Hospitali ya Benjamin Mkapa yaikosha kamati ya bunge kwa ubora wa huduma

Wizara ya Afya Tanzania

Official Account
Oct 1, 2020
58
124
Na. WAF, Dodoma
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Afya na Maswala ya UKIMWI imeipongeza menejimenti na uongozi wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Benjamin Mkapa kwa ubora wa Huduma na kuwatia moyo kwa kuendelea kuwahudumia wananchi .

Kauli hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Afya na Maswala ya UKIMWI, Mhe. Stansilaus Nyongo baada ya kupokea taarifa ya Huduma za kibingwa na bingwa bobezi zinazotolewa katika Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Benjamin Mkapa iliyopo Jijini Dodoma.

Mhe. Nyongo amesema kuwa Hospitali hiyo imekuwa ya mfano katika utoaji wa Huduma bora na usafi wa mazingira na kuleta ufanisi sahihi wa uwekezaji mkubwa ulofanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Sluhu Hassan.

“Hongereni kwa kazi nzuri mnayofanya ya kuwahudumia watanzania lakini pia Mkurugenzi husisite kutuma kutuma vijana wako kuendelea kujifunza ili Tanzania tuzidi kuwa kivutio cha tiba Utalii Afrika mashariki na Afrika nzima kwa ujumla”, Amesema Mhe. Nyongo.

Vile vile ametoa wito kwa uongozi huo kwendelea kuwa wabunifu katika kuongeza mapato ya hospitali hiyo ili kujiimarisha zaidi kiuchumi na kuacha kuwa tegemezi kwa serikali kuu.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Benjamin Mkapa, Dkt. Alphonce Chandika ameishukuru serikali chini ya uongozi imara wa Rais Samia Suluhu Hassan kwa uwekezaji mkubwa alioufanya katika Hospitali hiyo hususani katika vifaa tiba na vitendanishi, kusomesha wataalamu na upatikanaji wa dawa kwa wakati.
 
Dodoma walipora singida hospitali na ofisi ya kanda ya kati ya madini. Kiujumla Dodoma si katikati ya Nchi, uporaji ulianzia hapo. Singida imeporwa vingi sana na Dodoma. Cha Ajabu mpaka hivi Leo sababu hazijulikani.
 
Mjitahidi kuboresha huduma katika sekta ya afya. Msiwe wapiga makofi tuhh.
 
Dodoma walipora singida hospitali na ofisi ya kanda ya kati ya madini. Kiujumla Dodoma si katikati ya Nchi, uporaji ulianzia hapo. Singida imeporwa vingi sana na Dodoma. Cha Ajabu mpaka hivi Leo sababu hazijulikani.
Mkuu yote hii ni Tanzania usiwe 😾, welldone Kwa hospital 🏥 hii na pls m keep the standards zenu, na pia ninaomba mjitahidi kununua ambulances kwa wingi na zenye ubora, wafunzeni kwa ubora paramedics watakaofanya kazi kwenye ambulances hizi, yes hata ikibidi muwe na air ambulances, welldone guy's
 
Na. WAF, Dodoma
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Afya na Maswala ya UKIMWI imeipongeza menejimenti na uongozi wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Benjamin Mkapa kwa ubora wa Huduma na kuwatia moyo kwa kuendelea kuwahudumia wananchi .

Kauli hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Afya na Maswala ya UKIMWI, Mhe. Stansilaus Nyongo baada ya kupokea taarifa ya Huduma za kibingwa na bingwa bobezi zinazotolewa katika Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Benjamin Mkapa iliyopo Jijini Dodoma.

Mhe. Nyongo amesema kuwa Hospitali hiyo imekuwa ya mfano katika utoaji wa Huduma bora na usafi wa mazingira na kuleta ufanisi sahihi wa uwekezaji mkubwa ulofanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Sluhu Hassan.

“Hongereni kwa kazi nzuri mnayofanya ya kuwahudumia watanzania lakini pia Mkurugenzi husisite kutuma kutuma vijana wako kuendelea kujifunza ili Tanzania tuzidi kuwa kivutio cha tiba Utalii Afrika mashariki na Afrika nzima kwa ujumla”, Amesema Mhe. Nyongo.

Vile vile ametoa wito kwa uongozi huo kwendelea kuwa wabunifu katika kuongeza mapato ya hospitali hiyo ili kujiimarisha zaidi kiuchumi na kuacha kuwa tegemezi kwa serikali kuu.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Benjamin Mkapa, Dkt. Alphonce Chandika ameishukuru serikali chini ya uongozi imara wa Rais Samia Suluhu Hassan kwa uwekezaji mkubwa alioufanya katika Hospitali hiyo hususani katika vifaa tiba na vitendanishi, kusomesha wataalamu na upatikanaji wa dawa kwa wakati.
Hospitali zote za Tz ziboreshwe kama hiyo ya Benjamin. Mtakuwa mmewatendea haki sawa watanzania
 
Back
Top Bottom