Ludovick Joseph: Kilio cha usaliti - Sehemu ya pili

Mimi naona hoja za Mwampamba zina mashiko sana, na kwa wale vijana na watu wanaoona Mwampamba anatapata hapa wamelamba galasa. Mtela kabadirika sana kwa sasa anakuja na hoja za maana zinazoamsha fikra na mawazo ya vijana kujitambua. Kuna thread iliwahi kuletwa humu kwamba Mtela Mwampamba na Juliana Shonza ni watu hatari sana kwa ustawi wa Chadema watu watu wakachukulia mzaha.

Complicator,zingekuwa na mshiko pale tu angeyaeleza haya kabla haijatoka Youtube wala na yeye hajahama huko CHADEMA ,vinginevyo uwepo wake huko alikotoka ulikuwa siyo wa heri.Na kama anaweza kuwatukana waliokuwa viongozi wake huko alikotoka basi kuna uhakika hata huku aliko hawana imani naye.

Iangalie kwa namna hii,uko kwenye Interview,unauliza swali,meneja wako au supervisor wako yukoje huko uliko,au uliwahi kuwa na supervisor mkawa na ugomvi naye katika maisha yako ya uajiri?Unaanza kutoa matusi,kashfa na siri za ofisi uliyotoka,rafiki na uhakika hata kama unaqualification kubwa na wanazozihitaji hawatakuchukua kamwe,sababu wameshakujua wewe ni nani na hauwafai.Hivyo Mtela ajiangalie huko aliko.
 
watakanusha nini wakati kilichoelezwa na mwampamba ni facts. Ndiyo maana tunasema kuwa ukitaka kuachana achaneni kwa heri maana mkiachana kwa kashfa ziri zenu zote zitakuwa hadharani.
Fact ipi ya nani kamkana nani ni fact ndio maana nyie na mwenyekiti wenu wa CCM mumekosa maono utasikia mwenyekiti wa CCM ana simama kutukana serikali ya CCM ambayo raisi wake ni Kikwete ,utasikia mabilioni yameibwa na serikali ya kikwete eti wanamuasa aache duh hata walimu wa propaganda hawapo
 
Mtela Mwampamba. Endelea kurutubisha akili zisizofunguka. Wanaokwambia unapoteza heshima yako wanakudanganya, maneno yako yana nguvu ya risasi. Kila napoitazama cdm, naona inayumba, inazama. Usikate tamaa matusi yao ni yaleyale -umenunuliwa, utaolewa, njaa kali. Maneno yote hayo tumeyazoea, hawana hoja.
 
Mbona SLAA na MBOWE hawajitokezi kujibu hizi tuhuma, jamani ama ndo tuseme wameamua kukubali yaishe.
 
Mdogo wangu, nakuomba kafanye kazi nyingine maana siasa haikufai. Watakuja kukutema kama chupi ya malaya baada ya kufanikisha kazi zao, utakuwa huna mahali pa kuficha uso wako.....ushauri tu
 
ccm iwe makini na huyu mtu kwa kutomshirikisha siri za chama la sivyo atakuja kuzimwanga chaumma 2017. Huyu siye mwanaume kamili ila suruali. Nawatahadharisha na mabinti, ukiwa na mchumba kama huyu jamaa, siku mkiaachana basi utakuta picha zako kwenye mtandao au magazeti ya udaku. Hufaai kuaminiwa kabisa. Mambo mengi hayasemwi na wanaume hadharani kama unavyofanya. Usifikiri ccm wanawaona wa maana sana zaidi munapopayukapuka majukwaani na mwezio shonza, katu hawatawaamini kabisa katika uongozi wake.

kwa maelezo yako unatuthibitishia kuwa aliyosema mwampamba kuhusu mikakati ya chadema na mbinu zao chafu na usaliti wao ni sahihi kabisa. Isipokuwa unawatahadhalisha ccm wawe waangalifu na mwampamba ili wasimweleze kila kitu ili ikitokea amehama ccm wasivuliwe nguo kama wanavyovuliwa sasa cdm
 
Naomba uwabainishie Umma wa wanaJF kuwa lipi katika niliyoyaandika hapo juu si sahihi kuhusiana na DEUS na kukanwa kwake na watu hao. Na kwa bahati nzuri hatukuwa tunafanya mazungumzo ya mdomo pekee, ninazo meseji za simu na hata kauli za Mallya kwenye inbox yangu ya facebook yanaeleza haya niliyoyaeleza hapa.

Naomba kabla haujachelewa na kuonekana ni miongoni mwa wenye ukame wa fikra, njoo hata kwa kutunga uongo wako ubainishe ni kipi si sahihi ama ni uongo katika hayo niliyoyaandika.

wewe tueleze kwanza baba yako halisi ni yupi.unajua kuwa sio huyu mze mwampamba,alibebeshwa zigo tuu.come clean on this first before attaking others
 
Leo naona uandishi wake umenyooka kidgo, nahisi amepewa coaching na King maker wa Masalia.....
 
