Lowassa Kuanzisha ABC Television Arusha

kuupinga ufisadi si kupinga kila kitu kinachofanyika au kufanywa na hawa watu...kufungua redio jamani ni katika investment RAHISI sana hapa nchini kufanya, kama kuna mtu hajui aulize pale TCRA.
mi naona ni kitu cha kumpongeza na kumtaka aitumie kwa maendeleo ya eneo lile..tusiwe sana negative tukazani ndio mtazamo sahihi na kupinga hata vitu visivyo na nia mbaya kwa kutumia jazba la ufisadi....

ufisadi ulitengenezwa na serikali tuliyoiweka sisi wenyewe kwa kushindwa kusimamia rasirimali za nchi....tukumbuke kukumbatia maji kama jiwe ni ujinga...
 
acheni kelele.. sinamnalalamikaga mafisadi wanainvest out of the country only.. sasa lowassa anaemploy watu wangapi kwenye majumba yake 50, viwanda, makampuni ya alphatel, alpha high skul, alpha dry clearners, ranch yake, voda, sijui nini.. and all the rest that few know about...! Mtu akiwa mwizi sio maana yake kila alichonacho kaiba.. The man actually has what can be decribed as a business empire and regarless of how he got it (and I'm not defending him here.. kwakuwa simpendi na sikubaliani na vitu alivyo-anavyo fanya).. the fact remains anawalisha watanzania wengi.. more than all the people wasioiba maana who is to say wangeziona hizo hela anyway.. Political camps blind people from the cold facts sometimes.. (Lowassa is a cancer lakini kuweni objective mnapoongelea haya mambo ama hii JF nayo itakuwa genge tuu la wapayukaji if its not that already... and I seem to be convinced of the latter, the majority of the time nowardays..)
 
Kwa kweli kama ni kwa nia njema, hakuna ubaya kwa Lowassa kuanzisha TV popote iwe Dar ama Arusha. Lakini jambo moja ambalo lazima tuliangalia kwa makini ni kwamba hawa jamaa wamepania kuchukua nchi. Mind you "kuchukua nchi" na hawatanii, mnataka ama hamtaki. Kilichompata Lowassa na wenzake, wameona ni kutokana na nguvu ya media. Wameamua sasa na mumesikia ama kuona, magazeti kibao yakiongozwa na ununuzi wa New Habari. Wamenunua Channel Ten. Hatua itakayofuata na ambayo mchakato umeanza ni kuwadhibiti wamiliki wa vyombo wanavyoona itakuwa kikwazo kwao ikiwamo IPP Media.

Kwa ufupi ni kwamba kama tukiwa makini kidogo tu tutabaini kwamba, Tanzania yetu inaelekea kubaya. Tunajua kila mtu ana haki ya kutawala, lakini si urithi Mwalimu Nyerere aliotuachia kwamba uongozi ni kwa wenye fedha na vizazi vyao. Nawaambia hata ndugu zangu humu (Nawafahamu) ambao wana nia njema ya kuja kuingia katika siasa kihalali (wakiwamo wanaoshabikia EL kuanzisha TV) wajue kwamba bila fedha (za rushwa) hawatashinda kutokana na mfumo uliojikita na unaoendelea kuimarika vinginevyo wawe vibaraka wa wenye fedha. Hii ni HATARI sana na hapa tukijadili mambo tuangalie huko (2010-2020) maana wenzetu wamejipanga hivyo na kwa gharama zozote zile ikibidi hata za HATARI (nitajadili kwa wakati).
Umenikuna kwa hoja yako.Kama Watanzania wote mnaosoma hoja za JF mna nia njema na nchi hii msishabikie kabisa EL kuanzisha TV kwa si kwa nia njema kwa anachowaza yeye ni uongozi tuu wa nchi hii wakati ni fisadi na ni mtu wa visasi.Naomba sana CHADEMA,MENGI na Waandishi makini tushirikiane tuhakikishe mafisadi hawatambi katika nchi hii.EL na mafisadi wenzake ni kama MOBUTU,ABACHA na wahujumu wengine wa uchumi wa nchi zao.Mungu ibariki TZ.
 
