Lowassa Hafai! Yes I said It - Sababu ya I

Lowassa Hafai! Yes I said It - Sababu ya I

umekosea general meaning ya priority!!!
na najua unajua sema kwa sasa akili yako inatumiwa!!!
sera ya kilimo kwanza haikumaanisha kutoshuhulikia kero nyingine!!! na hata ya elimu kwanza haimaanisha hatashuhulika na kero nyingine!!!!
fungua ubongo bhana !!!
 
Nimeshangaaa sana post ambayo mwanakijiji ameiandika,ningemwona wa maana kama angesema tumchague Membe wake. Povu linalomtoka si bure. MSOMI GANI ANAEJIITA MCHAMBUZI anaetaka kutuaminisha kuwa kama jipaumbele cha mtu ni kitu fulani basi vitu vingine havitakwenda. Hivi mtu akisena mwaka huu kipaumbele changu ni ujenzi wa nyumba basi hatakula, hatawapeleka watoto shule, hatalala,hatajilinda na wezi, hatasali.
Ama kweli Mwanakijiji ni mchumia tumbo kama wachumia tumbo wengine.

Wewe ndie watu wanatakiwa wakushangae! Wanatakiwa wakushangae, tena sana, kwa sababu unaandika kitu usichojua. Inaonyesha kabisa huelewi hata ni nini kinachojadiliwa hapa! Halafu ulivyo na mawazo finyu unafikiria kila ambae anasema Lowassa hafai basi atakuwa ametumwa na Membe! Jaribu kupeleka upeo wako wa kufikiria level nyingine (ya juu) ndio utajua kinachojadiliwa hapa! NB: Nilitaka nikueleweshe walau kidogo lakini nadhani IQ yako haiwezi kupata sawasawa kitachoelezwa!
 
edward-lowassa.jpg


watanzania wanajaribu kuaminishwa kuwa lowassa anafaa kuwa rais wa tano wa jamhuri ya muungano wa tanzania. Wanaaminishwa kuwa ana maono ya kiuongozi ambayo yakitumika yanaweza kulinasua taifa letu toka hapa lilipo. Wanajaribu kuaminishwa kuwa lowassa ni kiongozi bora ambaye watanzania wanapaswa kumwangalia kwa matumaini - ndio maana ya "safari ya matumaini".

Wapo kati yetu ambao wameshazugika na pendekezo hilo na wamekuwa kama waliorogwa hivi. Wapo baadhi yetu kwa muda wote wa uongozi wa lowassa (hasa baada ya kuwa waziri mkuu na baadaye) tuliona kile ambacho labda kimefichika kwa wengi - lowassa hafai.

Hii si hukumu juu ya utu wake, heshima au ubinadamu wake; ni hukumu juu ya uongozi wake na maono yake kama kiongozi. Kumkataa lowassa, maono yake, uongozi wake na fikra zake siyo kumchukia yeye kama mtanzania mwenzetu au kama binadamu. Ni kuwa na tofauti naye na vile anavyowakilisha kiasi kwamba tofauti hizo hazijawezi kupatana (irreconcilable differences).

Katika siasa ni lazima tuheshimu uwepo wa tofauti hizi na tuelewe ndio msingi wa kutafuta viongozi bora zaidi au chama bora. Kwa kadiri yeye atakavyojaribu kujiuza ndivyo na sisi wengine tutazidi kuonesha kuwa hauziki au zaidi hanunuliki. Hii si chuki ni tofauti tu ya msingi (fundamental difference).

Pendekezo langu linatokana na hili; kwamba zipo na zimedumu tofauti za msingi kati ya maono ya baadhi yetu na maono ya mgombea huyu mtarajiwa kutoka ccm. Tanzania haihitaji maono na uongozi wa lowassa kwa sababu nyingi tu; nitaanza na moja ya leo na nitaendelea kwenye mada hii hii kila ninapopata nafasi hadi jina lake litakapotupwa na nec na yeye akaendelea kuwa waziri mkuu wa zamani.

