Lowassa Hafai! Yes I said It - Sababu ya I

Lowassa Hafai! Yes I said It - Sababu ya I

Ukweli ikiwa Edo ataupata uraisi itakuwa ni janga la kitaifa . Kwa nini

(1) Lazima hao marafiki zake waliomchangia watataka kurudisha hela zao na yeye pia atataka kurudisha fedha zake alizotumia kwani kila mtu anajua jinsi alivyomwaga fedha kununua kuungwa mkono. Wote tunajua hakuna atakayetoa hela yake bure bila kujua atazirudisha vipi kwani kama ungekuwa ni msaada basi hata hao watoa msaada wangeweza kunipa mimi nipeleke kanisani na msikitini lakini hawakufanya hvyo kwani walikuwa wanajua wanachokitafuta kupitia kwa Edo. Uraisi wake utakuwa wa kununua na si vinginevyo. Angalia tangazo la kwenye gazeti la Mwananchi la tarehe ya leo 26/5 ni tangazo la bei mbaya. Kizuri kinajiuza kibaya kinajitangaza.

(2) Uraisi wake utaongeza mpasuko ndani ya chama cha mapinduzi na serikalini hasa kwenye vyombo vya usalama na kutakuwa na kulipiza visasi na kuhujumiana sana kuonyesha kila upande ulivyo na uwezo mdogo wa utendaji jambo litakaloongeza gharama za uendeshaji na matumizi mabaya wa taasisi za serikali

(3) Kutokana na mambo hayo mawili ufanisi wa serikali na vyombo vyake utakuwa mdogo sana hivyo uchumi utayumba, rushwa itaongezeka sana na itatuumiza, kutakuwa na Serikali ya kulazimishana na kutokana na hilo vyama vya upinzania vitapata nguvu sana (4) Kuongezeka kwa nguvu ya vyama vya upinzania kutafanya Serikali izidi kuwa ya kigandamizi kuua kabisa haki za msingi za kiraia. Hivyo fedha nyingi sana na nchi zitatumika kwa ajili ya kugandamiza haki za binadamu badala kulipia gharama za maendeleo.

Kitendo cha kusema eti kama angeendelea kuwa Waziri Mkuu hii nchi ingekuwa na maendeleo zaidi ni kitendo cha kuiponda Chama Chake na Serikali iliyoko madarakani ambayo ni kitu kibaya sana kwa mshikamano wa Chama na Serikali. Sidhani kitu hicho kitavumiliwa na Watanzania wenye nia njema na nchi hii.

Vile vile kule kusema kuwa eti walimvizia Mkurugenzi wa Kampuni ya Maji ili wamfukuze kabla hajaenda mahakamani kupata zuio la kimahakama inaonyesha kabisa akipata Urais atakuwa Rais wa namna gani. Kila mtu awe mtanzania au sio ana haki ya kupata haki yake kupitia mahakami na hairuhusiwi Serikali wala mtu yeyote kuzuia haki kwa sababu yeyote.

Ninaomba Watanzania watafakari hilo.

ndio maana sisi wengine wenye maono ya mbali tunataka ateuliwe na chama chake kugombea uraisi ili huo mpasuko utokee na hatimaye "dubwasha" CCM life.
 
Sipati picha endapo kweli mamvi atakuwa raisi!!!
Mwakyembe, Sitta, Nape,Kirango, mzee Malecela, Maropu etc Hawa lazima wahame nchi
 
EL hafai kabisa tena hata wenyewe ndani ya CCM wanajua kuwa hafai. Labda unaweza ukaniuliza hafai kwa lipi au yepi??
1. Siyo msafi ndani ya chama hata nje ya chama. Rejea kauli ya Hayati Baba wa Taifa juu ya huyu ndg yetu.
2. Ametengeneza maadui wengi walio ndani ya mfumo rasmi wa kiutawala, hivyo ni hatari kwa mstakbari wa ustawi wa mfumo.
3. EL anaonekana kuwa amejipanga kinguvu kutinga Ikulu kwa ghalama yoyote kitu ambacho ni hatari sana kwa nchi.
Hivyo basi kwa sababu hizi chache naamini hawezi kupewa dhamana ya kukipigania chama.