kuupinga ufisadi si kupinga kila kitu kinachofanyika au kufanywa na hawa watu...kufungua redio jamani ni katika investment RAHISI sana hapa nchini kufanya, kama kuna mtu hajui aulize pale TCRA.
mi naona ni kitu cha kumpongeza na kumtaka aitumie kwa maendeleo ya eneo lile..tusiwe sana negative tukazani ndio mtazamo sahihi na kupinga hata vitu visivyo na nia mbaya kwa kutumia jazba la ufisadi....

ufisadi ulitengenezwa na serikali tuliyoiweka sisi wenyewe kwa kushindwa kusimamia rasirimali za nchi....tukumbuke kukumbatia maji kama jiwe ni ujinga...
Hiyo Serikali ilikuwa inaongozwa na nani kama si EL.Anzia tangu enzi za AICC na kitengo cha maafa Ofisi ya PM Lowassa alizuia wapi ufisadi,sasa hiyo TV kama si kulindia fedha alizokwapua.Ni vema asome alama za nyakati,hawezi kuongoza nchi hii labda atafute kibaraka kama alivyofanya kwa JK na kumkandia Dr.Salim.
 
ni haki yake kuwekeza anavyotaka na hakuna ubaya wowote ili mradi atafuata sheria zote za Media na kodi,mengine humu naona ni majungu tuu,kama mna kesi mbona mlishindwa kumweka ndani alivyojiuzuru!
 
ni haki yake kuwekeza anavyotaka na hakuna ubaya wowote ili mradi atafuata sheria zote za Media na kodi,mengine humu naona ni majungu tuu,kama mna kesi mbona mlishindwa kumweka ndani alivyojiuzuru!
CCM ni taleban wa ufisadi!-Koba
 
acheni kelele.. sinamnalalamikaga mafisadi wanainvest out of the country only.. sasa lowassa anaemploy watu wangapi kwenye majumba yake 50, viwanda, makampuni ya alphatel, alpha high skul, alpha dry clearners, ranch yake, voda, sijui nini.. and all the rest that few know about...! Mtu akiwa mwizi sio maana yake kila alichonacho kaiba.. The man actually has what can be decribed as a business empire and regarless of how he got it (and I'm not defending him here.. kwakuwa simpendi na sikubaliani na vitu alivyo-anavyo fanya).. the fact remains anawalisha watanzania wengi.. more than all the people wasioiba maana who is to say wangeziona hizo hela anyway.. Political camps blind people from the cold facts sometimes.. (Lowassa is a cancer lakini kuweni objective mnapoongelea haya mambo ama hii JF nayo itakuwa genge tuu la wapayukaji if its not that already... and I seem to be convinced of the latter, the majority of the time nowardays..)

TRUE watanzania ndio tunasababisha watu watoroshee pesa ulaya....utawala wa mwalimu na mwinyi mwanzoni [wakati wa ufagio wa chuma]....viongozi walikuwa wakiweka mapesa ulaya ..yanaajiri wazungu ...na kuzitumia kukopeshana ...mwisho zinapotelea huko wakifa..

sasa miaka hii viongozi mafisadi wanawekeza nyumbani..nadhani ni suala muhimu kupiga kelele kuzuia ufisadi...lakini kelele za kusema tuyazuie makampuni na mashamba au viwanda vyao hazitasaidia ...ni jukumu la takukuru kuzuia isitokee na wananchi tuunge mkono...lakini haileti mantiki kuzuia makampuni ambayo yamesha take off ...yanaajiri watanzania,yanalipa kodi,yanafanya corprate citizen responsibilities etc....kwani hiyo ndiyo njia pekee ambayo pesa yetu iliyoibiwa inaweza kurudhishwa...kwa kuzuia makampuni yasifunguliwe...hatutakuwa na njia ya kurudisha pesa zetu ...na zitaishia kutoroshwa..bila kuwa na faida kwetu....

natoa rai kwa watu wote wenye pesa wawekeze...na wasiogope kuulizwa,na sisi wananchi tutulie pesa ziwekezwe..kwani tukipiga makelele hatutakuwa na njia nyingine ya kuzirudisha anyway....mmeona wenyewe pesa za EPA zilizorudishwa ni kitendawili hadi leo...si bora zingeachiwa zika stimulate uchumi.....na watuhumiwa waendelee na mashtaka kama wao?

