Watanzania wanajaribu kuaminishwa kuwa Lowassa anafaa kuwa Rais wa Tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Wanaaminishwa kuwa ana maono ya kiuongozi ambayo yakitumika yanaweza kulinasua taifa letu toka hapa lilipo. Wanajaribu kuaminishwa kuwa Lowassa ni kiongozi bora ambaye Watanzania wanapaswa kumwangalia kwa matumaini - ndio maana ya "Safari ya Matumaini".
Wapo kati yetu ambao wameshazugika na pendekezo hilo na wamekuwa kama waliorogwa hivi. Wapo baadhi yetu kwa muda wote wa uongozi wa Lowassa (hasa baada ya kuwa Waziri Mkuu na baadaye) tuliona kile ambacho labda kimefichika kwa wengi - Lowassa hafai.
Hii si hukumu juu ya utu wake, heshima au ubinadamu wake; ni hukumu juu ya uongozi wake na maono yake kama kiongozi. Kumkataa Lowassa, maono yake, uongozi wake na fikra zake siyo kumchukia yeye kama Mtanzania mwenzetu au kama binadamu. Ni kuwa na tofauti naye na vile anavyowakilisha kiasi kwamba tofauti hizo hazijawezi kupatana (irreconcilable differences).
Katika siasa ni lazima tuheshimu uwepo wa tofauti hizi na tuelewe ndio msingi wa kutafuta viongozi bora zaidi au chama bora. Kwa kadiri yeye atakavyojaribu kujiuza ndivyo na sisi wengine tutazidi kuonesha kuwa hauziki au zaidi hanunuliki. Hii si chuki ni tofauti tu ya msingi (fundamental difference).
Pendekezo langu linatokana na hili; kwamba zipo na zimedumu tofauti za msingi kati ya maono ya baadhi yetu na maono ya mgombea huyu mtarajiwa kutoka CCM. Tanzania haihitaji maono na uongozi wa Lowassa kwa sababu nyingi tu; nitaanza na moja ya leo na nitaendelea kwenye mada hii hii kila ninapopata nafasi hadi jina lake litakapotupwa na NEC na yeye akaendelea kuwa Waziri Mkuu wa zamani.
Mara kwa mara baada ya sakata lake na katika jitihada za kujirudisha katika umuhimu (relevance) Lowassa amekuwa akizungumzia mwelekeo wa sera zake na kitu kitakachomuongoza. Aliamua kwenda kinyume na mwelekeo wa serikali ya chama chake ambayo iliweka mkazo kwenye "Kilimo Kwanza"; yeye ameamua kuja na hoja ya "Elimu Kwanza".
Alielezea kupinga kwake hoja ya Kilimo Kwanza miaka michache nyuma alipohojiwa katika kipindi cha Dakika45 (kinachorushwa na ITV). Alinukuliwa kusema "Mpango huu wa Kilimo Kwanza umekosa nguvu kwa sababu kuanzishwa kwake hakukuzingatia dhana ya ukombozi wa mwananchi wa kawaida. Tangu awali ndani ya chama (CCM) nilieleza kuwa sitaunga mkono hoja hiyo mpaka kuongezwe mashiko na kuwa Elimu Kabla ya Kilimo Kwanza"
Hoja hii ameirudia tena juzi kwenye mkutano wake na waandishi wa habari ambao bila ya shaka wengi wamekuwa 'charmed' na wingu la umaarufu wa Lowassa kiasi kwamba hakuna ambaye ameweza kumbana vizuri kwenye maswali. Anasema endapo atachaguliwa basi ataelekeza nchi kwenye "elimu kwanza"; kwamba hiki ndicho kipaumbele chake.
Ndio maana sisi wengine tunasema hafai; kwa sababu inaonekana siyo yeye wala chama chake ambao wamelielewa vizuri tatizo linaloikabili Tanzania; tatizo ambalo limeielekeza (orient) Tanzania kufuata njia ya Nigeria. Kwamba tunaweza kabisa kutengeneza uchumi wenye nguvu lakini wa taifa lenye umaskini uliokithiri, lisilo na usawa na la wasomi wasioweza kulipeleka taifa mbele. Tutakishia kujisifia wingi wa wasomi ambao wengi wataishia kwenda nje ya nchi kutafuta maisha. Taifa ambalo litakuwa limegawanyika sana kama Nigeria - licha ya kuwa na wasomi wengi.
Lowassa inaonekana ameshindwa kuelewa au hataki kukubali kuwa tatizo kubwa la Tanzania ni la aina tatu:
1. Ufisadi
2. Ufisadi
3. Ufisadi
Lowassa hatopambana na ufisadi kwa uzito unaostahili kwani haoni kuelewa kuwa ni tatizo la hatari zaidi kwa taifa "kuliko vita wakati wa amani" kama alivyosema Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere. Kutokuelewa kuwa Ufisadi ndiyo sekta haramu yenye nguvu zaidi katika nchi yetu ni kushindwa kuelewa tatizo letu hasa ni nini. Ufisadi umepenya (permeate) kwenye kila sekta nyingine zote (rasmi na zisizo rasmi). Umeathiri elimu, afya, usalama, na hata umoja wa taifa. Kutokulielewa tatizo hili kwa mtu anayetaka kugombea nafasi ya Urais (haijalishi anatokea chama gani) ni kutokuelewa namna ya kukabiliana na changamoto nyingine zote.
Kwa sababu hii peke yake Lowassa na mgombea mwingine yeyote ambaye haweki "ufisadi" kama ajenda yake ya kwanza na kubwa zaidi basi hafai. Kwa sababu atatuzungusha kwenye madudu mengine yote isipokuwa kwenye kumkoma nyani giledi.
Kikwete - kwa wanaokumbuka - alishabikiwa na wengi si kwa sababu ya "Ari Mpya, Kasi Mpya na Nguvu Mpya" bali zaidi kwa kuwapa Watanzania matumaini kuwa atashughulikia ufisadi vikali. Hotuba yake ya kulifungua Bunge na ile ya Ngurdoto na zile ziara zake za kutembelea Wizara ziliwafanya watu waamini kidogo kuwa hatimaye "kipele kimepata mkunaji". Leo hii miaka tisa baadaye ripoti ya CAG imeonesha kidogo tu kuwa tatizo hili la ufisadi halijapata mtatuzi ndani ya CCM na hata mtu anayeshabikiwa sana kuwa ati anaweza kuwa Rais inaonekana tatizo hili limempita kabisa.
Nikisema "hafai" simsingizii; nasema kilicho dhahiri; I'm just stating the obvious.
Wanaomtaka Lowassa - wapenzi, mashabiki na waumini wake - watuambie vita dhidi ya ufisadi ina umuhimu na uzito gani katika agenda za Lowassa. Wakituambia kuwa "ni mojawapo" ya mambo atakayoyashughulikia tuendelee kumkataa kwa sababu bado atakuwa hajaelewa tatizo letu hasa ni nini kama taifa.
Nitandelea...
NB: Kwa wageni wa hoja hizi warejee mada yangu ya 2007: Kikwete Siyo Safi, Yes I said it
Sasa naona Mzee Mwanakijiji umegeuka kuwa Kijana wa mjini!! dont jump the gun please! naona kama unajaribu kukataa ukweli kwamba ELIMU ndio ufunguo wa maendeleo; Elimu ndio Urithi endelevu! Elimu ndio STOCK IN TRADE ya watu walio wengi nchini mwetu na duniani kote! (msome hayati Lee kuan Yew; Founding father wa Island state ya Singapore; Hayati baba wa Taifa akiita Singapura!; Taifa Mama la dhana ya Matokeo makubwa Sasa;BRN inayowachanganya viongozi wetu wengi!)
Ukimuhukumu EL na kujaribu kushawishi wana CCM; CC; NEC na mkutano mkuu wa CCM "wamchinjilie mbali EL" kisa tu hakutamka kwamba moja ya agenda zake pindi akiteuliwa na hatimaye kuwa rais wa tano wa jamhuri ya muungano wa Tanzania ni "Kupambana na Ufisadi; Ufisadi na Ufisadi ni sawa na kutwambia kwamba "kutamka ni sawa na kutenda"!! aaaah wacha masihara Muzee; hiyo miujiza ni ya enzi za Nabii Issa Muzee mwanakijiji!! Wangapi wametamka na wakashindwa kufuatilia kauli zao kwa vitendo!! to talk is one thing; Mzee Mwana kijiji; BUT to walk the talk is quite a different creation Muzee wangu!!!
Hebu rejea kauli hizi: Ari mpya; Nguvu mpya na kasi mpya; tafsiri yake rahisi ni nini?!; Nina list ya Wauza mihadarati wote; wanapeta nje nje! Kinara wa ujangili yuko pale Arusha; lini alikamatwa?!; Tanzania bila Ukimwi inawezekana; Ukimwi uliisha lini?! Maisha bora kwa kila Mtanzania; yako wapi?! Kura ya maoni ya katiba pendekezwa ni April 2015; iko wapi?! Kura ya maoni iko pale pale; iko wapi?; tutakomesha mauaji ya watu wenye Albinism!; robo ya kwanza ya mwaka huu tumeshuhudia mauaji ya kutisha ya Albinos!
Nimetangulia kusema awali kwamba do not jump the gun! huyu EL ni wa kumsubiri kwenye campaign trail ikiwa atateuliwa kupeperusha bendera ya CCM: hapo abanwe kulia na kushoto kuhusu ufisadi na tuhuma mbali mbali za ufiadi zinazomzunguka yeye mwenyewe, wanahabari wacheze sehemu yao, wananchi kwenye mikutano ya kampeni; ndani ya midahalo na mitandao ya kijamii, atwambie kinaga ubaga agenda yake pana akiwa Rais; ufisadi included; mikakati ya utekelezaji wake na time frame.ni lazima pia atwambie mahusiano yake na watu wanaomzunguka ambao wana tuhuma lukuki za ufisadi pia na jinsi atakavyotnganisha kazi zake Ikulu na urafiki wakwe na watu hao!
tukifika mahali tukakubali as a nation mtu akatoa kauli tukashangilia tu kama mazuzu ili mradi katamka; bila kuhoji, kuuliza maswali magumu na kudai taarifa za utekelezaji na majibu husika tutakuwa tumekwisha kabisa na hilo ndilo lililotufikisha hapa tulipo!!
Elimu kwanza; yees! Elimu inajenga kujiamini kwa sababu mtu anakuwa anajua anachokisema kwa sababu amekifanyia kazi! anajua wapi kwa kupata taarifa sahihi; Elimu hiyo ndio itakayotuwezesha watu wetu kudai elimu ya uraia; kuhoji matumizi mabaya ya raslimali za umma; viongozi wetu kupenda starehe na kuishi nje ya uwezo wao (ostentation!); kudai nafasi yao sahihi katika uopngozi wa nchi yao; kukataa kufanywa watwana na viongozi wao; kusisitiza haki sawa kwa wanachi wote; kukemea usiginwaji wa haki za binadamu na demekrasia; watu wasio na elimu ya kutosha; elimu bora sio bora elimu katu hawawezi kuhoji ufisadi kwa sababu hawajiamini na hawana taarifa sahihi; kwa hiyo ni waoga ni rahisi kudanganywa na kukubali vizawadi zawadi vya kanga duni na fulani cheap na kazi yao ni kupiga makofi tuuu!
Muzee mwanakijiji; hebu vipange vipaumbele vyako vizuri zaidi, ufisadi ni mbaya ndio, EL huenda sio msafi ndio! lakini "wrong diagnosis leads to a wrong perscription"; dakitari akikosea kutambua ugonjwa lazima atatoa dawa ndivyo sivyo! mgonjwa atakufa mwana kijiji.
Mzee mwanakijiji; nina maoni mazito; (strong opinion) kwamba katika maswala nyeti ya nchi; You have your priorities TOP SIDE DOWN!!!!; hakuna kama elimu; it is second to none! Elimu hujenga kujitambua; kujiamini; kuweka vipaumbele sawasawa; kuwa na maono mapana kuhusu maisha na dunia kwa ujumla; not vice versa.