Ludovick Joseph: Kilio cha usaliti - Sehemu ya pili | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ludovick Joseph: Kilio cha usaliti - Sehemu ya pili

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mtela Mwampamba, Mar 20, 2013.

 1. M

  Mtela Mwampamba Verified User

  #1
  Mar 20, 2013
  Joined: Dec 19, 2012
  Messages: 537
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Wakati mwingine tunajikuta tunalazimika kuyasema hata yale ambayo hatukupanga wala kufikiria kuyasema.,nimekuwa nikipigiwa simu na ndugu zangu na rafiki zangu ambao bado wako chadema wakiniuliza kwanini nimeamua kuyasema ninayoyasema, tena kwa lugha kama hii (inayobainisha), nami nimekuwa nikiwajibu kuwa "hivi haiwi faraja kwenu kuwa yupo mmoja aliyewahi kuwa mfano wenu anayetaka kuwaokoa na hatari yenye kuangamiza..?

  Nadhani wengi katika wao wamenielewa lakini nitazidi kuwaeleweshaa wale ambao bado wanaubutu na kutu imejaa katika fikra na mitazamo yao.Nimeeleza juu ya kukanwa na usaliti uliofanywa kwa LuDOVICK na nikaishia hapo, nikidhani kuwa itakuwa imetosha kuwafungua mawazo na kuwasaidia vigezo na vipambanuzi vya kuwawezesha kufanya maamuzi sahihi, maamuzi huru ambayo yatatokana na fikra zinazojitawala za kila mmoja katika upekee wake, si fikra za mkumbo (mob psychology) wala si fikra mgando na zilizosinyaa (dormant and dead reasoning), lakini nitawaongeza na hili la leo kuyaamsha mawazo hayo yaliyoganda na kuwafanya muishi kwa Uhai wa fikra Huru.Napenda nianze kwa kuwaambia kuwa si mara ya kwanza kwa viongozi wa Chadema kuwakana wapambanaji wao na vijana waliokuwa wanajitolea hali na mali, wanajitolea nafsi na uhai kuipigania Chadema.

  Nitawaambieni juu ya wachache waliowahi kusalitiwa na kukanwa hadharani na vongozi waandamizi wa chadema kama ifuatavyo:-

  i) DEUS MALLYA:Kwa mara ya kwanza nakutana na DEUS ilikuwa ni mwaka 2007, nikiwa nimejiunga na chuo kikuu cha Dar es salaam, ambapo nilishakuwa mwanachadema kabla ya kuingia Chuo Kikuu, hivyo nilipofika chuo nilijaribu na kufanikiwa kukutana na vijana wapambanaji wa Chadema hasa wale waliokuwa wanatumikia Makao Makuu ndipo nilipokutana na DEUS MALLYA ambae alikuwa akitumika katika kuchapisha mabango na vipeperushi ambavyo vilikuwa vinabeba ujumbe wa Chadema na falsafa mbalimbali za Ukombozi ambazo chadema ilikuwa ikinajinasbisha nazo.

  Nilipokutana na DEUS tulipanga na kupeana ushauri wa jinsi ya kueneza na kusambaza vipeperushi hivyo na hatimae aliniunganisha na JOHN MNYIKA ambae kwa kipindi hicho alikuwa ni Mkurugenzi wa Vijana na Afisa wake akiwa Marehemu Regia Mtema, ambapo DEUS alikuwa ni mtu wa karibu na maafisa hao, hasa MNYIKA.Na walikuwa pamoja na kufanya mambo mengi, ninayoyakumbuka ni pamoja na;

  a) Safari ya DEUS mallya kuelekea LIBYA katika kongamano la vijana akiwa muwakilishi wa vijanakutoka chadema chini ya usimamizi wa Mnyika.
  b) Safari ya RUSSIA ambapo DEUS alinieleza kuwa alienda kwa mafunzo maalum.Lakini Mnamo mwezi wa tisa (9) mwaka 2008, baada ya kutokea kwa kifo cha kutetanisha cha Mheshimiwa CHACHA WANGWE ambapo DEUS alikuwa ni Dereva na mshukiwa wa kwanza katika ajali ile.

  JOHN MNYIKA alimkana DEUS mara mbili; mara ya kwanza ni pale apohojiwa na maafisa wa polisi juu ya kijana DEUS akamkana, na mara ya pili alipokutana na vyombo vya habari kuzungumzia sakata hilo akamkana kwa mara ya pili.

  Hata baada ya kesi ya DEUS kumalizika na kisha DEUS kuachiwa huru, nilizungumza na DEUS juu ya kukanwa na MNYIKA na DEUS alinijibu kuwa mshikaji alimuomba radhi na kumtaka asahau yaliyopita na DEUS alikiri kumsamehe na imebaki hivyo mpaka hivi sasa (hili anaweza kulithibitisha DEUS MALLYA mwenyewe kwakuwa yu-hai).

  Lakini haikuishia kwa MNYIKA pekee bali hata BENSON KIGAILA ambae ni Mkurugenzi wa Oganaizesheni na Mafunzo aliwahi kumkana na anaendelea kumkana mpaka leo hii, kiasi kwamba DEUS akienda pale Makao Makuu na akikutana na BENSON huwa anamuambia kuwa asiwe anakuja Makao Makuu maana Chama kitachfuka kwa kuonekana MALLYA pale.

  Ni mtu ambae hafikiri sawasawa tu ndie atakayeweza kusema USALITI huu hauna asili ya ndani na kuwa ni hulka za viongozi wakuu wa Chadema kuendelea asili yao hiyo.

  ANGALIZO:

  Nitasema kama nilivyokutangulia kusema hapo awali juu ya hatma ya vijana ndani ya chadema, na leo nitasema hivi;IKIWA HII MITI MIBICHI INATENDEWA HIVI., JE NINYI MITI MIKAVU MTATENDEWA VIPI..? ambao hata makao makuu ya Chama hamyajui wala hakuna anayewajua zaidi ya kuwatumia kwenye maandamano na mikakati yao.


  =====================
  MAJIBU YA J. J. MNYIKA
  =====================

   
 2. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #2
  Mar 20, 2013
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,109
  Likes Received: 323
  Trophy Points: 160
  Nimeamini adui mwombee njaa

  Unachofanya ww hapa ni nini? Hivi CDM haijawahi kukuweka mjini wewe??

  Anyway, mwageni ugali na mboga tupate info za kuchuja 2015.
   
 3. Mikael P Aweda

  Mikael P Aweda JF Gold Member

  #3
  Mar 20, 2013
  Joined: Dec 17, 2010
  Messages: 2,934
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Mkuu, nimekusoma lakini unapotosha kwa makusudi mwanzo mwisho, hakuna ukweli. Hata kama unapiga proganda kwa niaba ya ya ccm hii imezidi. Na hii haitawasaidia ccm 2015.
   
 4. T

  Tabby JF-Expert Member

  #4
  Mar 20, 2013
  Joined: Jan 8, 2008
  Messages: 10,157
  Likes Received: 6,093
  Trophy Points: 280
  So what?? Ninaona dalili za dissatisfaction. Ulidhani umeamua sahihi na sasa unaweze kuona namna gani ulivyokosea na ndiyo maana huna settled mind. Kwa sasa hutaweza tena. Tafuta namna nyingine ya kuwa busy na utulivu wa mawazo.
   
 5. F

  FJM JF-Expert Member

  #5
  Mar 20, 2013
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 145
  Ni lini Deus Mallya au Ludovick wamesema kuwa wamesalitiwa na CHADEMA? Huyu mleta uzi ni msemaji wa nani?
   
