Lukuvi akwepa mdahalo na Lissu

Lukuvi akwepa mdahalo na Lissu

TECH WIZ

JF-Expert Member
Joined
Jun 7, 2013
Posts
1,675
Reaction score
555
Waziri Lukuvi amekataa kushiriki katika mdaharo ulioandaliwa na asasi moja juu ya kilichojiri Bungeni kuhusiana na mchakato wa Katiba mpya.

Mdahalo huo ambao ulipangwa kufanyika Jumapili kuanzia saa Saba mchana hadi saa Kumi na mbili jioni ungewashirikisha Waziri Lukuvi na Mnadhimu wa Kambi ya Upinzani Bwana Tundu Antipasi Lissu.

Katika maelezo yake ya kwanini hatashiriki kwenye mdaharo huo Waziri Lukuvi alidai kuwa hana taarifa kutoka ofisini kwake juu ya mwaliko huo kwasababu alikuwa ziarani mikoani kwa shughuli za kikazi na kwamba anapanga kuelekea Mkoani Iringa leo kama mwendelezo wa ziara zake za Mikoani za kikazi.

-----------------

Katika hali inayosikitisha kabisa mnadhimu mkuu wa serikali bungeni, waziri nchi ofisi ya rais anayeshughulikia Bunge na sera, Mheshimiwa Willium Lukuvi(Mbunge wa Ismani-CCM) ameamua kwa makusudi kabisa kumkwepa na kumkimbia mnadhimu mkuu wa kambi ya Upinzani Bungeni Tundu Lissu(Mbunge wa Singida kusini-CHADEMA) katika mdahalo uliofanyika leo katika ukumbi wa Mlimani city uliokuwa unahusu mwenendo wa bunge katika mswaada wa kuandikwa kwa katiba mpya.
Willium alikataa katakata kuhudhuria licha ya waandaaji kumwalika kwa msisitizo zaidi ya mara mbili.

Tukio hili linatoa ishara mbaya kwa serikali na CCM kuwa inaogopa kupambana na wapinzani hadharani kwa hoja zenye nguvu na mvuto.
Kwa sasa umekuwa ni mtindo wa kawaida kwa viongozi wa CCM kukimbia midahalo na makongamano huru na muhimu ya kisiasa yanayohusisha wapinzani pia.

SOURCE:Nukuu katika Vyombo vya habari vya leo(Redio, magazeti, Runinga na Mitandao)
 
mkuu TECH WIZ hata kama ni mimi nikiitwa kwenye mdahalo halafu nikajua sina hoja, na mtu nitakayefanya naye mdahalo yuko vizuri kweli kweli; lazma niingie mitini. Simlaumu sana lukuvi maana sasa angefanyaje! na wakati akijaribu kuyapima maji; anaona wazi hawezi kuyavuka?
 
Last edited by a moderator:
ha ha ha ha lukuvi na nyumba ya bilioni moja mbezi beach
 
Haa haaa haaa Lukuvi si hua anasema sijui Lissu ni muongo mara ni kichaa sasa iweje aogope kupigwa knock out kwenye mdahalo!!
Hawa viongozi wetu kweli kichwani ni zero zero na mipasho tu.
Napendekeza wangeenda kabsa na Werema
 
mkuu TECH WIZ hata kama ni mimi nikiitwa kwenye mdahalo halafu nikajua sina hoja, na mtu nitakayefanya naye mdahalo yuko vizuri kweli kweli; lazma niingie mitini. Simlaumu sana lukuvi maana sasa angefanyaje! na wakati akijaribu kuyapima maji; anaona wazi hawezi kuyavuka?

