Lowassa anasafishwa!

Lowassa anasafishwa!

Hivi katika job description yake aliambiwa aendelee upuuzi wa ziara za kisiasa mikoani kama Lowassa?

Wazee nafikiri kwa kuwa ndio kwanza amechukua ofisi, nafikiri ziara ya utambulisho na kutangaza sera zake na mikakati yake ni muhimu japo kwa muda mfupi hivi inaweza kuwa ni mapema mno.
.
Alitakiwa akae ofisini kwanza atleast apate feedback mwenzake aliishia wapi kwenye kazi njema na kazi za richmond. All in all ngoja aende tu apigiwe makofi kidogo ili aweze ku-feel ukubwa wa mamlaka na madaraka aliyonayo.

Wizara aliyotoka inafanya tutarajie kuwa anafahamu vitu vingi sana huko mikoani. NA labda Cheo kipya kwake ni kama karandinga la kufukua maeneo yaliyomshinda akiwa waziri wa kawaida - serikali za mitaa.

Kama anafanya ziara ambazo zitakuwa productive kwa Taifa basi tumtakie safari njema tu, ila kama ni zile ziara za rangi ya kijani na nyeusi basi awe makini sana.
 
Kwa wadhifa aliokuwa nao ziara ni muhimu sana...tena sana

Waziri Kiongozi anaziara kwa kisiwa kidogo kama kile sembuse Waziri Mkuu
 
Wazee nafikiri kwa kuwa ndio kwanza amechukua ofisi, nafikiri ziara ya utambulisho na kutangaza sera zake na mikakati yake ni muhimu japo kwa muda mfupi hivi inaweza kuwa ni mapema mno.
.
Alitakiwa akae ofisini kwanza atleast apate feedback mwenzake aliishia wapi kwenye kazi njema na kazi za richmond. All in all ngoja aende tu apigiwe makofi kidogo ili aweze ku-feel ukubwa wa mamlaka na madaraka aliyonayo.

Wizara aliyotoka inafanya tutarajie kuwa anafahamu vitu vingi sana huko mikoani. NA labda Cheo kipya kwake ni kama karandinga la kufukua maeneo yaliyomshinda akiwa waziri wa kawaida - serikali za mitaa.

Kama anafanya ziara ambazo zitakuwa productive kwa Taifa basi tumtakie safari njema tu, ila kama ni zile ziara za rangi ya kijani na nyeusi basi awe makini sana.


Give me a break!!

PINDA hahitaji kufanya "ZIARA YA KUJITAMBULISHA" hii yote ni wasting Tax payers money

Yeye alitakiwa atekeleze sera ya CCM kama chama tawala na sijaona katika sera zao wamesema watawala kila wakichaguliwa lakima watembee nchi nzima kujitambulisha


Watawala wasitegee watu wa chini watawasikiliza kama wao hawatekelezi yale ambayo wanaamrisha na moja wapo ni UFUJAJI WA PESA ZA WALIPA KODI

Hizi populist politics ilitakiwa waziache na waanze kuwa accountable kwa wananchi.PINDA kama hawezi kazi akae pembeni
 
Kwa mtizamo wangu, nafikiri ni mapema mno kuanza kumlaumu Pinda, labda tumchambue kwa maneno anayosema, lakini kwa vitendo nafikiri bado ni mapema mno,

Ofisi ya Waziri Mkuu, ni mikoa na wilaya at its core, sasa ni wajibu wake kusafiri mikoani, kujionea mwenyewe, bado siko tayari kuhukumu matendo yake Pinda, lakini kwa sasa nitamhukumu kwa maneno yake.
 
Kati ya Ofisi zinazo-waste taxpayer's money ni Ofisi ya waziri mkuu sababu kazi nyingine ni redundancy kwani zinafanywa na ofisi nyingine kama ya makamu wa Raisi, wizara ya kilimo, nk. Nafikiri tatizo lipo kwenye muundo wa ofisi au mgawanyo wa madaraka wa nani afanye hiki na kile kifanywe na nani. Vinginevyo taxpayers money is there kuliwa.
 
Ofisi ya Waziri Mkuu, ni mikoa na wilaya at its core, sasa ni wajibu wake kusafiri mikoani, kujionea mwenyewe, bado siko tayari kuhukumu matendo yake Pinda, lakini kwa sasa nitamhukumu kwa maneno yake.
Vipi kuhusu wizara ya tawala za mikoa,Je wizara hii sio ndio hasa inawajibika na mikoa na wilaya zake, Iwapo Ofisi ya Waziri Mkuu nayo inaundwa na mikoa na wilaya zake.. basi ni vema kwa waziri mkuu ambae ana uzoefu mkubwa wa tawala za mikoa kwenda mikoani hadi wilayani katika kutekeleza sehemu ya majukumu yake.

Utaratibu wa kutojiwekea mipaka katika uongozi na mzuri na unazidisha kasi ya utendaji. Hapa nina maana kuwa Waziri Mkuu anapokuwa Mikoani uwezo kutekeleza majukumu yake huwa na kasi kubwa kuliko akiwa ndani ya ofisi yake wizarani.
 
