HOTUBA YA MHE. MIZENGO KAYANZA PETER PINDA (MB) WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA WAKATI AKIFUNGUA RASMI MAFUNZO YA WAKURUGENZI WAPYA WA HALMASHAURI YALIYOFANYIKA HILUX HOTEL MOROGORO, TAREHE 13-08-2007
8. Ndugu Wakurugenzi, kwa maelezo hayo machache ni wazi kwamba majukumu mliyo nayo ni mazito. Kwa mfano majukumu yote ya Kisheria ambayo mengine sikuyataja hapa, msipoyatekeleza mnaweza kushitakiwa na kufunguliwa kesi Mahakamani. Ikithibitika Mahakamani kwamba kweli ulifanya makosa unaweza kufungwa. Madhara ya kifungo sote tunayafahamu.
Mambo yakiharibika nyie ndio watu wa kwanza kunyoshewa kidole. Tafadhalini sana tusifike huko. OWM-TAMISEMI kwa upande wake itashirikiana na nyinyi kuhakikisha kwamba mnatimiza wajibu wenu ipasavyo
10. Taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali.
Ndugu Wakurugenzi, historia inaonyesha kuwa suala la utunzaji wa vitabu vya hesabu za Halmashauri nchini limekwa ni tatizo kubwa kwa muda mrefu, japokuwa hivi karibuni hali imeanza kuwa nzuri kwa mujibu wa Taarifa za Mkaguzi Mkuu wa Mahesabu ya Serikali kwa mwaka 2004/05 na 2005/06 ikilinganishwa na miaka ya 2000 hadi 2003. Mwaka 2004/05 kati ya Halmashauri 117, Halmashauri 62 zilipata hati safi, 4 zilipata hati chafu na 51 zilipata hati zenye masharti. Mwaka 2005/06 kati ya Halmashauri 122, 52 zilipata hati safi, 4 zilipata hati chafu na 61 zilipata hati zenye masharti. Pamoja na mafanikio haya, bado kuna changamoto kubwa ya kuhakikisha kuwa Serikali inapata thamani kwa fedha zinazotolewa na kutumika katika Halmashauri kwa kuhakikisha kuwa, Halmashauri nyingi zinapata hati safi. Hii itawezekana tu iwapo Halmashauri zote zitazingatia Sheria, Kanuni na Taratibu za matumizi ya fedha za Serikali. Halmshauri zenu nyingi bado ni mpya. Hivyo, napenda kuwaagiza yafuatayo:
Maneno ya kuwawajibisha wakurugenzi yamerudiwa baada ya kupewa u-PM. Alishindiwa wapi wakati akiwa TAMISEMI?