Lowassa Hafai! Yes I said It - Sababu ya I

Lowassa Hafai! Yes I said It - Sababu ya I

Ndio Mkuu Mzee Mwanakijiji, unasema kuwa Lowassa Hafai, and yes you said it so what?!.
Ila sio Lowassa tuu hafai, kama nakumbuka vizuri uliwahi kusema hata JK hafai, and you said it!, pia uliwahi kusema hata CCM haifai and yes you said it!, ni JK ndiye aliyechaguliwa na CCM ndich chama tawala mpaka leo, na leo tena amesema Lowasa hafai, sitashangaa ikiwa ni Lowasa na 2015 ni CCM tena, ila hizi "Yes I said It" za Mkuu Mzee Mwanakijiji, zitaendelea kwa hao wanaofuata!.

Na kwa ajili ya kuweka kumbukumbu safi, hizi ni baadhi ya yes I said it za Mkuu


  1. [*][h=3][URL="http://www.google.com/url?sa=t&rct=j&q=&esrc=s&source=web&cd=2&ved=0CCkQFjAB&url=http%3A%2F%2Fwww.jamiiforums.com%2Fjukwaa-la-siasa%2F15618-rostam-msabaha-kikwete-and-richmond-yes-i-said-it-again-7.html&ei=joJkVaWjA8SxygPPlYHoCw&usg=AFQjCNHIxxq05spU3z_OFkl2GRUumm28QA&bvm=bv.93990622,d.bGQ"]Rostam, Msabaha, Kikwete and Richmond - Yes I said it again ...
    [/h]
  2. [h=3]Rashid Othman: Umeshindwa Jiuzulu! - Jamii Forums[/h]
  3. [h=3]Ni lazima tugawanyike; Lazima tusiwe na umoja! -Yes I said it ...[/h]Ingekuwa kauli hizi za Yes I said it, zinaandamana na doing something kuzitekeleza, ingekuwa something, lakini kama ni kauli tuu za Lowassa Hafai! Yes I said It, baada ya hapo nothing more, nothing less, then 2015 rais wetu ni Edward Ngoyai Lowassa, say it or don't, it makes no difference!.

    [/URL]
Pasco
Lowasa,CCM hata ikichaguliwa tena haitaondoa ukweli kwamba ni wezi mafisadi,ni unafiki tu lakini kivipi wanashinda unaujua
 
hadithi ndefuu kuonyesha upeo wako wa kufikiri ulivyo mdogo,umekurupuka but kukurupuka kwako kutakusaidia leo...

Elimu kwanza ndio msingi,,elimu inabeba dhana zote ambazo wewe unapinnga,,watu wakielimika vyema watafundishwa kujiajiri,,wakielimika vyema wataffundishwa namna bora ya kilimo,,wakifundishwa vyema watajua namna ya kusaka masoko na kushindana,,usipoelimika vyema huwezi jua hata kama unaibiwa na haki zako,elimu itasaidia kufuta ufisadi unaosema wewe

kabla ya maneno yako jipime na aloandika kwanza, ila kwa kua watanzania wengi vichwa tikiti maji nawe huenda ni miongoni mwao.
 
Watanzania wanajaribu kuaminishwa kuwa Lowassa anafaa kuwa Rais wa Tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Wanaaminishwa kuwa ana maono ya kiuongozi ambayo yakitumika yanaweza kulinasua taifa letu toka hapa lilipo. Wanajaribu kuaminishwa kuwa Lowassa ni kiongozi bora ambaye Watanzania wanapaswa kumwangalia kwa matumaini - ndio maana ya "Safari ya Matumaini".
Mkuu sio Watanzania wanaaminishwa bali huu ndio ukweli wenyewe, ukweli halisi kuwa
Lowassa anafaa kuwa Rais wa Tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Lowassa ana maono ya kiuongozi ambayo yatalinasua taifa letu toka hapa lilipo. Lowassa ni kiongozi bora ambaye Watanzania wanapaswa kumwangalia kwa matumaini - ndio maana ya "Safari ya Matumaini" na inazinduliwa Jumapili hii katika Uwanja wa Sheikh Amri Abedi mjini Arusha, napendekeza kwa wale wote wenye mapenzi mema na nchi hii, tuungane kumpa support hata kwa kupitia tuu kwenye luninga na redio zetu ambazo zote zitatangaza live!.

