Lowassa kuongea na vyombo vya habari

ila jamani tukiacha chuki ambazo hazina msingi, ni halali lowasaa kuandamwa hivi? Tukumbuke na mema alioifanyia nchi yake

Mema yapi unayoyazungumzia mkuu! Usikute unazungumzia utekelezaji wa majukumu yake! Maana tumekuwa na udhaifu wa kudhani kiongozi anapotekeleza wajibu au ahadi zake ni hisani. Wake up my friend. Ni jambo gani alilolifanya ambalo lilikuwa nje ya majukumu yake ili leo na tusimame na tuseme anastahili pongezi!
 
lowassaaa hoeeeee nakupenda sna mzaziiiii umefanya mengi TZ hlo 1 halinitishii sna kwangu, bt jua kwamba binadamu ndo tulivyooo na kusema ni jadi yetu mdomo hatulipii vat so. Mollel busara unayo, na alikuwa kimya sababu maji yakija kwa kasi yapishe yapite. Silence mean something sishangaiiii
 
Lowassa anataka kujibu mapigo kwa SS baada ya mahojiano na ITV juzi J4.
Hakika hii ni vita kali ndani ya CCM. Kikwete asipokuwa makini CCM kinamfia mikononi. Yetu macho na masikio.

Lowassa hajaanza tu kuzungumza na waandishi wa habari???
 
MANENO YA MILYA JUU YA NAPE LOL!!(Wakati tunasubiri kauli ya lowasa taatifa yake iko hapa https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...ape-ni-vuvuzela-na-saratani-ndani-ya-ccm.html)

Nape Nnauye, Katibu Mwenezi wa CCM (Kundi fulani linalowania Urais 2015)

Kijana huyu namfananisha na saratani ndani ya mwili. Hivyo sintakosea nikisema ni "Saratani na Janga kwa CCM". Badala ya kueneza sera za CCM ameamua kueneza sera za upande mmoja na kujaribu kuutukana upande ambao hakubaliani nao kisiasa. Siamini kama anaeneza chochote kinachohusu au kitakachosaidia CCM kukubalika na wananchi na wana-CCM. Amekuwa vuvuzela la baadhi ya watu.

Historia ya kijana huyu inafahamika. Alifukuzwa na Baraza la Umoja wa Vijana wa CCM Taifa kwasababu ya upotoshaji wake wa dhamira njema ya Baraza hilo la Umoja wa Vijana. Vijana walishamkataa siku nyingi, tungeulizwa kwanini tumeshindwa kumvumilia.

Wiki hii itakua mbaya sana kwa baadhi ya Mafisadi; naona hata wale waajiriwa wa Nape wana-comment kichovu kweli, woga umewajaaa....wasikimbie hata mmoja hakuna cha shift wala nini leo, wabaki hapahapa
 
Viongozi wa nchi hii wamekaa kwa kulindanalindana tu, sasa huyu lowasa hata mwalimu Nyerere aliwahi kuhoji wapi alipata hizo mali anazo miliki na akampinga alivyotaka kugombea urais, still akaingiza nchi kwenye kashifa ya richmond, leo hii bado tu yupo huru tena kwenye medani za siasa, jamani sheria na vyombo vya usalama vinafanya kazi zake kweli???? ingekuwa ni amri yangu ningemkamata hapohapo kwenye press conference. Ingekuwa China leo hii Lowasa angelikuwa ni historia tu.
 
Mbona huhoji Manji pamoja na kudhihirisha kwamba ni mshiriki wa Wizi wa Pesa za EPA kwa kurudisha serikalini lakini bado hajawahi kushtkiwa!
 
si maskini..Mara anajitindua Gamba..LAKINI KUWEMA UKWELI NINAONA KWA KASHFA YA BABA YETU HUYU...HERI YAKE KULIKO JK ANAKOTUPELEKA SASA.....TUPIME MARA 2 2 .....he looks better for only one scandal than ..........jklisation
 
Viongozi wa nchi hii wamekaa kwa kulindanalindana tu, sasa huyu lowasa hata mwalimu Nyerere aliwahi kuhoji wapi alipata hizo mali anazo miliki na akampinga alivyotaka kugombea urais, still akaingiza nchi kwenye kashifa ya richmond, leo hii bado tu yupo huru tena kwenye medani za siasa, jamani sheria na vyombo vya usalama vinafanya kazi zake kweli???? ingekuwa ni amri yangu ningemkamata hapohapo kwenye press conference. Ingekuwa China leo hii Lowasa angelikuwa ni historia tu.

he he he siasa za mfumo wa kifisadi zinawalinda na kuwaongezea nguvu wale mafisadi wakuu, kaka jua hili sisi Tz ya leo tupo kwenye mfumo wa kifisadi lugha ya kitaalam ni kleptocracy na huyu ni top kleptocrat
 
Viongozi wa nchi hii wamekaa kwa kulindanalindana tu, sasa huyu lowasa hata mwalimu Nyerere aliwahi kuhoji wapi alipata hizo mali anazo miliki na akampinga alivyotaka kugombea urais, still akaingiza nchi kwenye kashifa ya richmond, leo hii bado tu yupo huru tena kwenye medani za siasa, jamani sheria na vyombo vya usalama vinafanya kazi zake kweli???? ingekuwa ni amri yangu ningemkamata hapohapo kwenye press conference. Ingekuwa China leo hii Lowasa angelikuwa ni historia tu.