Hivi wakati wa bajeti si kila wizara including ya Waziri Mkuu, zinaomba pesa kwa kusema specifically watazitumiaje, kwa hiyo sidhani kwamba sasa hivi Pinda, anaposafiri anatumia hela za fungu lisilokuwa la safari kutoka kwenye bajeti ya wizara yake, ndio maana ninasema nitakuwa na tatizo kubwa kuskikia Pinda, anasafiri kwa hela kutoka kwenye mfuko wa kusaidia vilema, badala ya zile ambazo wizara yake ilipewa kwa ajili ya safari.
 
Hivi katika job description yake aliambiwa aendelee upuuzi wa ziara za kisiasa mikoani kama Lowassa?

Tulilalamika kuwa Lowassa na ofisi yake kazi yao ilikuwa ni kumaliza Tax payers mmoney kutembea mikoani bila sababu yoyote ya msingi

Mbona ofisi ya waziri mkuu haitoi mchanganuo wa hizi ziara?

Zina cost kiasi gani? ujumbe wake huwa ni watu wangapi? na zishaleta matunda yepi?

This is very disappointing to the max

Sidhani kama ni busara kukaa tu ofisini na kusikiliza shida na matakwa ya wananchi kupitia watu wengine.

Inabidi asafiri na kuwafuata wananchi huko huko walipo (Mikoani/Wilayani/Vijijini), asikilize shida, raha, hoja na maoni yao kisha akae ofisini na kuyatendea kazi, na sio tu akae ofisini kusubiri kupelekewa taarifa na watu wengine.

Sikumfahamu Pinda, lakini nilisoma hapa hapa JF kwamba mbali na kuwa mbuge, pia alifanya kazi ofisi ya Waziri Mkuu (correct me if I'm wrong), in that case anajua nini kinatakiwa katika ofisi husika (I hope).

Ni hayo tu.
 
Exactly...na mifano iko mingi tu!!

Huku GA kuna county moja inaitwa Clayton county. Population ni 90% African American....school district sasa hivi iko kwenye verge ya kupoteza accreditation. Budget ya district ni dola millioni 500 kwa mwaka lakini shule hazina vitabu na walimu wa kutosha kuwafundisha wanafunzi 52,000....where does all that money go? Halafu watu walioko kwenye bodi ni wale wale miaka nenda rudi huku kiwango cha elimu kikishuka mwaka baada ya mwaka. Kumbuka hawa watu huwa wanachaguliwa...kwa hiyo hizo nafasi za kwenye bodi ni kama za kisiasa...kama walivyo ma-district attorneys....yaani wee acha tu....mifano iko mingi mno

Mbona waafrika mnapenda kujishusha hadhi kiasi hicho? Kichaka si alisema anaenda kuibua WMD kule Iraq? "Irag has WMD and we know where they are" Halafu akaamua kufanya uvamizi mbao umeua na kufanya wakimbizi mamilioni ya Wairaq. Pia uvamizi huo ambao hadi sasa umegharimu $600 bilioni umeongeza kwa kasi sana budget deficit ya Marekani.

Hebu imagine tangu mwaka 2003 kama Marekani ingeamua kutumia pesa kama hizo hadi hii leo kuboresha mambo mbali mbali US, Kungekuwa na improvement kubwa mbali mbali ya mabarabara yenye ubovu wa kutisha, madaraja yaliyochoka kwa kukosa matengenezo na mengine yanaanguka yenyewe, Wamarekani chungu nzima kutokuwa na healtth coverage n.k. Badala ya kusema Waafrika ndivyo tulivyo kwa nini tusiseme binadamu ndivyo tulivyo!? Waafrika acheni kujishusha hadhi kiasi hicho! Msipojithamini nyinyi wenyewe hapa duniani, kamwe hakuna atakayewathamini. Hata wazungu wanavurunda kwenye mambo mengi tu!
 
Pinda kaenda kwao na ameenda kwao kama Waziri Mkuu. Sasa badala ya kwenda tu na kutembea na kusalimia ndugu kaenda kikazi. Nina uhakika itamchukua muda mrefu sana kurudi tena Mpanda kijijini. Nadhani kama Mbunge wa Mpanda anayo haki ya kutembelea huko na nina uhakika atakuwa anaenda kimya kimya kama Mbunge wao. Lakini katika hili anahitaji pia kufanya jambo jingine; kuileta Rukwa kwenye ramani ya Tanzania.

Rukwa ni miongoni mwa mikoa ya "pembezoni" ambayo imesahauliwa sana , sasa kwa wao hatimaye kutua kiongozi wa tatu wa kitaifa siyo tu kunawafanya wajulikane lakini pia kunasababisha wajibu wa aina fulani hivi.

