Waziri Lukuvi amekataa kushiriki katika mdaharo ulioandaliwa na asasi moja juu ya kilichojiri Bungeni kuhusiana na mchakato wa Katiba mpya.Mdaharo huo ambao ulipangwa kufanyika Jumapili kuanzia saa Saba mchana hadi saa Kumi na mbili jioni ungewashirikisha Waziri Lukuvi na Mnadhimu wa Kambi ya Upinzani Bwana Tundu Antipasi Lissu.Katika maelezo yake ya kwanini hatashiriki kwenye mdaharo huo Waziri Lukuvi alidai kuwa hana taarifa kutoka ofisini kwake juu ya mwaliko huo kwasababu alikuwa ziarani mikoani kwa shughuli za kikazi na kwamba anapanga kuelekea Mkoani Iringa leo kama mwendelezo wa ziara zake za Mikoani za kikazi.
Mkuu midahalo ya wenzetu inakuwa so organized na inakuwa imeandaliwa na taasisi ambayo haifungamani na upande wowote, usifananishe midahalo hii na huu upup wa kitanzania ambao kwanza watu wanakaa na kutafuta namna ya kumkaanga mwingine na mnaletewa mtu kama R.K kuongoza mdahalo unategemea nini? mfano mzuri ni huu ambao LUKUVI ameukataa, tayari ilishafamika kuwa miongoni mwa wataohusika moja kwa moja ni mkuu wa SAUT, yule CDM 100% au mtu kama LWAITAMA au KAKOBE wahudhurie mdahalo what do you expect? Tanzania hatuna taasisi za kuandaa midahalo, inabidi kwanza tulione hilo badala ya kukimbilia kuwa mashabiki tu.
Kwa kiongozi wa serikali kawaida tu hakuna la kushangaza mkuu, mtumishi wa siku nyingi sana yule, huwezi kumlinganisha na kiongozi tu wa chama cha siasa ambao nao wana nyumba za aina hiyo.
Serikali ilishashtukia midahalo inayoandaliwa na kwa udhamini wa WAPINZANI, halafu hata hivyo kama wana hoja si wangepingana naye bungeni kama siyo ushahidi tosha kuwa wanatumia media vibaya.
Acha uwongo dogo!!,Hakuna serikali yoyote duniani inayoandaliwa midahalo na media zenye mwelekeo wa Upinzani, hata mimi ningeshangaa kuona Serikali inaingia mkenge kiasi hicho.