Mara kwa mara baada ya sakata lake na katika jitihada za kujirudisha katika umuhimu (relevance) lowassa amekuwa akizungumzia mwelekeo wa sera zake na kitu kitakachomuongoza. Aliamua kwenda kinyume na mwelekeo wa serikali ya chama chake ambayo iliweka mkazo kwenye "kilimo kwanza"; yeye ameamua kuja na hoja ya "elimu kwanza".

Alielezea kupinga kwake hoja ya kilimo kwanza miaka michache nyuma alipohojiwa katika kipindi cha dakika45 (kinachorushwa na itv). Alinukuliwa kusema "mpango huu wa kilimo kwanza umekosa nguvu kwa sababu kuanzishwa kwake hakukuzingatia dhana ya ukombozi wa mwananchi wa kawaida. Tangu awali ndani ya chama (ccm) nilieleza kuwa sitaunga mkono hoja hiyo mpaka kuongezwe mashiko na kuwa elimu kabla ya kilimo kwanza"

hoja hii ameirudia tena juzi kwenye mkutano wake na waandishi wa habari ambao bila ya shaka wengi wamekuwa 'charmed' na wingu la umaarufu wa lowassa kiasi kwamba hakuna ambaye ameweza kumbana vizuri kwenye maswali. Anasema endapo atachaguliwa basi ataelekeza nchi kwenye "elimu kwanza"; kwamba hiki ndicho kipaumbele chake.

Ndio maana sisi wengine tunasema hafai; kwa sababu inaonekana siyo yeye wala chama chake ambao wamelielewa vizuri tatizo linaloikabili tanzania; tatizo ambalo limeielekeza (orient) tanzania kufuata njia ya nigeria. Kwamba tunaweza kabisa kutengeneza uchumi wenye nguvu lakini wa taifa lenye umaskini uliokithiri, lisilo na usawa na la wasomi wasioweza kulipeleka taifa mbele. Tutakishia kujisifia wingi wa wasomi ambao wengi wataishia kwenda nje ya nchi kutafuta maisha. Taifa ambalo litakuwa limegawanyika sana kama nigeria - licha ya kuwa na wasomi wengi.

Lowassa inaonekana ameshindwa kuelewa au hataki kukubali kuwa tatizo kubwa la tanzania ni la aina tatu:
1. Ufisadi
2. Ufisadi
3. Ufisadi

lowassa hatopambana na ufisadi kwa uzito unaostahili kwani haoni kuelewa kuwa ni tatizo la hatari zaidi kwa taifa "kuliko vita wakati wa amani" kama alivyosema baba wa taifa mwalimu nyerere. Kutokuelewa kuwa ufisadi ndiyo sekta haramu yenye nguvu zaidi katika nchi yetu ni kushindwa kuelewa tatizo letu hasa ni nini. Ufisadi umepenya (permeate) kwenye kila sekta nyingine zote (rasmi na zisizo rasmi). Umeathiri elimu, afya, usalama, na hata umoja wa taifa. Kutokulielewa tatizo hili kwa mtu anayetaka kugombea nafasi ya urais (haijalishi anatokea chama gani) ni kutokuelewa namna ya kukabiliana na changamoto nyingine zote.

Kwa sababu hii peke yake lowassa na mgombea mwingine yeyote ambaye haweki "ufisadi" kama ajenda yake ya kwanza na kubwa zaidi basi hafai. Kwa sababu atatuzungusha kwenye madudu mengine yote isipokuwa kwenye kumkoma nyani giledi.