Lowassa inaonekana ameshindwa kuelewa au hataki kukubali kuwa tatizo kubwa la Tanzania ni la aina tatu:
1. Ufisadi
2. Ufisadi
3. Ufisadi
Kwa sababu hii peke yake Lowassa na mgombea mwingine yeyote ambaye haweki "ufisadi" kama ajenda yake ya kwanza na kubwa zaidi basi hafai. Kwa sababu atatuzungusha kwenye madudu mengine yote isipokuwa kwenye kumkoma nyani giledi.
Hiki ni kipaumbele chako lakini kiukweli kabisa tatizo la Tanzania sio ufisadi bali ni elimu!. Kupanga ni kuchagua, unaweza kupanga kipaumbele chako ni ufisadi na ukauchagua ufisadi na yeye amepanga kipaumbele chake ni elimu na amechagua elimu!.

Wanaomtaka Lowassa - wapenzi, mashabiki na waumini wake - watuambie vita dhidi ya ufisadi ina umuhimu na uzito gani katika agenda za Lowassa.
Haina umuhimu wowote na wala sio agenda kabisa kwa sababu ufisadi ndio the one and only means to an end, and the end justifies the means!.

JK aliingia madarakani kwa ufisadi wa EPA, CCM ndio kiongozi wa harakati zote za ufisadi mkubwa mkubwa, viongozi wa serikali ya CCM ndio ma sterling kwenye grand corruption, hivyo kutaka kumbebesha Lowassa agenda ya ufisadi ni kutaka tuu kumuonea, hoja ya msingi ingekuwa CCM hawafai kwa ufisadi, hivyo tuwaweke pembeni CCM, tatizo as of now bado hatuna mbadala, uiweke CCM pembeni halafu nchi yetu tumpe nani?!, au vinginevyo na wewe kama uko kwenye kundi la kukubali tuitumie ikulu yetu kwa majaribio ya mabadiliko, tuwapishe tuu UKAWA hivyo hivyo tuwajaribishe?!.

Pasco
 
Nani anafaa?

Wakati mwingine mtu huchaguliwa si kwa sababu anaonekana anafaa, bali kwa kuwa mgombea/wagombea wengine ni dhahiri hawafai. Tunaweza kuita by elimination.

Wakati tunatafakari nani awe Rais na kuangalia sifa zao, ni bora tukaanza kuyakaa makapi moja kwa moja ili tubaki na watu wachache wa kuwafanyia tathmini.

Watu aina ya Lowassa ni kejeli kubwa sana kuwafikiria achilia mbali kuwachagua.
 
Mwanakijiji uchambuzi safi, nchi hii kweli imekua kama haina mwenyewe na ni ngumu kuamini mtu. Asilimia kubwa ya wachangiaji ni wachumia tumbo bila kuwa objective! Ikulu inatafutwa kwa fedha, uongo, uchawi, ufisadi na hata ubabe wa kupoteza maisha ya watu. Wapo watu makini ila wataiweza hii mikikimikiki ya kuweka maisha rehani

-- mfano kuliko huyu el afadhali hata dr. Augustine mahiga, augustino ramadhani, dr. Magufuli na wengine na sio huyu ambaye historia yake ni mbaya na watu wengi wanaijua ila tunajidai eti hatuijui na tunamnadi kama vile hii nchi sio yetu


--- tafadhali tuwe wazalendo ili kupata mtu makini na mzalendo wa kweli.
Mwaka 2005 alivyodondoka mkulu pale jangwani kuna kina mama sehemu mbalimbali nao walidondoka kwa presha, hii ilikua ni dalili ya wazi wazi kuwa taifa lilikua linaenda kudondoka na yametokea kweli, kwa hii miaka 10 karibu kila sekta imebaki hoi bin taabani na watu waliokua wa kawaida kabla ya hii miaka kumi kwa kwa sasa ni mabilionea
 
Ni kweli kabisa Mzee Mwanakijiji, Nigeria ina idadi kubwa zaidi ya wasomi wengi wa viwango vya Kimataifa, kuliko pengine nchi yoyote nyingine Afrika. Siyo hilo tu, kulingana na takwimu za 2014, Nigeria ndiyo nchi yenye uchumi mkubwa zaidi Afrika (GDP: $509.9b), ikifuatiwa na Afrika Kusini (GDP: $370.3b). Nigeria ndiyo nchi ya kwanza Afrika kwa uzalishaji wa mafuta, na ya kumi na moja, duniani. Kulingana na takwimu za Forbes 2014, tajiri NA.1 Afrika, anatoka Nigeria, na katika matajiri 50 walio matajiri zaidi Afrika, 13 kati yao wanatoka Nigeria! Pamoja na yote haya, Ufisadi Nigeria ni sehemu ya maisha!