Kwanza yeye ni nani hivi leo kiasi cha kupewa prominance kiasi hiki na tunamsafisha kwa maslahi ya nani. Alijiuzulu baada ya yeye mwenyewe kupima uzito wa tuhuma, na kwa uamuzi wake wa kujiuzulu alithibitisha ukweli wa tuhuma dhidi yake. Tatizo letu Wtz ni unafiki, siku JK akimweka ndani au CDM ikichukua madaraka na kuwashughulikia mafisadi wote, sitoshangaa hao wanaompigania wakamgeuka.

Ukiachilia mbali sakata la Richmond, hivi aliyefanya mazungumzo ya kuleta mvua ya kutengezwa kutoka Thailand ni nani, JK, Riz au Lowassa!!!

Hivi mwanzilishi wa siasa uchwara katika nchi hii ni nani kama sio EL na rafiki yake RA, leo wanamlalamikia nani. Leo hii vyombo vyao vinadiriki hata kuwazushia watu magonjwa wasiougua, wana lengo gani kama sio kuuhadaa umma wa Watanzania kwa ajili ya malengo yao ya 2015.

Tuache unafiki na porojo zinazotutoa kwenye mijadala ya maana zaidi kwa ujenzi wa taifa letu.
 
Hatimae CCM wataenda ku-rest in Peace, ila swali la msingi ni kwamba kwanini asisubiri Mwakyembe arudi kwanza ndio aseme analotaka kusema? kwanini Sitta aliongea aliyoyaongea na sasa Lowasa nae anajitokeza hadharani? Uko wapi ule utaratibu wa Magamba wa kutumia vikao? hakika mwisho umewadia...
 
azungumze tu, lakini urais atausikia kwenye bomba, habadilishwi kitu mtu hapa.
Hii nchi inaendeshwa kama movie.
Hebu tuangalie vigezo hivi:
1. Shutuma nzito kama hizi mtu maarufu, mwenye akili timamu, mwanasiasa na tajiri unaweza kukaa kimya miaka minne wakati unajua kabisa kwa kufanya hivyo unailazimisha jamii ikubaliane na tuhuma dhidi yako?

2. Hii courage ya kuongea na waandishi wa habari ameipata wapi wakati huu.

3. Je tunaweza tukasema kwamba ni coincidence kwamba kinara wa tuhuma dhidi yake (Mwakyembe) anaugua ugonjwa usiojulikana na hayupo ndani ya nchi na yeye kufanya ayafanyayo au ni mkakati?

4. Katika mazingira haya, tusubiri tusikie atasema nini, tusubiri tuone hatima ya Mwakyemba itakuwa nini.

Maswali yapo mengi ya kujiuliza ila tujadili haya machache.
 
Mi nilitegemea agenda zake zingine ingekuwa " kutoa maamuzi juu ya azimio la NEC la kujivua gamba". hana lolote anakuja tu kujikosha katika harakati zake za kutafuta urais 2015. Ki ukweli CCM hakuna asiyekifahamu, na sisi wengine tumewahi kuwa machipukizi wa ccm toka muda mrefu tukakiacha kutokana na kubadilika kwake hasa baada ya kifo cha Nyerere. Katika misingi ya maadili, pale ambapo kelele za umma zinapokuwa nyingi dhidi yako hasa kuhusiana na maadili, huna sababu tena ya kufikiria madaraka ya juu ya kitaifa kama uwaziri mkuu tu ulikushinda kwa tamaa ya fedha. lazima tuwe majasiri EL si mtu wa kuwa rais wa Tanzania hata kidogo hata baba wa taifa alimkataa, sasa kama tunataka laana ya mwalimu basi tuendelee kumshabikia tusubiri kiama chetu. Mimi natoa maoni huru kwa jinsi nijuavyo CCM na mwenendo ya viongozi wetu wa sasa. Mtu mwenye tamaa kubwa ya fedha hatuna sababu ya kumfikiria awe rais wetu na kama CCM watafanya makosa hayo ya kumteua agombee kupitia CCM basi wajue nao watalaaniwa na Nyerere.
CCM siku hizi kila mtu amekuwa msemaji, ndo mana wana gongana kila kukicha na hiyo inatokana na udhaifu wa Mwenyekiti wa chama kuamua kunyamaza kimya huku akiona makundi yana shamiri. Chama legelege huzaa serikali legelege, ndo CCM. Kikwete achia tu uenyekiti yakutokee kama ya Thabo Mbeki.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom