. Warudie kufanya mtihani mwingine na gharama zifidiwe na wazembe waliosababisha usimamizi mbovu. Ikiwezekana wazazi walipe ada ya kuendesha mitihani ya watoto wao! Wasimamizi mali zao zipigwe mnada kufidia gharama za mtihani walioshiriki kuvujisha.

2. Wanafunzi waliofutiwa matokeo warudi tena darasani kwa mwaka mmoja zaidi yaani wasome kwa miaka minane elimu ya msingi ili wafanye mtihani kama watahiniwa wengine wa mwaka huo!

Kumbukeni kuendelea kuboresha maslahi ya walimu waondokane na rushwa ndogo ndogo kama 25000/= ambazo zinakosti utumishi wao na kudhalilisha kada za elimu nchini.
 
Nadhani watoto sio sawa kuadhibiwa kwa adhabu kubwa sana kwa makosa na ushawishi uliofanywa walimu.

Wabafunzi ambao ni watoto kiumri wakiwa na wastani wa miaka 12-14 hawana access na wapi mitihani inawekwa.

Baraza litoe adhabu ya kufuta matokeo ila iwape nafasi ya kufanya mtihani upya kwa kulipia gharama za mtihani.

Walimu wapewe adhabu kali kwa kuiba mtihani na kuwashawishi watoto kushiriki uhalifu.

Barrick na Kampuni mama ya Airtel (Barti Airtel) toka India; wote hawa ilithibitika kusababisha hasara au kukwepa kodi na ilikuwa kosa. Ila hawakufutiwa usajili wa kufanya kazi Tanzania na kuondolewa.

Walirekebisha makosa hayo na biashara kuendelea.

Sio haki mtoto kupewa adhabu kubwa sana wakati yeye hakuwa primary cause ya wizi wa mtihani.

Freddie M.
 
Back
Top Bottom