Ha ha ha!Wenzie walishajua ratiba yake ya ziara ilikuwa inamalizikia jana Ijumaa na ndio maana Mdaharo ukapangwa ufanyike Jumapili lakini kwakuwa Mkuu alijua ataumbuliwa akaamua kujipangia ziara nyingine ya Iringa lengo likiwa ni kuhalalisha hoja yake ya kukwepa mdaharo na Lissu
 
Last edited by a moderator:
Teh..teh..Lukuvi, Lukuvi...my school mate has nothing to share there, hana agenda yoyote inayoweza kumshinda kamanda Lissu
 
Waziri Lukuvi amekataa kushiriki katika mdaharo ulioandaliwa na asasi moja juu ya kilichojiri Bungeni kuhusiana na mchakato wa Katiba mpya.Mdaharo huo ambao ulipangwa kufanyika Jumapili kuanzia saa Saba mchana hadi saa Kumi na mbili jioni ungewashirikisha Waziri Lukuvi na Mnadhimu wa Kambi ya Upinzani Bwana Tundu Antipasi Lissu.Katika maelezo yake ya kwanini hatashiriki kwenye mdaharo huo Waziri Lukuvi alidai kuwa hana taarifa kutoka ofisini kwake juu ya mwaliko huo kwasababu alikuwa ziarani mikoani kwa shughuli za kikazi na kwamba anapanga kuelekea Mkoani Iringa leo kama mwendelezo wa ziara zake za Mikoani za kikazi.

bora hata ameamua kuachana na mdahalo huo, kwa sababu ukiangalia washirki wengine wa mdahalo huo utagundua kuwa ni wa kupangwa kwa makusudi ili kuishambulia serikali, safi sana, nani ambaye hajui kilichonyuma ya pazia kwa kuwashirkisha watu kama yule mkuu wa SAUT? ambao hamjui nitafuteni kwenye private niwamegee.
 
ningemshangaa kama anagehudhuria.
yaani wewe uambiwe huu mto una mamba alafu na wewe useme ngoja nijaribu kuongelea hawezi kuningata.
Lukuvi nakusihi tena kaa mbali na Lisu atakuvua nguo

Hakuna serikali yoyote duniani inayoandaliwa midahalo na media zenye mwelekeo wa Upinzani, hata mimi ningeshangaa kuona Serikali inaingia mkenge kiasi hicho.
 
Lukuvi hana jipya

Hilo alilolifanya ni la maana sana, na kwa ujumla mission ya wapinzani itakuwa imefeli kwa vile tayari inasemekana mdahalo ungejumuisha mkuu wa SAUT ambaye ni swaiba(schoo mate) mkubwa wa kiongozi wa chama kimoja cha siasa. Good na nadiriki kusema SERIKALI ina intelijensia kali sana.
 
ningemshangaa kama anagehudhuria.
yaani wewe uambiwe huu mto una mamba alafu na wewe useme ngoja nijaribu kuongelea hawezi kuningata.
Lukuvi nakusihi tena kaa mbali na Lisu atakuvua nguo

Viongozi wa serikali ya Ccm wanaingoza hii nchi kama waganga wa kienyeji, hawana hoja za kupambana na hoja, huwa wanapenda speech za upande mmoja, kama walivyo potosha wananchi ITV kuhusu kilicho tokea bungeni, Wasira, Lukuvi na dakika 45 sasa wameona Lissu anakwenda kuwapa ukweli wa kilichotokea bungeni, jamaa kaingi pori, hahahaaaaaa! Ccm bwana! inafurahisha sana
 
Mbona jibu ulikuwa nalalo kuanzia mwanzoni kwa akili yako unafikiri Lukuvi yuko tayari kwenda kukadhalilishwa na Lisu hapana labda mwingine lakini sio lukuvi tunayemfahamu coz hana hoja zaidi ya jazba pia Lukuvi is among the people who are in the list of Kainerubaga msemakweli of shody Diploma and degrees holder.
 
Tofautisha kuandaa na kushiriki,media imeandaa tu lakini washiriki wengine,basi waandae TBC uone kama Lukuvi hukutoka nduki atakimbia tuu.Lisu maji marefu ukiingia tu nyesi linakukaukia kwenye nguo ya ndani
 
Tangu habari hii ilipokuwa wazi mimi nilisema I bet my neck huyo nabii wa uongo William Lukivi hawezi kufanya mdahalo na Tundu Lissu. Hii habari ya kukacha huo mdahalo sio habari. Habari ingekuwa kama Lukuvi ANGEKUBALI kushiriki huo mdahalo dunia nzima ingeshangaa!!.

