Kinondoni Hospital na Madaktari Bingwa wa India kushirikiana kutoa huduma kwa Wagonjwa wa Saratani

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,812
11,988
Kinondoni Hospital imetangaza programu ya siku mbali kuwa itashirikiana na wataalamu kutoka Hospitali ya HCG ya nchini India katika kutoa huduma za kitaalamu kwa wagonjwa wa Saratani.

Akizungumzia programu hiyo leo Oktoba 3, 2023 Kinondoni Jijini Dar es Salaam, Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Kinondoni, Dkt. Charles Basir Kafaiya amesema hospitali hiyo kwa kushirikiana na Madaktari Bingwa kutoka Hospitali ya HCG wanatarajia kuanza programu ambayo itawawezesha watu ambao tayari wamegundulika na saratani pamoja na wale wenye viashiria vya ugonjwa huo.

photo_2023-10-03_18-05-49.jpg
"Tunatambulisha Programu yetu ambayo tunatarajia kuianza tarehe 13-14, 2023, tarehe 13 tunatarajia kuanza program kuanzia saa nne asubuhi hadi saa 11 jioni lakini tarehe 14 tutaanza saa tatu asubuhi mpaka saa nane mchana," amesema Dkt. Charles.

Ameongeza kuwa "Program hii ni ushirikiano baina ya Hospitali ya Kinondoni kupitia wataalamu wetu na wataalamu kutoka Hospitali ya HCG na hawa ni wataalamu wa Ugonjwa wa Saratani."

Aidha, amefafanua kuhusu program hiyo inalenga kuwagusa watu gani "Walengwa katika program hii ni wagonjwa wote ambao wameshagundulika kuwa na Saratani na wale wagonjwa ambao wana viashiria vya Saratani."

Akitolea mfano wa aina za Saratani ambazo wamejiandaa kuzitolea huduma amesema kuwa ni pamoja na saratani ya titi, ini, tezi dume pamoja Saratani tumbo, damu.
photo_2023-10-03_18-05-40.jpg
Ameeleza sababu za kushirikiana na wadau hao kutoa huduma hizo kupitia programu hiyo, ameeleza Hospitali Kinondoni imekuwa na takwimu za kupokea wagonjwa wa Saratani hasa ambao wameshafikia kwenye hali mbaya zaidi, amesema kwa kulibaini hilo wameona kuna umuhimu wa kulipa uzito suala hilo.

"Sababu ya kuanzisha hii program ni kwamba katika hospitali yetu tunapokea wagonjwa wengi wakiwa kwenye 'stage' za kansa ambazo zipo juu zaidi, hivyo hata matibabu yake yanakuwa changamoto, ili kuendelea kutoa huduma bora tumeamua kuwasogezea hizi huduma ambazo zamani watu walikuwa wakizifuata nje ya Nchi," amesema Dkt. Charles.

Amefafanua milango itakuwa wazi kwa Watanzania wote huku akibainisha kutakuwepo na gharama kidogo tofauti na ilivyozoeleka.
photo_2023-10-03_18-05-43.jpg
Amesema kwa siku za zamani wagonjwa wengi wa saratani kwenye huduma zitakazotolewa walikuwa wakilazimika kuzifata kwenye mataifa ya nje tena kwa gharama kubwa zaidi.

Naye, Mwakilishi wa Hospitali ya HCG ambayo ujishughulisha na huduma za kansa amesema kuwa hospitali yao ina madaktari bingwa wengi wa ugonjwa wa Saratani, hivyo imeona hupo umuhimu wa kushirikiana na Tanzania katika kusaidia wagonjwa wa Saratani walioko nchini.

Pia amewataka wagonjwa wa changamoto hiyo kujitokeza kwa siku zilizobainishwa hili kupatiwa huduma.

Itakumbukuwa wagonjwa wa Saratani wamekuwa wakitajwa kuongezeka nchini licha ya Serikali kuendelea kuweka jitihada mbalimbali kupambana na ugonjwa huo ambao unatajwa kuwa chanzo cha vifo vingi, Serikali imekuwa ikinunua mashine za kisasa pamoja na kuleta wataalamu mbalimbali ili kupambana na ugonjwa huo.

Katika mkakati wa Kitaifa kupambana na ugonjwa huo Mwaka 2019 Serikali kupitia Waziri wa Afya Ummy Mwalimu alizindua muongozo wa taifa wa tiba ya saratani.
 
Back
Top Bottom