Lowassa kuongea na vyombo vya habari

Atoe YOTE ya moyoni mwake ili kujisafisha zaidi.

Akichanga vizuri karata hii, 2015 anaweza kuwa rais wa 5 wa TZ na amewahi vizuri tu kila la kheri LOWASSA leo

 
Huyu jamaa anajaribu kuwaweka sawa wajumbe wa CC na NEC ya chama chake kabla hawajakutana kumvua gamba. Anataka kuwafundisha woga ili wafanye "maamuzi magumu" ya kumvua gamba.

He is very tactical na kwa umbumbumbu wa CCM ya sasa hawataweza kumvua gamba. Then anajipanga na uchaguzi wa 2012 ili kumng'oa JK na kuchukua kiti chake. Hiyo ndio namna pekee ya kupata ridhaa ya "chama chake" kugombea urais 2015. So he start from the second step as the 1st one ya kuwaweka vizuri viongozi UVCCM na CCM mkoa imeshafanikiwa kukigawa chama na kumpatia watetezi kwenye agenda ya kumng'oa m/kiti.

My take ni kwamba mtafararuku utazidi kukomaa, JK atahakikisha EL anavuliwa gamba. Hatakubali kuachia uenyekiti, atawaweka kwenye chama "watu wake" na mwisho wanaompinga this time hawataogopa kujitoa, akiwemo EL, na hatimae "mgombea" wao 2015 atakuwa na upinzani mkali na hatimae, kama ilivyotokea kwenye kanu huko kenya, ccm itashindwa vibaya.

Na mtazamo wangu, cdm watatangazwa rasmi kuwa chama tawala.
 
Ingekuwa busara tusubiri azungumze kwanza ndio tuchangie maoni. Haiwezekani tuwe na shauku muda mrefu kujua kilichojiri alafu leo kabla hata hakidhi kiu yetu tunaanza kutoa 'conclussions' zisizo na maana. Tungoje tujue atazungumza nini, anaweza akachafua hali ya hewa zaidi ndani ya CCM. Tumuunge mkono asifiche kitu...! TUNA KIU...!
 
Je watarajia nini toka kwake? Kujiuzulu? Kuibua mapya? Kukana uhusika wake ama kujisafisha? Au kutangaza nia 2015?
 
kuna mtu anajua ni saa ngapi huyu jamaa anaongea na wanahabari?
 
Lowassa represents ward-heelers who are dedicated at siphoning and embezzling public funds at any cost.

He is purported culprit behind irrefragible Richmond scandal but seems to remain incurable even after all the criticisms and disaproval against his involvement in accepting that exploitative deal which in turn brought TANESCO to its knees and subsequently plunging the state into incessant power rationing plights.

I'm pretty sure that his image is now damaged beyond any surgical manouvre and any attempt to repair it will do no better but exacerbate the situation. He should simply understand that he can't fool all the people all the time and the night is over.
 
Ni mda mrefu sana E Lowassa amekuwa akiandamwa sana na ccm na baadhi ya watu kwa maslahi yao wanayojua wenyewe.

Lakini tukiacha ushabiki wa kisiasa na kufikilia kwa undani Lowassa amesaidia mengi sana Tanzania. Kila mtu ana mapungufu yake hivo alionayo Lowassa si ya ajabu. CCM ina ajenda ya siri ya kumuua Lowassa kisiasa, kwa kuwa leo ataongelea mambo yote ambayo amekuwa akituhumiwa,tumsikilize vema ili tuchambue ukweli na uongo wake.
 
Kuna taarifa ya aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Lowassa kuzungumza na vyombo vya habari nchini. Ametaja ajenda tatu ambazo ni pamoja na Richmond & UVCCM. Huyu jamaa ni miongoni mwa watu wawili wanaotakiwa kujivua gamba. Ni imani yangu atakapokutana na waandishi lazima ataulizwa msimamo wake kuhusu kujivua gamba.
 
Mbona hilo la kujivua gamba kwa huyo jamaa alishalitolea maelezo? Huyu ni mjasiria mali wa kura za 2015 hakuna la ziada.
 
naomba leo aitumie vizuri kabisa ..aseme yote kabisa....

Baada ya hapo tunaweza sema tumelala maskini na leo tumeamka matajiri (Wapinzani), Mamnvi mwaga kila kitu toka moyoni mwako watu wachambue mchele na pumba, waandishi nanyi msilaze damu kwa kumpatia maswali makini ili muuze magazeti kiuhalali na sio mtuletee ngonjera zenu kwani tunasikia kuwa mnajali sana mishiko siku hizi
 

Similar Discussions

1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom