Lowassa Kuanzisha ABC Television Arusha

Nakubaliana na wewe kuwa sikijui kiswahil.Unajua siku zote huwa na sema mtu usiongee kitu usicho kijua usije jikuta kwenye matatizo bure.najua wewe unamshabikia Mwanakijiji kwa kuwa makala makala zake zina kuvutia,ungejua yeye anatumiwa hizo na makala halafu yeye ana copy na kupaste hapa.sitaki kuongea mengi kuhusu Mwanakijiji nisije onekana nina nia mbaya nae au nime tumwa,maana waswahili hamchelewi.maandishi ya rangi nyekundu hapo juu: hapa atupo kutukanana au kakashifiana bali tupo kujenga hoja na kuelimishana pamoja na kukosoana.

Josm,

Mmmmhhhh!!!!! Kama kweli Mwanakijiji anatumiwa kama unavyotaka tuamini, basi anatumiwa vizuri sana. Mwanakijiji, endelea kukubali kutumiwa ili kupitia kwako tuyajue mengi zaidi.

Tiba
 
I see,

Watawapata "Ze Komedi" wengine na kuwatumia! Subiri uone. Vipindi vitakuwa merged na Televisheni yenu ya Taifa. Mtaangalia mtake msitake!

Wamejipanga mkuu...

mimi sitishiki ikishindikana najua tuta chukua silaha, kwani ni lipi haliwezekani?

wapo vijana kibao pale mwenge mlalakua makomandoo na wanalalamika kutotendewa haki jeshini, subiri tu.

Mtu kama rostam na wenzake it's just a matter of few minutes anateketea.
 
Katika vita Ngumu ya kupata Uhuru, tanzania hatukumwaga damu japo baadhi ya mababu zetu walimwaga damu.

Nina uhakika katika vita hii ya Kiuchumi na Kifikra tutashida. Kila kitu na wakati wake na Zama zake.

Time. Time. Time will tell. And soon and very soon all will be clear.

God Bless Tanzanians!

Mzee maneno mazito sana hayo, japokuwa kweli maadui wanamaguvu na mbinu tele! Mimi pia naamini iposiku tutashinda ingawaje sometimes tunaweza kubadili silaha hapa na pale kutegemea na adui anavyo badilika pia.
 
Huyu bwana tangia atoke madarakani amekuwa kimya sana na mambo yake anfanya kichinichini - Waogope sana watu wasiopenda kupayuka, hujui atapiga wapi na lini!

Baada ya kuanzisha mtandao wa media, tusuburi kampeni ya kumsafisha mtu, watanzania ni wepesi sana wa kusahau. Muda si mrefu tutamwona tena ENL kwenye uongozi wa juu; time will tell!
 
Last edited:
El amefanya jambo jema kufungua TV station, huu ndio ujasiriamali tunaotaka wazawa waufanye na kupanua uwigo wa ajira ndani ya nchi.

Anatekeleza kwa vitendo Ilani ya uchaguzi ya chama chake. Na hii iwe ni changamoto kwa wengine miongoni mwetu kufuata mfano mzuri huu.

Watakuwepo wapinganji wa hapa na pale hilo ni jmabo la kawaida waswahili husema "panapo riziki hapakosi fitna" Namuomba mzee wetu huyo asife moyo hizi ni kelele za malngo tu...
 
Huku Arusha kuna Studio ya TANMEDIA imeanza kujengwa, ni ghofa tatu maeneo ya Njiro na ni studi ya Radio na TV na inasemekana ni ya Lowasa, pengine ndo maandalizi ya Redio hiyo ambayo baadaye itakuwapo na TV pia.

Thank you Ibra. Here are more details:

Source: HabariLeo: Gwiji la habari Tanzania | Flamingo yapigwa jeki

John Mhala, Arusha

Daily News; Thursday,December 18, 2008 @21:15

Kampuni ya Tan Media inayomiliki kituo cha redio 5 FM cha Arusha imetoa msaada wa vifaa mbalimbali vya michezo kwa timu ya Flamingo SC vyenye thamani ya Sh 500,000. Akikabidhi vifaa hivyo jana Meneja wa kituo hicho, Dioniz Moyo alisema kuwa kampuni yake imeamua kutoa msaada huo baada ya kupokea maombi ya muda mrefu kwa viongozi wa timu hiyo.

