Lowassa anasafishwa!

Duh jamaa mi sikumwelewa anaongea nini pale, na niliwaambia ile kitu si live mana hata yeye anajua wananchi wana hasira naye. yani tulijiandaa na simu ana bahati sana huyu baba yeye anadhani anaweza kubaili mawazo ya watanzania kw sasa?na hao waliompokea nina mashaka ufisadi uliwapitia, mtz mwenye akili hawezi kwenda pale. wewe kiongozo wa ccm [mkoa unampokea kamanani kwa kweli sipati jibu na hao waliotandika red carpet sijui wamedata au?yetu macho ila 2010 si mbali watanzania tutachagua tunayeona atafaa.Ati kamati haikumtendea haki,alitaka aulizwe nini wakati alikubali yote yatokee chini yake.halafu anasema ndege ya tz inapaa?sasa imeanguka naye na asubiri hata huo ubunge atakosa mana original wamasai wataamua wanamtaka nani kati yake na sokoine


Hao waliotandika red carpet akili yao imeshughulikiwa na fedha za Richmonduli kiasi kwamba ile "Conscience" imewatoka na wanaendeshwa kwa "Remote Control" Ndege ya EL iliyokuwa inapaa ikiwa imebeba 'Mshiko"-152 Milioni za Watz imetunguliwa na Kombora la JF, hitima ikasomwa na Kamati Ya Mwakyembe.
 
1. Nina wasi2 Tz tunaelekea kuwa kama Nigeria kuwa rushwa na wizi na kupora kuwa ni poa na jamii inaonekana kuvumilia!

2. Je ni wangapi hadi sasa wamekamatwa over Richmond and EPA?

Nasema siku zote tunahitaji sheria za China for next 15-20 years- then ndo demokrasia ya magharibi. Demokrasia gani mtu anatuhumiwa kuiba mamalioni yet leo anapokelewa kwa zulia jekundu?

Je hii ni Monduli na Askofu KKKT kumpongeza kwa kuwaibia watu maskini? Hii demokrasia Muflisli ya Ulaya na US ambapo in over 50 years imeturudisha zaidi nyuma!

Is this ok?

We need Change.. Now!!!
 
Lowassa ni too senior kwenda kuwa balozi...
At most may be kwasababu kuna mwanamtandao UN (Dr. Migiro), kwa mtazamo wangu finyu, Lowassa anaweza pewa kazi ya heshima kusimamia mambo fulani serbia huko etc lakini Lowassa mwenyewe akitaka. Otherwise ni kubanana banana humu humu tu Tanzania.

Huko UN hawawezi kumchukua kwani ameshachafuka. Mahali pekee ambapo anaweza kupeta ni ndani ya siasa za Bongo. Sina hakika hata SADDC kama wanaweza kumuajiri.
 
Binafsi nafikiria haya mawili:

1. TVT hawakupaswa kumweka Ndugu Lowassa hewani kwa kuwa ni majuzi tu Ndugu Pinda alitueleza kwamba kaunda task force ya kufatilia namna ya utekelezaji wa ripoti ya Mwakyembe. Kitendo cha TVT kuruhusu Lowassa atumie chombo icho kujieleza/kujisafisha wakati bado task force ya Pinda haija-come out with resolutions ninakichukulia kama ni kitendo kinachojaribu kuvuruga maamuzi ya task force. Kitendo ichi pia kinaweza kufanya jopo la pinda kuwa biased towards Lowassa.

2. Kwa kuwa TVT ipo chini ya ofisi ya waziri mkuu, basi nina wasiwasi zaidi kuwa the outcome of investigation ya task force ya Pinda imeshakuwa wazi kwamba ndugu Lowassa is clean. Kama outcome ya investigation ingekua/itakua ni vinginevyo basi Mzee wa Security System (Pinda) angetumia IQ na uwezo wake wa kufikiri kuzuia taasisi iliyo chini ya mamlaka yake (TVT) isifanye ilichokifanya.

HITIMISHO:

Kwa kuunganisha mambo yaliyotokea within a very short period of time wakati watanzania wakisubiri kwa makini kuja kusikia Ndugu Pinda atatuelezaje kuhusiana na outcome of investigation of the task force aliyoiunda basi WaTZ tusishangae kuja kusikia kutoka kinywani mwa Ndugu Pinda kwamba Ndugu Lowasa is very clean na hakuhusika na Richmond. Ninafikiri ni bora ndugu Pinda aelezwe wazi kwamba sisi waTZ tumeshaishtukia "Danganya toto" yake.
 
Mugo"The Great";145531 said:
Hao waliotandika red carpet akili yao imeshughulikiwa na fedha za Richmonduli kiasi kwamba ile "Conscience" imewatoka na wanaendeshwa kwa "Remote Control" Ndege ya EL iliyokuwa inapaa ikiwa imebeba 'Mshiko"-152 Milioni za Watz imetunguliwa na Kombora la JF, hitima ikasomwa na Kamati Ya Mwakyembe.


Wewe Askofu…….please stay aside…………huu MZIKI (JF) huuwezi….ni mzito kweli kweli, tukiingia anga zako usije lalamika….maana ndioukuni huo huo unaosema……kwani itakuwa zamu yako kuungua

tehetehetehtehetehetehet..hahahahaha
 
Nadhani mchango wake ungekuwa na maana zaidi angechangia bungeni akiwa kama mbunge wa kawaida.

Haya mambo ya kukimbilia vichochoroni ( Yes.. TvT ni kichochoroni ) hayamsaidii chochote kujisafisha.

Ili mtu ujisafishe kwanza unatakiwa utumie maji safi, vyombo/nyenzo safi, na mikono yako iwe safi. Lowassa huwezi kujisafisha kwa kutumia tope unajichafua zaidi, better remain quite unawatia machungu watu bure..

Masatu are you back ? Karibu . Haya ndiyo mambo ya Monduli baadaye tutataka kujua mahela ya shughuli hii kama hakuna sehemu ya 152m kwa siku .
 
Ninavyoona mambo yanavyokwenda:

a)Haiwezekani yakawepo mabadiliko ya kwli ndani ya serikali. Yaani kinachofanyika ni watu kuchichanganya wengine katika harakati za kujitetea.

b)Wananchi wa hali ya chini hasa kule vijijini hawajui ni lipi linaloendelea na walio wengi ndo wapiga kura wanaopelekea kuwapa hawa jamaa ushindi wa unaoitwa "katrina na Tsunami".

c) Sasa ushindi wa "Tsumani" uliokuwa unaongelewa mwaka 2005 tumejua maana yake ni nini...maana yake ni kwamba watakomba kila kitu serikalini na mwananchi atabaki bila kitu...je Tsumani ya 2004 kule Indonesia, India, Maldvise...nk, mnakumbuka ilifanya nini...mpaka sasa watu wengi hawajarudi katika maisha yao ya hali ya kawaida.

d) Sasa ndo Tsunami ya kisiasa hapa Tanzania inavyotutafuna na kutuacha bila kitu...na bado maafa makubwa yanakuja...Tsunami Richmond, EPA...na kuendelea...

Haya jamani hakuna kulala...tufanye kazi na tuwafikie wale wenzetu ambao hawajafunuliwa tuwaweke sawa ili Tsunami namba 2 ikija iwakute wako macho na kuweza kupambana na madhara yake...

Pamoja tutaishinda Tsumani ya kisiasa Tanzania. Unajua ili gonjwa "FISADI" halina dawa ila kinga yake iko kwa wananchi wa vijijini na mijini hasa wale wanaoendelea kuteseka na Tsunami itokanayo na vijidudu na upepo unaoitwa FiSADI...na SISIEM, SISIEM, SISIEM...
 
Haya...mihela ya EPA na Richmond
 

Attachments

  • michKP.jpg
    michKP.jpg
    25 KB · Views: 52
Pesa za wananchi hzio ndugu...sasa analakiwa na umati ili iweje...nashangaa sana. Kwa kweli ni kufilikisa kimawazo na inaonyesha jinsi watu wetu walivyo na uwezo mdogo wa kufikiria...

Labda watu wa huko monduli wote ni Mafisadi?

Mwizi hashangiliwi kama shujaa, kwetu Manzese ni mawe na moto tu.
 
