Kujua au kufahamu kuwa lowasa hafai kuwa kiongozi wa nchi hakuhitaji kuvaa miwani ya kuona
Heko kwa Mwanakijiji kwa mada nzuri. Story yako imenikumbusha ya mitaani, kwa zaidi ya mara 3 sasa tangu NEC ya CCM itoe taarifa yao fupi, Nimeshuhudia taflani mitaani kwenye vimeza vya Magazeti pale anapo jitokeza mtu Kumsifia Lowassa kwamba jamaa anafaa....... ehhhhhhhhh..... analaluliwa kama nini bwana!
Haya tusonge mbele na mada,
Sijawahi kusikia Mh Lowassa akisema jambo lolote linalo husu tatizo la wizi wa fedha za Wananchi (UFISADI)!
Tatizo letu kubwa Watanzania ni
1. UFISADI (Wizi wa fedha za wananchi)
2. RUSHWA (kutokupata haki na kusababisha hasara kwa wananchi na Watanzania kwa ujumla kama rushwa inahusisha miradi mikubwa ya Kitaifa)
Miaka ileeeee,, Nyerere alisema adui wakubwa kwa Watanzania ni
1. Maradhi
2. Ujinga
3. Umaskini
Kwa sasa idadi ya maadui imeongezeka na kubwa kuliko zote ni UFISADI. Hata hivyo, ili tuepuke na maadui hao nyenzo aliziona wakati ule na bado zinafaa, soma hapa chini
Ili Taifa lisonge mbele tunahitaji vitu vine
1. Watu; Kwa sasa watu tunao
2. Ardhi; Ardhi inazidi kuporwa na wachache
3. Uongozi Bora; Kwa sasa hatuna
4. Siasa Safi; Kwa sasa hili ni janga
Angenda ya kutokomeza ufisadi iwe namba moja na isiwe tu kuitaja! Bali anaye taka urais atuwekee yafuatayo
1. Plan and time frame(namna gani atashughulikia na kwa ratiba maalum)
2. Implementation strategies (atalitekeleza kwa taratibu zipi, yepi yatakayofanyika kukomesha UFISADI)
3. Monitoring and Evaluation (Namna gani atafanya tathimini ya mafanikio)
Yeyote anaye utaka Urais aje na agenda na utekelezaji wake kama nilivyo ainisha hapo juu, hakuna bla bla.... matumaini hewa ya Kikwete 2005 yanatosha! This time tuwe wazungu zaidi, hakuna Ubongo bongo!