Lowassa anasafishwa!

Lowassa anasafishwa!

Kosa sio kosa mpaka lirudiwe.

Kosa lililorudiwa sio kosa mpaka kosa lililorudiwa lirudiwe.

Kosa lililorudiwa likirudiwa sio kosa mpaka kosa lililorudiwa likarudiwa lirudiwe.

Kosa lililorudiwa .....you get the point

Kwa logic hii hamna kosa.

..ukistaajabu ya musa,utayaona ya firauni!
 
Machale yanicheza ile mbaya juu ya Urafiki wa Jakaya Kikwete na Eddy lowassa.

Hisia zangu zinaniambia kitu kimoja, macho yangu yanaona kitu kingine tofauti na hisia zangu na masikio yangu yanasikia kitu tofauti na kilichomo kwenye hisia na kionwacho na macho yangu. Huu ni mchezo wa kuigiza uchezwao na MH Lowassa na MH Jakaya Kikwete ili kutuzuga WaTZ kwamba kuna jambo la maana linaendelea.

MH Kikwete na Lowassa wote wako kwenye ile timu ya waTanzania 11 maarufu kama Mafisadi. Wote wawili wametuliza kwa mtindo mmoja kwa nyakati tofauti.JMK alianza kutuliza enzi zile za IPTL na mwenzie Lowassa amemalizia na RDC wote wamecheza mchezo mmoja kuhusu jambo moja.

Leo hii kwa makusudi kabisa naona wote ytumeamua kumsamehe MH Jakaya mrisho Kikwete kuhusu Uharamia wake tu kwa sababu yeye ni rais wa nchi. jambo hili la kufumbia macho uovu wa JMK ndilo litufanyalo tushindwe kujadiri mambo yote kwa nguvu moja. Dhambi aliyo ifanya Lowassa ndo hiyo hiyo imefanywa na Kikwete lakini hukumu yote anapewa Lowassa wakati yeye mwenyewe hajakubali bado kuwa Mbuzi wa Kafara.

Kikwete naye ni mwizi na haramia na hafai kabisa kuendelea kukalia kiti cha Urais wa nchi. Tukitambua kwamba mtu tunaye mtegemea naye si tegemeo tutatoka kwenye usingizi na kunawa matongo tongo tayari kuandika ukweli kuhusu serikali ya SISIEMU Rais wake na WM wa zamani MH Lowassa.

Siamini kabisa kwamba sasa hivi urafiki wao uko mashakani au umefutika. Lowassa na Kikwete bado wako kwenye timu moja na nia yao ni moja. Ila wametumia matukio haya ya uharamia wao kutugawa watanzania katika Mafungu ili waweze kutimiza hila zao za kutawala kwa zamu bila matatizo. Kikwete na Lowassa wanatumia kanuni ya Divide and Rule in a new perspective.

Watu walio kitu kimoja wamejifanya kujigawa makundi mawili yanayo jifanya kupingana ili Watanzania nao waingie mkenge na kujigawa. Watanzania wakijigawa kama ilivyo nia yao yenye kila uovu, Wao kina JMK na Lowassa wanawapa nafasi ya kupanga njama za hali ya juu zaidi za kulirudisha kundi lote la Lowassa kushika madaraka na kuiongoza nchi pindi muda ukifika kwa kisingizio cha kutuzuga wananchi kwamba kundi la Kikwete limeshindwa na hivyo nguvu mpya ya mageuzi imeingia.

Ni ujinga na ulimbukeni kufuata Ujuha wa Rais Kikwete na shoga yake Lowassa. Hawa ni wasanii, hawataacha kufanya usanii mpaka azma zao zikamailke.
Ndiyo maana hapa JF sasa hivi kumezuka mawazo ya kufukirika juu ya wachafuzi hawa huku uadui wa kinadhari kati ya Kikwete na Lowassa ukisambazwa na kupandikizwa kila kona ya JF na kulegeza misimamo ya wanachama wengi.

Kama Kikwete na Lowassa hawako kwenye kundi moja hakuna mtu angethubutu kuanzisha ujinga kule kwenye jimbo la Dr Mwakyembe kuhusu ujio wa Dr mwakyembe jimboni kwake. Dr Mwakyembe sasa hivi ndiye Victim wa sakata la RDC. Watanzania wote tupendao maendeleo ya taifa letu ni lazima tumlinde mtu huyu.

Haramia lowassa anapokelewa kwa nderemo na vifijo na serikali inakaa kimya lakini MH Mwakyembe anafedheheshwa mbele ya wapiga kura wake kwa kosa ambalo limefanywa na timu ya Lowassa na Kikwete ili tu kumlinda MH huyu aliye zaliwa aishi na kuwa Rais wa Tanzania.
Mwanya huo wa kuzuia Dr mwakyembe asishangiliwe ni dalili tosha ya urafiki wa Kikwete na Lowassa katika umoja wao wa Kiharamia.

Niliwahi kusikia kwamba MH Lowassa alisambaza na kuwapandikiza watendaji katika level ya Mkoa ,Wilaya, tarafa na kata kote nchini Tanzania kuhakikisha kwamba zamu yake ya kuukwa Urais ikifika anatimiza azma yake hiyo, Watanzania wapende wasipende.

Wakati ule nilidhani ni maneno ya watu sasa lakini kwa uthibitisho huu wa kilichotokea katika jimbo la Mwakyembe nadhani simulizi zile ni za kweli, kwani tayari watu waliowekwa na Lowassa ili kufanya kazi atakayo watuma wakati wowote wamekwisha anza kwa Ari na kasi mpya ya kichawi kuifanya kazi hiyo.

Nani alisambaza taarifa ya hofu na chuki dhidi ya Dr Mwakyembe?????

Kwa nini asambaze taarifa kama hiyo wakti Mwakyembe ni mmoja kati ya Watanzania wachache waliojitolea muhanga?

Hivi Watanzania tumefikia hatua ya kupenda pesa ,sifa vyeo na mamlaka kiasi cha Kushangilia Majambazi waibao na kuua bila huruma na kuwalaani waungwana walio tayari kusema kweli daima???

Binafsi nadhani wakati ukifika nitalazimika kuchukua hatua ya juu zaidi kuhakikisha MH Lowassa kamwe hapati nafasi ya kuwa rais Tanzania. Sioni mtu wa kunizuia.
Hatua nitakayo ichukua itamfanya ashiindwe kufurukuta kabisa kwa sababu hakuna binadamu katika historia ya dunia amewahi kufurukuta baada ya hatua hiyo kuchukuliwa.
Nitafanya hivyo endapo tu MH lowassa na kundi lake la kiYAKUZA wataendeleza mchezo wao huu mchafu wa kugeuza siasa za tanzania kuwa za magenge ya kiharamia.

Dawa yamoto ni moto sumu yake ni maji.

Ni hatua gani nitakayo chukua? Hiyo ni siri.
Siri kwa kawaida ni ya mtu mmoja.

Nasema yote haya ili wafuasi na mashabiki wake na yeye mwenyewe Lowassa wasije lalamika kwamba dhoruba aliyopewa ni uonevu na ni kinyume na haki za binadamu.
 
Walisema sisi tunabeba mabox huku majuu, tumewakubalia inabidi tuyabebe.

Lakini isije kuwa zuga ulikuwa hapa na jina lako la zamani. Kwi kwi kwi.............. Hivi kweli ilikuwaje ukae muda wote huo bila kupiga kope?
 
Walisema sisi tunabeba mabox huku majuu, tumewakubalia inabidi tuyabebe.

Lakini isije kuwa zuga ulikuwa hapa na jina lako la zamani. Kwi kwi kwi.............. Hivi kweli ilikuwaje ukae muda wote huo bila kupiga kope?

nilikuwa nachungulia siku moja moja ! kila mtu humu ana zawadi leo, na itabidi mnishukuru !
 

Give me a break!!

PINDA hahitaji kufanya "ZIARA YA KUJITAMBULISHA" hii yote ni wasting Tax payers money

Yeye alitakiwa atekeleze sera ya CCM kama chama tawala na sijaona katika sera zao wamesema watawala kila wakichaguliwa lakima watembee nchi nzima kujitambulisha


NI kweli kujitambulisha peke yake haina uzito, lakini ndani ya kujitambulisha kama kunakuwa na msisitizo wa mambo flani ambayo ni sehemu ya strategies zake za uongozi bado naona ni muhimu kupita mikoani na na mawilayani na kuwaeleza mwelekeo mpya wa serikali ya Pinda.

Mzee Game viongozi wetu wa kitaifa wakikaa ofisini tu tutakuwa tunaumia zaidi. Wao wakiwa si mafisadi na wakitaka kupambana na ufisadi nchi nzima ni bora wapite hukohuko mawilayani na miakoani wajionee wenyewe nini kinaendelea. Ufisadi unaojulikana sana ni huu katika ngazi ya kitaifa. Tujiulize ni pesa kiasi gani za watanzania zinapotea kupitia ufisadi wa kwenye mawilaya, mikoani, na kwenye miradi mbali mbali ya nchi nzima. Nafikiri wakaguzi wa mahesabu wanayo picha halisi ni jinsi gani tunaumizwa kupitia huko mikoani. Kuna barabara nyingine zimeanza kujengwa miaka mingi sasa hazijakamilika, kuna shule nyingi hazina walimu huko vijijini, hospitali nyingi hazina madaktari na madawa muhimu. Viongozi wa kitaifa wasipokuwa jirani na wananchi wa kawaida wataishiwa kuletewa ripoti za kutunga huko maofisini wakati watu wanaumia. Ni bora waende hukohuko wajionee wenyewe taabu za watu. tena ikiwezekana wafanye zile ziara za kushtukiza kama za Lyatonga Mrema enzi zake.

Ziara za kisiasa tunazipinga lakini kama kutakuwa na ziara zenye malengo flani nafikiri ni jambo jema kwa nchi yetu. Tanzania haiishii Dar es salaam tu. Ukipita huko vijijini kunasikitisha sana, hata wewe utatamani Rais angekuwepo ajionee wapiga kura wake wanavyoumia.
 
Madela Wa Madilu

Huko ndiko kumkoma hasa Nyani Giladi.
 
Good to see you back Kada........tuendelee na mijadala kuhusu mustakabali wa Taifa letu
 
Good to see you back Kada........tuendelee na mijadala kuhusu mustakabali wa Taifa letu
hamna neno, tuendelee na maneno !

Kwa hiyo sasa tutamuona mugongomugongo na tafiti then jadili? Karibu sana japokuwa hatukuku-miss sana🙂

wewe Kitila mi nilifikiri haupo hapa, anyway hao watu mugongo x2 ba tafiti then jadili hata sijui walitokea wapi !
 
Back
Top Bottom