Eeeh bwana kwa taarifa yako hata kama Migiro yuko UN hawezi kuwa na influence yoyote ya kumuunganisha Lowassa ilo haliwezekani kabisa...kwani kuna watu kibao wenye uzoefu sana ambao Lowassa kwao ni mtoto...sana sana ana uzoefu wa hapo Tanzania lakini anga za kimataifa hamna kitu....wala usitarajie kitu kama hicho.

You are correct by content but my view was context based and therefore content was held constant.
 
Lunyungu,

Lete habari zaidi. Ila jamani acheni kuwaita Wamasai wote Richmond. Hii ya kuadhibu Wamasai wote shauri ya kosa la mtu mmoja sio sahihi kabisa.

Waliomshauri wamekosea, angetulia kwanza kama miezi kabla ya kujitetea kwenye TV. Watanzania sasa bado tuna hasira za kutuibia, hata aseme nini, hatuwezi kumwamini.

Bila kujali katendewa haki au hapana, kujiuzulu kwake kwa scandal ni somo zuri mno kwa viongozi wa TZ na faida yake ni kubwa kuliko hasara chache
kwa Lowassa.

Muda wake umepita na sasa tuangalie hao walioingia madarakani.

Mbona Pinda sasa karibu wiki mbili na hatuoni hata strategies mpya za kuifanya Tanzania ipae?


Wamasai Waache kumshangilia mwizi Lowassa.

Hebu fikiria Askofu Laizer na Nyali wote wameunganishwa na ujio wa mwizi wetu MH Lowassa huko Arusha.
Mchungaji na mwizi wote wanamshabikia Fisadi nani mchungaji na nani mwizi hapo?

Katika somo la Bilogy hiyo kitu inaitwa Fiendish Union.
 
Binafsi sioni hoja yoyote kwa Lowassa kujikosha TVT, ni haki yake maadam afahamu kwamba maoni yake yote yataweza kutumika against him in the court of law.
Kakanusha kabisa kuchukua Rushwa, sawa kwani hakuna mtu ama sehemu/ kipengele ktk report ya Mwakyembe inayomshutumu yeye kwa kuchukua Rushwa. Inaonesha wazi hakusoma vizuri ile report na muda wote huu kautumia vibaya kutofahamu yaliyomkuta zaidi ya kutafuta boya ya kuelea baharini.

Ukisoma maelezo yake kwa makini utaona dhahiri aliweka mkono wake ndani ya taratibu zote za Tender hiyo kiasi kwamba alifahamu kila hatua iliyofikiwa....Hii haikuwa kazi yake!..
Kisha ajabu ni kwamba maneno yote aliyoambiwa na wataalam aliyaona kuwa ni fix wakati wa Net group lakini sivyo ilipofikia kwa Richmond....Kwani Richmond hawakuomba muda zaidi?..kuna tofauti gani kati ya kampuni hizi mbili hadi yeye kuweka mguu wake ktk swala ambalo kwa ujinga fulani anadai ni malalamiko ya mitaani.. yaani fununu kama vile hakupelekewa maelezo ya kimaandishi kuhusu tender nzima ya Tanesco.
Again, hata hivyo bado anakosea kwani swala la Ufisadi huu, ni nani aliyetoa order baada ya Order kusisitiza Richmond kupewa tender hiyo?...Hakuna kipengele cha report kinachozungumzia kwa nini ilishindikana kuvunja contract.
Halafu anachozungumzia hapa ni wakati wa Net group.... wakati uhujumu wa Uchumi uliofanyiwa uchunguzi ni toka pale majina ya mashirika yenye uwezo wa kutuletea Umeme yalipoanza kuchujwa. Richmond ilikuwa kati ya makampuni yaliyo fail vibaya sana, lakini bado kutokana na shinikizo toka ofisi yake walipewa tender hiyo.
Uhalifu ilianza kabla hata contract haijawa signed na nadhani kama alikuwa hana mkono wake angeanza kuwaambia watu kushiriki kwake kabla/toka siku ya uchaguzi wa kampuni hiyo na sio baada uya kuwa signed..
What they (Richmond) could or couldn't hawezi jificha chini ya kivuli cha waziri ama wakubwa wenzake hali udhaifu wa Richmond ulikuwa wazi ktk report zote zilizotangulia.
Kama waziri mkuu hawezi ku rely on word of mouth, hali nyaraka zinazoeleza vizuri masharti yaliyotakiwa zipo na position ya Richmond ilijulikana.

Swali lilikuwa:- Kwa nini Richmond walipewa Tender hiyo?...Jibu la kamati lilikuwa ni nguvu toka ofisi ya Waziri mkuu. Hadi wakati huu hajajibu kabisa nafasi yake wakati tender ikitolewa..isipokuwa anazungumzia baada ya contract kuwa signed.
 
unajua lowassa anachezea watu akili, sababu anataka kuja kugombea urais uko mbeleni ndio sababu analeta habari hata za rais ahm.

issue ni simple sana, all lowassa has to do is;;;

tangaza mali zako zote wewe na familia nzima, ili wananchi tuone kama kweli mambo ya rushwa sio yako.

short of that unaleta wazimu na mchezo wa kuigiza kama degree uliyonayo.
 
Mvua....atawapelekea wamasai wenzake wakati anachunga nao...hakuna cha mvua wala manyunyu hapo....

Msee K, ikiwezekana pungusa ukali ya maneno yako sidi ya jamii ya Kimasai, nafikiri mfua ni jambo muhimu kwa makabila yote!! Hiyo mfua ya Richmond hatuitaki huku lengai

Kishaju,

Hiyo juu haijapendeza. Ukabila tena ndugu yangu duh. Tupunguze hasira katika kujenga hoja na tufikishe ujumbe pasipo kuwaumiza wasiohusika.

oooh samahani sana....kwa kweli sikuwa na nia mbaya na kosa kama ilo halitajitokeza sana....samahani kwa wote ambao wameguswa moja kwa moja...na ninaapa kwamba kosa kama ili ili halitatokea tena maana mafisadi wanatoka pande zote za Tanzania,,,
Kishaju, apology accepted. Now lead the way please!
 
Lowasa ni msanii kweli kweli.

Anasema kulikuwa na Dharura Tanesco hawakuonyesha kushughulikia suala hilo kidharura.
Tanesco walikuwa na Donge wakitaka wao wanunue mitambo ya kuzarishia umeme.

Kwa hiyo kwa uamuzu wake mwnyewe kama Waziri mkuu aliunda Government Negotiation Team. Hapo ndipo Kimbembe kilipo zaliwa.

Donge la Tanesco lilianza wakati gani? Baada ya yeye Lowassa kuwanyang'anya tenda au kabla?

Kama kazi ya kununua mitambo ya kuzarishia umeme ni yao Tanesco ni vipi wawe na Donge badala ya kuchangamkia Tenda?
Lowassa sijamwelewa hata kidogo!

Je ana ushahidi kuonyesha kwamba Tanesco walishindwa kufanya kazi hiyo?

Mitambo ya umeme ya Kidato na Mtera ilinunua GNT?

Hilo kundi lote la watu alowataja na Tanesco nani ana uzoefu na mitambo ya kuzarishia umeme?

Kwa nini asiunde tume ya kuhimiza au kuwa sukuma tanesco washughulikie tatizo hilo haraka?

Kwa nini yeye mwenyewe asitumie Rungu kuhakikisha Tanesco wanatoa kipa umbele kwenye kazi hiyo ya umeme wa dharura?

Yeye ndiye aliyemwingiza mwanasheria kwenye ununuzi wa mitambo ya kuzarishia umeme ili mambo yakiharibika amnawie kama anvyojaribu kufanya sasa.

Kwa nini Lowassa amegoma kutoa maelezo kuhusu kuwasiliana na rais?
Je Lowassa anamlinda Rais Jakaya Mrisho Kikwete kwenye hii soo?

Matamshi kwamba Richmond haina tatizo lolote yaliyotolewa na Lowassa kbala ya uchunguzi wa Takukuru na baada ya uchunguzi wa takukuru mbona yako kinyume na maelezo yake baada ya kujihuzuru?

Ni lini lijua kwamba Kaatibu mkuu kiongozi, mwanasheria na BOT na vingunge wote alowataja walimwingiza mjini?

Ni lini alijua kwamba Richmond ni kampuni hewa?

Kwa nini hakuwashikia Bango kama alivyozoea kuwashikia Bango wakuu wa wilaya akiwa ziarani?

Lowassa anaongea ukweli aua anaongezea uongo juu ya uongo wa awali?

Kwa nini leo hii Lowassa anawanawia viongozi aliowateua mwnyewe kushughulikia suala la umeme wa dharura?

Kamati ya GNT na yeye Lowassa nania likuwa na nguvu ya kusema NO?

Alipoonamuda unakwenda na RDC inashindwa hata kufungua aacount muhimu za awali kwa nini ofisi ya waziri mkuu isichukue jukumu la kuichinguza RDC bila kupitia ofisi nyingine ya serikali?

Ni kwlei alipata maelezo kutoka kwenye magazeti au kutoka JF na matangazo ya KLH au Mwankijiji?

Sisi JF tulipochunguza na kubaini kwamba RDC ni kampuni fake na kutoa Anuani yao na ukweli kwamba Mohamed Gire anamiliki Printing Company jambo lilokuwa ukweli mtupu mbona alisema tuna wivu kama tumenyang'nywa mchumba?

Kwa nini amejibu swali kuhusu mmiliki wa Dowan na RDC kwamba hamjui je hiyo si uongo?

KWa hiyo Lowassa alipokataliwa msimamo wake aliamua kuungana na kamati ya GNT na kukubali yote waliyosema na kusimamam kidete kusema RDC ni kampuni swanu sasa leo analia lia nini?

Kuna sentensi moja ambayo Lowassa amesema uongo juu ya taarifa ya kamati ya Dr Mwakyembe. Amesema kamati lisema yeye Lowassa ndiye aliyetia saini mkataba wa RDC jambo ambalo anadai si kweli.
Sentensi hiyo ya Lowassa ni ya uongo kabisa kamati ilisema yeye Lowassa alitoa shinikizo la kiserikali na kuwaamuru Tanesco kusaini mkata wa RDC.
Kwa nini Lowassa nasema uongo juu ya hilo?

MH Kikwete naye anasuasua katika kutoa maelezo juu ya kuwajibika kwa waziri mkuu.
Waziri mkuu amewajibika kwasababau niu yeye aliyeamua kulivalia njuga suala la umemem kwa kulinyakua toka mikononi mwa Tanesco la kuliweka chinya kamati ya GNT ambayo aliiunda na kuiendesha Kiimla. Lakinkwa sababau kimekunywa sasa anaona ni bora kila mtu aingie kwenye dimbwi chafu hata kama ni yeyey Lowassa ndiye muhusika mkuu.

Ninyi watu wa TVT ni mamruki kabisa, mmeshindwa kumwuliza maswali ya maana mnamwacha anajieleza huku akipindisha ukweli mbele ya Kamera zenu.
Naona nguvu ya Agenda 21 imeanza kufanya kazi.

Ole wenu safari hii wengi mtakwenda na maji.
 
Habari ambazo zimepatikana hivi punde kutoka kwa chanzo chetu zinasema kwamba,kuna baadhi ya waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali vya habari inasemekana wamehongwa na mmoja wa aliyekuwa waziri ktk baraza la mawaziri lililovunjwa aliyekuwa anahusishwa na ufisadi wa richmond ili wamsafishe kwa kumwandika vizuri na kuwa tume haikumtendea haki,chanzo chetu kinasema kuwa waandishi hao wenye roho za kimaskini na wasio na uchungu na nchi yao wamehongwa kiasi kikubwa cha pesa na hivyo wamehaidi kuifanya kazi hiyo.kwa mtindo huu jamani ufisadi utaisha?


Hii yote ni kuendekeza tamaa.

Hao waandishi (kama wapo), wao pia ni MAFISADI.

Shame on them.
 
lowassanandege.jpg


Aliyekuwa Waziri Mkuu Bw. Edward Lowassa (Monduli-CCM)hatimaye akishuka kwenye ndege yake ndogo iliyotua mjini Arusha akielekea kijijini kwake kuzungumza na wapiga kura wake. Picha kwa hisani ya Mroki Mroki
 
Aliyekuwa Waziri Mkuu Bw. Edward Lowassa (Monduli-CCM)hatimaye akishuka kwenye ndege yake ndogo iliyotua mjini Arusha akielekea kijijini kwake kuzungumza na wapiga kura wake. Picha kwa hisani ya Mroki Mroki

Lowassa ana ndege siku hizi?
 
Back
Top Bottom