Waziri mkuu atoa salamu za pole kifo cha William Lukuvi

Waziri mkuu atoa salamu za pole kifo cha William Lukuvi

Habari za Zanzibar

JF-Expert Member
Joined
Dec 18, 2024
Posts
394
Reaction score
277
WAZIRI MKUU ATOA SALAMU ZA POLE KIFO CHA WILLIAM LUKUVI

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mwigulu Lameck Nchemba, akiwa katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano Arusha (PICC) kushiriki Mkutano wa 110 wa Wadau wa Elimu kwa Umma (WASHITIRI) leo Machi 25, 2026, ametoa salamu za pole kufuatia kifo cha aliyekuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu) na Mbunge wa Jimbo la Isimani, William Vangimembe Lukuvi, aliyefariki dunia majira ya saa moja asubuhi.

Taarifa ya kifo hicho imetangazwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, ikieleza kuwa marehemu amefariki katika Hospitali ya Benjamin Mkapa alipokuwa akipatiwa matibabu ya ugonjwa wa mshtuko wa moyo.

Soma Pia:
Mwigulu Nchemba: Niliongea na Lukuvi jana tukapanga kikao
Waziri William Lukuvi (na Mbunge wa Isimani) afariki Dunia


Rais Dkt. Samia ametuma salamu za pole kwa Spika wa Bunge, familia ya marehemu, wananchi wa Jimbo la Isimani pamoja na Watanzania wote kufuatia msiba huo mkubwa wa kitaifa.

IMG-20260325-WA0122.jpg
Screenshot_20260325_175647_Facebook.jpg
 
Kila anayekufa utasikia jana nimeongea nae alikuwa mzima wa afya 🙄🙄🙄hili bunge kama hawata jiuzul wataisha wote
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom