Isijekuwa mbio za panya..... kwa uzoefu wangu, wapinzani baada ya uchaguzi na matokeo kutangazwa huwa hawaridhishwi na kupinga vikali, lakini mwisho wa siku huishia kuwa wapole. Swali: Mmejipanga vipi kusimamja malalamiko ya kudai kitu ambacho mtakuwa mkikikidai kuwa ni haki ambayo kwa wakati huo baada ya uchaguzi? Je, Endapo matokeo hamtayakubali, mna ubavu wa kutumia nguvu ya umma ambayo ndio slagan yenu, angalau hata kwa siku 5 mfululizo mkiipinga serikali iliyowekwa madarakani kwa mujibu wa matokeo? Uzoefu unaonyesha watanzania sio wavumilivu wa kusimamia jambo kwa umoja kwa muda mrefu mfululizo.