Kikwete - kwa wanaokumbuka - alishabikiwa na wengi si kwa sababu ya "ari mpya, kasi mpya na nguvu mpya" bali zaidi kwa kuwapa watanzania matumaini kuwa atashughulikia ufisadi vikali. Hotuba yake ya kulifungua bunge na ile ya ngurdoto na zile ziara zake za kutembelea wizara ziliwafanya watu waamini kidogo kuwa hatimaye "kipele kimepata mkunaji". Leo hii miaka tisa baadaye ripoti ya cag imeonesha kidogo tu kuwa tatizo hili la ufisadi halijapata mtatuzi ndani ya ccm na hata mtu anayeshabikiwa sana kuwa ati anaweza kuwa rais inaonekana tatizo hili limempita kabisa.

Nikisema "hafai" simsingizii; nasema kilicho dhahiri; i'm just stating the obvious.

wanaomtaka lowassa - wapenzi, mashabiki na waumini wake - watuambie vita dhidi ya ufisadi ina umuhimu na uzito gani katika agenda za lowassa. Wakituambia kuwa "ni mojawapo" ya mambo atakayoyashughulikia tuendelee kumkataa kwa sababu bado atakuwa hajaelewa tatizo letu hasa ni nini kama taifa.

Nitandelea...

Nb: Kwa wageni wa hoja hizi warejee mada yangu ya 2007: kikwete siyo safi, yes i said it

ndugu yangu wewe ndiye umenena na hamasisha watu kujiandikisha huyu lowassa atayarudisha mafisadi wezake2,eti watu wanasema ile siyo kashifa yake alilibebeshwa2 sasa kama kweli mkweli na anapenda maendeleo ya nchi si angetoboa2 mbona kafulila alitoboa?,babu huyo watarudi wote hadi kina anthoni diaro bila kusahau rostoma na wengine kibao hafu nigekuwa mchawi ninge mpoteza huyu m2 anaboa sana…
 
Je, njia tatu Dar zitarudi? Na kwa nini ziliondolewa kimya kimya kama lilikuwa ni wazo zuri na pilot yake ilizaa matunda?
 
ndugu yangu wewe ndiye umenena na hamasisha watu kujiandikisha huyu lowassa atayarudisha mafisadi wezake2,eti watu wanasema ile siyo kashifa yake alilibebeshwa2 sasa kama kweli mkweli na anapenda maendeleo ya nchi si angetoboa2 mbona kafulila alitoboa?,babu huyo watarudi wote hadi kina anthoni diaro bila kusahau rostoma na wengine kibao hafu nigekuwa mchawi ninge mpoteza huyu m2 anaboa sana…

Uchaguzi mkuu huu unaelekea kuwa kati ya CHAGUA UFISADI (CCM) vs CHAGUA MABADILIKO (UKAWA). Tuingie mitaani na vijijini kuhamasisha kura ya "CHAGUA MABADILIKO".

Jambo moja linalonifariji kutoka upande wa CCM ni ile propoganda ya umri ('uzee' vz. 'ujana') kuyeyushwa na mapenzi waliyo nayo kwa EL. sasa hivi watakuwa wamebakiwa na propoganda moja tu ya udini.
 
Huyu hafai kuwa rais kama alifumbia ukweli was richmond kwa kulinda serikali itufisadi hataweza kuidhibiti rushwa na pia mfumo uleule hataleta mabadiliko.Watanzania tumeshafumbuka macho na masikio yanasikia
 
For this,lets put other issues aside.
Lowassa hafai kuwa rais wa Tanzania kwa wakati huu.
Labda baadae baada ya huu ufisadi kushughulikiwa IPASAVYO.
 
Mwanakijiji mzee wa kanzi leo hii amegeuka mwanasiasa bila data; Unajulikana kuwa uko TIMU Membe, Unajulikana kuwa ww ni Vatican Mkereketwa, unajulikana kuwa Mzee Mwanakijiji anajaribu kupotosha ukweli ulio wazi kuwa Kilimo kwanza ililetwa na USA kupitia UN organs FAO, UNDP kwa maslahi ya Land Grabbers wa Dunia hii!!! Leo hii watanzania wanamiliki sehemu ndogo sana ya ardhi yao wakati makampuni makubwa ya kimarekani yakimiliki malaki ya hekari na mengine yanawakodishia wananchi!!!! Mzee Mwanakijiji anajua kuwa tatizo kubwa la nchi hii ni 1. EHM 2. EHM 3. EHM wanaolazimisha hata Gesi yetu ichukuliwe na wageni... MM anajua kuwa Richmond ni mradi wa Marekani, anajua kuwa Lowassa hakubaliani na ujinga wa kuwanufaisha wageni kwanza then wananchi wapewe makombo au kutumiwa kama vibarua!!! MM anadai kuwa hajui kuwa sasa hivi tunatazo la ajira lililosababishwa na watu wa Vatican kwa kiasi kikubwa ... Itoshe kusema Mzee Mwanakijiji na EHM wengine hamtaweza kumzuia Lowassa kuingia Ikulu this time ..
Mkuu hapa umesema vizuri sana na kuonyesha kwamba UFISADI ndio adui yetu mkubwa kwa sababu kama Ufisadi huo wa nchi za Magharibi uliweza kuharibu KILIMO Kwanza utashindwa vipi kuharibu tena ELIMU kwanza ikiwa vichwa ni vile vile vinavyotegemea mikaakti ya nchi za Magharibi?.

La kujiuliza, hii sera ya KILIMO KWANZA ilitakiwa ifanyiwe vipi ktk Utekelezaji wake, vipaumbele viwe vipi badala yake hawa hawa wakauza ardhi ya nchi tena nakumbuka sana Lowassa alipokuja huku akiwa Waziri mkuu katika kuuza nchi akakutana na kundi la wawekezaji Wahindi akawaacha wananchi wakutane na mawaziri wenngine kina Karamagi yeye kenda zake Mexico kuuza nchi.

Kwa hiyo, Ukianza na uuzaji wa Richmond tena akidai kwamba hata Clinton alisifia kuwa mradi safi wakati hajui kwamba Clinton anafurahia shirika la Marekani kuwekeza Tanzania na hivyo kuongeza pato la nchi yake ktk GDP kama shirika lao nje. Ikumbukwe pia Waziri mkuu Harper wa Canada alipokuja nchini aliulizwa kama anaweza kutusaidia juu ya Barrick kutolipa kodi ama tupewe share kidogo kuuvunja mkataba wa Mkapa akasema yeye hawezi kuingilia makubaliano ya kibiashara baina ya Barrick na Tanzania.

Ufisadi hauna sura, Ufisadi sio kuiba tu fedha za Mashirika ya Umma na Benki kuu bali hata mikataba yao, kama unakumbuka mkataba wa Buzwagi kusainiwa Hotelini London na Karamagi ambaye leo Lowassa anamsifia kama mfano bora wa MaTajiri. Kuna haja gani ya Karamagi kuendesha kazi ambayo Bandari kama chombo cha Umma wanaiweza, huu kama sio kupeana ni kipi zaidi?. Na mikataba mingine mingi tu hao marafiki za ndio wenye kuunda share ama kushikiriki ili majina yao yasionekane katika umiliki japo ni wao. Mnataka muambiwe vipi jamani mfike mahala mseme basi imetosha Ufisadi lazima upigwe vita na kila Mtanzania maana mnalishwa kipande cha samaki tu wao wakiendelea wakivua..
 
Hilo nalo ni swali zuri sana.

Ila naona walau Mzee Mwanakijiji kafanya kitu ambacho mimi na wewe tunaweza tukakisambaza kwa tunaowajua wasio na uwezo wa kuifikia tovuti hii.
Yes! heri kusema kuliko kukaa kimya, heri kuwaambia kuliko kukaa kimya
Tusije aminishwa kuna Masiah mwingine kaja kumaliza matatizo ya nchi hii peke yake. Eti tunaambiwa malimau (lemon) na mchangwa hayapo kundi la Citrus! Tunachikona sana ni Limau, tunachouziwa ni Chungwa!
 
Mnapokosoaga walioonesha nia mtajage na mbadala wake!!
 
Mkuu

Kukaa kimya Watanzania wakilishwa peremende badala ya mlo si kuwatendea haki.

Jana nilikuwa naangalia BBC nikaona mgao wa mafuta katika taifa mwanachama wa OPEC Nigeria.

Sababu kubwa ni kutokana na ufisadi ambao umefikia mahala pa kuiweka serikali mateka
Kwa wasioona wanaweza kudhani hilo lipo Nigeria na kwingine.

Guess what! anayedhani hivyo anahitaji msaada wa wataalamu wa macho, masikiona ubongo. Tatizo lipo nchini na linaimarika kila siku

Ukubwa wake nchini ni zaidi ya Nigeria. Kule Nigeria tunafahamu ufisadi na utapeli ni sehemu ya maisha (norm)

Hapa kwetu limeingia kwa kasi kiasi kwamba, mafisadi wananunua na kuchagua nani aende Ikulu nani awe nani

Katika mkutano wa juzi Lowassa amesaidia wasiomjua. Ameeleza, pesa anazopata zinatoka kwa marafiki zake.

Utaratibu wa nchi yetu vyama hudhamini watu wao na kuendesha kampeni kwa niaba ya mgombea wao.

Ndilo chimbuko la ruzuku za vyama vya siasa. Sasa Lowassa anapotuambia anachangiwa na marafiki zake, je huo ndio utaratibu wa CCM wa siku hizi? Kwanini hakusimama ili sheria ya mgombea binafasi kama yeye ipite? Marafiki zake ni akina nani, wanamchangia ili iweje?

Kuhusu suala la Elimu, akiwa mbunge hakuna kumbu kumbu zinazoonyesha kama aliwahi kupingana na chama chake ndani ya vikao kuhusu kilimo kwanza au elimu kwanza.

Pengine ushahidi mzuri ungekuwa yeye kujiuzulu nafasi za uongozi kupinga sera zisizo sahihi. Hakufanya hivyo. Leo anaingia na sera yake

Hapa anatuambia, anachotaka kufanya si sera za wana CCM bali ana zake.

Ukichanganya na hoja ya kuchangiwa na marafiki, hakuna shaka kuna 'kachama' kake pembeni kanakohitaji 'label' au logo ya CCM

Lakini pia, tunataka EL atuambie, anasimama vipi katika ufisadi ambao ni tatizo linalodumaza Kilimo kwanza na Elimu kwa upana wake?

Huwezi kufanikisha sera ya elimu akiwa umefungwa mikono na miguu na mafisadi waliowekeza kumpeleka Ikulu

Tuna mahali pa kuanzia na si kutekwa na wafanyakazi wake wanaoaminisha umma, anafaa bila kutueleza kivipi.

Umeongea vizuri sana mkuu!
 
mtu ambaye hataweza kuwatia ndani mafisadi hatufaiiiiiiii
 
This time ccm wananyolewa upara kwa bati lenye kutu bila kutia maji nywele!. Watu walisema pelekeni mafisadi wa Richmondi mahakamani mkalindana ,leo wanasema walionewa,majuto mjukuu! Kina Kanywamaji wanatembea vifua mbele. October Ccm mnanyolewa.
 
Kamwe hautapata jibu...

Nimefuatilia mijadala kila kona leo watu wanasema Lowassa hafai lakini hakuna hata mmoja amependekeza anayefaa. Ni sawa na mzazi kuwaambia wanaye ugali na maharage ni chakula kibaya lakini hajanunua chakula mbadala. Nani anafaa jamani? Ina maana aliyepo Lowassa peke yake? Na kwa kuwa hafai tunamchagua hivyo hivyo?

We mbona mvivu wa kufikiri? Unataka kutafuniwa kila kitu? Hakuna spoonfeeding hapa JF. Umeshaonyeshwa njia...tembea mwenyewe...hakuna wa kukubeba
 
Back
Top Bottom