mbogo31
JF-Expert Member
- Nov 28, 2008
- 711
- 173
Mada za kumchafua EL zimekua nyingi sasa. Inanifanya nijue yy ni bora kwa jinsi mnavyokesha kumchafua
kaka samahani elezea ubora wake na umtetee kwa hoja kama alivyoweka mwenzako.
Mada za kumchafua EL zimekua nyingi sasa. Inanifanya nijue yy ni bora kwa jinsi mnavyokesha kumchafua
Mimi kwangu hamna jipya ulilolisema na ninajua fika ya kwamba Bw.Lowasa ni fisadi lakini bado Nitampa Kura yangu kama akigombea, na sababu ni rahisi tu sioni mbadala wake, kama ni Mbowe pia aniaambie ni kwa nini alisema Serikali inafuja mali ya Umma kwa kununua mashangingi akarudisha lake na kulichukua tena na mpaka leo hii analitumia na juzi alikutwa nalo Mombasa, Kenya likiwa na namba za Kiraia, Je yeye siyo sehemu ya Ufisadi unaofanywa na Serikali aliokuwa analalamikia? Na kama akiwa raisi au Chama chake atwezaje kuondokana na ubadhirifu huu kama sasa hivi ameshindwa?
Hilo la kwanza la pili Serikali ya kifisadi ya CCM inaongeza Mishahara na marupurupu kwa Wabunge wote na wa upinzani sijasikia Mbunge yoyote yule kuanzia wa Upinzani wanaomuita Lowasa fisadi mpaka wa CCM akilalamikia hii dhuluma siajabu kubwa kulko yote TanZania kwa maana Majimbo ya akina Tundu Lisu haya zahanati wala Dawa lakini yuko kimya kwenye hilo, hivyo maadamu mimi sipati majibu ya maswali kama haya basi mimi kura yangu mpaka sasa hivi ni Fisadi Lowasa tu angalau namjua kuliko hawa nisiowajua!
Kweli mkuu, hapo itakuwa shida.Rostam Aziz,Andrew Chenge,Nazir Karamagi=Edward Ngoyai Lowassa.Ndio mnataka tuwakabidhi nchi hawa? Zinachaji kichwani kweli nyinyi?
Hii nchi ina leadership crisis kubwa sana.
Swali ni je, wananchi walio wengi wanalitambua hilo?
Nina uhakika kabisa unajua wananchi hawalitambui hili tatizo bali wanaona tuna viongozi wenye vipaji vya hali ya juu! Na hilo ndio tatizo letu!Hii nchi ina leadership crisis kubwa sana.
Swali ni je, wananchi walio wengi wanalitambua hilo?
Lowassa ufisadi kwake sio agenda
mkuu nikukumbushe ZITTO peke yake ndo alikataa hizo posho za bunge wezake wakamkejeri,cha ajabu zaidi juzi wote kwa pamoja waliomba pension mil 289, wafanye kampain lkn hawakuziomba kufanya maendeleo, wanasiasa wote wezi hakuna msafi hata moja.
Mbona hujadli hoja za Mzee Mwanakijiji juu ya Lowasa kutofaa kuchaguliwa? Kwa hoja ya Mwanakijiji, Lowasa hafai kwani haoneshi kwamba tatizo kubwa la Tanzania ni Ufisadi. Hata ukaweka mikakati mikubwa kiasi gani ya kuinua elimu kama hujadhibiti rushwa na ufisadi juhudi zote zitakuwa bure kwani zitahujumiwa na ufisadi!Kwaio wewe unataka raisi awe nani labda
Haki sawa mm sina ugomvi na mtu ila nataka uniambie mtu mwingine unayefikiri anafaa. Acha siasaNyie ndio wale mwenyekiti wenu jana aliwaita Makuwadi jana ?
![]()
Watanzania wanajaribu kuaminishwa kuwa Lowassa anafaa kuwa Rais wa Tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Wanaaminishwa kuwa ana maono ya kiuongozi ambayo yakitumika yanaweza kulinasua taifa letu toka hapa lilipo. Wanajaribu kuaminishwa kuwa Lowassa ni kiongozi bora ambaye Watanzania wanapaswa kumwangalia kwa matumaini - ndio maana ya "Safari ya Matumaini".
Wapo kati yetu ambao wameshazugika na pendekezo hilo na wamekuwa kama waliorogwa hivi. Wapo baadhi yetu kwa muda wote wa uongozi wa Lowassa (hasa baada ya kuwa Waziri Mkuu na baadaye) tuliona kile ambacho labda kimefichika kwa wengi - Lowassa hafai.
Hii si hukumu juu ya utu wake, heshima au ubinadamu wake; ni hukumu juu ya uongozi wake na maono yake kama kiongozi. Kumkataa Lowassa, maono yake, uongozi wake na fikra zake siyo kumchukia yeye kama Mtanzania mwenzetu au kama binadamu. Ni kuwa na tofauti naye na vile anavyowakilisha kiasi kwamba tofauti hizo hazijawezi kupatana (irreconcilable differences).