mimi binafsi napendekeza tupate rais hasiye na marafiki wengi,ili akipata wasianze kupangana kwenye nafasi ili wakaibe,au tupate mgombea binafsi,
 
Kwa kuwa marais masikini wameshatuongoza vya kutosha,na wametufikisha tulipo. Kwa nini tusimpe urais tajiri ili nae tuone atatupeleka mpaka wapi!? Akizingua si tunammwaga tu muda ukifika!

Kufikiri kijima huku! Na tajiri akishindwa utasema ''tujaribu mwanamke'' na mwanamke akishindwa utasema ''tujaribu mwenye kitambi'' na mwenye kitambi akishindwa.... Hatuchagui rais ''kwa kujaribu''! Tunachagua rais ambaye tunaona anafaa.
 
Elimu jimboni kwake imemshinda , ataiweza nchi Nzima?
Mamvi akipata urais basi wakulima waandike wameumia hasa wale wa kilosa ambao kila uchao wanaugomvi Na wafugaji !
Huwezi kuwa Na elimu bora kama huna uhakika wa chakula !

huyu MWANAKIjiji anaonekana ana uchovu wa kilimo cha jembe la mkono bila elimu sahihi ya kilimo,lowasa atamsaidia,nina imani kwa mazingira ya kijijini huu ni muda wa kupiga komoni,chimpumu,gongo,ulanzi kisha kurudi nyumbani chakari na mabaki ya machicha kwenye mustachi,wala simshangai
 
Last edited by a moderator:
EDUCATION S POWER,UKIONA MSOMI AMAIBA UJUE ELIMU YAKE NI HAFIFU MAANA MSOMI ANATAFUTA FULSA MBALIMBALI ZA KUMPA KIPATO PASIPO KUIBA, mf angalia nchi kama china idadi kubwa ya wasomi wako kwenye tafiti kujipatia kipato ndani na nje ya nchi,sisi hatuna wasomi.

Sikatai elimu kuwa kipaumbele. Ninachosema hakuna kipaumbele kitafanikiwa ikiwa ufisadi hautashughulikiwa.

Kwenye ufisadi fedha za kujenga shule, vyuo na kuajiri waalimu wakutosha zitatoka wapi kwenye ufisadi? Je vitabu na vifaa na madawa ya maabara? Mikopo kwa ajili ya elimu ya juu?
 
mimi binafsi napendekeza tupate rais hasiye na marafiki wengi,ili akipata wasianze kupangana kwenye nafasi ili wakaibe,au tupate mgombea binafsi,
rais wa aina hiyo utampata kuzimu,hiyo timu ya kampeni na wapambe watakuwa wanaitwaje? naona unaishi nchi ya kusadikika
 
Semeni anayefaa. mnapoteza muda

Mkuu mleta mada kajikita kwa huyu Mh kutokana na ukweli kuwa ndy pekee ambaye mpaka muda huu amakamia kuingia pale pahala na hilo linathibitishwa na namna alivyo na anavyoendelea kujipambanua ndani na nje ya nchi. Sasa mi nadhani mpe nafasi kwanza amalize makala yake, kwa maana hii ni Part One ya EL. Tuwe ba subira mkuu mi naamini hili jamvi ni la GREAT THINKERS so let us be patient he will with the next.
 
edward-lowassa.jpg

Mzee Mwanakijiji mada yako nzuri na inajitosheleza.
Lakini mada inashindwa kuona the otherside of the coin.
EL alikuwa mwanamtandao, mtandaoni watu walikula yamini kuitawala nchi hii lakini hawakuwa na succsession plan baada ya Kikwete kutoka madrakani!

Tatizo lililodhahiri na linaonekana wazi ni kwamba uadui kati ya waliokuwa wanamtandao ni mkubwa hata kuliko uadui na vyama pinzani.
Its a do or die situation.

Lowassa anajua fika kuwa asiposhinda kinyang'anyiro cha urais, rais ajaye atamgeuza piriton.
The gentleman is between an stone and a hard place!
 
Last edited by a moderator:
Mwanakijiji ni team membe lazma ampinge lowassa kwa kila namna... hawa ndio walikuwa waanzilishi wa CCJ na kina Sitta... hana jipya huyu mtu ni mchumia tumbo tuu..
 
Kaka mukubwa masikio sasa yanataka kuzidi kichwa...! sipo na wewe,pamoja na kwamba moja kwa moja sifungamani na EL mpaka pale utakapo tokea m'badala otherwise bora EL kwa asilimia zote! Kuliko hawa wengine waliotangaza nia au wenye viashiria vya kushika nafasi ya juu ndani ya chama chao.

Hakika hizo ni chuki kama si chuki naomba jiridhishe...kwanza Tanzania mbali na changamoto nyingine shida kuu sio 'UFISADI' kama ambavyo mimi binafsi unataka niamini...io analysis kwamba shida yetu kuu ni ufisadi umejiridhisha nayo? au nikujiona wewe ni bora katika kutafakari m'badala wa wengine? Bado naamini Ujinga ambao dawa yake ni Elimu ndio shida yetu kuu,kwanini? arithmetic nyepesi tu,uwiano wa mafisadi na rasilimali zetu ni tofauti kubwaaa saaana,wataona wanaiba lakini katu amini nakwambia hawawezi maliza,sasa kwa nini nasema bado naamini changamoto yetu kuu bado ni Elimu,watu wetu wanatakiwa kusoma na kupata maarifa...time is coming!

Chambua bila kuonesha upande,kweli yawezekana EL hafai lakini katika hawa wanaoonesha nia nani unadhani anafaaa?maana rais lazima atoke miongoni mwetu,ukimkataa huyu na ukamkubali yule,uo uhalali wa sisi kumkubali uyo mwingine ni wako si wa jumuiya...nasisitiza mimi binafsi ufisadi sio shida kuu! ELIMU ELIMU ELIMU,huu wimbo sahihi kwa waTanzania

Think big! Utamalizaje ujinga bila nyenzo? Jibu ni huwezi. Hivyo yabidi uwe na nyenzo ndio uushinde ujinga! Fedha zilizopotea kwenye kashfa zote zilizotokea kwa kipindi cha miaka kumi iliyopita (zilizojulikana na zisizojulikana) zingetumika kwenye elimu tungekuwa na shule bora kabisa. Wewe unaona logic, kwa mfano, ya kuongeza majimbo ya uchaguzi wakati hatuna shule za kuridhisha? Again think big!
 
HIVI MWANAKIJIJI, kwani mtu akisema kipaumbele chake ufisadi inamaanisha kuwa vitu vingine havitafanyika?
 
Sikatai elimu kuwa kipaumbele. Ninachosema hakuna kipaumbele kitafanikiwa ikiwa ufisadi hautashughulikiwa.

Kwenye ufisadi fedha za kujenga shule, vyuo na kuajiri waalimu wakutosha zitatoka wapi kwenye ufisadi? Je vitabu na vifaa na madawa ya maabara? Mikopo kwa ajili ya elimu ya juu?

Asante sana mkuu. Wanasema eti kipaumbele kitakuwa elimu wakati ufisadi umetanda kila kona! Hizo fedha watatoa mbinguni? NI SAHIHI kabisa kusema umaskini wetu unasababishwa na ufisadi! Ona wanatudanganya wataweka vipaumbele kwenye elimu wakati wanazidi kuongeza majimbo ya uchaguzi kwa wabunge wasiokuwa na mchango wowote katika maendeleo ya nchi yetu bali hasara tupu!
 
Back
Top Bottom