Moyo alisema vifaa vilivyokabidhiwa ni jezi seti mbili, soksi, koni 30, vizibao 18, vizuia ugoko 18, mipira 10 na glavu seti tatu. ‘’Sisi kama kampuni tumewapa changamoto wachezaji na viongozi wa Flamingo SC kuhakikisha wanafanya vyema katika ligi hiyo ili waweze kuutangaza vyema Mkoa wa Arusha katika ligi za ngazi ya juu’’alisema Moyo.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Flamingo, Ramadhani Siwayombe alishukuru kwa msaada na kudai timu yake ilikuwa ikikabiliwa na hali ngumu ya vifaa wakati inashiriki ligi. Mpaka sasa Flamingo imeshinda michezo yote minne iliyocheza na kubakiwa na mechi tatu ili iweze kuingia hatua ya pili ya ligi hiyo. Flamingo inafuatiwa na Bishop inayoshika nafasi ya pili kwa kujikusanyia pointi 11 sawa na Olduvai lakini kwa tofauti ya mabao ya kufunga na kufungwa.

Pia angalia:

Source: TCRA|Tanzania Communications Regulatory Authority

APPLICATIONS SERVICES LICENSES

47Tan-Communication Media Limited
3rd Floor, CCM Building
P. O. Box 11843
ARUSHA

OR

P.O. Box 33723
DAR ES SALAAM
Tel: 0754 328222, Fax: 0754 780890
Email: tanmedia@yahoo.com

From: 16th January 2009
License Category: National Application Services

NB: Address ya ABC TV na cha 47Tan-Communication Media (P.O. Box 11843 is the same) ambao pia wanamiliki Radio ya 5 FM.

Also note that the License is not for Arusha but NATIONAL.
 
hivi wewe unamjua Mwanakijiji vizuri kweli? kwa taarifa yako Mwanakijiji ni Ndumilakuwili achelewi kukugeuka mda wowote,pia anatumiwa na baadhi ya watu kwenye shughuli zao.Hivyo kuweni makini nae sana hasa Thread zake anazo anzisha ilikupima upepo wenu then anapeleka report kwa wahusika.be care full guys.

hahahahhaah... well.. wenzio wanadandia mabasi mlangoni.. wewe unadandia treni kwa mbele? Jipange mstari, kuna msururu wa wenzako.
 
Yessir,

subiri ina kuja orodha ya member wa JF wanao tumiwa ha baadhi ya watu hapa,

hiyo orodha itakuwa tofauti na ile iliyoanzishwa na Mhe. Gembe ambamo mimi nilikuwa wa kwanza? maana kwenye hiyo orodha yako sitakubali kuwa chini ya namba moja!
 
El amefanya jambo jema kufungua TV station, huu ndio ujasiriamali tunaotaka wazawa waufanye na kupanua uwigo wa ajira ndani ya nchi.

Anatekeleza kwa vitendo Ilani ya uchaguzi ya chama chake. Na hii iwe ni changamoto kwa wengine miongoni mwetu kufuata mfano mzuri huu.

Watakuwepo wapinganji wa hapa na pale hilo ni jmabo la kawaida waswahili husema "panapo riziki hapakosi fitna" Namuomba mzee wetu huyo asife moyo hizi ni kelele za malngo tu...

- Kufungua station sio tatizo, ila anataka kuitumia for what maana record yake sio nzuri sana na kila anachokigusa.

Respect.

FMES
 
Now kwenye hoja:

Kama mtu ameamua kuanzisha biashara yake nihaki yake kwa kadiri ya kwamba biashara hiyo imeanzishwa kihalali na fedha zilizotumika ni za halali. Hadi hivi sasa sijaona madai kuwa hawa jamaa wametumia kwa namna yoyote fedha za serikali au nafasi ya kisiasa ya Lowassa kujipatia leseni hiyo au mtaji wa biashara yao.

Lakini vile vile, hatuwahukumu watoto moja kwa moja kwa makosa ya wazazi wao isipokuwa kama watoto hao wanatumika na wazazi wao kuficha madhambi yao. So, kwenye hili mimi sijui hawa jamaa wanabiashara gani nyingine ya kuweza kuwapatia kipato cha kuweza kuanzisha televisheni. Kama uwezo huo wanao kibiashara basi ni haki yao kama mtanzania yeyote mwenye uwezo, kipaji na nia ya kutumia uwezo huo kujipatia mlo wa kila siku.

Vinginevyo, endapo kuna tetesi zenye kuashiria kuwa fedha hazikupatikana kihalali, utaratibu wa leseni haukufuatwa au sheria zimepindwa au kuvunjwa katika mchakato mzima basi vidokezwe. Vinginevyo, ABC kama zilivyo shughuli nyingine itapimwa kwa matunda yake, na tutaipima kwa kadiri inavyotumika aidha katika kupinga ufisadi, kutetea utawala bora na utawala wa sheria au kama itatumika kinyume na hayo. Hapo ndipo hukumu ya wananchi inapaswa kutolewa.

Kwa sasa nawapa asilimia 100!
 
who is elias lukumay?

Source: ThisDay
. . . . .

Warehouses operated by the following firms, with the names of their respective company directors in brackets, have also been shut down by TRA:
. . . . .
Also suspended are NAM Enterprises Limited (Stephen Lukumay, Elias Lukumay, Alex Lukumay and Namnyax Lukumay), Aluminium Africa Limited (Safal Investment of Mauritius and Treasury Registrar), Mazrui company (Said Hemed Salum, Abdallah Hemed Salum and Salim Hemed Salim), Rasco (Ahmed Said Abdallah, Humud Saleh Humud and Rashid Said Abdallah), C.M. Company Limited, Sozmy, F.K Motors, and Mrina company.
 
Source: DATE

PREACHER: MCH. ELIAS LUKUMAY WA USUPUKO DAYOSISI YA MKOANI ARUSHA

TOPIC: LUKA 4.18, ROHO WA BWANA YU JUU YANGU
 
Nafasi za Kazi hizoooooo...!

Hakika kwa wale wenye utaalamu wa mambo MEDIA, kazi ndo hizo! Ni lazima aajiri watu kutoka miongoni mwenu!

Sasa ishu ni kwamba je watakaoingia huko watafanya kazi kwa kufuata taaluma zao au kwa maslahi ya hawa mabwana - mi sijui.

Naendelea kujifunza kuwa, kumbe Media ina nguvu sana... kwanini kila mwenye hela zake anataka kumiliki ya kwake?

I just keep my eyes wide open! - time will tell.
 
Ama kweli!
JF imekuwa kama nyati aliyeangukiwa na mti mkubwa.
Sasa sijui huyu nyati kavunjwa mgongo tayari?!
 
Now kwenye hoja:

Kama mtu ameamua kuanzisha biashara yake nihaki yake kwa kadiri ya kwamba biashara hiyo imeanzishwa kihalali na fedha zilizotumika ni za halali. Hadi hivi sasa sijaona madai kuwa hawa jamaa wametumia kwa namna yoyote fedha za serikali au nafasi ya kisiasa ya Lowassa kujipatia leseni hiyo au mtaji wa biashara yao.

Lakini vile vile, hatuwahukumu watoto moja kwa moja kwa makosa ya wazazi wao isipokuwa kama watoto hao wanatumika na wazazi wao kuficha madhambi yao. So, kwenye hili mimi sijui hawa jamaa wanabiashara gani nyingine ya kuweza kuwapatia kipato cha kuweza kuanzisha televisheni. Kama uwezo huo wanao kibiashara basi ni haki yao kama mtanzania yeyote mwenye uwezo, kipaji na nia ya kutumia uwezo huo kujipatia mlo wa kila siku.

Vinginevyo, endapo kuna tetesi zenye kuashiria kuwa fedha hazikupatikana kihalali, utaratibu wa leseni haukufuatwa au sheria zimepindwa au kuvunjwa katika mchakato mzima basi vidokezwe. Vinginevyo, ABC kama zilivyo shughuli nyingine itapimwa kwa matunda yake, na tutaipima kwa kadiri inavyotumika aidha katika kupinga ufisadi, kutetea utawala bora na utawala wa sheria au kama itatumika kinyume na hayo. Hapo ndipo hukumu ya wananchi inapaswa kutolewa.

Kwa sasa nawapa asilimia 100!

Wakati nasoma Mafundisho ya kipaimara tulifundishwa kuwa mwsho wa Amri unasema nanukuu mistari michache "Nawapatiliza wana wa maovu ya Baba zao hata kizazi cha tatu na cha nne cha wanichukizao ....nami nawarehemu maelfu elfu wanipendao na kuzishika amri zangu"
 
hivi wewe unamjua Mwanakijiji vizuri kweli? kwa taarifa yako Mwanakijiji ni Ndumilakuwili achelewi kukugeuka mda wowote,pia anatumiwa na baadhi ya watu kwenye shughuli zao.Hivyo kuweni makini nae sana hasa Thread zake anazo anzisha ilikupima upepo wenu then anapeleka report kwa wahusika.be care full guys.

Hivi MSWAHILI yuko wapi Jamani amepotea sana Jamvini vp Josm unajua aliko?

Asante
 
Back
Top Bottom