Hao waandaaji wasingetenda haki sana kwa kumpambanisha Lukuvi na Lissu, jamani hakika hawaendani, Lukuvi mimi najua tu ni cheo kikubwa tu lakini ukweli hana kitu, zile ni natural confidence za kabila lake na kwa vile yuko chama kama CCM anaonekana mtu makini kweli hasa kwa serikali ya Kikwete, ukiongezea na hasira zake za asili plus ushushu uhakika wa kula ndani ya chama na serikali hii bado anao.
Kwa ccm watu makini hawana chao, ukimkuta mtu ulikuwa unamfahamu ni makini ndani ya mfumo wa ccm ya sasa anachofanya kwanza ni kuficha uelewa wake kwanza na kujifanya mbumbumbu ili aweze kuendana na mfumo na baada ya hapo maisha husonga mbele, yaani anakubali kuwa mnafiki kwanza. Mifano ipo mingi kwa wafatiliaji wa mambo mnajua, mfano mdogo sana mnaweza kumbuka lile kundi la ccm la wapinga ufisadi tangu enzi la Richmond, sio kwamba hawapo , lakini wametulia kimya ili kuendana na mfumo wao.
Tanzania yetu ina hali mbaya sana chini ya ccm ya sasa kuliko labda wakati mwingine wowote kwenye uhai wa nchi hii. Lukuvi anajijua alivyo, binafsi nampongeza kwa kutokubali huo mdaharo, ila tu asisingizie kutokuwa na taarifa, mara ziara nk, yeye aseme wazi hana uwezo wa kusimama na mtu makini kama Tundu Lissu kwenye mjadala wa kitaifa na kikanuni kama huo.