Tunayoyashukudia kwenye ufisadi ni hali ya kawaida ya mpito wa kiuchumi toka kwenye uchumi wa kijamaa hadi uchumi wa kibepari...,kwa kuwa hatukuweka njia muafaka sustaibable ya kutengeneza mamilionia wetu....na kuwa na uwazi basi imesababisha wenye nafasi kuiba....lakini nchi kama china,urusi na hata marekani....wana mifuko maalumu isiyo na riba au ruzuku za kuibua biashara kubwa kubwa....hii kusaidia kuondoa haja ya magenge ya matajiri kupanga na kutekeleza ufisadi...uwazi hujenga imani kwa wananchi wakijuwa kuwa hata wao wakiwa na miradi wanaweza kupata funding....

rais KIKWETE aLIIKUWA na dhima ya kuzalisha mabilionia 100 wazawa..waandishi mliuliza?????...kama angepata uelekezi na ushauri ....he could do the russian way..pale walipotoka kwenye hali ngumu ya uchumii....lakini ulikosekana uwazi....ukageuka wizi...,nataka mjuwe mipango iliyoanzishwa tangu wakati wa mwinyi ya import support,mpango wa mkapa wa SME guarantee wa benki kuu...ingesimamiwa vema ..tungefanikiwa kujenga tabaka la nguvu la kati[STRONG MEDIUM CLASS].....hapa kwenye tabaka la nguvu la kati ...ingekuwa rahisi kuchuja na kupata watanzania 100 Waliofanya vema zaidi..ambao tungewapa mikopo isiyo na riba mikubwa kabisa...ili wawe LARGE ENTREPREUNEURS......mambo yalikuwa holele ndio maana kwenye EPA unakuta watu ambao hawaajawahi hata kuwa SME"S GHAFLA WANAPATA BILIONS...do you think they can manage the money apart from ordering the latest cars every time the new brand arrives....imagine wanashindana na watu kama bakhresa ...au mengi...kuagiza new brand ?.everything has to go step by step....

In conclussion lets not discourage local investors who seek to invest there money locally by branding them names...we are poor one of the reason is our ecomomy is controlled largely by foreigners......if locals show up..be it massawe,mengi,rostam,lowassa et al......tuwaache wawekeze nyumbani...munataka wapeleke south africa????? tuache midomo midomo.....zuia ufisadi..tupambane usitokee..lakini usizuie investments!!!!!....nashauri pitieni historia za nchi kama India,china ..russia MUONE namna walivoweza kuwezesha uchumi wao kushikiliwa na wafanyabiashara wazawa....

kwenye azimio la arusha tulisema "NJIA ZOTE KUU ZA UCHUMI KUMILIKIWA NA UMMA"""

nadhani tuje na azimio jipya "NJIA ZOTE KUU ZA UCHUMI KUMILIKIWA NA WAZAWA"

WAZAWA NI NANI"??? mTANZANIA kwa asili na kuzaliwa...HAIJALISHI RANGI ...!!!

Mzee IDD SIMBA anayo paper nzuri sana juu ya kuibua wazawa!!!!....nakumbuka wakati siasa za mageuzi zinaaza hii ndio moja ya sera nzuri ya wapinzania ambayo CCM wanajitahidi kuiiba lakini wanakosema utekelezaji...tushirikiane kama taifa kuiandika na kuitekeleza vema sera ya UZAWA!!!
 
Haa! sidhani jibu ni ndiyo kwani unapopata ndamu huyo wewe umeshaarithrika kwa kumkosa ngo'mbe wako(psychologically and materially).
 