Kwa sababu ya ufisadi uliokithiri Nigeria, hali ya kijumla ya maisha ya wananchi Nigeria inatisha, kwa mfano, siku za karibuni kumekuwa na uhaba wa mafuta uliosababisha foleni za kutisha na kugombea mafuta, kwa bei ya kulanguliwa! Bila kushughulika na ufisadi, yote ni bure! Nchi za mashariki anazozisema Lowassa siyo tu walitoa kipaumbele kwa elimu, lakini kipaumbele kikubwa zaidi kilikuwa, na hata sasa, ni vita kali dhidi ya ufisadi. Kwa mfano China, hukumu ya Ufisadi, ni kifo, na bila huruma, wameuawa matajiri na wenye vyeo vikubwa serikalini, kwa sababu ya ufisadi. Tatizo la Tanzania, ni ufisadi uliokithiri. Bila kiongozi anayechukia ufisadi, na mwenye dhamira ya kweli ya kuupiga vita ufisadi, Tanzania hatuwezi kutoka hapa tulipo. Je Lowassa na Meneja wake wa Kampeni, Rostam Aziz na wapambe wake akina Karamagi na Chenge, kweli, wana nia na uwezo wa kuupiga vita Ufisadi????? TUTAFAKARI!!!!!!
 
Elimu bila kushughulikia ufisadi kutakuwa na tofauti gani na sasa? au unafikiria hawaweka mkazo kwenye elimu? si watakuonesha shule, vyuo na idadi mbalimbali "nyingi" tu? Hili la nani mwingine siyo hoja ya sasa wala haitusumbui sana; hakuna ambaye ameenda mbali katika kujinadi sana kama Lowassa. Hata kwa wenzetu US.. kwa demokrati anayefuatiliwa sana ni Hillary Clinton.. simply kwa sababu anaonekana ndiye mwenye uwezo wa kupitishwa kule... Hawaulizwi watu mbona wengine "hamwajadili"? labda hawana umuhimu kama wa Lowassa?


Nashauri tufanye kama marekani, tuwaoji wagombea wote,miaka yote iliyopi katika nafasi zao wamelifanyia nini taifa hili,haiingi akili mtu ata mbomba la maji la mtaa hajawai kujenga au shule ya chekechea then anasema ataleta maendeleo kwa vipi? hata mtoto shule lazima ahanze kuandikia penseli ndo atumia karamu ya wino (hasiyeweza kidogo hata kikubwa hawezi)
 
hadithi ndefuu kuonyesha upeo wako wa kufikiri ulivyo mdogo,umekurupuka but kukurupuka kwako kutakusaidia leo...

Elimu kwanza ndio msingi,,elimu inabeba dhana zote ambazo wewe unapinnga,,watu wakielimika vyema watafundishwa kujiajiri,,wakielimika vyema wataffundishwa namna bora ya kilimo,,wakifundishwa vyema watajua namna ya kusaka masoko na kushindana,,usipoelimika vyema huwezi jua hata kama unaibiwa na haki zako,elimu itasaidia kufuta ufisadi unaosema wewe


Hakuna sera yoyote itakayofanikiwa ikiwa ufisadi utaendelea Tanzania. Iwe afya, elimu au kilimo, ni lazima kwanza kuondoa ufisadi ili angalau kuwe na nafasi ya kufanikiwa.

Fisadi anaogopa kutaja neno ufisadi maana roho inamsuta. Sikiliza hotuba zake zote.
 
Mimi naungana kabisa na mtoa mada na nimemuelewa kiukweli EL tunatakiwa kumuogopa kama ebola kwakweli
 
mtaa gani huo,acheni kutuingia vijana makini na hao wanaolipwa kushadadia.siwezi kumuunga mkono mtu aliyezungukwa na mijitu ya ajabu ajabu Rostam,Karamagi,Chenge!