Katika siasa ni lazima tuheshimu uwepo wa tofauti hizi na tuelewe ndio msingi wa kutafuta viongozi bora zaidi au chama bora. Kwa kadiri yeye atakavyojaribu kujiuza ndivyo na sisi wengine tutazidi kuonesha kuwa hauziki au zaidi hanunuliki. Hii si chuki ni tofauti tu ya msingi (fundamental difference).
Pendekezo langu linatokana na hili; kwamba zipo na zimedumu tofauti za msingi kati ya maono ya baadhi yetu na maono ya mgombea huyu mtarajiwa kutoka CCM. Tanzania haihitaji maono na uongozi wa Lowassa kwa sababu nyingi tu; nitaanza na moja ya leo na nitaendelea kwenye mada hii hii kila ninapopata nafasi hadi jina lake litakapotupwa na NEC na yeye akaendelea kuwa Waziri Mkuu wa zamani.
Mara kwa mara baada ya sakata lake na katika jitihada za kujirudisha katika umuhimu (relevance) Lowassa amekuwa akizungumzia mwelekeo wa sera zake na kitu kitakachomuongoza. Aliamua kwenda kinyume na mwelekeo wa serikali ya chama chake ambayo iliweka mkazo kwenye "Kilimo Kwanza"; yeye ameamua kuja na hoja ya "Elimu Kwanza".
Alielezea kupinga kwake hoja ya Kilimo Kwanza miaka michache nyuma alipohojiwa katika kipindi cha Dakika45 (kinachorushwa na ITV). Alinukuliwa kusema "Mpango huu wa Kilimo Kwanza umekosa nguvu kwa sababu kuanzishwa kwake hakukuzingatia dhana ya ukombozi wa mwananchi wa kawaida. Tangu awali ndani ya chama (CCM) nilieleza kuwa sitaunga mkono hoja hiyo mpaka kuongezwe mashiko na kuwa Elimu Kabla ya Kilimo Kwanza"
Hoja hii ameirudia tena juzi kwenye mkutano wake na waandishi wa habari ambao bila ya shaka wengi wamekuwa 'charmed' na wingu la umaarufu wa Lowassa kiasi kwamba hakuna ambaye ameweza kumbana vizuri kwenye maswali. Anasema endapo atachaguliwa basi ataelekeza nchi kwenye "elimu kwanza"; kwamba hiki ndicho kipaumbele chake.
Ndio maana sisi wengine tunasema hafai; kwa sababu inaonekana siyo yeye wala chama chake ambao wamelielewa vizuri tatizo linaloikabili Tanzania; tatizo ambalo limeielekeza (orient) Tanzania kufuata njia ya Nigeria. Kwamba tunaweza kabisa kutengeneza uchumi wenye nguvu lakini wa taifa lenye umaskini uliokithiri, lisilo na usawa na la wasomi wasioweza kulipeleka taifa mbele. Tutakishia kujisifia wingi wa wasomi ambao wengi wataishia kwenda nje ya nchi kutafuta maisha. Taifa ambalo litakuwa limegawanyika sana kama Nigeria - licha ya kuwa na wasomi wengi.
Lowassa inaonekana ameshindwa kuelewa au hataki kukubali kuwa tatizo kubwa la Tanzania ni la aina tatu:
1. Ufisadi
2. Ufisadi
3. Ufisadi
Lowassa hatopambana na ufisadi kwa uzito unaostahili kwani haoni kuelewa kuwa ni tatizo la hatari zaidi kwa taifa "kuliko vita wakati wa amani" kama alivyosema Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere. Kutokuelewa kuwa Ufisadi ndiyo sekta haramu yenye nguvu zaidi katika nchi yetu ni kushindwa kuelewa tatizo letu hasa ni nini. Ufisadi umepenya (permeate) kwenye kila sekta nyingine zote (rasmi na zisizo rasmi). Umeathiri elimu, afya, usalama, na hata umoja wa taifa. Kutokulielewa tatizo hili kwa mtu anayetaka kugombea nafasi ya Urais (haijalishi anatokea chama gani) ni kutokuelewa namna ya kukabiliana na changamoto nyingine zote.
Kwa sababu hii peke yake Lowassa na mgombea mwingine yeyote ambaye haweki "ufisadi" kama ajenda yake ya kwanza na kubwa zaidi basi hafai. Kwa sababu atatuzungusha kwenye madudu mengine yote isipokuwa kwenye kumkoma nyani giledi.
Kikwete - kwa wanaokumbuka - alishabikiwa na wengi si kwa sababu ya "Ari Mpya, Kasi Mpya na Nguvu Mpya" bali zaidi kwa kuwapa Watanzania matumaini kuwa atashughulikia ufisadi vikali. Hotuba yake ya kulifungua Bunge na ile ya Ngurdoto na zile ziara zake za kutembelea Wizara ziliwafanya watu waamini kidogo kuwa hatimaye "kipele kimepata mkunaji". Leo hii miaka tisa baadaye ripoti ya CAG imeonesha kidogo tu kuwa tatizo hili la ufisadi halijapata mtatuzi ndani ya CCM na hata mtu anayeshabikiwa sana kuwa ati anaweza kuwa Rais inaonekana tatizo hili limempita kabisa.
Nikisema "hafai" simsingizii; nasema kilicho dhahiri; I'm just stating the obvious.
Wanaomtaka Lowassa - wapenzi, mashabiki na waumini wake - watuambie vita dhidi ya ufisadi ina umuhimu na uzito gani katika agenda za Lowassa. Wakituambia kuwa "ni mojawapo" ya mambo atakayoyashughulikia tuendelee kumkataa kwa sababu bado atakuwa hajaelewa tatizo letu hasa ni nini kama taifa.
Nitandelea...
NB: Kwa wageni wa hoja hizi warejee mada yangu ya 2007: Kikwete Siyo Safi, Yes I said it
Mbona hujadli hoja za Mzee Mwanakijiji juu ya Lowasa kutofaa kuchaguliwa? Kwa hoja ya Mwanakijiji, Lowasa hafai kwani haoneshi kwamba tatizo kubwa la Tanzania ni Ufisadi. Hata ukaweka mikakati mikubwa kiasi gani ya kuinua elimu kama hujadhibiti rushwa na ufisadi juhudi zote zitakuwa bure kwani zitahujumiwa na ufisadi!
Ukweli ikiwa Edo ataupata uraisi itakuwa ni janga la kitaifa . Kwa nini
(1) Lazima hao marafiki zake waliomchangia watataka kurudisha hela zao na yeye pia atataka kurudisha fedha zake alizotumia kwani kila mtu anajua jinsi alivyomwaga fedha kununua kuungwa mkono. Wote tunajua hakuna atakayetoa hela yake bure bila kujua atazirudisha vipi kwani kama ungekuwa ni msaada basi hata hao watoa msaada wangeweza kunipa mimi nipeleke kanisani na msikitini lakini hawakufanya hvyo kwani walikuwa wanajua wanachokitafuta kupitia kwa Edo. Uraisi wake utakuwa wa kununua na si vinginevyo. Angalia tangazo la kwenye gazeti la Mwananchi la tarehe ya leo 26/5 ni tangazo la bei mbaya. Kizuri kinajiuza kibaya kinajitangaza.
(2) Uraisi wake utaongeza mpasuko ndani ya chama cha mapinduzi na serikalini hasa kwenye vyombo vya usalama na kutakuwa na kulipiza visasi na kuhujumiana sana kuonyesha kila upande ulivyo na uwezo mdogo wa utendaji jambo litakaloongeza gharama za uendeshaji na matumizi mabaya wa taasisi za serikali
(3) Kutokana na mambo hayo mawili ufanisi wa serikali na vyombo vyake utakuwa mdogo sana hivyo uchumi utayumba, rushwa itaongezeka sana na itatuumiza, kutakuwa na Serikali ya kulazimishana na kutokana na hilo vyama vya upinzania vitapata nguvu sana (4) Kuongezeka kwa nguvu ya vyama vya upinzania kutafanya Serikali izidi kuwa ya kigandamizi kuua kabisa haki za msingi za kiraia. Hivyo fedha nyingi sana na nchi zitatumika kwa ajili ya kugandamiza haki za binadamu badala kulipia gharama za maendeleo.
Kitendo cha kusema eti kama angeendelea kuwa Waziri Mkuu hii nchi ingekuwa na maendeleo zaidi ni kitendo cha kuiponda Chama Chake na Serikali iliyoko madarakani ambayo ni kitu kibaya sana kwa mshikamano wa Chama na Serikali. Sidhani kitu hicho kitavumiliwa na Watanzania wenye nia njema na nchi hii.
Vile vile kule kusema kuwa eti walimvizia Mkurugenzi wa Kampuni ya Maji ili wamfukuze kabla hajaenda mahakamani kupata zuio la kimahakama inaonyesha kabisa akipata Urais atakuwa Rais wa namna gani. Kila mtu awe mtanzania au sio ana haki ya kupata haki yake kupitia mahakami na hairuhusiwi Serikali wala mtu yeyote kuzuia haki kwa sababu yeyote.
Ninaomba Watanzania watafakari hilo.
Nina uhakika kabisa unajua wananchi hawalitambui hili tatizo bali wanaona tuna viongozi wenye vipaji vya hali ya juu! Na hilo ndio tatizo letu!