Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 1,898
- 942
UTOAJI WA HUDUMA ZA AFYA UMEZINDULIWA KWENYE HOSPITAL KUU YA MUSOMA VIJIJINI
Leo, Jumanne, tarehe 9.8.2023, Mkuu wa Wilaya wa Musoma (DC), Dkt Khalifan Haule amezindua utoaji wa Huduma mbalimbali za Afya kwenye Hospitali ya Halmashauri yetu ya Wilaya ya Musoma (Musoma DC)
Hospitali imejengwa katikati ya Halmashauri yetu, kwenye Kitongoji cha Kwikonero, Kijiji cha Suguti, Kata ya Suguti.
Hospitali hii yenye kutoa huduma za Afya kwa kiwango cha hadhi ya Hospitali ya Wilaya, hadi sasa Serikali imeishatoa Tsh bilioni 3.49 kwa ajili ya ujenzi, na Tsh milioni 600 kwa ajili ya ununuzi wa vifaa tiba na dawa.
Majengo muhimu tisa (9) yamekamilika, na majengo mengine sita (6) yanaendelea kujengwa likiwemo jengo la kufulia (laundry)
Hospitali ina vifaa vya kisasa, vikimemo: Digital X-ray, Ultrasound na Mitambo ya kutengeneza Oxygen ambayo inapelekwa sehemu ya matibabu kupitia mtandao wa paipu.
Mitungi ya Oxygen ipo ikiwa ni kwa matumizi ya dharura au kusaidia mahitaji ya hospitali nyingine, vituo vya afya na zahanati.
Viongozi mbalimbali wa Chama na Serikali wamehudhuria uzinduzi huo. Chama kiliongozwa na Mwenyekiti wa Chama cha CCM Wilaya ya Musoma Vijijini, Ndugu Denis Ekwabi. Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini, Prof Sospeter Muhongo alishiriki kwenye uzinduzi huo.
Tafadhali sikiliza CLIP/VIDEO iliyoambatanishwa hapa kutoka kwenye tukio la uzinduzi wa huduma za Afya kwenye Hospitali kuu ya Musoma Vijijini.
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini
www.musomavijijini.or.tz
Tarehe:
Jumanne, 9.8.2023