Tukubari tu Watanzania viongozi wa CCM ni janga la Kitaifa. Just imagine mgombea urais anakwepa mdahalo na bado Watanzania wanamchagua kuwa RAIS. This is ONLY possible in Tanzania. Yaani Uhuru Kenyatta akwepe mdahao na Odinga Wakenya wamchgue kuwa RAIS? Au Barack Obama akwepe mdahalo na Romney wamerakani wamchague kuwa RAIS? Jiulize maswli hayo ukipata majibu yake ndiyo utaona njisi Watanzania tulivyo MAZOBE!

Hongera Lukuvi unatekeleza ILANI ya CCM kwa vitendo. Sitoshangaa akiibukia DK 45 za ITV
 
ha ha ha ha lukuvi na nyumba ya bilioni moja mbezi beach

Kwa kiongozi wa serikali kawaida tu hakuna la kushangaza mkuu, mtumishi wa siku nyingi sana yule, huwezi kumlinganisha na kiongozi tu wa chama cha siasa ambao nao wana nyumba za aina hiyo.
 
Tangu habari hii ilipokuwa wazi mimi nilisema I bet my neck huyo nabii wa uongo William Lukivi hawezi kufanya mdahalo na Tundu Lissu. Hii habari ya kukacha huo mdahalo sio habari. Habari ingekuwa kama Lukuvi ANGEKUBALI kushiriki huo mdahalo dunia nzima ingeshangaa!!.

Tukubari tu Watanzania viongozi wa CCM ni janga la Kitaifa. Just imagine mgombea urais anakwepa mdahalo na bado Watanzania wanamchagua kuwa RAIS. This is ONLY possible in Tanzania. Yaani Uhuru Kenyatta akwepe mdahao na Odinga Wakenya wamchgue kuwa RAIS? Au Barack Obama akwepe mdahalo na Romney wamerakani wamchague kuwa RAIS? Jiulize maswli hayo ukipata majibu yake ndiyo utaona njisi Watanzania tulivyo MAZOBE!

Hongera Lukuvi unatekeleza ILANI ya CCM kwa vitendo. Sitoshangaa akiibukia DK 45 za ITV

Mkuu midahalo ya wenzetu inakuwa so organized na inakuwa imeandaliwa na taasisi ambayo haifungamani na upande wowote, usifananishe midahalo hii na huu upup wa kitanzania ambao kwanza watu wanakaa na kutafuta namna ya kumkaanga mwingine na mnaletewa mtu kama R.K kuongoza mdahalo unategemea nini? mfano mzuri ni huu ambao LUKUVI ameukataa, tayari ilishafamika kuwa miongoni mwa wataohusika moja kwa moja ni mkuu wa SAUT, yule CDM 100% au mtu kama LWAITAMA au KAKOBE wahudhurie mdahalo what do you expect? Tanzania hatuna taasisi za kuandaa midahalo, inabidi kwanza tulione hilo badala ya kukimbilia kuwa mashabiki tu.
 
Hahahaha! Mimi nawalaumu waandaaji wa Mdahalo. Hata siku moja huwezi kumpiganisha bondia wa Heavy weight (Tundu Lissu) vs Feather weight (Lukuvi). Nilijua tu, visingizio lazima vitolewe dakika za mwisho kutoka kwa huyu jamaa yetu wa La saba, Fisadi wa elimu.
 
Mbona jibu ulikuwa nalalo kuanzia mwanzoni kwa akili yako unafikiri Lukuvi yuko tayari kwenda kukadhalilishwa na Lisu hapana labda mwingine lakini sio lukuvi tunayemfahamu coz hana hoja zaidi ya jazba pia Lukuvi is among the people who are in the list of Kainerubaga msemakweli of shody Diploma and degrees holder.

Serikali ilishashtukia midahalo inayoandaliwa na kwa udhamini wa WAPINZANI, halafu hata hivyo kama wana hoja si wangepingana naye bungeni kama siyo ushahidi tosha kuwa wanatumia media vibaya.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom