Lucy Mahenga: Huduma katika Hospitali Kuu ya Mkoa wa Dodoma sio ya kuridhisha

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,877
6,326
Mbunge wa Viti Maalum, Lucy Mahenga, amesema huduma katika Hospitali Kuu ya Mkoa wa Dodoma sionza kuridhisha, vitu vingi vina kasoro na wananchi wamekuwa wakilalamika.

Akiwa Bungeni amesema, "Hospitali imekuwa ikihudumia Wagonjwa wengi sana, hasa kutokana na kwamba idadi kubwa ya Wananchi wamehamia hapa Dodoma. Ultrasound haifanyi kazi kwa muda mrefu".
 
Ngoja nicheke kwanza
Kuna hospital ya taifa ya magonjwa ya akili mashine za clinical chemistry hazifanyi kazi ni miaka sasa lakini unasikia bungeni tumetenga milions kwa ajili ya mahospital unawasikiliza tu unasema hawa wanasiasa hawaaaa ayiiii.
 
Msitusumbue bana kama hazifanyi kazi kuna kujifukizisha na nyungu🤸🤣🐒
 
Hali ni mbaya hospital nyingi sana hali ni mbaya dawa hakuna !!! Wakati wa mwndazake walificha matatizo haya ili kumfurahisha
 
Hospitali za serikali karibia zote huduma zao sio za kuridhisha na mazingira machafu
 
Back
Top Bottom