Mahali fulani kwenye maandiko panasema "asiyejali wa kwao, ni mbaya kuliko asiyeamini". Kitu pekee ambacho kitakuwa ni kama Lowassa ni pale atakapoanza ziara za rukwa kila kukicha na kuanza kutengeneza kunda la Rukwa kama alivyofanya Lowassa na Arusha. Baadaya miezi miwili hivi akirudi Rukwa tena kama waziri mkuu tutakuwa na sababu ya kuanza kushtuka; lets cut him some slack.
 
Waungwana mi naona tumpe muda huyu mheshimiwa maana hajamaliza hata mwezi toka apewe ofisi, na si vibaya kwenda kwao kujitambulisha na kutoa shukrani kwa wanakijiji wenzake.
Lets pray for him lets pray for our country lets pray fo LOWASA, MSABAHA AND KARAMAGI to bring back our money.
 
Leo hii Kikwete akitutoka ghafla (Mungu apishie mbali) Dr. Shein ndiye atakuwa Rais wetu na makamu wake ni Mizengo Pinda.

Naogopa kusema nawaona hawa wawili kama mazezeta fulani hivi. Anyway, tusubiri tumpe Pinda muda zaidi! Labda na yeye iko siku itabidi akabidhiwe mkasi wa kukata utepe kwenye ziara zisizoisha nini? (Brazameni upo?)
 
Pale bungeni kila mmoja aliyetangaza kujiuzulu alionyesha wazi kuwa "ameonewa" na kimsingi hakufanya kosa lolote kama kamati ilivyo_point out!

Bunge na kamati yake wameonyesha kuwa watu wale walijiuzulu sio viongozi bora. Wananchi wote na wengi wa watanzania wanaamini kuwa viongozi wale ni mafisadi wala hakuna haja ya wao kujitetea na kusafishana kama hali inavyoendelea kwa sasa.

Nani anaweza kusema au kudhibitisha kuwa toka moyoni Raisi anaunga mkono mtizamo na msimamo wa Bunge,kamati yake na watanzania tulio wengi? Ni nani anaweza kuonyesha kuwa Makamu wa raisi na waziri mkuu wanaungana na bunge na watanzania katika kukemea kwa dhati kile kilichodhibitishwa na kamati ya bunge?

Kama kweli viongozi hao wanaona kama wanachi na bunge wanavyoona na hawana tofauti yeyote..wapi wamedhihirisha hilo kwa dhati bila mashaka yeyote?

Wapi wamekemea ufisadi wa RDC na waliohusika kwa dhati ya moyo, akili, fikra na kauli ya wazi kabisa?

Kama kinachoonekana ni kweli Wabunge watakuwa kwenye position gani juu ya hilo?

Mwakyembe na kamati wasipona publicaly viongozi wa juu wa taifa wakionyesha moyo wa furaha na kusema wazi mioyo yao juu ya kukemea Ufisadi wa viogozi husika dhidi RDC wao watajione vipi?

vijana wa vyuo vikuu na wengine wameandamana wazi kuupinga ufisadi wa RDC na majina ya wahusika wameandika kwenye mabango kwani bungeni walidhibitishwa. Kama vijana wale hawasikii kauli rasmimi juu ya Viongozi wa juu wa taifa wakiungana mkono na bunge ...vijana wale watapata ari ya kufanya maadamano na kuonyesha ari ya kweli dhidi ya Ufisadi? watajionaje?

Nauliza ni hakika na ni kweli kuwa viongozi wa juu wa Taifa wako pamoja na bunge na kamati yake kuukemea mafisadi wa RDC?
 
...hapohapo tuna methali zetu kuwa "mwana wa nyoka ni nyoka", "zimwi likujualo...." (hebu ziweke kwenye context, "mwana wa fisadi ni...." "fisadi akujuaye ....." nk)...

umenikumbusha mbali mkuu. methali hizi mimi mhh!! " mpanda ngazi hushuka; aliye juu mgonje chini; kutangulia si kufika; haraka haraka haina baraka;" wee acha tuu.
 
njia bora ya kusafisha wale walitajwa kama mafisadi ni kupitia mahakama. yanapotumika majukwaa ya kisiasa kufanya hiyo kazi nadhani ni kupandisha hasira za wananchi na kutupeleka kubaya
 
huyu PINDA anakaa wiki nzima kwao ndio kutafuta wachawi wamtengeneze? si alikabidhiwa rozali mburahati kanisani?
Bomu lingine hana kitu.
 
Waungwana mi naona tumpe muda huyu mheshimiwa maana hajamaliza hata mwezi toka apewe ofisi, na si vibaya kwenda kwao kujitambulisha na kutoa shukrani kwa wanakijiji wenzake.
Lets pray for him lets pray for our country lets pray fo LOWASA, MSABAHA AND KARAMAGI to bring back our money.

Nyota njema....
 
Kosa sio kosa mpaka lirudiwe.

Kosa lililorudiwa sio kosa mpaka kosa lililorudiwa lirudiwe.

Kosa lililorudiwa likirudiwa sio kosa mpaka kosa lililorudiwa likarudiwa lirudiwe.

Kosa lililorudiwa .....you get the point

Kwa logic hii hamna kosa.
 
Back
Top Bottom