 6. Amoeba

  Amoeba JF-Expert Member

  #6
  Mar 20, 2013
  Joined: Aug 20, 2009
  Messages: 3,328
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 0
  Hapa ulikuwa unaongelea nini? Haueleweki nia na malengo yako!
   
 7. Mashamba

  Mashamba JF-Expert Member

  #7
  Mar 20, 2013
  Joined: Sep 1, 2011
  Messages: 416
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Maji taka na wivu wa kike,ushakula talaka tatu CDM endelea ku2mika kwa bwn ako mpya,kabla ya kukata pumzi ya mwisho kisiasa ndipo uje nikupe shule ya kata maeneo ya Laela pale ufundishe na kulima mahnd.
   
 8. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #8
  Mar 20, 2013
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,109
  Likes Received: 323
  Trophy Points: 160
  Kwa hiyo wangwe? CDM? Aisee
  Hii muvi hii kali sana.
   
 9. Alinda

  Alinda Platinum Member

  #9
  Mar 20, 2013
  Joined: Jun 26, 2008
  Messages: 1,543
  Likes Received: 226
  Trophy Points: 160
  Mambo ya kusalitiana kwenye siasi naona ni mambo ya kawaida Zitto aliwahi kumsaliti Ben saa8, Rais Kikwete aliwahi kuisaliti Downs na nk.
   
 10. M

  Mkeshaji JF-Expert Member

  #10
  Mar 20, 2013
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 4,264
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Peleka ushahidi wako Polisi badala ya kukesha kwenye mitandao ya kijamii.
   
 11. Complicator EM

  Complicator EM Senior Member

  #11
  Mar 20, 2013
  Joined: Dec 20, 2011
  Messages: 155
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mimi naona hoja za Mwampamba zina mashiko sana, na kwa wale vijana na watu wanaoona Mwampamba anatapata hapa wamelamba galasa. Mtela kabadirika sana kwa sasa anakuja na hoja za maana zinazoamsha fikra na mawazo ya vijana kujitambua. Kuna thread iliwahi kuletwa humu kwamba Mtela Mwampamba na Juliana Shonza ni watu hatari sana kwa ustawi wa Chadema watu watu wakachukulia mzaha.
   
 12. Lizaboni

  Lizaboni JF-Expert Member

  #12
  Mar 20, 2013
  Joined: Feb 21, 2013
  Messages: 33,793
  Likes Received: 13,797
  Trophy Points: 280
  Mkuu watakutana sana lakini usichoke mwishowe watanyamaza na hakika watanzania tutakuwa tumefunguka na kujua hasa malengo ya CHADEMA katika msatakabali wa taifa letu.
   
 13. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #13
  Mar 20, 2013
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,109
  Likes Received: 323
  Trophy Points: 160
  Ujue wapiga kura na sie tuko hapa kwa karibu tunapembua pumba na mchele??

  Msi-underestimate kivileee, wanasema viongozi wengi huuawa na walinzi wao walioamua kuasi.

   
 14. M

  Mtela Mwampamba Verified User

  #14
  Mar 20, 2013
  Joined: Dec 19, 2012
  Messages: 537
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Naomba uwabainishie Umma wa wanaJF kuwa lipi katika niliyoyaandika hapo juu si sahihi kuhusiana na DEUS na kukanwa kwake na watu hao. Na kwa bahati nzuri hatukuwa tunafanya mazungumzo ya mdomo pekee, ninazo meseji za simu na hata kauli za Mallya kwenye inbox yangu ya facebook yanaeleza haya niliyoyaeleza hapa.

  Naomba kabla haujachelewa na kuonekana ni miongoni mwa wenye ukame wa fikra, njoo hata kwa kutunga uongo wako ubainishe ni kipi si sahihi ama ni uongo katika hayo niliyoyaandika.
   
 15. SOTI

  SOTI Member

  #15
  Mar 20, 2013
  Joined: Sep 9, 2011
  Messages: 80
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 15
  Ganzi ninayekujua leo hii na wewe unakesha kwenye mitandao wakati tunasoma chuo hata gazeti kwako ilikuwa msamiati! Anayejua maana ya neno ganzi hawezi kukushangaa pengine umeshavuta! Eti nawewe kesho tusikie umepewa UDC.
   
 16. Alinda

  Alinda Platinum Member

  #16
  Mar 20, 2013
  Joined: Jun 26, 2008
  Messages: 1,543
  Likes Received: 226
  Trophy Points: 160
  Sasa katika mada hii mshiko huko wapi? mna wapa kichwa bure! halafu akiweka topic anasepa si angekuwa anabaki kujibu maswala ya wadau kama wafanyavyo vijana wenzake! yeye ni kusepa tu hizo 5m alizolipwa zitamtokea puani!
   
 17. Lizaboni

  Lizaboni JF-Expert Member

  #17
  Mar 20, 2013
  Joined: Feb 21, 2013
  Messages: 33,793
  Likes Received: 13,797
  Trophy Points: 280
  Afadhali Mtela anaelezea facts tupu, CHADEMA wanakesha kwa majungu tu humu JF. Mwacheni kijana afunguke halafu tutamkaribisha SHONZA naye afunguke ili taifa liendelee kutawalika na amani yetu idumu.
   
 18. Gwalihenzi

  Gwalihenzi JF-Expert Member

  #18
  Mar 20, 2013
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 5,118
  Likes Received: 52
  Trophy Points: 145
  Mtela, unapoteza heshima yako na ya vijana wenzio hapa Tanzania! nadhani hata hao CCM si muda mrefu watakuchoka na kukutupa jalalani. Panga mikakati yenye manufaa kisiasa kwako na kwa taifa, acha kupanga mikakati ya hila kama hii. Wewe bado ni kijana utachokwa sio muda mrefu.
   
 19. AshaDii

  AshaDii Platinum Member

  #19
  Mar 20, 2013
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 16,247
  Likes Received: 300
  Trophy Points: 180
  Mtela Mwampamba... Kusema kweli haijalishi kama haya ni kweli ama ni uongo. Inachojalisha ni kuwa wewe ndiye umeyatoa, baada ya kuwa mwana CCM baada ya kushindikana kuwa mwana CDM. Kwamba siku zote uliona sawa kumezea na sasa ndiyo wakati wa kuyaanika?

  Kwa mwananchi yeyote atakae kuwa anatumia habari hizi ama Siasa za gutter politics zinazotumika kama kigezo pekee cha kuki judge Chadema atakuwa bado ni mchanga katika kutambua vigezo vya kuchagua chama na ni dalili ya kuwa ndiyo wale washabiki hata kura siku ya mwisho hapigi!

  Hakuna Chama kisicho na madhaifu, kama ilivyo Chadema na madhaifu yake... Ila hii nguvu na devotion yenu juu ya Chadema na Viongozi wake inatupa walakini wa nia yenu huku ikitoa picha ya woga mkubwa mlio nao juu ya Chama na viongozi wa Chadema.

  Kinachosikitisha zaidi ni kuwa inafanywa na vijana ambao wanawaza kuwa tegemezi katika taifa kwa kuwawakilisha wananchi ipasavyo badala ya kukesha kila siku kwa kuwaza namna ya uharibifu na uteketezi wa chama kingine! Punguzeni selfshness jamani... Mfikirie na m'Tanzania wa kawaida anaye hitaji ukombozi toka hali mbaya tuliopo sasa!
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 20. s

  security guard JF-Expert Member

  #20
  Mar 20, 2013
  Joined: Sep 27, 2011
  Messages: 706
  Likes Received: 259
  Trophy Points: 80
  nafikiri CDM mngemjibu kwa hoja sio kujibu kama mpo chooni mmeshateleza hiyo imekula kwenu
   
Loading...