Lowassa kuongea na vyombo vya habari

ni vyema watanzania wakajua ukweli maana naamini kama hukutenda wewe umebeba siri ya watendaji wa mchezo huu mchafu jisafishe mapema kwa kuonyesha wahusika maana nahisi hutaambulia kitu kwa kutunza siri au kama wewe ndo muhusika wa moja kwa moja.Ngoja nikusikilize labda unaweza badili fikra nilizonazo juu yako!

nadhani ndio wakati wa kufunguka sasa bila kujali nani alisababisha tatizo kwani ata mwakyembe ameenda nje ili kukwepa kuhojiwa kwani nyaraka nyingi alizozikuta ni za mzee ndi maana alitoa kauli ya ( ikifika wakati atasema mpaka yale ambayo aliyaweke na kuzuia yasisemwe)
 
Lowassa tunamtegemea sana kubadilisha upepo wa siasa za CCM, yeye amekuwa mbuzi wa kafara tu. Hizi scandal zote ni za CCM as a whole, inapotokea mmoja wao anabebeshwa lawama it si completely unfair. Lowassa anazo siri nyingi zinazowahusu hao wengine mimi naamini kuwa akija public na kusema kila kitu itatusaidia sisi kufahamu ins and outs za hizo scandal.

Ninawaomba mpeni nafasi ya kuzungumza ili tuyapate kwa undani hayo yote. Ninamini akitumika vizuri anazo nguvu za kutenganisha uenyekiti wa CCM na urais wa Tanzania.
 
Ukweli peke yake utamweka huru na hakika kama akiongea ukweli wake kuna watu watapata shida hakika. yetu macho na masikio kwake leo
 
aseme ukweli na kuomba radhi kwa yale yote aliyotupitisha tutamsamehe, atasafishika kwa sababu itakua ujasiri wa aina yake kwa kiongozi mwandamizi haswa hii Africa yetu kuomba msamaha
 
nadhani leo kila baada ya sentensi atamalizia kwa kusema ''watanzania wanajua na dunia inajua'''
 
Nitashukuru mhe Lowasa ukiongea na kuweka wazi fitina, chokochoko na uchafu unaofanywa na baadhi ya viongozi walioko madarakani. SEMA BILA WOGA NCHI IPONE kwani tunaona unafiki na ubinafsi wa wengi walioko madarakani. Nchi inadidimia, wananchi wanaumia.
 
Lowassa anataka kujibu mapigo kwa SS baada ya mahojiano na ITV juzi J4.
Hakika hii ni vita kali ndani ya CCM. Kikwete asipokuwa makini CCM kinamfia mikononi. Yetu macho na masikio.
 

Similar Discussions

1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom