Lowassa anasafishwa!

Lowassa anasafishwa!

Je, ilikuwaje kila mara wabunge walipohoji mkataba wa Richmond ulikuwa unawazuia wasifanye hivyo!? Ulikuwa unafanya hivyo kwa maslahi ya Tanzania, CCM au wewe mwenyewe? Hili la Netgroup Problems Watanzania wengi tulilijua tangu mwanzo. Kampuni ambayo ilikuwa inashughulikia kuuza stationery na ambayo haijui lolote kuhusiana umeme kwenda kupewa management ya shirika kubwa kama TANESCO ilikuwa ni ufisadi wa hali ya juu, lakini wakati huo hatukukusikia kusema chochote kupinga uamuzi huo, kwani ni dhambi kuwa upande mmoja na wananchi katika kupinga maamuzi yasiyo na maslahi kwa wananchi?

Watanzania wengi wakiwemo wafanyakazi wa TANESCO tulilipinga kwa kila hali hadi ikabidi waingizwe TANESCO wakiongozwa na FFU na mtutu wa bunduki, na hatima ya makaburu hao kupewa management ya TANESCO tunaijua pamoja na kulipwa mabilioni ya pesa ambazo hawakustahili.


Posted Date::2/23/2008
Lowassa ajitetea kutopata chochote kutoka Richmond
*Asema ni mkewe pekee aliyejua kuwa atajiuzulu
*Askofu Laizer akataza Wamasai kuitwa Richmond


Na Daniel Mjema, Arusha
Mwananchi


WAZIRI Mkuu mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli, Edward Lowassa jana alipokelewa kama shujaa katika uwanja mdogo wa Arusha na katika Jimbo lake la Monduli huku msafara wake ukikadiriwa kuwa na magari zaidi ya 100.

Akihutubia katika mkutano wa hadhara jimboni kwake, Lowassa alisema jana kuwa, alikuwa amesubiri kwa hamu na kwa muda mrefu siku hiyo ili aeleze kile anachokifahamu kuhusu kampuni ya Richmond Devolopment iliyomfanya ajiuzulu.

“Siku nilipoamua kujiuzulu nilimuuliza mke wangu uko tayari? Na yeye akaniuliza na wewe uko tayari?Niwaambie ukweli hakuna mtu mwingine zaidi ya mke wangu aliyekuwa anajua nakwenda kujiuzulu,” alisema Lowassa.

Akizungumzia suala la Richmond, Lowassa alisema ukame wa mwaka 2006 ulifanya taifa kuwa na tatizo la umeme. Kutokana na tatizo hilo, serikali iliamua kutafuta mitambo ya dharura.

Wakati Serikali ikifanya hivyo, wataalamu wakamuarifu kuwa liko tatizo la kupata mitambo hiyo kwa sababu mingi ya mitambo hiyo ilikuwa ikipelekwa nchini Iraki.

“Ikumbukwe kuwa Net Group Solutions wakati huo walikuwa wameomba kuongezewa muda wa kuendelea kuliendesha shirika la umeme TANESCO wakakataliwa hivyo wakawa na usongo na Serikali, ” alisema na kuongeza;

"Tulivyokazana kuwaambia waagize mitambo hiyo, wao walikuwa wanapiga chenga ili ionekane kuwa bila wao isingewezekana kupata mitambo hiyo…hapa tukagundua kuwa wanatuhujumu.”

Lowassa alifichua kuwa, ndani ya Net Group Solutions kulikuwepo na baadhi ya mabosi wa kampuni hiyo ambao nao walikuwa na nia ya kuagiza mitambo hiyo kwa maslahi yao jambo ambalo yeye alilishitukia.

Waziri Mkuu huyo aliyejiuzulu alisema, hapo ndipo walipoamua kuachana na TANESCO na kuamua kutumia timu ya wataalamu wa Serikali wakiongozwa na Mwanasheria mkuu wa Serikali Johnson Mwanyika.

Alisema baada ya kupatikana kwa kampuni ya Richmond alianza kusikia minong’ono huku vyombo vya habari vikiandka juu ya kuwepo kwa matatizo katika mchakato mzima wa kuipata kampuni hiyo.

“Nikaanza kusikia minong’ono nikamwita Waziri mwenye dhamana(Hakumtaja kwa jina) nikamuuliza mbona naanza kusikia harufu mbaya kuhusu Richmond lakini Waziri akanihakikishia kila kitu kiko sawa,” alisema.

Kadri siku zilivyozidi kelele juu ya Richmond zikazidi hivyo akaamua kuwaita wakubwa wote serikalini wakiongozwa na katibu mkuu kiongozi, Philemon Luhanjo na kuwambia waangalie uwezekano wa kuvunja mkataba huo.

Lowassa alijitetea kuwa, wakubwa hao wakaomba awape muda wa saa moja kupitia vipengele vya mkataba huo na baada ya hapo walikuja na maneno kuwa isingewezekana kuvunja mkataba huo kwani serikali ingepata hasara.

“Lakini mimi niliwauliza mbona tumevunja mkataba na City water wakaniambia aah mzee achana na hilo jambo kwa sababu liko mahakamani, hii ndio hali halisi ya mkataba wa Richmond,"alisema Lowassa.

Alisema binafsi amekubali kuwajibika kwa makosa ya walio chini yake lakini alirejea kauli yake kuwa kamati teule ya Bunge haikumtendea haki kwa kutomhoji kwani anaamini kama ingemhoji isingeandika taarifa kama ile.

"Niliona nisipoachia ngazi hali ya mambo katika chama changu ingekuwa mbaya. Napenda niweke jambo hili sawa kuwa sikuwajibika kwa sababu nilipata chochote Richmond.”

Lowassa aliwataka wananchi wa Jimbo la Monduli kutembea kifua mbele, huku wakitambua kuwa yeye hajawahi kupokea rushwa wala hana mpango wa kufanya hivyo bali amewajibika kwa makosa ya walio chini yake.

Kwa upande wake, Askofu wa Dayosisi ya mkoani Arusha ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania(KKKT), Thomas Laizer alitumia nafasi huyo kuwapiga vijembe wale wanaodhihaki kujiuzulu kwa Lowassa.

“Ukuni ulioko kwenye kona usiucheke ukuni ulioko jikoni ukiungua kwa sababu nao unasubiri kuungua,”alisema Askofu Laizer bila kufafanua lakini akashangiliwa na mamia kwa maelfu ya wananchi waliohudhuria mkutano huo.

Hata hivyo baada ya kijembe hicho ndipo Askofu Laizer alipotoa kauli yeye utata akitaka kila mtu abebe mzigo wake na akakemea tabia iliyoibuka hivi sasa ambapo kila Mmasai anayeonekana mjini anaitwa Richmond.

“Kuhusu ufisadi na rushwa sisi hatujui kilichotokea lakini kama ni ufisadi basi tunaungana na Rais Jakaya Kikwete kupita vita rushwa…kejeli dhidi ya wamasai kuitwa Rinchmond haifai kila mtu anabeba mzigo wake,” alisema.

Lowassa aliwasili katika uwanja mdogo wa ndege wa Mjini Arusha saa 6:51 mchana na kulakiwa na viongozi mbalimbali wa chama cha mapinduzi(CCM) na wale wa kidini pamoja na umati mkubwa wa wananchi.

Katika eneo hilo la uwanja, makundi ya vijana,wanawake na wanaume wakiwa wamebeba mabango mbalimbali ya kumkaribisha Lowassa huku mengine yakimtambulisha kama Shujaa wa karne.

Baadhi ya mabango hayo yalisomeka ‘Shujaa wetu umeonyesha mfano usife moyo, Tupo pamoja nawe, Wana Monduli tunakuamini na Mheshimiwa Lowassa wewe ni Mbunge wetu 2005-2025.”

Mara baada ya kusalimiana na baadhi ya viongozi na wananchi waliojitokeza kumlaki uwanjani hapo, Lowassa alipakia katika gari aina ya Toyota Landcruiser likiwa limewekewa ngao ya jadi mbele ya namba za usajili za gari hilo.

Msafara wa Lowassa ambao haujawahi kuonekana kutokana na wingi wa magari na wananchi ulianzia katika uwanja huo wa ndege huku magari yakifunga barabara ya Arusha-Monduli yakitembea pande zote mbili za barabara.

Hii ilifanya magari yaliyokuwa yakitokea Babati, Hanang, Mto wa Mbu, Karatu na mikoa mingine kwenda Arusha yanayotumia barabara hiyo kujikuta yakiegeshwa pembeni ya barabara ili kupisha msafara huo.

Alipofika Jimboni kwake alikwenda moja kwa moja hadi nyumbani kwake na kupumzika kwa muda kisha alikwenda katika eneo aliloandaliwa kuhutubia huku akiwa ametandikiwa zulia jekundu kama viongozi wa kitaifa.
 
Hii nimenakili kwenye hansard za tarehe 7 feb 2008, kikao cha saa 11 jioni baada ya Lowassa kutangaza asubuhi yake kuwa anajiuzulu.

(Saa 5.11 Asubuhi Bunge lilifungwa mpaka Saa 11.00 Jioni)
(Saa 11.00 jioni Bunge lilirudia)

SPIKA: Waheshimiwa Wabunge…!

MHE. LUCAS L. SELELII: Mheshimiwa Spika, Kuhusu utaratibu!

SPIKA: Kuhusu utaratibu Mheshimiwa Selelii Kanuni ipi?

MHE. LUCAS L. SELELII: Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Mwenyekiti wa Kamati Teule ya Bunge, nasimama kuhusu utaratibu chini ya Kanuni ya 59 (d) ili niweze kutoa taarifa inayotokana na Kikao chetu cha dharura cha Kamati Teule leo hii kuhusu mchango uliotolewa na Waziri Mkuu leo asubuhi ambao bila ufafanuzi kutoka kwenye Kamati Teule unaweza ukalipotosha Bunge lako na kuathiri mwenendo wa mjadala.

SPIKA: Hujawa wazi, unajaribu kusema kwamba alipochangia Mheshimiwa Waziri Mkuu kunahitajika ufafanuzi?

MHE. LUCAS L. SELELII: Mheshimiwa Spika, ndiyo na ndiyo maana nimetumia Kanuni ya 59 (d).

SPIKA: Sawa, endelea.

MHE. LUCAS L. SELELII: Mheshimiwa Spika, nakushukuru sana kwa kunipa nafasi hii ili niweze kutoa maoni kwa niaba ya Mwenyekiti wa Kamati Teule ya Bunge lako Tukufu ambayo tulifanya Kikao cha dharura mchana huu baada ya kusitisha
shughuli za Bunge mchana.

Mheshimiwa Spika, kwanza Mheshimiwa Waziri Mkuu ameituhumu Kamati Teule kwamba imesema uongo ndani ya Bunge na kumsingizia. Katika taarifa yetu yenye kurasa 165 hakuna sehemu hata moja tuliyosema uongo au kumsingizia, hivyo tunadai uthibitisho wa kauli yake au ifute kauli hiyo, vinginevyo Kamati teule itachukuwa hatua chini ya Kanuni ya 63( ya Kanuni ya Kudumu za Bunge, Toleo la 2007. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, Waziri Mkuu amedai kuwa kitabu cha viambatisho cha Kamati teule kimejaa majedwali pamoja na magazeti mengi mpaka ya udaku lakini kwenye maelezo ya Waziri Mkuu hakuna hata moja. Tunamtaka Waziri Mkuu aseme hayo magazeti ya udaku ni yapi katika taarifa yetu. Vilevile kitabu cha Kamati Teule cha viambatisho kina jumla ya nyaraka 104, hiki hapa chenye uthibitisho wa hoja zetu zote za msingi. Ili kuwapunguzia kazi Wabunge kuzitafuta nyaraka hizo zinazomhusu Waziri Mkuu kwenye kitabu hiki nimezitenga chache na naomba kibali chako ili nyaraka hizo zigawiwe kwa Waheshimiwa Wabunge sasa hivi. Zote zinatoka, viambatisho vyote tumeviweka katika taarifa yetu.

SPIKA: Itabidi nivione mezani kujiridhisha.

MHE. LUCAS L. SELELII: Mheshimiwa Spika, sawa. Aidha, Waziri Mkuu amedai alikupa wewe ushahidi wa maandishi ambao Kamati Tuele haikuujumuisha kwenye taarifa yake ya mwisho. Naomba tuwe wakweli, ushahidi huo wa maandishi anaouongelea Waziri Mkuu ni barua yenye Kumbukumbu Namba PM/P/567/2/40 ya tarehe 21/09/2006 yenye kurasa mbili ambayo Waziri Mkuu alimwandikia Waziri wa Nishati na Madini wakati huo Mheshimiwa Dr. Ibrahim Msabaha, Mbunge, akimshauri awe mwangilifu na Kampuni ya Richmond, kampuni ambayo yeye mwenyewe aliiteua tarehe 21/06/2006.

Mheshimiwa Spika, barua hii tuliipata tarehe 28/01/2008 kupitia kwako tukiwa hapa hapa Dodoma. Kamati Teule isingeweza kuitumia barua hiyo kwenye taarifa yake kwa sababu mbili kubwa. Kwanza, Taarifa ya Kamati Teule ilikuwa imekwishawasilishwa kwako Mheshimiwa Spika tarehe 31/12/2007. Hivyo isingekuwa rahisi kwa Kamati Teule kuichomeka barua hiyo kwenye Taarifa iliyokwisha wasilishwa kwa Spika.

Mheshimiwa Spika, kama mchezo huo unafanyika sehemu nyingine, kwa Kamati Teule hii ikiongozwa na Mwanasheria aliyebobea, Wajumbe makini wenye nia njema kwa taifa hili na Sekretarieti yenye usiri mkubwa na uaminifu mkubwa mchezo huo usingewezekana. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, pili, hata kama tungeitapata hiyo barua kabla hatujawasilisha taarifa kwa Mheshimiwa Spika, isingemwondoa kabisa Mheshimiwa Waziri Mkuu kwenye lawama. Ni barua hiyo hiyo ambayo ilinukuliwa na Gazeti la Rai la tarehe 12/04/2007, inatamka nanukuu: "Kama unavyofahamu yapo maneno mengi sana yanayosemwa kuhusu uwezo wa kampuni tajwa kuagiza Gas turbines kama alivyopewa
Mkataba wa TANESCO baada ya kushinda zabuni." Yameandikwa pia katika Gazeti la This Day la jana. Barua hiyo ambayo aliisaini yeye mwenyewe kuthibitisha kwamba alifahamu kuwa Richmond haikuwa na uwezo wa kifedha wa kuagiza gas turbines, ajabu ni kwa nini aliendelea kukaa kimya kwa kuachia maamuzi ya kuahirisha Mkataba huo baada ya kuuvunja ili kulisaidia Taifa kuokoa fedha za walipa kodi? (Makofi)

Mheshimiwa Spika, Waziri Mkuu amedai hakutendewa haki kwa kutoitwa na Kamati Tuele. Hii si Kamati ya kwanza kumhusisha Waziri Mkuu. Mara ya kwanza ilikuwa kwenye suala la Mheshimiwa Malima na Ndugu Mengi ambapo Waziri Mkuu alidaiwa kuwatuhumu Wabunge kwa kupokea rushwa. Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge ilipotaka Waziri Mkuu aitwe kwenye Kamati hiyo ya Bunge ulitumia busara zako na kuishauri Kamati hiyo kutomwita kutokana na nafasi nyeti aliyonayo Waziri Mkuu katika uongozi wa taifa, Waziri Mkuu hakulalamika. Kwa busara hiyo hiyo Kamati Teule haikutaka kumwita kwa kuwa ilikuwa na ushahidi unaojitosheleza. Naomba Waziri Mkuu na Wabunge wengine waisome taarifa ya Kamati Teule na viambatisho vyake kwa makini kuanzia mwanzo mpaka mwisho na Kamati tuele tumegundua kuwa Waziri Mkuu hajasoma taarifa hiyo kwa makini. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, jambo la nne. Katika sura ya sita ya Taarifa uk. 125 – 144, Kamati imeeleza bayana kuwa wamiliki na Richmond ni akina nani. Hakuna hata sehemu mmoja tuliyemtaja Waziri Mkuu anamiliki Richmond. Richmond ni Kampuni ambayo sisi wajumbe ambao ulituteua kwenye Kamati hii na ningependa kulisema kwa faida ya Watanzania wote waelewe na watazamaji wanaotuangalia sasa hivi kwamba ni kampuni inayohusika na Printing. Ni Printer, kwa Tanzania hii unaweza kuifananisha na Masumin. Sisi hatujasema Richmond inamhusu Waziri Mkuu wala hatujasema Richmond inahusu viongozi wengine. Kwa hiyo, tunaomba Wabunge wote na viongozi wote someni taarifa hiyo, inajitosheleza kwa maelezo yote mtaelewa. Ningeomba Idara yako ya Hansard isambaze viambatisho vyote ili Wabunge wote waweze kuelewa ukweli ambao tumeupata kwa kuchunguza jambo hili ambalo tumemtanguliza Mwenyezi Mungu.

Narudia kumtaka Waziri Mkuu kufuta kauli yake ya asubuhi au athibitishe, ahsante sana.
(Makofi)

SPIKA: Mheshimiwa Selelii umesema maneno mengi sana lakini pia Mheshimiwa Waziri Mkuu katika mchango wake nae pia alisema mengi tu. Sasa tunapodai kwa mujibu wa Kanuni kauli ifutwe ni lazima tuwe mahususi kwamba ni ipi.

Ama sivyo itakuwa sasa hatuelewi na ingekuwa vizuri tu ukatamka hilo ambalo unaona kwamba si sahihi ili tuendelee baada ya hapo.

MHE. HALIMA J. MDEE: Mwongozo wa Spika!

SPIKA: Subiri kwanza msiwe na haraka.

MHE. LUCAS L. SELELII: Mheshimiwa Spika, nakushukuru tena kwa kunipa nafasi hii kufafanua. Kauli ya kwanza ambayo tunapenda Mheshimiwa Waziri Mkuu aifute ni ile ya kusema tumesema uongo na kumsingizia. Ukichukua hata hansard ambayo amezungumza leo asubuhi, maeneo hayo amesema uongo na taarifa yetu hii ni ya uongo na ni jambo la kumsingizia. Jambo la pili ambalo tunataka Waziri Mkuu athibitishe ni yale magazeti ya Udaku ambayo tumeyatumia kwenye taarifa yetu ambayo alisema kwamba taarifa yetu imejaa magazeti mengi ya Udaku. Kwa hiyo, na hilo tunapenda athibitishe kuweza kutuambia kwamba ni magazeti gani ambayo ya Udaku.
Jambo la tatu ambalo Mheshimiwa Waziri Mkuu athibitishe ni lile ambalo amesema hatukumtendea haki kwa sababu hatakuunganisha ushahidi wake aliokupa wewe kwenye taarifa yetu, wakati sisi tumekupa taarifa yetu tarehe 31/12/2007 na wewe umetupa barua aliyotoa ushahidi tarehe 28/01/2008. Ni hayo tu.

SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, nadhani hapa naliondoa hili suala la magazeti ya Udaku kwa sababu haliihusu Kamati moja kwa moja. Maneno haya si ya msingi sana na kuhusu barua pia ni suala la fact. Nadhani la msingi ni kwamba matamshi ya Waziri Mkuu kwamba Kamati Teule imesema uongo na kumsingizia. Hilo ndilo la kutaka ufafanuzi. Kwa hiyo, namwita Mheshimiwa Waziri Mkuu.

WAZIRI MKUU: Mheshimiwa Spika, ahsante sana kwa kunipa nafasi nijibu hoja ya Mheshimiwa Selelii. Mimi nilifikiri nimeanza mjadala, mambo haya kwa kweli ni sehemu ya mjadala. Suala lile la uongo na kunisingizia, kusingizia nadhani libaki, uongo niliokuwa namsumbua Mheshimiwa Selelii ambalo amelisema sasa hivi, kuna mstari kwenye Kitabu chenu mnasema, "Kampuni ya Richmond ni ya Mheshimiwa Waziri Mkuu na swahiba wake Rostam Aziz." Hiyo ndiyo sentensi ambayo nimeiona na kwa maoni yangu siyo sahihi. Kama hiyo sentensi haipo na ina maana nyingine basi naweza kuiondoa lakini maana yangu ilikuwa hiyo. (Makofi)

SPIKA: Namshukuru sana Mheshimiwa Waziri Mkuu kwa ufafanuzi huo, nadhani wametupa mwanya hapo. Tusitangulize huo mjadala kwa maana ya kutafuta utaratibu, nadhani cha msingi hapa tuendelee na utaratibu tuliopanga kama ni uongo utajulikana tu. Nyinyi ni wengi hapa, mmeomba watu 44 kuongea, kama kuna la ukweli na uongo yatagundulika humo humo na haizuii wakati wowote Mbunge yeyote akibaini kati ya haya kuweza kusimama kuhusu utaratibu.

Nitamruhusu na tutaendelea kwenda mbele. Naona tusigande hapa tukibishania jambo moja ambapo tuna michango ambayo naitazamia kutoka kwa Waheshimiwa Wabunge 44.
 
Hapa mama Kilango-Malecela akaamua kumkoma nyani giladi, mchana kweupe!

MHE. ANNE. K. MALECELA: Mheshimiwa Spika, kwanza nashukuru kuwa msemaji wa kwanza lakini mtaniwia radhi kidogo nitakohoa. Naomba nitoe pongezi za dhati kabisa kutoka kwenye moyo wangu kwa Kamati Teule tuliyoiomba sisi wenyewe na ukaiunda wewe kwa kufuata taratibu na Kanuni za Bunge hili kwa kutuletea taarifa ambayo naomba niiunge mkono asilimia mia moja. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, Mbunge ni mchaguliwa au ni mwakilishi wa wananchi, sisi wote tulikaa hapa ndani ni Tanzania ikijumlisha Tanzania Visiwani na Bara. Wananchi wa Tanzania wanatutegemea kuliko tunavyofikiri sisi wenyewe na wanategemea tuwatendee haki lakini naomba nizungumze ukweli kabisa hata kama ukweli huo uta-cost ndiyo kazi ya siasa. Wenzetu watendaji wa Serikali wametutia aibu! (Makofi)

Mheshimiwa Spika, nimetumia muda wangu mwingi sana kusoma hivi vitabu, yote waliyozungumza kwenye taarifa ya Kamati Teule yana vithibitisho. Kuanzia Waziri Karamagi, Waziri Msabaha, Waziri Mkuu pamoja na Mwanasheria Mkuu, hakuna kitu ambacho hakina kithibitisho. Nitavitoa vichache hapa, kwa sababu nina wasiwasi kuna wengine hawajakipitia kitabu hiki. Mimi nimekwenda Hansard kwa sababu nipo serious.
(Makofi)

Mheshimiwa Spika, naomba nianze kwa kumnukuu Mheshimiwa Rais Jakaya Kikwete alipokuwa Pemba juzi tarehe 3 mwezi huu. Alikiri mwenyewe kwamba kuna viongozi wasio waadilifu, wametuponza. Naomba kwa ruhusa yako ninukuu maneno machache aliyosema. Alisema hivi: "Imani ya wananchi kwa viongozi inaanza kupungua kutokana na ukosefu wa uadilifu na uaminifu hali ambayo inahitaji kushughulikiwa haraka kabla haijawa mbaya." Mwisho wa kunukuu. Hili ni gazeto la Habari Leo na ni gazeti la Serikali si gazeti la Udaku. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, Rais alikwishaona matatizo haya tuliyonayo hapa, mimi nilisimama siku moja hapa nikauliza swali la Richmond kwa sababu nilikuwa ninajua hiki kitu kipo. Saa hiyo hiyo niliandikiwa barua na kuitwa, "njoo, usiseme hili neno hapa ndani". Kwa nini? Mtoto ukimwambia acha unamtuma, basi mimi ndiyo nilianza kazi, nilienda TANESCO nikachukua documents zangu, nilihangaika kila kitu nikachukua.

Mimi niligundua mapema kwamba si mchezo msafi; na yule aliyeniandikia barua naomba nimsihi asirudie kuwaandikia barua Wabunge. (Makofi)

Wabunge tunapozungumza mambo ya nchi, taifa, yanayogusa wananchi tuachwe tuseme. Mimi ni Mbunge wa Chama cha Mapinduzi, kazi yangu ni kuishauri Serikali na kuisimamia. Hivi mnataka nimwachie Zitto Kabwe? No! Mimi mwenyewe nitaisimamia Serikali yangu ili iendelee kutawala. Inapokosea niikosoe ili iendelee kuwa madarakani, siwezi kumwachia Zitto Kabwe hata siku moja! (Makofi)

Mheshimiwa Spika, naomba niseme ukweli kitabu hiki wapewe Wabunge wote.

Ukiangalia barua zilizokuwa zinatoka kwa Waziri Msabaha, zinakwenda kwa Waziri Mkuu nyingine sijui kwa Waziri Karamagi, utagundua kuwa wenzetu walikuwa wanatuchezea. Wakati mwingine Mawaziri wanakaidi hata amri au matamko yanayotoka kwenye Baraza la Mawaziri linaloongozwa na Mheshimiwa Rais. Baraza la Mawaziri linasema Songas, kesho yake Waziri anaandika hapana ni Richmond. Sasa hapo mtu anasema ameonewa nini? (Makofi)

Mheshimiwa Spika, siwezi kupitia vilelezo vyote, vyote viko hapa. Mimi sikulala jana si kwamba nakohoa, sijalala! (Kicheko)

Mheshimiwa Spika, kwenye hiki kitabu kuna barua pia za Waziri Mkuu, kuna barua zinatoka kwa Mheshimiwa Msabaha anasema; "Jamani kama nilivyoagizwa na Mheshimiwa Waziri Mkuu..." Zipo hapa na tena nimeziwekea alama. "Kwa Katibu wa Waziri, Nishati na Madini Bungeni Dodoma". "Ununuzi wa mitambo mipya" sijui nini!

"Tafadhali rejea Dokezo Sabili la tarehe 10/06/2006 la Waziri wa Nishati na Madini, Mheshimiwa Ibrahim Msabaha kwa Mheshimiwa Waziri Mkuu, kuhusu ununuzi wa mitambo mipya wa Megawati 100 Ubungo. Mheshimiwa Waziri Mkuu ameagiza ...."

Mambo yapo hapa! Sasa Waheshimiwa Wabunge hamjasoma kwamba Mheshimiwa Karamagi anahusika, ni kweli na Mheshimiwa Msabaha anahusika, ni kweli, na wote ni marafiki zangu hawa! Lakini linapofika jambo la nchi sina urafiki na mtu hata angekuwa ni John Malecela! (Makofi/Kicheko)

SPIKA: Mheshimiwa unaweza ukakosa pa kulala leo! (Kicheko)

MHE. ANNE K. MALECELA: Mheshimiwa Spika, tukubaliane kabisa wananchi wameanza kupoteza imani na Serikali ya Chama Cha Mapinduzi kama alivyosema Rais. Wananchi wameanza kupoteza imani na Wabunge wa Chama cha Mapinduzi, tunazomewa kwamba hatufanyi kazi tuliyotumwa. Tunaomba tuwahakikishie wananchi kuanzia leo kazi ni moja tu, tukimaliza hili tutaleta la TICS. Yote tutaondoa na kusafisha Serikali yetu ya Chama cha Mapinduzi lakini kwamba tukiache Chama cha Mapinduzi kife au Serikali ya CCM iharibike kwa sababu ya kumpendelea mtu hilo sitafanya. Mkono wangu wa kulia utakibeba Chama cha Mapinduzi na Serikali ya CCM, mkono wa kushoto marafiki zangu nitawakosoa ili Serikali iendelee kuwa safi. (Makofi)

Mheshimiwa Waziri Mkuu ni rafiki yangu, Mheshimiwa Msabaha ni rafiki yangu, Mheshimiwa Karamagi tuligombana kwa sababu ya Richmond hii hii, kwa hiyo, hatuna urafiki kabisa! (Kicheko)

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, ndugu zangu naomba niseme kwamba tusipoteze muda, viongozi tunawakosea wananchi wetu. Sasa hivi Mtanzania amebebeshwa mzigo mkubwa sana wa bei ya umeme na Richmond na huu mkataba mbovu kuliko yote wa Richmond. Mkataba huu kwanza Baraza la Mawaziri lilisema uwe wa mwaka mmoja ukapindishwa ukawa wa miaka miwili. Miezi sita baada ya kuingia Mkataba mabwawa yakajaa na Mtera ikajaa kufurika, kwa hiyo, sasa ikawa hakuna haja ya hii mikataba tena kuendelea na wa Richmond ambaye dada yake ni Dowans. Sasa wako wamekwishafunga mitambo yao wanatudai sasa kila siku! Naomba ninukuu kitabu hiki: "kwa mujibu wa mkataba Richmond Development Company inalipwa dola za kimarekani 121,811 sawa na shilingi za Tanzania 152,264,000 kwa siku kama gharama za kudumu za uwezo wa mitambo yao (capacity charge). Fedha hizi zinalipwa kila siku bila kujali kama Richmond imezalisha umeme au la". Anayelipa ni TANESCO na TANESCO anapolipa lazima hizi fedha azipeleke kwa nani kwa mlaji ambaye ni mwananchi maskini halafu nyie mnatuambia TANESCO ndiye ambaye anapandisha umeme. Sio TANESCO ni wenzetu hawa. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, katika watu ambao walikataa kata kata Muswada wa Karamagi, nilisimama mimi. Nikamwambia Karamagi, hata utuweke siku nne, huo Muswada hatuutaki. Nilitaka nione kwanza, nani ameifikisha TANESCO ICU, ni wenzetu! Sasa kama TANESCO inalipa kwa siku fedha kiasi hiki, kwa siku lazima amlipe Dowans hizi fedha maana yake ni biashara hii! Yeye atazipeleka wapi? Lazima ampelekee mtumiaji wa umeme akachukue kwake. Kwa hiyo, mliowaumiza ndugu zetu ni nyinyi mliouchezea huu mkataba. Ni nyinyi mmewaumiza wananchi. Hatuwezi Serikali ya CCM kukubali! Hatuwezi Serikali ya CCM kukubali! Kwa hiyo, naomba niunge mkono mapema maamuzi na mapendekezo yote ambayo wenzetu walitoa. Yale mapendekezo waliyotoa ni mapendekezo sahihi. Mtu akiona ameshindwa kutumikia wananchi; akiona ameshindwa kabisa kuwa mwaminifu, akae kando, tuendelee na waadilifu kama Rais alivyosema. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, wakati namalizia, naomba nikwambie kitu kimoja. Huku duniani kuna viongozi wa aina mbili: Kuna viongozi ambao wakifa, wamekufa! Kuna viongozi wakifa, wanaendelea kuishi daima! Sijui mnanielewa? Hebu tuwe viongozi ambao tukifa tutaendelea kuishi daima kwa mazuri ambayo tumewatendea wananchi. Tutaendelea kuishi! (Makofi)

Mheshimiwa Spika, naomba niipokee hii taarifa vizuri na niseme kwamba hii taarifa ni nzuri kwa sababu moja kubwa, ina vithibitisho. Na naomba Waheshimiwa Wabunge wapatiwe hivi vitabu. Mimi nimevifuata mwenyewe kwa sababu nilitaka kufanya kazi yenye uhakika. Nawasihi Wabunge wapewe, wapitie ukurasa wa kwanza mpaka wa mwisho. Hakuna gazeti la Udaku, kuna vithibitisho vya mkataba mbovu na wenzetu wameiingiza nchi kwenye hasara kubwa sana. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, naomba kuunga mkono hoja hii na niwapongeze tena na niwatie moyo na niwaambie wenzangu aluta continua, tuisafishe Serikali ya CCM.

Asante sana
(makofi)
 
Utetezi wa Karamagi! Mbona ilikuwa raha huko! Nimeyamisi sana haya mambo! Mtaniwia radhi, ni marefu haya ma-hansard!

WAZIRI WA NISHATI NA MADINI: Mheshimiwa Spika, nashukuru kwa
kunipa fursa hii na mimi kuweza kuchangia hoja iliyo mbele yetu na kwa sababu ya
muda, nitachangia kwa yale ambayo yananigusa mimi.

Mheshimiwa Spika, naomba kwanza Bunge lako Tukufu na wananchi wote
Tanzania watambue kwamba nilihamishiwa Wizara ya Nishati na Madini mwezi Oktoba,
2006 wakati mkataba wa Richmond ulikuwa na uhai wa miezi sita tayari. Mimi
sikuhusika katik…. (Makofi/Kelele/Miguno)
Mheshimiwa Spika, naomba unilinde!

SPIKA: Utulivu jamani! Waheshimiwa utulivu, utulivu! Tumpe nafasi yake ya
kujieleza.
48
WAZIRI WA NISHATI NA MADINI: Mimi sikuhusika. Kama kuna vielelezo
ndani ya kabrasha ambalo lilikuwa linaelezwa ambapo kuna barua yangu ama kuandaa
mkataba ama kuongoza mkataba kwa njia yoyote, vingetoka. Lakini hilo haliniondolei
wajibu kwamba nilikuwa Waziri katika Serikali hii katika collective responsibility wakati
maamuzi haya yanatokea.

Mheshimiwa Spika, vilevile, nataka niwarudishe nyuma mwezi wa Oktoba.
Nilipoingia Wizara hii hali ya umeme ilikuwaje katika nchi yetu? Umeme wetu ambao
kiasi kikubwa unatokana na mabwawa (hydro) ulikuwa umeshuka kutoka megawatt 560
mpaka megawatt 120. Hiyo ndiyo hali tuliyokuwa nayo. Gridi ya Taifa ingeweza
kukatika wakati wowote na nchi ikawa gizani. Hayo ndiyo mazingira ambayo
wanaohusika wote katika kufanya maamuzi walikuwa wanafanya kazi nayo. Katika nchi
nyingine hiyo ungeiita kama state of emergency ku-declare state of emergency! Mimi
mwenyewe nilipoingia pale kila siku ilikuwa nnapokea ripoti ya mabwawa yote Tanzania
na wakati mwingine kuweza kusema hapa zima na hapa washa ili kuinusuru nchi yetu
katika giza.

Sasa hapa suala la kwanza linalonigusa, wanasema kwamba mimi nilishiriki
kukataa ama kushinikiza TANESCO isifute mkataba wa Richmond Oktoba, 2006.
Mheshimiwa Spika, mimi nilipoingia Wizarani pale pamoja na Katibu Mkuu, kazi
yetu kubwa ya kwanza ilikuwa kuona namna gani ya kufuta huu mkataba. Lakini si
kufuta mkataba kwamba tusiongezewe gharama, ni kufuta mkataba ili tuweze kumpata
mwingine kwa sababu wakati ule umeme ulikuwa haupo, tulikuwa tunahitaji umeme.
Ilikuwa ni namna gani ya kufuta mkataba na kumpata mwingine…… (Miguno)
Mheshimiwa Spika, naomba unilinde!
SPIKA: Endelea Mheshimiwa Waziri!

WAZIRI WA NISHATI NA MADINI: Kwa hiyo, tukaanza tarehe 5 – haya
mambo ya Dowans yamekuja baadaye. Tarehe 5 Oktoba, Katibu Mkuu kamwandikia
Mwanasheria Mkuu ili kutupa vigezo ambavyo tunaweza kutumia katika kuvunja huo
mkataba na ili kutomwezesha Richmond kwenda mahakamani kwa sababu ya kuvunja
mkataba. Tulipewa ushauri ambao tuliwaagiza TANESCO waangalie vipengele gani
wanaweza kutumia katika kufanikisha huo mchakato ambao ulikuwa umeanzishwa na
Katibu Mkuu.

Barua ambayo imeambatanishwa ya tarehe 27 Oktoba, 2006, ilikuwa ni jibu la
hiyo barua na ukiisoma vizuri, iliandikwa na Meneja Mkuu wa TANESCO wakati ule
alikuwa ni…. Jina lake silikumbuki, wale wa Net Group Solution. Pamoja na mengine
alitaja katika kifungu kwamba mkataba huu tuondokane nao kwa sababu Richmond
hajaweza kutoa umeme unaotakikana ambao ingebidi upatikane on commercial operating
date, haijaandikwa ndani ya mkataba, imeachwa blank. Akaomba, na mwenyewe
ameweka kwenye barua ambayo iko bayana kwamba pengine tunaweza kutumia zile
minutes ambazo tulikuwa tunakaa tunazungumza, labda ziwe ndiyo vithibitisho vya
kuweza kusema ameshindwa.

49
Lakini hapa Waheshimiwa Wabunge, tunao wanasheria na Kamati Teule ilikuwa
na Mwansheria tena aliyebobea, kama minutes za vikao hazikuandikwa ndani ya mkataba
kwamba zitakuwa viambatanisho kwenye mkataba, ukizitumia mahakamani,
hazitakubalika. Palikuwepo na vipengele vingine ambavyo tungeweza kuvitumia,
kampuni haijaorodheshwa hapa, haiko Marekani. Lakini, mkisoma vizuri hiyo ripoti na
mimi nimeisoma vizuri, utaona kwamba kufuatilia hivyo vipengele, Richmond angeweza
kwenda mahakamani, akatuchelewesha hata kama tungempata mkandarasi mwingine
ambaye tulikuwa tunamhitaji sana wakati anazalisha megawatts 120 za nchi nzima, siyo
kitu kidogo. Angeweza kuweka Court Injunction za kutukataza, tungeweza kupoteza
muda mrefu.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, tulichukua njia mbili: Moja, tuache mkataba ufe
wenyewe ukifika mwezi wa pili na kwa kutumia njia hiyo, wengine ambao tunaweza
kuwapata ambao wanaweza kutunusuru kwenye hili tunaweza tukawa-engage bila kupata
Court Injunction ya Richmond. Na kwa njia hiyo ndiyo sababu tuliweza kumpata Alstom,
kuweza kumchukua Mwanza ku-stabilize gridi ya taifa bila kuwa na matatizo na
Richmond kwa sababu hatukuwagusa. Tulijua tukiwagusa, atatuchukua kortini.
Tukivunja mkataba, anaweza kudai fidia ama akaweka injunction ya kutuchelewesha, na
sisi wakati ule hatukuwa Mungu, tusingeweza kujua kwamba Januari mvua itanyesha.
Tulikuwa tunajitayarisha kwa muda mrefu na wataalamu walikuwa wanasema inaweza
ikachukua takriban miaka mitatu hivi ili mabwawa yetu yaweze kurejea hali yake ya
kawaida.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, ili Kamati Teule kutenda haki kwa maamuzi
waliyosema, kwanza, wangeonyesha wapi Karamagi nimeshinikiza? Maana yake wote
huko katika vielelezo wameeleza: "Wakati Waziri anashinikiza ama anaandika barua au
anaita Menejimenti kuiagiza au Bodi, kwa hili sikuona mahala popote zaidi ya ile kwa
Kiingereza wanaita circumstantial na nafikiri kuhukumu mtu kwa hili wakati
hujajirudisha kwenye mazingira wakati ule tulipokuwa tunafanya maamuzi, mimi
kwangu naona kwamba haikuwa sahihi.

Mheshimiwa Spika, kwa sababu sina muda mrefu, kuna hoja nyingine ambayo
ilikuwa inaelekeza kwamba mimi mwenyewe kama Waziri niliwekea shinikizo
TANESCO ili i-assign (kuhuisha) huo mkataba wa Richmond kwa Dowans.
Tunachokizungumzia hapa kama nilivyokwisha sema, ni mwezi wa Novemba na
mwezi wa Desemba na sijui kama kwenye viambatanisho wameonyesha level ya maji
ilivyokuwa Mtera ambayo tayari ilikuwa chini kabisa. Ilikuwa ama mashine zile karibu
zlikuwa zinavuta upepo. Kwa hiyo, tulikuwa tumeanza kuzima mashine Mtera na Kidatu
kusudi tuzitumie tu gridi ya taifa ambayo ilikuwa inakatika katika mara kwa mara
inapozima, kwa sababu bila ya Mtera na Kidatu, gridi ya taifa ingezimika, nchi nzima
ingekuwa kwenye giza na hata ukiwa na hizi za Songas, IPTL, Aggreko, haziwezi
kuwasha gridi ya taifa. Kwa hiyo, ilibidi hayo maji yaende chini, ilikuwa hatari kabisa.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, nilikuwa safarini Canada. Nilipopata kwenye EMail
yangu kwamba Richmond wana mpango wa ku-assign ile contract kwa Dowans,
50
kwanza nilifurahi kwamba sasa tuna opportunity labda ya kuweza kumpata mtu
anayeweza. Lakini nikaona tusije tukaingia kwenye tatizo kama la Richmond kwa sababu
tulikuwa tumekwishagundua kuwa Richmond ni kama tapeli. Hivyo mpaka nafika pale,
tulikuwa tumekwishagundua kwamba Richmond ni tapeli. Kwa hiyo, ili tusiingie tatizo
kama la Richmond, mimi kama Waziri wa Nishati na Madini nikaona nisingoje hiyo ziara
ambayo sijui ilikuwa inachukua muda gani, nikaona nimpigie simu Mwenyekiti wa Bodi
ya TANESCO, Mheshimiwa Kazaura, nikamwambia: "chonde chonde nimesikia taarifa
hizi, chonde chonde msi-assign huo mkataba bila kufanya yafuatayo:-….."

Yameorodheshwa kwenye page 90 na kweli Kamati imenifanyia haki kwa sababu
imeeleza vilevile kama nilivyotahadharisha. Lakini pamoja na tahadhari hizo,
hawakunipongeza kwamba angalau na mimi nilianza kuchukua due diligence.
Wakanituhumu kwamba hiyo tahadhari ni kama shinikizo kwa TANESCO. (Kicheko)
Mheshimiwa Spika, Baniani mbaya, kiatu chake dawa! Akifanya jambo zuri,
jamani mpongezeni! Najua inaweza kuwa ni jambo jema siku hizi style nzuri unapotaja
jina la Karamagi, inaonekana vizuri. Labda ilionekana kama hii ripoti kama haikutaja
Karamagi, haitanoga. Lakini kwa hili…! (Kicheko/Miguno)
SPIKA: Lakini Mheshimiwa Waziri, kama tapeli anapendekeza mkataba wake
uende kwa mwingine, hushituki?! (Makofi)

WAZIRI WA NISHATI NA MADINI: Mheshimiwa Spika, wewe ni
Mwanasheria, kama tapeli, amekuingiza katika mkataba ambao uko halali, ukiukatisha
kinyume na mkataba huo, unampa uwezekano wa yeye kunufaika, akakuchukua
mahakamani, ukamlipa pesa ya bure!
SPIKA: Aah! Endelea tu Mheshimiwa!

WAZIRI WA NISHATI NA MADINI: Labda ile isingenoga, kwa hiyo,
ikaonekana niunganishwe kwenye hiyo ripoti. Lakini kweli nilichokuwa nafanya kwa
moyo wangu, nikatumia profession yangu ya Finance kwamba wafanye due diligence
physically. Mheshimiwa Spika, naomba zile minutes nilizotumia uniongezee kidogo.
Wafanye physical due deligence, amezitaja. Nikizitaja, ziko ukurasa wa 90, utazisoma,
physical.

Lakini wakati ule management ya TANESCO na yenyewe ikatoa kwamba zaidi ya
physical, watafanya financial due diligence ambayo ni sawa! Sasa jamani, naomba kwa
hili mtupongeze kwamba angalau kwa mara ya kwanza tulifanya mambo ambayo yako
sahihi.

Mheshimiwa Spika, sasa nimalizie, kwa sababu kengele ya pili karibu ilie, nikuquote
tu wakati unaomba msamaha ambapo ulisema kwamba, "tafsiri ya mambo
ukiyatumia vibaya ama kwa ubinafsi, yana matatizo". Na mimi naona hapa mtiririko wa
mambo yalivyokuwa ni sawa, lakini inapokuja conclusion, inakuja tafsiri nyingine. Kwa
hiyo, naona hiyo hainifanyii haki.
51

La pili, niwapongeze Waheshimiwa Wabunge walio wengi, wamenitumia
messages mbalimbali za kunipa faraja. Lakini wa mwisho ambaye amenifurahisha,
ambalo niliseme, amesema, "Yesu hakutenda dhambi, lakini alitolewa kafara", ukienda
kwenye vitabu vya dini, ili kusudi atusaidie sisi wengine duniani tusiwe na dhambi. Kwa
hiyo, kwa kuzingatia hilo na kwa kuzingatia dhana ya uwajibikaji na maslahi ya taifa na
heshima ya Chama changu, leo asubuhi, nimemwandikia Mheshimiwa Rais barua ya
kujiuzulu wadhifa wangu, bado nangoja maamuzi yake kwa sababu ndiye aliyeniteua.
Lakini hiyo barua nimekwishamtumia. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwa hayo machache, naona tujadili hii ripoti lakini tujadili
siyo kwa ushabiki. Aliyekosea azungumzwe, lakini yale mengine ambayo yananifaa,
tuyaweke pembeni. Naomba kuwasilisha! (Makofi/Kicheko)
SPIKA: Spika anaruhusu ushabiki kwa nchi ya Tanzania. Ushabiki uwepo tu
lakini tushabikie maslahi ya nchi yetu! (Makofi)
 
..............WAKUU NASIKIA ANNA KILANGO AMELAZWA MUHIMBILI..nani ana nyeti??..maana mimi nipo nje ya masikani yangu ya kupiga box...
 
Namalizia na hii ya Bangusilo Ibra Msabaha. Kwanza aliongea kisomi (kamkumbusha Mwakyembe kuwa ana PhD pia, na siyo ya "desa"), kistaarabu sana kwa kweli, na sense of humor (utani na wanyamwezi na wasukuma).

WAZIRI WA USHIRIKIANO WA AFRIKA MASHARIKI: Mheshimiwa
Spika, awali ya yote, naomba kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kunifikisha hadi leo
nikiwa hai na pia kumshukuru kwa yote.
Mheshimiwa Spika, pili, napenda nitoe pongezi za dhati kwa Kamati,
Wanakamati, Mwenyekiti wa Kamati na Bunge lako Tukufu. Napenda hasa nimpongeze,
Ndugu yangu, Mheshimiwa Harrison Mwakyembe kwa sababu yeye na mimi
tunafahamiana kutokana na huko tulikotoka kihistoria kwenye mambo ya taaluma katika
Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Napenda nimpongeze kwa jinsi alivyowasilisha kwa
staili yake na alipomaliza baada ya saa moja na nusu akamfanya kila mtu aamini yote,
nampongeza sana. Nampongeza pia kwa kuonyesha kwamba yeye pamoja na Kamati
walikuwa na dhamira ya kufanya kazi hii na kufanikisha dhamira nzuri waliyokuwa
nayo.
Mheshimiwa Spika, baada ya kusema hayo, naomba nichukue nafasi hii kwa
namna ya pekee kabisa, kumpongeza Mheshimiwa Waziri Mkuu. Amekuwa Waziri
Mkuu wangu kwa miaka yote hii miwili na hasa kwa kitendo chake cha leo cha
kutangaza kwamba anakusudia kujiuzulu.
Mheshimiwa Spika, kule nyumbani kwetu sisi, wewe Mnyamwezi sisi Wazaramo,
mtu kama huyu tunamwita Kilongola yaani anayeonyesha njia. Kwa hiyo, nampongeza
59
sana Mheshimiwa Lowassa kwa kuwa Kilongola, kaonyesha njia na sisi wengine
tutafuata. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, sikusidii kujibu hoja kwa hoja, hakuna haja, hapa lipo jambo
muhimu sana linajadiliwa na kama yapo mambo au upungufu katika taarifa ile, hayo ni
mambo ya kushauriana namna ya kuyaboresha ili iwe nzuri zaidi kwa ajili ya
kumbukumbu za Bunge na kwa ajili ya manufaa ya nchi yetu. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, isipokuwa nataka nitoe mfano mmoja tu. Kwa mfano, jana
wakati Mheshimiwa Mwakyembe, anawasilisha hoja yake, alinishtua kidogo alipotaja
kwamba Richmond walilipwa dola milioni 10/-. Kama ni kweli basi kulikuwa na tatizo
kwa sababu nakumbuka suala hili lilizuiwa wakati mimi nikiwa Waziri wa Nisahati na
Madini mpaka naondoka. Sasa kama walilipwa wakati ule, itakuwa ni suala la kutafuta
ilikuwaje kwa sababu najua lilizuiwa na Waziri wa Fedha alilizuia na mpaka viongozi wa
juu walilizuia. Natoa mfano wa vitu ambavyo vinaweza pengine vikaboreshwa pengine
wakati wa kupitia upya.
Mheshimiwa Spika, mfano mwingine ni kama ile hali yenyewe ya dharura na
ufanyaji maamuzi nyakati za dharura, huko mbele ya safari tunafanyaje, mfumo wa
mawasiliano unakuwaje, kwa sababu mambo mengine ni mambo ya kimfumo unayakuta
katika Serikali!
Mheshimiwa Spika, wewe ni mzoefu wa mambo haya na jinsi yanavyokwenda ni
hivyo hivyo, dokezo linatoka kwa Waziri linakwenda kwa Waziri Mkuu, linatoka kwa
Waziri Mkuu linakwenda kwa Rais, tuchukue mfano, au pengine ni mambo
yanayokwenda kwenye Kamati Maalumu au Cabinet, yakitoka kule yanakwenda kupata
idhini na kadhalika. Sasa haya ni mambo ambayo nadhani yanaweza yakatizamwa ni
namna gani tunaweza kuboresha mfumo wetu kwa kuzingatia Sheria zetu.
Mheshimiwa Spika, lingine ambalo linaweza kuboreshwa hata katika presentation
hii, ukurasa 147 mpaka 148. Hii naitoa kwa ajili ya Kamati, ukiisoma unaweza ukadhani
ndiyo mambo yale niliyokuwa ninasema mimi Bangusilo, kuna maneno ambayo
yanazungumzia habari ya uwajibikaji wa Waziri na Katibu Mkuu, ilivyoandikwa
inakuwa kama vile hawa wanawajibika kama kafara na mimi nadhani pengine maana
yenyewe siyo hiyo.
Mheshimiwa Spika, kama nilivyosema awali, nipo tayari kushirikiana na Kamati
katika maeneo ambayo nadhani yakipitiwa tena yanaweza yakaboreshwa vizuri zaidi kwa
ajili ya kumbukumbu sahihi na kwa ajili ya Taifa letu.
Mheshimiwa Spika, pia katika mtiririko huu yapo mambo ambayo nayaita kama
ni ya kiufundi. Nadhani Mheshimiwa Dr. Mwakyembe kwa background ambayo
nimeisema kwamba wote tumetokea huko, atakubaliana nami kwamba wakati mwingine
unapofanya uchunguzi ama utafiti ukiondoka na dhana fulani …
MBUNGE FULANI: Hypothesis!
60
WAZIRI WA USHIRIKIANO WA AFRIKA MASHARIKI: Siyo hypothesis,
nasema ukiondoka na kwa mfano uamuzi…
MBUNGE FULANI: A pre-inquest.
WAZIRI WA USHIRIKIANO WA AFRIKA MASHARIKI: Ndiyo, a preinquest
of idea siyo hypothesis, unaweza ukaenda nayo ukajikuta wewe tayari
umeshapata jibu sasa unatafuta njia ya kuhalalisha. Ninachosema ni kitu ambacho
unapaswa uwe kidogo mwangalifu na ukiipitia taarifa hii wakati mwingine inatoa sura
hiyo ambayo pengine siyo sahihi kabisa, hiyo ni moja.
Mheshimiwa Spika, lakini la pili, pale mahali ambapo alikuwa anatoa nadhani
kwenye maagizo sijui kama iko humu kwenye taarifa maana sikupitia neno kwa neno,
jana wakati anatoa taarifa hapa alimpa pole ndugu yetu yule Kubenea lakini jinsi
alivyosema ikaonekana kama vile kuna connection baina ya RICHMOND na matatizo
aliyopata ndugu yetu Kubenea, ndiyo!
Mheshimiwa Spika, niliwahi kuulizwa mahali kwamba wewe umewahi kuhojiwa
juu ya ndugu yetu Kubenea? Nikawaambia hili ni jambo la kushangaza lakini
ninachosema yote hii inatokana na jinsi ule mtiririko ulivyo unaweza ukatoa taswira
ambayo siyo sahihi.
Mheshimiwa Spika, unapokuwa unafanya utafiti kama huu wenye mambo ya
kisiasa, ni rahisi sana kuweza kuteleza namna hiyo na mimi nadhani ni vizuri
tukashauriana namna ya kuboresha.
Mheshimiwa Spika, kama nilivyosema, kama ni suala la kwenda hoja kwa hoja,
tutapata muda huo baadaye wa kuweza kushauriana kwa maana ya maeneo yanayohitaji
kuboreshwa. Lakini mimi kwa kweli nia yangu ya kusimama hapa, kwanza, ni kusema
kwamba mimi si mwoga, ni muadilifu, sipendi rushwa na ni mchapa kazi na nashirikiana
na watu. Katika Bunge hili nadhani ni mashahidi, Wasukuma na Wanyamwezi humu
ndani wanaweza wakakubali kwamba mimi ndiye Babu yao humu ndani, sina tatizo na
ushirikiano na watu. Kwa hiyo, nilitaka hili niliseme tu kwa sababu wakati mwingine
inawezekana ni tabia imejionyesha…
SPIKA: Kwa umbile lako Mheshimiwa Waziri, inaonyesha kabisa wewe ni
Mnyamwezi au Msukuma. (Kicheko)
WAZIRI WA USHIRIKIANO WA AFRIKA MASHARIKI: Mheshimiwa
Spika, nalisema hili kwa sababu wakati mwingine yanaposemwa haya maneno kama
alivyosema ndugu yangu Mwakyembe jana, ya ubabe na kiburi, sasa kiburi naogopa
sana. Sisi Waislamu tunasema kiburi ni sifa ya Mwenyezi Mungu siyo ya binadamu,
naogopa. Sasa inawezekana wameyapata haya huko chini huko kwa watendaji, ni bahati
61
mbaya lakini nataka niseme kwamba kwa kweli si sifa nzuri kwa binadamu ya ubabe,
kiburi, jeuri na kadhalika, Mwenyezi Mungu atupishilie mbali.
Mheshimiwa Spika, nataka niseme tu kwamba nimesimama kusema yale ambayo
yameonekana. Kwanza, nakubali kuchukua collective responsibility pia responsibility ya
wale ambao wako chini yangu kwa yale ambayo wameyafanya ambavyo siyo sawasawa
kama Kamati ilivyoona. Kwa maana hiyo, siogopi kuwajibika na najua kuwajibika katika
context yetu sisi labda katika suala kama hili lakini katika mambo mengine inaweza kuwa
kidogo kila siku Waziri mmoja yupo katika matata kwa sababu ya hali yetu ya maisha
ilivyokuwa duni. Lakini kimsingi mimi ni mtu ninayeamini katika uwajibikaji, katika
utawala bora na katika mambo yale ambayo yanadumisha na kuendeleza wananchi wetu.
Mheshimiwa Spika, niliona niseme kutokana na hali jinsi ilivyo kwa sababu siasa
ni suala la imani ya watu. Kuwa kiongozi wa kisiasa ni imani ya watu na jinsi watu
wanavyoona ni lazima kiongozi wa kisiasa uwe na imani ya wale unaowaongoza na
perception yao ni jinsi wanavyokutazama na lazima pia iwe ni sawasawa. Sasa
inawezekana kabisa hata wakikutazama kwamba uko hivyo lakini hauko hivyo inatosha
kwako kusema kwamba kwa kweli ni vizuri mtu ukae kando ili shughuli za Kitaifa
ziendelee na wewe uweze kuchangia kwa njia nyingine.
Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, nimesimama hapa kwa kweli kwa heshima ya nchi
yangu, Chama changu, Jimbo langu na kwa heshima kwa kweli ya Bunge langu, ni
muhimu sana hii taasisi, kusema hivi, ndiyo maana nikamwita Mheshimiwa Waziri
Mkuu, yeye ni Kilongola kwamba alionyesha njia, asubuhi ya leo nimekwenda kumwona
Mheshimiwa Rais na kumweleza dhamira yangu ya kujiuzulu na kama ilivyo kawaida
kama ambavyo wewe mwenyewe ulivyosema wote sisi tunangojea amri yake.
Mheshimiwa Spika, lakini namshukuru sana Mheshimiwa Rais kwa heshima
kubwa aliyonipa, namshukuru mke wangu na familia yangu kwa ujumla kwa msaada
wote ambao wamenipa, nawashukuru wananchi wa Kibaha na hasa Kibaha Vijijini,
Jimboni kwangu, wanakijiji wenzagu wa Kijiji cha Soga na wale Wasukuma na
Wanyamwezi mnakaribishwa, mfundishwe namna ya kula kwa nazi, nakushukuru sana
Mheshimiwa Spika, Naibu Spika na Waheshimiwa Wabunge wote. Hapo Mheshimiwa
Rais atakapokubali, naamini nitapata fursa tena nyingine ya kukaa pamoja nanyi na
kuwashughulikia Wasukuma ipasavyo, nashukuru sana. (Makofi)
SPIKA: Mheshimiwa Waziri, unataka kututoa kafara sisi Wasukuma sasa.
Tunaendelea Waheshimiwa, ahsante sana, nimeguswa sana na namna ulivyowasilisha
hotuba yako, ahsante sana. (Kicheko/Makofi)
 
Mjadala wote wa siku hiyo uko hapa: [media]http://www.bunge.go.tz/Polis/PAMS/Docs/HS-10-8-2008.pdf[/media]
 
..............WAKUU NASIKIA ANNA KILANGO AMELAZWA MUHIMBILI..nani ana nyeti??..maana mimi nipo nje ya masikani yangu ya kupiga box...

Ni kweli Phil, huyo mama alilazwa Muhimbili zile wodi za MOI siku kama 4 hivi zilizopita na inaelezwa alikuwa anasumbuliwa na malaria kali. Habari nilizopata jana asubuhi ni kuwa ilikuwa aruhusiwe maana alishapata nafuu.
 
Namalizia na hii ya Bangusilo Ibra Msabaha. Kwanza aliongea kisomi (kamkumbusha Mwakyembe kuwa ana PhD pia, na siyo ya "desa"), kistaarabu sana kwa kweli, na sense of humor (utani na wanyamwezi na wasukuma).

WAZIRI WA USHIRIKIANO WA AFRIKA MASHARIKI: Mheshimiwa
Spika, awali ya yote, naomba kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kunifikisha hadi leo
nikiwa hai na pia kumshukuru kwa yote.
Mheshimiwa Spika, pili, napenda nitoe pongezi za dhati kwa Kamati,
Wanakamati, Mwenyekiti wa Kamati na Bunge lako Tukufu. Napenda hasa nimpongeze,
Ndugu yangu, Mheshimiwa Harrison Mwakyembe kwa sababu yeye na mimi
tunafahamiana kutokana na huko tulikotoka kihistoria kwenye mambo ya taaluma katika
Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Napenda nimpongeze kwa jinsi alivyowasilisha kwa
staili yake na alipomaliza baada ya saa moja na nusu akamfanya kila mtu aamini yote,
nampongeza sana. Nampongeza pia kwa kuonyesha kwamba yeye pamoja na Kamati
walikuwa na dhamira ya kufanya kazi hii na kufanikisha dhamira nzuri waliyokuwa
nayo.
Mheshimiwa Spika, baada ya kusema hayo, naomba nichukue nafasi hii kwa
namna ya pekee kabisa, kumpongeza Mheshimiwa Waziri Mkuu. Amekuwa Waziri
Mkuu wangu kwa miaka yote hii miwili na hasa kwa kitendo chake cha leo cha
kutangaza kwamba anakusudia kujiuzulu.
Mheshimiwa Spika, kule nyumbani kwetu sisi, wewe Mnyamwezi sisi Wazaramo,
mtu kama huyu tunamwita Kilongola yaani anayeonyesha njia. Kwa hiyo, nampongeza
59
sana Mheshimiwa Lowassa kwa kuwa Kilongola, kaonyesha njia na sisi wengine
tutafuata. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, sikusidii kujibu hoja kwa hoja, hakuna haja, hapa lipo jambo
muhimu sana linajadiliwa na kama yapo mambo au upungufu katika taarifa ile, hayo ni
mambo ya kushauriana namna ya kuyaboresha ili iwe nzuri zaidi kwa ajili ya
kumbukumbu za Bunge na kwa ajili ya manufaa ya nchi yetu. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, isipokuwa nataka nitoe mfano mmoja tu. Kwa mfano, jana
wakati Mheshimiwa Mwakyembe, anawasilisha hoja yake, alinishtua kidogo alipotaja
kwamba Richmond walilipwa dola milioni 10/-. Kama ni kweli basi kulikuwa na tatizo
kwa sababu nakumbuka suala hili lilizuiwa wakati mimi nikiwa Waziri wa Nisahati na
Madini mpaka naondoka. Sasa kama walilipwa wakati ule, itakuwa ni suala la kutafuta
ilikuwaje kwa sababu najua lilizuiwa na Waziri wa Fedha alilizuia na mpaka viongozi wa
juu walilizuia. Natoa mfano wa vitu ambavyo vinaweza pengine vikaboreshwa pengine
wakati wa kupitia upya.
Mheshimiwa Spika, mfano mwingine ni kama ile hali yenyewe ya dharura na
ufanyaji maamuzi nyakati za dharura, huko mbele ya safari tunafanyaje, mfumo wa
mawasiliano unakuwaje, kwa sababu mambo mengine ni mambo ya kimfumo unayakuta
katika Serikali!
Mheshimiwa Spika, wewe ni mzoefu wa mambo haya na jinsi yanavyokwenda ni
hivyo hivyo, dokezo linatoka kwa Waziri linakwenda kwa Waziri Mkuu, linatoka kwa
Waziri Mkuu linakwenda kwa Rais, tuchukue mfano, au pengine ni mambo
yanayokwenda kwenye Kamati Maalumu au Cabinet, yakitoka kule yanakwenda kupata
idhini na kadhalika. Sasa haya ni mambo ambayo nadhani yanaweza yakatizamwa ni
namna gani tunaweza kuboresha mfumo wetu kwa kuzingatia Sheria zetu.
Mheshimiwa Spika, lingine ambalo linaweza kuboreshwa hata katika presentation
hii, ukurasa 147 mpaka 148. Hii naitoa kwa ajili ya Kamati, ukiisoma unaweza ukadhani
ndiyo mambo yale niliyokuwa ninasema mimi Bangusilo, kuna maneno ambayo
yanazungumzia habari ya uwajibikaji wa Waziri na Katibu Mkuu, ilivyoandikwa
inakuwa kama vile hawa wanawajibika kama kafara na mimi nadhani pengine maana
yenyewe siyo hiyo.
Mheshimiwa Spika, kama nilivyosema awali, nipo tayari kushirikiana na Kamati
katika maeneo ambayo nadhani yakipitiwa tena yanaweza yakaboreshwa vizuri zaidi kwa
ajili ya kumbukumbu sahihi na kwa ajili ya Taifa letu.
Mheshimiwa Spika, pia katika mtiririko huu yapo mambo ambayo nayaita kama
ni ya kiufundi. Nadhani Mheshimiwa Dr. Mwakyembe kwa background ambayo
nimeisema kwamba wote tumetokea huko, atakubaliana nami kwamba wakati mwingine
unapofanya uchunguzi ama utafiti ukiondoka na dhana fulani …
MBUNGE FULANI: Hypothesis!
60
WAZIRI WA USHIRIKIANO WA AFRIKA MASHARIKI: Siyo hypothesis,
nasema ukiondoka na kwa mfano uamuzi…
MBUNGE FULANI: A pre-inquest.
WAZIRI WA USHIRIKIANO WA AFRIKA MASHARIKI: Ndiyo, a preinquest
of idea siyo hypothesis, unaweza ukaenda nayo ukajikuta wewe tayari
umeshapata jibu sasa unatafuta njia ya kuhalalisha. Ninachosema ni kitu ambacho
unapaswa uwe kidogo mwangalifu na ukiipitia taarifa hii wakati mwingine inatoa sura
hiyo ambayo pengine siyo sahihi kabisa, hiyo ni moja.
Mheshimiwa Spika, lakini la pili, pale mahali ambapo alikuwa anatoa nadhani
kwenye maagizo sijui kama iko humu kwenye taarifa maana sikupitia neno kwa neno,
jana wakati anatoa taarifa hapa alimpa pole ndugu yetu yule Kubenea lakini jinsi
alivyosema ikaonekana kama vile kuna connection baina ya RICHMOND na matatizo
aliyopata ndugu yetu Kubenea, ndiyo!
Mheshimiwa Spika, niliwahi kuulizwa mahali kwamba wewe umewahi kuhojiwa
juu ya ndugu yetu Kubenea? Nikawaambia hili ni jambo la kushangaza lakini
ninachosema yote hii inatokana na jinsi ule mtiririko ulivyo unaweza ukatoa taswira
ambayo siyo sahihi.
Mheshimiwa Spika, unapokuwa unafanya utafiti kama huu wenye mambo ya
kisiasa, ni rahisi sana kuweza kuteleza namna hiyo na mimi nadhani ni vizuri
tukashauriana namna ya kuboresha.
Mheshimiwa Spika, kama nilivyosema, kama ni suala la kwenda hoja kwa hoja,
tutapata muda huo baadaye wa kuweza kushauriana kwa maana ya maeneo yanayohitaji
kuboreshwa. Lakini mimi kwa kweli nia yangu ya kusimama hapa, kwanza, ni kusema
kwamba mimi si mwoga, ni muadilifu, sipendi rushwa na ni mchapa kazi na nashirikiana
na watu. Katika Bunge hili nadhani ni mashahidi, Wasukuma na Wanyamwezi humu
ndani wanaweza wakakubali kwamba mimi ndiye Babu yao humu ndani, sina tatizo na
ushirikiano na watu. Kwa hiyo, nilitaka hili niliseme tu kwa sababu wakati mwingine
inawezekana ni tabia imejionyesha…
SPIKA: Kwa umbile lako Mheshimiwa Waziri, inaonyesha kabisa wewe ni
Mnyamwezi au Msukuma. (Kicheko)
WAZIRI WA USHIRIKIANO WA AFRIKA MASHARIKI: Mheshimiwa
Spika, nalisema hili kwa sababu wakati mwingine yanaposemwa haya maneno kama
alivyosema ndugu yangu Mwakyembe jana, ya ubabe na kiburi, sasa kiburi naogopa
sana. Sisi Waislamu tunasema kiburi ni sifa ya Mwenyezi Mungu siyo ya binadamu,
naogopa. Sasa inawezekana wameyapata haya huko chini huko kwa watendaji, ni bahati
61
mbaya lakini nataka niseme kwamba kwa kweli si sifa nzuri kwa binadamu ya ubabe,
kiburi, jeuri na kadhalika, Mwenyezi Mungu atupishilie mbali.
Mheshimiwa Spika, nataka niseme tu kwamba nimesimama kusema yale ambayo
yameonekana. Kwanza, nakubali kuchukua collective responsibility pia responsibility ya
wale ambao wako chini yangu kwa yale ambayo wameyafanya ambavyo siyo sawasawa
kama Kamati ilivyoona. Kwa maana hiyo, siogopi kuwajibika na najua kuwajibika katika
context yetu sisi labda katika suala kama hili lakini katika mambo mengine inaweza kuwa
kidogo kila siku Waziri mmoja yupo katika matata kwa sababu ya hali yetu ya maisha
ilivyokuwa duni. Lakini kimsingi mimi ni mtu ninayeamini katika uwajibikaji, katika
utawala bora na katika mambo yale ambayo yanadumisha na kuendeleza wananchi wetu.
Mheshimiwa Spika, niliona niseme kutokana na hali jinsi ilivyo kwa sababu siasa
ni suala la imani ya watu. Kuwa kiongozi wa kisiasa ni imani ya watu na jinsi watu
wanavyoona ni lazima kiongozi wa kisiasa uwe na imani ya wale unaowaongoza na
perception yao ni jinsi wanavyokutazama na lazima pia iwe ni sawasawa. Sasa
inawezekana kabisa hata wakikutazama kwamba uko hivyo lakini hauko hivyo inatosha
kwako kusema kwamba kwa kweli ni vizuri mtu ukae kando ili shughuli za Kitaifa
ziendelee na wewe uweze kuchangia kwa njia nyingine.
Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, nimesimama hapa kwa kweli kwa heshima ya nchi
yangu, Chama changu, Jimbo langu na kwa heshima kwa kweli ya Bunge langu, ni
muhimu sana hii taasisi, kusema hivi, ndiyo maana nikamwita Mheshimiwa Waziri
Mkuu, yeye ni Kilongola kwamba alionyesha njia, asubuhi ya leo nimekwenda kumwona
Mheshimiwa Rais na kumweleza dhamira yangu ya kujiuzulu na kama ilivyo kawaida
kama ambavyo wewe mwenyewe ulivyosema wote sisi tunangojea amri yake.
Mheshimiwa Spika, lakini namshukuru sana Mheshimiwa Rais kwa heshima
kubwa aliyonipa, namshukuru mke wangu na familia yangu kwa ujumla kwa msaada
wote ambao wamenipa, nawashukuru wananchi wa Kibaha na hasa Kibaha Vijijini,
Jimboni kwangu, wanakijiji wenzagu wa Kijiji cha Soga na wale Wasukuma na
Wanyamwezi mnakaribishwa, mfundishwe namna ya kula kwa nazi, nakushukuru sana
Mheshimiwa Spika, Naibu Spika na Waheshimiwa Wabunge wote. Hapo Mheshimiwa
Rais atakapokubali, naamini nitapata fursa tena nyingine ya kukaa pamoja nanyi na
kuwashughulikia Wasukuma ipasavyo, nashukuru sana. (Makofi)
SPIKA: Mheshimiwa Waziri, unataka kututoa kafara sisi Wasukuma sasa.
Tunaendelea Waheshimiwa, ahsante sana, nimeguswa sana na namna ulivyowasilisha
hotuba yako, ahsante sana. (Kicheko/Makofi)

Mimi I love you wewe JF maana ni nondo tu kila mara .Tuzidi kuchambua tuone wapi Ndanda Kosovo alionewa .Tusikurupuke
 
Lowassa is sinking on quick sand, he is done kauli zake ni za Mfa maji haishi kutapatapa.

I will volunteer to have an interview with him and let any TV station or Radio Station in the world cover the interview.I will strip him naked and he will never dare to call for aninterview for a long time about this RDC sheit!

One pissed off clergy!
 
kwa mujibu wa mahojiano yake yaliyorushwa na TVT na kupatikana kwa Mhshimiwa sana Mwanakijiji lowasa anasema nanukuu...
“Lakini inafahamika kwamba mara mbili nilijaribu kuonya kuhusu mradi huo wa Richmond, uliokuwa uzalishe umeme wa dharura. Kwanza mwishoni mwa Septemba 2006 niliandika kwa Waziri wa Nishati na Madini, nilitaka Richmond ichunguzwe na Serikali ijiridhishe kama kampuni hiyo ina uwezo, na mara ya pili, ni Oktoba mwaka huo huo, alipoitisha kikao cha wakuu wa idara, kama ya Usalama na vyombo vingine, kutaka kujua hali ya mambo ilikuwaje,”

Kwa mujibu wa watu wa karibu waliohojiwa na gazeti la This Day ambalo lilikuwa la kwanza kutilia mashaka Kampuni hii, Lowasa hawajibiki na ulaji wa pesa ya Richmond ila kuna watu walitumia mgongo wake tuu.

So I am curios, what did Usalama said at the meeting? what was their role on the whole issue? Was it Apson who was Chief of TISS or Othman when this meeting took place?

Then what was the role of Hoseah and TAKUKURU when they ran their investigation, didn't they compare notes with their cousins at TISS?

If the whole RDC is now known to be bogus, where was TISS on this? aren't they supposed to do a due dilligence and background investigation on behalf of Serikali? or RDC is another Kagoda since the money to finance the whole programme was from WB/IMF and not GVTZ?
 
lowassanandege.jpg


Hii ni ile Richmond Force 1​
 
Ndege ya Lowassa ilipotua... (picha)

Hii statement ina maana kama 6 hivi.... 3 polemical, 1 neutral na 2 positive !!
 
Mnataka kusema kwamba Muungwana anataka kula matapishi yake.
 
BAADA YA KUJIUZULU…

::Watu 10,000 na magari 400 wampokea
::Akaribishwa kwa zulia jekundu Monduli
::Askofu Laizer amwombea, amtabiria mema
::Yeye apasua bomu, aichambua Richmond

Na Deodatus Balile, Monduli

WAZIRI Mkuu aliyejiuzulu hivi karibuni, Edward Ngoyai Lowassa, jana amepokewa kama mfalme jimboni kwake Monduli.

Vikundi vya Morani wa kimasai, wanawake maarufu kama yeyo, vikongwe maarufu kama koko, mabinti maarufu kama ndito na wazee, wote walijitokeza.

Si hao tu, kwani maaskofu, mapadri, mashekhe na wachungaji walijitokeza kwa wingi kuungana na umati wa watu wanaokadiriwa 10,000 kumpokea Lowassa jimboni.

Maneno aliyokuwa anayatumia mwanasiasa maarufu kutoka Morogoro, hayati Thadeus Kasapira, kuwa haijapata kutokea, ndiyo yaliyotokea jana kwenye mji wa Monduli.

Magari zaidi ya 400 yakiwa mchanganyiko kati ya mabasi, magari madogo, malori kwa teksi, yaliufanya mji wa Monduli kulipuka kwa furaha jana.

Wananchi wa Mkoa wa Arusha waliokuwa wakionyesha furaha na bashasha ya hali ya juu walikuwa wamebeba mabango mengi yenye ujumbe mzito kwa Serikali na Lowassa katika sakata zima la Richmond .

Baadhi ya mabango hayo yalisomeka hivi: “Nyota yako bado inawaka, shujaa wetu umeonyesha mfano usife moyo, mtu kwao karibu nyumbani, tupo pamoja nawe usife moyo, wana Monduli tunakuamini, hongera mheshimwa Lowassa kwa usimamizi wa sekondari za Kata utakumbukwa.” Ukiacha mabango hayo, kubwa lililowaacha wengi midomu wazi ni bango lililosomeka hivi: “Mmasai haibi hela, anaiba ng’ombe.”

Lowassa yeye alitua katika Uwanja wa Ndege wa Arusha saa 6:55 mchana na kukuta umati mkubwa wa watu.

Akiwa katika shati nyeupe, tai yenye rangi nyeusi na mistari ya kijivu, huku suruali yake nyeusi na viatu vyeusi vikiwa vinang’aa, Lowassa aliyejiuzulu Uwaziri Mkuu, Februari 7, mwaka huu, akiongozana na mkewe Regina, alirejea Monduli kwa mara ya kwanza tangu aachie wadhifa huo huku mkewe akionyesha tabasamu la mwaka.

Lowassa hakuficha hisia zake alipopewa nafasi ya kuhutubia wananchi katika Ofisi za CCM, Monduli: “Siku hii nimeisubiri kwa hamu kubwa tangu yalipotokea haya yaliyotokea (akashangiliwa).”

Huku mkewe mama Regina naye akionyesha furaha ya dhati kutokana na wingi wa watu, alionekana kumuunga mkono mumewe na kufurahishwa na wingi wa watu na kupunga mkono muda mwingi.

Akiwa katika gari aina ya Land Cruiser maarufu kama shangingi namba T181 ATU, Lowassa aliwasili katika Viwanja vya Monduli saa 8:32 mchana, na kukuta umati uliokuwa ukimsubiri bila kujali jua kali lililokuwa likiwaka.

Wananchi wengi wakiwa wamevaa fulana zilizoandikwa ‘Karibu nyumbani shujaa wetu E. N. Lowassa- CWT Monduli,’ walionyesha nyuso za bashasha na matumaini makubwa juu ya mbunge wao, Lowassa.

Kama miujiza vile, wakazi wa Monduli walimwekea zulia jekundu, kuashiria mapenzi yao na utambuzi wa mamlaka aliyonayo kiongozi huyo katika jimbo lao na majukumu ya kitaifa.

Lowassa jana alisimikwa tena katika jamii ya Kimasai. Walimfunga mgolole, wakampa mundu, mkuki na kifimbo, huku wakiimba kuwa yeye ni Simba wa Yuda angurumaye katika nyika. Sehemu ya salamu za wana-CCM Monduli zilimtaka Lowassa kutokuwa na hofu: “Usiangalie nyuma kwa masikitiko, bali uangalie mbele kwa ushindi,” ilisema sehemu ya risala ya wana-Monduli.

Huku akipongezwa kwa kufungua ukurasa mpya wa uwajibikaji katika siasa za Afrika, Lowassa aliambiwa asiwajali wananchi wachache wenye masilahi binafsi wenye kumtembezea kejeli dhidi yake nchi nzima.

“Tunakupenda, tunakuamini na tunakupa moyo katika vita mpya kwa ajili ya mabadiliko,” alisema msoma risala na kushangiliwa kwa nguvu kubwa. Pia walimpongeza mama Regina kwa uvumilivu wa hali ya juu wakati huu wa shida.

Kwa mshangao wa wengi, wenyeji wa Kijiji cha Twatwatwa wilayani Kilosa, waliambatana na Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Mvomero kuja Monduli jana kumpokea Lowassa na kueleza wanayoyakumbuka katika uongozi wake.

Pamoja na mambo mengine, walitaja maelekezo ya Lowassa kuwashauri wajenge shule maalumu kwa ajili ya watoto wa wafugaji, waliosema leo shule hiyo ina watoto 160 na kwao ni alama isiyofutika. Askofu Thomas Laiser wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri (KKKT), alikuwa mmoja wa watu waliohudhuria ujio wa Lowassa katika Jimbo la Monduli jana. Akizungumza kwa mamlaka makubwa na kuonyesha kwamba kweli maaskofu ni wawakilishi wa Mungu duniani kutokana na watu walivyokaa kimya wakati akihutubia jamii kutokana na sauti yake ya mamlaka, kwanza Askofu Laizer alimbariki Lowassa.

Alieleza mambo matatu ya msingi. Alisema umati ule ulikuwa umekusanyika kumpa pole kwa yaliyotokea, pili akamhakikishia kuwa wapo pamoja naye, na jambo la tatu, akasema kama kweli ulitokea ufisadi basi yeye anaungana na Rais Jakaya Kikwete kwa hatua alizochukua, ila akamalizia kwa kibwagizo: “Sisi Wamasai tunasema panya akiuawa anakuja kuozea kwenye nyumba ya mama yake.” Maneno haya aliyasema kwa Kimasai na kuyatafsiri hali iliyozua hamasa kubwa kwa wenyeji.

Mpendwa msomaji, kama ungekuwapo basi si ajabu na wewe ungekuwa mmoja wa watu waliotokwa na machozi baada ya Lowassa kusimama kueleza kilichotokea katika sakata la Richmond.

Tofauti na wiki mbili zilizopita, Lowassa akionyesha uchangamfu na sauti kali ya uchungu na matumaini ndani yake jana, alifafanua kilichotokea.

Alieleza mchakato mzima wa Richmond ulivyokwenda na ingawa hakutaja majina maelezo yake yalithibitisha kuwa aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini, Dk. Ibrahim Msabaha, alimwingiza mtegoni.

Kabla ya kufafanua kilichojiri wakati wa sakati la Richmond, alieleza jinsi alivyofikia uamuzi wa kujiuzulu: “Nilimweleza mke wangu, nikamwambia nataka kujiuzulu uko tayari? Yeye akaniuliza ‘wewe uko tayari?’ Nikamwambia niko tayari.

“Baada ya hapo nikaenda bungeni, kimya kimya watu wawili tu tulikuwa tukijua mimi na mke wangu, kwamba nakwenda kujiuzulu… maandiko matakatifu yanasema baba na mama wanakupa mali na urithi wa duniani, lakini mke mwema hutolewa na Mungu.” (akashangiliwa).

Alipofikia kuzungumzia sakata la Richmond, Lowassa alifafanua kuwa Net-Group Solutions kampuni iliyokuwa inaongoza manejimenti ya TANESCO walithibitika kuwa na nia ya kufanya hujuma katika mchakato wa kupata umeme wa dharura nchi ilipokumbwa na ukame mwaka 2006.

Alisema baada ya kubaini hilo kutokana na uzembe wa hali ya juu uliokuwa ukionyeshwa na watendaji wa Net-Group Solutions, yeye kama Waziri Mkuu chakaramu, asiyetaka mambo yaharibike akiangalia, aliamua kuondoa mchakato wa ununuzi wa mitambo ya kuzalisha umeme wa dharura kutoka mikononi mwa TANESCO kwenda chini ya timu maalumu ya iliyoundwa na viongozi waandamizi wa Serikali.

Alisema timu hiyo iliundwa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Johnson Mwanyika, ambaye wakati wa kuhojiwa na Kamati ya Dk. Harrison Mwakyembe, alisema hajui lolote, Katibu Mkuu Hazina, Grey Mgonja, Mwakilishi kutoka Benki Kuu, TANESCO, Wizara ya Nishati na Madini.

Timu hii aliiundwa kwa nia ya kuharakisha mchakato wa kupata umeme wa dharura, lakini hata mambo yalipoonekana hayaendi alishauri mkataba kati ya Richmond na Serikali uvunjwe, ila maafisa wakuu wa Serikali walimkamtalia.

Kwamba je, nini kilitokea na Lowassa angefanyaje na ni hatua zipi alichukua usikose nakala ya Mtanzania kesho.

Huyu Balile alivyoripoti habari hii utadhani ni makala binafsi (note hizo sentensi bold).Reading between lines,nakubaliana kabisa na tetesi kwamba kuna waandishi wameshanunuliwa kwa minajili ya kumrejesha Lowassa ndani ya serikali.
 
.... anatarajia kurejea serikalini kwa nguvu zote na kwamba ameanza kujifananisha na alhaj Ali Hassan Mwinyi, yule rais wetu wa awamu ya pili..... na hakika wabaya wake watakiona cha mtema kuni. Nadhani ana uhakika huo na habari zinasema ameshamueleza Kikwete....nia yake ya kuiongoza Tanzania inafanikiwa kwa njia yoyote ile. Kumbuka amekuwa na nia hii siku zote mara baada ya kuingia kwenye siasa baada ya kuwa amechuma fedha nyingi kutoka AICC na maeneo mengine, ikiwemo kipato kikubwa kutoka kwenye nyumba zake nyingi Dar na Arusha ambazo zote ziko kwenye prime areas.

1.Yeye Kurejea na Kuiongoza Tanzania-'Over my dead body' and i suppose i speak for many Tzns.

2.Kujifananisha na Mzee wetu Ruksa ni Kosa lingine kubwa sana-Mzee wetu aliwajibika kikazi,Yeye Aligundulika kwa WIZI wa mali ya Umma.

3.Yeye ndiye mbaya wa Watanzania,na-si vinginevyo!!

4.Hata kama wamechuma pamoja,wanakunywa chai pamoja huku wakijadili jinsi watakavyo PANGISHANA ktk hiyo NYUMBA iliyeko kwenye PRIME AREA,lakini Watanzania Hatutosita kuhoji,isitoshe marehemu Babu alishasema:'...Pale mahala huwa hapakimbiliwi!!!'

**Huyu Bwana amekurupuka na kuanza kujieleza kwenye vyombo vya habari, akidhani labda atabadili 'Moods' & 'Views' za watu,Nani anataka kusikiliza Maelezo yake??Yeye asubiri tutapo mburuza mbele ya vyombo vya Sheria,ndiyo ajieleze kwa minaajili ya kujitetea.
 
Amekuwa akitamba kwenye private kuwa atakuwa rais tu hata iweje 2010, which raises more questions kuliko majibu, including anajiamini nini hasa huyu baba?

Kwani mwenyezi Mungu kuna aliowaumba ili wawe viongozi tu na wasiwe waongozwa? Viongozi wenye busara za siasa hunyamaza kimyaa wanapotoka, na kufanya mambo yao kwa siri, huku wakiwaaachia wananchi kuamua ukweli na uongo, lakini baba huyu toka atoke amekuwa kwenye media hata kuliko alipokuwepo kwenye power, kulikoni? Kwani wa kuamua awe kiongozi au asiwe ni nani yeye au sisi wananchi?

Huyu amekatishwa nini hasa anaocholilia kila kukicha na maneno mengi mapya yuanayojaribu kuikwepa ripoti ya Mbunge Mwakyembe, ambayo ameshindwa kuijibu akiwa madarakani, sasa ataweza vipi kuijibu akiwa nje? It is about time mtu mzima amwambie wazi kuwa we do not miss him, na kwamba as a nation wa are just doing fine!
 
Naona sasa JK anataka azame naye, haina shida tusubiri!!!!!!!!!
 
Haya anayoyasema Lowassa kwenye mikutano ya hadhara alishindwa nini kuyasema bungeni siku ripoti ya Kamati Teule ilipomdondoshea tuhuma hizo? Au ni kwa kuwa hapo hakuna wabunge kama kina Selelii na Kilango wa kumjibu?

Na bado nazidi kuamini kuwa kitendo cha kutokuhojiwa na kamati kilipangwa, pengine hata kina Mwakyembe hawakujua kuwa wanaingizwa mkenge waliposhauriwa ama walipoamua kutokumhoji Lowassa. Huyo aliyepanga na kufanikisha hili ni tactician hasa aliyefuzu intelligensia ya kifisadi!
 
Back
Top Bottom