Mimi nadhani tunakubaliana kwamba Lowasa hafai kua rais wa nchi yetu. Jenga hoja kwenye hili jambo na punguza jazba sizizo akisi Utanzania wetu.
 
Najiuliza hv kwa nn mtu huyu anaesemwa kila siku ni fisadi lkn bado watu wengi wanaendelea kumsapoti tu!?ni coincidence ama ni nn!???km bado ni mchafu na bado watu wanamkubali basi ndo chaguo la mungu hilo..na ana makusudi yake..jinsi alivyosemwa kwa miaka yote ilikua ni tosha kwa watu kumkataa lk ndo kwanza nyota inazidi kungara..poleni mnaoshindana na ukweli.
 
EL hafai kabisa tena hata wenyewe ndani ya CCM wanajua kuwa hafai. Labda unaweza ukaniuliza hafai kwa lipi au yepi??
1. Siyo msafi ndani ya chama hata nje ya chama. Rejea kauli ya Hayati Baba wa Taifa juu ya huyu ndg yetu.
2. Ametengeneza maadui wengi walio ndani ya mfumo rasmi wa kiutawala, hivyo ni hatari kwa mstakbari wa ustawi wa mfumo.
3. EL anaonekana kuwa amejipanga kinguvu kutinga Ikulu kwa ghalama yoyote kitu ambacho ni hatari sana kwa nchi.
Hivyo basi kwa sababu hizi chache naamini hawezi kupewa dhamana ya kukipigania chama.
 
hadithi ndefuu kuonyesha upeo wako wa kufikiri ulivyo mdogo,umekurupuka but kukurupuka kwako kutakusaidia leo...

Elimu kwanza ndio msingi,,elimu inabeba dhana zote ambazo wewe unapinnga,,watu wakielimika vyema watafundishwa kujiajiri,,wakielimika vyema wataffundishwa namna bora ya kilimo,,wakifundishwa vyema watajua namna ya kusaka masoko na kushindana,,usipoelimika vyema huwezi jua hata kama unaibiwa na haki zako,elimu itasaidia kufuta ufisadi unaosema wewe

naunga mkono hoja,ila abadilishe mitaala ya vyuo ili tupate wasomi wanaoamini katika kujiajiri sio kuajiliwa,
 
endeleeni kutoa hii elimu kwa kweli mie niko kwenye maombi..ya nguvu. maana ikitokea jamaa akaa kuna miaka kumi mingine ya mateso na dhiki kubwa ..mungu tusaidie
 
Za kuambiwa changanya na zako.
Hakika safari ya matumaini imeanza ingawa kuna miba,mbigili na kila aina ya vikwazo,lakini kwake yeye hakika tutapata tumaini jipya la kutuondoa mahali tulipo na kutupeleka mbali kiuchimu,kielimu na ustawi wa maisha yetu.
Tusikubali kudanganywa na watu waliofirisika kifikra na wenye mawazo mgando yenye kumpaka matope kiongozi shupavu,mwadilifu,mwaminifu na mvumilivu wa kila aina ya vikwazo.
Hakika EL ni tishio na kiboko cha wezi ingawa hatothubutu kuwaadhibu wale wote waliojichotea fedha za umma kwa manufaa yao,kwani safari ya kujenga uchumi itatumia rasilimali na fursa zilizopo pamoja na kuziba mirija yote ya unyonyaji na ukandamizaji wa haki kwa kutumia mbinu mpya na mifumo mbalimbali yenye kuleta matokeo chanya kwa haraka.
 
Hakuna sera yoyote itakayofanikiwa ikiwa ufisadi utaendelea Tanzania. Iwe afya, elimu au kilimo, ni lazima kwanza kuondoa ufisadi ili angalau kuwe na nafasi ya kufanikiwa.

Fisadi anaogopa kutaja neno ufisadi maana roho inamsuta. Sikiliza hotuba zake zote.

EDUCATION S POWER,UKIONA MSOMI AMAIBA UJUE ELIMU YAKE NI HAFIFU MAANA MSOMI ANATAFUTA FULSA MBALIMBALI ZA KUMPA KIPATO PASIPO KUIBA, mf angalia nchi kama china idadi kubwa ya wasomi wako kwenye tafiti kujipatia kipato ndani na nje ya nchi,sisi hatuna wasomi.
 
Back
Top Bottom