Angalia Baadhi ya watanzania tulivyokuwa naive kiasi hiki ,halafu tunakaa na kusikitika eti viongozi wetu si waadilifu, ni sisi baadhi yetu akili zetu ni vivu zilizojaa vumbi eti kama ananzisha hiyo Tv hapo arusha ni vyema kwa faida ya Taifa ,wanasahau kujiuliza nini lengo lake hasa la badae ?kuna masuala mingi ya kujiuliza hasa baada ya matokeo yanayoendelea kuhusu ufisadi zidi ya badhi ya viongozi.
 
Umenikuna kwa hoja yako.Kama Watanzania wote mnaosoma hoja za JF mna nia njema na nchi hii msishabikie kabisa EL kuanzisha TV kwa si kwa nia njema kwa anachowaza yeye ni uongozi tuu wa nchi hii wakati ni fisadi na ni mtu wa visasi.Naomba sana CHADEMA,MENGI na Waandishi makini tushirikiane tuhakikishe mafisadi hawatambi katika nchi hii.EL na mafisadi wenzake ni kama MOBUTU,ABACHA na wahujumu wengine wa uchumi wa nchi zao.Mungu ibariki TZ.

Ni vizuri akianzisha hiyo TV Station watanzania wapate ajira. Kumuhukumu mtu kwamba ni fisadi ni makosa makubwa, kama ni fisadi mbona hamkumfungulia kesi mahakamani akahukumiwa huko, acheki chuki binafsi na roho za kwanini na kuhukumu watu ovyo mtoe ushahidi.
Mtanzania akiwa na pesa kwa vile ni kiongozi basi mnamwita fisadi bila kuwa na ushahidi wowote. Tembelea Monduli uone maendeleo yalioletwa nae na ongea na wananchi wa jimbo lake uone anavyokubalika kutokana na misaada anayoitoa kwa wananchi wake. Wahukumuni wengine na ushahidi mtoe lakini sio Lowassa hapo mtachemsha.
 
...wabongo wanapenda sana kufanya mambo kwa majungu na kulaumu pasipotakiwa,huyu lowassa kama ni fisadi na kawaibia kwa nini asifikishwe mahakamani? simtetei lakini sioni sababu yeyote ya kuangalia kila anachofanya kama ni motive ya kuchukua nchi tuu...na kama kweli ni fisadi na ana nia ya kuchukua nchi ni bora kuliko kuachia serikali iliyopo kuendelea maana wameshindwa kazi yao na hawana tofauti na hao tunaowaita mafisadi na wezi,tatizo ni hao waliopo madarakani sasa ambao inaonekana wana kila ushahidi wa Lowassa kuwa fisadi lakini wameshindwa hata kumfungulia mashtaka na kubaki kutupigia majungu tuu
 
Alishanunua RAdio 5 ya Arusha. Mikakati ndio hiyo.Sii ajabu akaibukia mgombea binafsi.
 
Alishanunua RAdio 5 ya Arusha. Mikakati ndio hiyo.Sii ajabu akaibukia mgombea binafsi.
Wewe Bwana, anunue tu ziwepo nyingi hizo. Tupo wengi hivi sasa- unafikiri sote tunaweza kujibanza ITV na kwa Tido tu. Wacha wigo upanuke - tunahiataji ajira Bwana.
 
Wakuu kuna move inafukuta kwa kasi kabisa kuhusu issue hii. Nadhani sasa huo mpango ambao mmoja wetu aliubandika hapa sasa unaokena kuwa uko kwenye operational stage na hata wana uslama wanashindwa kuuzuia. Sasa hivi jamaa anachukua watangazaji TBC anakomba mmoja mmoja, na watu wanamiminika arusha as we speak. Radio itakuwa operational in a short moment na TV itakuwa tayari as soon as December.
Maandalizi ya 2010 na 2015 yameanza.
 
Haya ni maendeleo watu watapata habari na habari zitawafikia watu wengi kwa karibu. Hatua kama hii tunaikaribisha.
 
Hiyo bomba bwana, kama ameamua kuwekeza nchini hiyo jamaa namfagilia kuliko wazee wa vijisenti wametuibia lakini hatuoni kuwekeza zaidi ya kugawa umaskini kwa dada zetu.

Lowasa Hureeeeeeeeeeeeeeeee
 
Back
Top Bottom