Lowassa Kuanzisha ABC Television Arusha

Superman

JF-Expert Member
Mar 31, 2007
5,695
1,696
Source:

Daily News, Friday, 24th October 2008, Page 22.

Public Notice

Application for Content Services Licences (Broadcasting Licences) to TCRA.

Name of Station:
ABC Television
P.O. Box 11843
Arusha

Shareholders:
Robert Francis Lowassa (Tanzanian) - 60%
Elias Stephen Kordun Lukumay - 40%

Who is Robert Francis Lowassa and Elias Lukumay?

Source: www.parliament.go.tz/Polis/PAMS/Docs/HS-4-44-2006.pdf

BUNGE LA TANZANIA
________
MAJADILIANO YA BUNGE
________
MKUTANO WA NNE
Kikao cha Arobaini na Nne – Tarehe 16 Agosti, 2006
(Mkutano Ulianza Saa Tatu Asubuhi)
. . . . . .
SPIKA: Sina shaka mtakubaliana nami Waheshimiwa Wabunge kwamba, hiyo ni hoja kabambe ya kuahirisha Bunge. Kabla sijawahoji, kuna matangazo mafupi yafuatayo:-

Napenda tutambue kuwepo kwa familia ya Mheshimiwa Waziri Mkuu, Mheshimiwa Mama Regina Lowassa, Bwana Fred Lowassa, Bwana Robert Lowassa na Master, kwa hiyo, huyu ndiyo mdogo mdogo tu Richard Lowassa. Wale ambao mmeshiriki vizuri kwenye Bunge na mnahudhuria mara kwa mara, mtakumbuka kwamba, Richard si mgeni sana, hapa kwa sababu mara kwa mara tunaonana naye pale nje, sielewi Mwenyezi Mungu, mambo haya sijui yanakuwaje? Hatujui hatma ya Richard, lakini Mungu aendelee kumsaidia inaelekea anapenda sana Bunge. Pia marafiki zao Bwana John Bakilana na Bwana Elias Lukumai. Karibuni sana na ahsante kwa ushiriki wenu.
. . . . . . . . . . . .

Last week ABC Television waliitwa na Bodi ya TCRA kwa ajili ya Interview ya Kupewa Leseni . . . . .

Habari ndo hiyo . . . . . .
 
HATARI tupu! Mwishowe tutasikia wameinunua na TBC kama sio kujimilikisha kijumla. Yote hayo ni katika maandalizi yaleee kama sio 2010 basi 2015! Yetu macho!
 
Source:

Last week ABC Television waliitwa na Bodi ya TCRA kwa ajili ya Interview ya Kupewa Leseni . . . . .

Habari ndo hiyo . . . . . .

Superman
Hiyo ni HABARI NJEMA sana.
Hiyo TV IKITUMIWA VEMA, NI KWA MAENDELEO YA TAIFA LETU.
 
Vinginevyo wangeziacha visiwani Jersey kama mzee wa vijisenti au wangenunua nyumba mpaka za mashemeji USA kama Ballali, bora watumie nyumbani.
 
mwizi akikuibia ng'ombe akaenda akamtunza vizuri na hatimaye ng'ombe akawa na ndama, halafu mwizi huyo huyo akaja kukuuzia maziwa na ndama yule wakati unajua ng'ombe mwenyewe alikuwa wa kwako utashukuru kwa ukarimu wake?

majibu yanaelekea kuwa ni 'Ndiyo' kwa sababu tu hakumchinja yule ng'ombe!
 
Kwa kweli kama ni kwa nia njema, hakuna ubaya kwa Lowassa kuanzisha TV popote iwe Dar ama Arusha. Lakini jambo moja ambalo lazima tuliangalia kwa makini ni kwamba hawa jamaa wamepania kuchukua nchi. Mind you "kuchukua nchi" na hawatanii, mnataka ama hamtaki. Kilichompata Lowassa na wenzake, wameona ni kutokana na nguvu ya media. Wameamua sasa na mumesikia ama kuona, magazeti kibao yakiongozwa na ununuzi wa New Habari. Wamenunua Channel Ten. Hatua itakayofuata na ambayo mchakato umeanza ni kuwadhibiti wamiliki wa vyombo wanavyoona itakuwa kikwazo kwao ikiwamo IPP Media.

Kwa ufupi ni kwamba kama tukiwa makini kidogo tu tutabaini kwamba, Tanzania yetu inaelekea kubaya. Tunajua kila mtu ana haki ya kutawala, lakini si urithi Mwalimu Nyerere aliotuachia kwamba uongozi ni kwa wenye fedha na vizazi vyao. Nawaambia hata ndugu zangu humu (Nawafahamu) ambao wana nia njema ya kuja kuingia katika siasa kihalali (wakiwamo wanaoshabikia EL kuanzisha TV) wajue kwamba bila fedha (za rushwa) hawatashinda kutokana na mfumo uliojikita na unaoendelea kuimarika vinginevyo wawe vibaraka wa wenye fedha. Hii ni HATARI sana na hapa tukijadili mambo tuangalie huko (2010-2020) maana wenzetu wamejipanga hivyo na kwa gharama zozote zile ikibidi hata za HATARI (nitajadili kwa wakati).
 
