Lowassa Kuanzisha ABC Television Arusha

Tatizo letu nini sisi wa-tz? Kwanini tuhoji uwezo wa mtu eti kwa sababu kajitokeza kuwekeza humu nchini! Kwani kuna wateule wa ktk kumiliki media au kisa ni lowasa's family? Tumeona hapa ndani zain wamesulubu wa-tz na jamvi ndio venue ya kwanza kulalamikia hili jambo, sasa mmasai/mmeru amewekeza na kuashiria ajira kwa wenzetu wenye taaluma hizo imekuwa soo na minong'ono isiyo na tija.

Binafsi naipongeza familia ya lowasa kwanza kwa kuthubutu kwa ujasiri kuishi ktk maisha ya kawaida na kujihusisha na shughuli za kawaida kama watanzania wengine walio na fursa.

Pili kitendo cha kuanzisha stesheni ya runinga hilo jambo jema na ukombozi wa kijamii hususani pale tunapotaka huduma za msingi za kijamii ziwasogelee wananchi wote.

Mzee edward ngoyayi lowasa, simama ktk kile unachoamini kwa faida ya wote. Kila la heri abc tv
 
Acheni roho mbaya ya chuki,mbona fisadi nyangumi anamiliki televisheni 3,redio 3 na magazeti lukuki na hamzungumzi habari zake?Kuweni wabunifu katika masuala ya kuendeleza Taifa letu si kuangalia fulani kala nini!

hata mimi mwenyewe na shindwa kuelewa hawa wanaopinga EL kuanzisha TV.nadhani wanatumiwa na PAPA a NYANGUMI.
 
Vita ya fikra ni ngumu kuliko ya risasi za moto. JF ni mfano dhahiri. Kwa vile Rome haikujengwa kwa siku moja, basi nasisi tutafika tu. Walikuwepo kina Shah Iran, wakapotezwa, wakawepo kina Marcos Philippines nao wakapotezwa, its only a matter of time.

The clock is ticking.... The writting is on the wall.

Jamani pamoja na siasa, nawapongera watanzania wote ambao wanawekeza hapa nyumbani. Uchumi wetu hauwezi kujengwa na the so called 'Wawekezaji' utajengwa na sisi wenyewe. Hivyo wote wenye vijisenti please fungulieni watoto wenu miradi mikubwa. Taratibu na sheria zote za nchi zitumike kuwaangalia, kukikwamua ni sisi WENYEWE.
 
hivi wewe unamjua Mwanakijiji vizuri kweli? kwa taarifa yako Mwanakijiji ni Ndumilakuwili achelewi kukugeuka mda wowote,pia anatumiwa na baadhi ya watu kwenye shughuli zao.Hivyo kuweni makini nae sana hasa Thread zake anazo anzisha ilikupima upepo wenu then anapeleka report kwa wahusika.be care full guys.

Josm,

Mwenzetu hata Kiswahili hufahamu. Wahaya wanasema "Usijigambe mbele ya Wagambirwa". Sasa nani hapa kasema ANAMJUA Mwanakijiji? Anayemjua Mwanakijiji ni Mkewe (na nyumba ndogo kama zipo au X-Wake). Hapa wengine wanamfahamu tu Mwanakijiji.

Maandishi ya mtu kwa asilimia kubwa huonyesha huyo mtu ni wa aina gani. Mwanakijiji yuko USA, FMes yuko USA, una uhakika gani hawa watu hawafahamiani? Pia juzi tu FMes aliandika kuwa alionana na Mwanakijiji Tanzania. Humu kwenye mtandao wapo karibu kila siku ya Mungu. Je unauhakika kuwa hawana mawasiliano zaidi ya haya ya wavuni?

Sasa tuje kwako. Wewe ni secretary wa Mwanakijiji? Maana inaonekana unafahamu hadi anatumiwa na nani? Nani anamlipa hela? Yeye ni ndumilakuwili, je ulishaona hivyo vichwa vyake vyote na kuthibitisha hivyo?

Kama kuna mtu atasema kuwa ANAMFAHAMU mwanakijiji na nisipinge basi hapa wavuni wanafahamika na katika hao wewe haumo maana ungelikuwemo, basi ungelikuwa unafahamiana na FMes na Mwanakijiji pia na usingeliandika PUMBA nyepesi kama hizo juu ambazo hata Nguruwe mwenye njaa atakataa kuzila.
 
Kila aliyefanikkiwa ana siri yake. Menge , manje na wengine. Wanasiasa inaeleweka moja kwa moja hamna siri ni matumizi ya vyeo vyao. Sasa tunasubiri matonya afungue tv ndio tuseme ni sawa??
 
ufisadi,alikuwa anakosa pa kusemea,sasa tusubiri.Tutayajua mengi tu nduguzanguni!!
 
kwa mwamko ulioanza kujengeka ndani ya wananchi, mimi naimani mafisadi tutawashinda tu ! ni suala la muda tu.
 
Josm,

Mwenzetu hata Kiswahili hufahamu. Wahaya wanasema "Usijigambe mbele ya Wagambirwa". Sasa nani hapa kasema ANAMJUA Mwanakijiji? Anayemjua Mwanakijiji ni Mkewe (na nyumba ndogo kama zipo au X-Wake). Hapa wengine wanamfahamu tu Mwanakijiji.

Maandishi ya mtu kwa asilimia kubwa huonyesha huyo mtu ni wa aina gani. Mwanakijiji yuko USA, FMes yuko USA, una uhakika gani hawa watu hawafahamiani? Pia juzi tu FMes aliandika kuwa alionana na Mwanakijiji Tanzania. Humu kwenye mtandao wapo karibu kila siku ya Mungu. Je unauhakika kuwa hawana mawasiliano zaidi ya haya ya wavuni?

Sasa tuje kwako. Wewe ni secretary wa Mwanakijiji? Maana inaonekana unafahamu hadi anatumiwa na nani? Nani anamlipa hela? Yeye ni ndumilakuwili, je ulishaona hivyo vichwa vyake vyote na kuthibitisha hivyo?

Kama kuna mtu atasema kuwa ANAMFAHAMU mwanakijiji na nisipinge basi hapa wavuni wanafahamika na katika hao wewe haumo maana ungelikuwemo, basi ungelikuwa unafahamiana na FMes na Mwanakijiji pia na usingeliandika PUMBA nyepesi kama hizo juu ambazo hata Nguruwe mwenye njaa atakataa kuzila.

Nakubaliana na wewe kuwa sikijui kiswahil.Unajua siku zote huwa na sema mtu usiongee kitu usicho kijua usije jikuta kwenye matatizo bure.najua wewe unamshabikia Mwanakijiji kwa kuwa makala makala zake zina kuvutia,ungejua yeye anatumiwa hizo na makala halafu yeye ana copy na kupaste hapa.sitaki kuongea mengi kuhusu Mwanakijiji nisije onekana nina nia mbaya nae au nime tumwa,maana waswahili hamchelewi.maandishi ya rangi nyekundu hapo juu: hapa atupo kutukanana au kakashifiana bali tupo kujenga hoja na kuelimishana pamoja na kukosoana.
 
Hii ni hatari! Lowassa anataka kuwa RAIS wa nchi hii kwa gharama yoyote ile. Anataka kununua urais. Lakini ukiacha kashfa zake nyingi za UFISADI (hata Mwl Nyerere alimshtukia) mtu huyu ana uwezo kweli wa kuongoza taifa hili? Lowassa na mwenzake ROSTAM AZIZ (Muajemi) wana agenda gani hasa? Hawa wawili ni watu hatari sana kwa usalama wa taifa hili. Agenda yao kuu ni kujilimbikizia mali kadiri iwezekanavyo, utadhani wana mkataba na Mungu kuwa wataishi milele. Mtayakumbuka maneno yangu: Watu hawa hawafai kwani ni wezi wakubwa, wakipewa nafasi watawauza hata Watz wenyewe! Hebu waTz amkeni acheni kushabikia watu hatari kama hawa kuanza kumiliki vyombo vya habari.
Huyu Lowassa ni VINDICTIVE kupita kiasi. Nyie mchekeeni tu MTAJUTA KUMFAHAMU!
Lakini zaidi ya yote sio mtu intelligent. Ni mtupu sana kichwani. Hivi kwa nini waTz bado tunapenda kuongozwa na watu wasio ok kichwani? TAFAKARI!
 
Nakubaliana na wewe kuwa sikijui kiswahil.Unajua siku zote huwa na sema mtu usiongee kitu usicho kijua usije jikuta kwenye matatizo bure.najua wewe unamshabikia Mwanakijiji kwa kuwa makala makala zake zina kuvutia,ungejua yeye anatumiwa hizo na makala halafu yeye ana copy na kupaste hapa.sitaki kuongea mengi kuhusu Mwanakijiji nisije onekana nina nia mbaya nae au nime tumwa,maana waswahili hamchelewi.maandishi ya rangi nyekundu hapo juu: hapa atupo kutukanana au kakashifiana bali tupo kujenga hoja na kuelimishana pamoja na kukosoana.
duh hio tuhuma nzito,you need to be more open.i would like to know nani anamtuma na for what purpose etc
 
hivi wewe unamjua Mwanakijiji vizuri kweli? kwa taarifa yako Mwanakijiji ni Ndumilakuwili achelewi kukugeuka mda wowote..

Kudos kwa kuligundua hilo.

Mwenyewe anajijua na alishasema wanaofuata kila anachoandika ni stupid, lakini hawakomi. We waache, watakuja kufa kama walivyokufa wafuasi wa Kibwetere.
 
Jamani pamoja na siasa, nawapongera watanzania wote ambao wanawekeza hapa nyumbani. Uchumi wetu hauwezi kujengwa na the so called 'Wawekezaji' utajengwa na sisi wenyewe. Hivyo wote wenye vijisenti please fungulieni watoto wenu miradi mikubwa. Taratibu na sheria zote za nchi zitumike kuwaangalia, kukikwamua ni sisi WENYEWE.

Tatizo uwekezaji TZ haumlindi mzawa badala yake unamlinda mgeni. Ndiyo sababu wawekezaji wengi wa nje wanatanua Bongo. Vilevile hii ndiyo sababu wazawa wengi wenye pesa hawawekezi badala yake wanatafuta shares kwa wawekezaji wa nje. Sasa ukiona hawa jamaa pamoja na kuwa na pamoja na TZ kuwa na opportunities nyingi lakini wao wanakimbilia kwenye habari ni jambo zuri kama tukaangalia sababu. Je wana nia njema katika hivyo vyombo vya habari??? Nchi maskini kama TZ kwa nini tunakuwa na TV station, magazeti na redio nyingi kuliko hata South Africa. Kweli hawa jamaa wanataka kutuambia kuna pesa kiasi gani huko mpaka wote wapate faida?? Mfano mzuri wa kuanglia ni TV Africa, kwa nini hawakufanikiwa na hawa jamaa walikuwa wanarusha matangazo Africa nzima?? Sasa kama kuna watu wanaamini hawa jamaa wanatuletea maendeleo kwenye TV, Ok!!!!....................
 
Yessir,

subiri ina kuja orodha ya member wa JF wanao tumiwa ha baadhi ya watu hapa,
 
Source:

Daily News, Friday, 24th October 2008, Page 22.

Public Notice

Application for Content Services Licences (Broadcasting Licences) to TCRA.

Name of Station:
ABC Television
P.O. Box 11843
Arusha

Shareholders:
Robert Francis Lowassa (Tanzanian) - 60%
Elias Stephen Kordun Lukumay - 40%

HIvi ni wapi wameandika Rober Francis Lowassa ni Edward Ngoyai Lowassa??
 
Nakubaliana na wewe kuwa sikijui kiswahil.Unajua siku zote huwa na sema mtu usiongee kitu usicho kijua usije jikuta kwenye matatizo bure.najua wewe unamshabikia Mwanakijiji kwa kuwa makala makala zake zina kuvutia,ungejua yeye anatumiwa hizo na makala halafu yeye ana copy na kupaste hapa.sitaki kuongea mengi kuhusu Mwanakijiji nisije onekana nina nia mbaya nae au nime tumwa,maana waswahili hamchelewi.maandishi ya rangi nyekundu hapo juu: hapa atupo kutukanana au kakashifiana bali tupo kujenga hoja na kuelimishana pamoja na kukosoana.

1. Ni kweli Kiswahili hukijui ila UNAKIFAHAMU.

2. Mie siyo Mshabiki wa mtu yeyote hapa. Alipoleta makala yake ya kumsifu Sofia Simba, nilikuwa mmoja wa wapinzani kwani ninaamini kuwa mama huyo alinnua ushindi.
3. Kwamba anatumiwa makala zake, si kila mtu anafahamu hilo? Mbona hata yeye huandika juu ya hilo? Hivi anaposema KA-INZI nimekarusha na kameleta habari mwenzetu huwa UNAELEWA au alikuacha Solemba? Kwama anaishi USA si kila mtu anafahamu hilo? Sasa atapataje habari za Tanzania na yeye yuko USA kama si KA-INZI kumtumia habari?
Pia si kweli kwamba habari zake anazi-copy na kupast tu. Kwa kufahamu kwangu mie, MJKK anapata habari zake nyingi sana kwa nyia tofauti. Anatumia kila uwezekano uliopo ili kuzipata. Nyingine anazipata humuhumu wavuni au kwa msaada wa wana JF na nyingine ana chanel zake. Kama wee unaona ni RAHISI kiasi hicho, basi si na wewe kuwa Mzee wa data hapa? Tutakushangilia sana kwa kutupa habari ila hatutakuwa mashabiki wa kuburuzwa pale unapotupa feki.

4. Mwisho wee unaogopa watu watasema "umetumwa..." wakati huo unamkalia kooni Mwanakijiji kuwa "anatumwa..." Mkuki kwa nguruwe siyo?
Sawa mzee naona wewe pia UMETUMWA ...... upppss tayari nimesema.

5. Maandishi ya Rangi nyekundu ni kupinga hiyo namba 4 hapo juu.

Wanasema USIRUSHE MAWE kama na wewe waishi nyumba ya Vioo.

Zaidi ya hapo nakubaliana na wewe kuwa tupo hapa kuelimishana na si KUKASHIFIANA. Kwa hiyo, au uliza utajibiwa na siyo kuanza kurusha shutuma zisizo na kichwa wala miguu. Ukiulizwa THIBITISHA utaweza? Hapa tupo kumkoma nyani, mengine wala si muhimu sana.
 
Ni kweli jamaa wanajipanga vilivyo with long term strategies. I think it could be unthinkable if we accept defeat and give them space to implement their evil whims.I still believe things will change for better, and such discussions as here are one step towards that achievement.Kama mtotoanavyoanza kutambaa kabla hajatembea, ndivyo nasi taratibu kwa kuelimishana na kujua extent ya uovu unaondlea tunaanza kufumbuka macho. Siku moja tutaweka pembeni hili blangeti jeusi linalotaka kutia upofu macho yetu kuona tunachotakiwa kuona, inshallah
 
Back
Top Bottom