Mtela Mwampamba. Endelea kurutubisha akili zisizofunguka. Wanaokwambia unapoteza heshima yako wanakudanganya, maneno yako yana nguvu ya risasi. Kila napoitazama cdm, naona inayumba, inazama. Usikate tamaa matusi yao ni yaleyale -umenunuliwa, utaolewa, njaa kali. Maneno yote hayo tumeyazoea, hawana hoja.

ndoto za mchana kweupe sera za majimbo ya kichama CDM na M4C kiboko cha ajuza CCM concept imemswaga ajuza CCM mwenyekiti amebaki anafungua hata viunga vya umwagiliaji maua ili aonekane dah
 
kwa maelezo yako unatuthibitishia kuwa aliyosema mwampamba kuhusu mikakati ya chadema na mbinu zao chafu na usaliti wao ni sahihi kabisa. Isipokuwa unawatahadhalisha ccm wawe waangalifu na mwampamba ili wasimweleze kila kitu ili ikitokea amehama ccm wasivuliwe nguo kama wanavyovuliwa sasa cdm

ukweli ni kwamba propagandist wa CCM ni marehemu hatushangai mwenyekiti wao GPA 2.0 rekodi yake haijawahi kuvunjwa na mwanafunzi yeyote katika historia ya chuo kikuu cha Dar es -salaam,katibu mwenezi form four siasa d- kiswahili d dvision four ya 29 ha ha kila linaloanzishwa linabuma na kuipaisha CDM asilimia 1000
 
nafikiri CDM mngemjibu kwa hoja sio kujibu kama mpo chooni mmeshateleza hiyo imekula kwenu


Huyu inaonekana ana tamaa za kuzidi. Tutafuatilia habari zake huko alikozaliwa inaonekana ni msaliti wa kuzidi, hata baba yake anaweza kumsaliti kwa vijisenti vya sisiem. Yuda iskariot
 
Angalia movie ya Jet Li "The bodyguard" na sehemu nyingine wanaiita "the defender". Kuna sehemu alimwekea Boss wake mguu wa kuku "handgun" au "pistol" baada ya kuona adui anataka kumdhulu boss wake, kilichofata ni yule adui kufikiri kwamba jet li ni mwenzako hivyo akaacha jet li amalize kumbe ile ilikuwa adaa na akageuziwa kibao. Hiyo sehemu ilituma kufundishia na jet li aliulizwa kwanini akasema wakati mwingine inabidi utishie kuua unayemlinda kuzubaisha maadui.
Mheshimiwa utalalama kwamba wamesalitiwa bila kujua kinachoendelea. Ludovick kama ilivyozamani Deus yuko mikononi mwa dola sasa kama kuna ulazima wa kuonyesha wanajuana na akina silaa iache serikali idhibitishe. Kesi si sherehe is about proving every detail
 
Tatizo lililopo wengi wetu tumelewa propaganda za CDM inafika wakati hata jambo la maslahi linapo kuja ambalo lina pingana /linaenda kinyume na CDC tunaliona halina maana namleta jambo hilo tunamuona kilaza.

Sasa hili nalo lina maslahi gani?
Hi linasaidia watoto wetu kufaulu hili?
Litasaaidia kupunguza au kumaliza ufisadi hili?
Litasaidia kupunguza makali ya maisha hili?
Litasahidia kuboreka kwa huduma za afya?
Je litasaidia huduma za umeme na mají nchi hii?
 
nafikiri CDM mngemjibu kwa hoja sio kujibu kama mpo chooni mmeshateleza hiyo imekula kwenu
Binafsi napenda kuona posts zenye mashiko ya 'kukubali' au 'kukanusha' tena kwa hoja, kushambuliana pasipo hoja ni kupoteza muelekeo wa kujadiliana.
 
Mbona SLAA na MBOWE hawajitokezi kujibu hizi tuhuma, jamani ama ndo tuseme wameamua kukubali yaishe.

Mtu ye yote mwenye busara na akili timamu hawezi kubishana na mjinga vinginevyo hadhira haitaweza kutofautisha kati ya MTELA na SLAA. SLAA & MBOWE na viongozi wote wa CDM endeleeni na kuongoza mapambano na msijibishane na hawa waganga njaa.
 
Ulikuwa wapi siku zote usiseme hii pumba yako leo ndiyo umeona uje useme huu mpasho wako au? Nakushauri kijana, kama umeshapata hela ya hao walioku2ma ingia mitini kama hujapata kitu ndiyo maana una magadhabu na CDM, hii imekula kwako
 
Back
Top Bottom