Vita ya fikra ni ngumu kuliko ya risasi za moto. JF ni mfano dhahiri. Kwa vile Rome haikujengwa kwa siku moja, basi nasisi tutafika tu. Walikuwepo kina Shah Iran, wakapotezwa, wakawepo kina Marcos Philippines nao wakapotezwa, its only a matter of time.

The clock is ticking.... The writting is on the wall.
 
Niliposema mafisadi watashinda.... sikuwa natania.. sisi wengine ni mabingwa wa kulalamika mno; aidha tuwekeze nguvu zetu kwenye urithi wetu au tuwaache watutawale wapendavyo!
 
Niliposema mafisadi watashinda.... sikuwa natania.. sisi wengine ni mabingwa wa kulalamika mno; aidha tuwekeze nguvu zetu kwenye urithi wetu au tuwaache watutawale wapendavyo!

Kesho utasema kuwa utapigana hadi mwisho, no retreat no surrender. Huna msimamo. Hueleweki licha ya kuwa huaminiki, ona hapa.
 
mafisadi watashinda kwa sababu wamejipanga vizuri, wanajua wanachokitaka, wanajua what is at stake (nafasi yao), na zaidi ya yote wana nia isiyo na shaka ya kufikia malengo yao.

Na hawalali, wako makini wanawatizama. Najua kuna watakaobeza lakini wajue wako makini sana. Hapa Arusha nilipo kwa sasa wamewasiliana na wanafuatilia kwa makini tunachojadili na mtasikia ama kuona wanavyojipanga wakizingatia kwa makini mjadala huu. Watu wako kazini, kina MM wanajitutumua tu wakitegemea "Malipo kwa vizazi vyetu vijavyo" wakati jamaa wanahesabiwa muda wao wa kukesha, na wazee wakiamka wanapata briefing ya nguvu.
Currently Active Users Viewing This Thread: 31 (7 members and 24 guests) Halisi, Ipole, Maverick, Mtu wa Kawaida, Quemu, Rubabi
 
- Lowassa alipokuwa Waziri Mkuu, alikuwa anahaingaika kumjibu kuanzia kwenye magazeti, mpaka humu JF kumjibu member mwenzetu Mwanakijiji, ilikuwa ni kwa sababu haaminiki, haeleweki, na hana msimamo!

- Na juzi Rostam, alikuwa anahaha kumtafuta Mwanakijiji apunguze mashambulizi, kwa sababu haeleweki, haaminiki, na hana msimamo!

- Mkulu Mwanakijiji, I hope hukatishwi tamaa wala kuogopeshwa na hizi kelele za mlango, sio siri kwamba kuna wasioweza kuelewa masilahi ya taifa na ya binafsi, lakini kwenye demokrasia hatuna jinsi ila kuwa nao tu, lakini mapambano yanaendelea. Kuna ishu ambazo sikubaliani na Mwanakijiji, lakini sio kupiga vita ufisadi, kwenye hili tupo pamoja mkuu MMJ, na job welldone keep it up!

Respect.

Wazee wa sauti ya umeme FMES!
 
FMES mimi nafikiri hapo umeweka bayana na sidhani kama kuna chengachenga maana kama Antenna basi ipo clear mno. Watu kelele sana na nafikiri tunashindwa kutofautisha maslahi ya taifa na maslahi binafsi ila natumaini MKJJ na sisi wengine wala hatutochoka kwenye kupambana mpk mwisho. Ila nasema hivi HUYU JAMAA HATA KAMA ATAFUNGUA CNN LAKINI WANANCHI SASA HIVI TUMESHANAWA USO HAKUNA TONGOTONGO TENA
 
Wafungue TV mikoa yote mpaka vijijini lakini watambue kuwa hakuna ambaye anaweza kushindana na nguvu ya UMMA. Itakuwa kama Fisadi RA alipochapisha matoleo 2 ya gazeti lake kwa siku moja. Haisaidii lolote, wakileta fyokox2 watakula MBOKO kama kawaida. Mtanzania wa leo si wa kudanganywa kwa kupewa godoro eti akupe kura tu. Watachukuwa magodoro na kwenye Kura watalala CHALI.

Kwa hiyo waanzishe TV, that's fine lakini wafuate maadili ya uandishi wa habari. Wakiendekeza ya New Habari Corporation then hakuna ambaye atafungua channel(s) yao.
 
mwizi akikuibia ng'ombe akaenda akamtunza vizuri na hatimaye ng'ombe akawa na ndama, halafu mwizi huyo huyo akaja kukuuzia maziwa na ndama yule wakati unajua ng'ombe mwenyewe alikuwa wa kwako utashukuru kwa ukarimu wake?

majibu yanaelekea kuwa ni 'Ndiyo' kwa sababu tu hakumchinja yule ng'ombe!

Hapa sijakuelewa naomba ufafanuzi kama ikiwezekana. Maana anaweza kuku-uzia maziwa ambayo yako genetically modified hili uwe zezeta zaidi na aendelee kukuibia au kusahau kudai haki zako.

A lie, if audacious enough and repeated enough times, will be believed by the masses.
 
Katika vita Ngumu ya kupata Uhuru, tanzania hatukumwaga damu japo baadhi ya mababu zetu walimwaga damu.

Nina uhakika katika vita hii ya Kiuchumi na Kifikra tutashida. Kila kitu na wakati wake na Zama zake.

Time. Time. Time will tell. And soon and very soon all will be clear.

God Bless Tanzanians!
 
Back
Top Bottom