Curriculum Specialist
JF-Expert Member
- Oct 8, 2007
- 2,732
- 750
Mtuhumiwa Mashuhuri wa Richmond ataongea muda si mrefu bungeni, kumbukeni hii itakuwa ni Mara ya pili kuongea bungeni toka achaguliwe 2010!
Ni kauli aliyoitoa wakati akichangia bungeni na kutoa tahadhari kama viongozi hawawezi kufanya maamuzi na wao wakajiunga kwenye kundi la kulalamika, hali hii inaashiria kuwa na nchi ya malalamiko, viongozi wachukue hatua badala ya na wao kulalamika.
Kaongelea issue za ajira kwa vijana, Elimu na miundo mbinu; lakini hao aliowaambia wanaambilika?
Monday, November 4, 2013
Edward Lowassa.![]()
Katika hali isiyo ya kawaida, Waziri Mkuu aliyejiuzulu, ambaye huongea kwa nadra bungeni, Edward Lowassa leo amenguruma na kutaka taifa kuacha kuweka vipaumbele vingi visivyotekelezeka kwa wakati.
Alitaka serikali kuweka nguvu katika vipengele vichache vya msingi kama ajira, afya, elimu na miundombinu.
Aliwapongeza mawaziri John Magufuli kwa kuimarisha barabara na Dk. Harrison Mwakyembe kwa kubuni mbinu za kupunguza foleni jijini Dar es Salaam, alizosema zinachangia kuharibu uchumi kwani watu wengi wanakaa barabarani badala ya kufanya kazi.