Loose ends Kifo cha Martha Towo

Loose ends Kifo cha Martha Towo

Familia iko kwenye msiba mzito. Tunawapa pole. Ni kifo kinachotokana na mauaji hivyo hakiwezi kukosa mijadala na msingi wa hiki kifo cha mauaji lazima kiwe na sababu, kiwe na viashiria.

Kiwe na mhusika/wahusika wakuu
Kiwe na bajeti
Kiwe na watendaji/watimiza lengo. Kwa msingi huu wauaji
Kiwe na mpango kazi
Kiwe na fool proof
Kusiwe na dosari kuanzia kupanga, kutekeleza na hatimaye kutawanyika na kumalizana kama kuna malipo ya mwisho yalikuwa bado

Uchunguzi wa kifo hiki ni rahisi sana na si chini ya watu 20 wanaweza kuhusishwa nacho, ambapo watachujwa mpaka watabaki si chini ya watano .. Na ni uchunguzi rahisi kutokana na makosa mengi waliyofanya wauaji.. Hawakuwa wajuzi maana wajuzi huwa hawaachi alama! Japo kuna kosa moja dogo sana hufanya na kufumua mpango wote.

Uchunguzi wake utaanzia kazini kwake, maisha yake nje ya kazi, marafiki zake, wateja wake, mishe na dili zake, mawasiliano yake pamoja na mahusiano.. Hapa ni kwa ajili ya ku 'establish' Msingi wa kesi na 'motive' ya muuaji/wauaji.

Uchunguzi wa pili ni eneo lilikofanyika tukio.. Pori la Mitamba linalosifika kwa matukio ya mauaji, Mitamba halina tofauti sana na Mabwepande na kama linaweza kuchunguzwa vizuri kuna maiti ngingi mule zinaweza kuwa zimezikwa.

Mitamba liko Kibaha njia ya kwenda Bagamoyo eneo linaitwa Pangani.. Sehemu kubwa ya pori la Mitamba ni eneo la wizara ya mifugo na uvuvi na kuna kipindi matapeli wa viwanja Kibaha walilivamia na kuwauzia watu viwanja mpaka serikali ikaingilia kati.

Marehemu ni mkazi mwenyeji wa Kibaha Kwambonde kakulia hapo, kosoma Tumbi nknk. Wazazi wake wanaishi hapo mpaka sasa na ni watu unaoweza kuwaita maarufu eneo hilo na hata kanisani kwao Tumbi. Kwanini muuaji/wauaji wakachagua kuja kummaliza 'nyumbani kwao'?

Marehemu alisafiri salama salimini toka kituo chake cha kazi Shinyanga mpaka nyumbani Kwambonde Kibaha. Pengine alitumia ndege, usafiri binafsi au wa jumuiya lakini alifika salama.

Je, wauaji walikuwa wanamfuatilia kote huko?
Je, wauaji ndio walimuita aje Kibaha?
Je, lengo lake la kuja nyumbani Kibaha lilikuwa ninini?
Je, mpango wa kummaliza Kibaha pori la Mitamba ulikuwa mpango plan A au B?

Marehemu siku ya tukio alikuwa kanisani na ndugu zake.. Ni wazi alipata wito wa kuitwa nje mara moja ama kwa ishara ya mtu alikuwa ndani ya kanisa ama kwa simu kwakuwa mikoba yake aliacha alipokuwa kaketi. Hakurudi!

Ni wazi walimuita walikuwa nje kabisa ya kanisa barabarani! Kanisa la KKKT Tumbi liko pembezoni mwa barabara ya kuelekea Tumbi hospital. Ni wazi kulikuwa na gari ambalo ama alipanda kwa hiari ama kwa lazima/Kutekwa.

Ni wazi safari ilianza kuelekea Pangani pori la Mitamba.. Macho ya marehemu yata 'reveal' kilichotokea ndani ya gari kwa hicho kipindi chote mpaka kufika Mitamba kumwagiwa Petrol na kuchomwa moto!



Ukurasa wa pili juu ya mpango kazi ambao ninaamini ndio plan A.

Wauaji waliona eneo salama la kummaliza ni eneo la nyumbani alikozaliwa. Wauaji ni wenyeji wa Kibaha wanaofahamu vema jiografia ya Kibaha hasa eneo la Mitamba Pangani ambako hakuna doria za polisi, kuko kimya na mbali na makazi ya watu. Pia ni eneo lenye gate away nzuri kwahiyo ni rahisi kupoteza maboya mtu anayekufuatilia.

Unaweza kutokea Kimara
Unaweza kutokea Baobab
Unaweza kutokea Kibaha maili moja eneo la shell
Unaweza kutokea NIDA
Unaweza kutokea picha ya Ndege
Unaweza kutokea Loliondo nk na kote huko mtu asijue umetokea Mitamba Pangani

Kwa vyovyote mwenye mpango wake alikodi watu wa kumsaidia kuutimiza
  • Dereva
  • Mfuatiliaji aliyekuwa kanisani
  • Mtu aliyempatia sindano ya sumu
  • Backup
  • Hapa kuna watu wa kati hawakosekani
  • Malazi, kama watekeleza mpango walitoka mbali ni wazi walilala gesti za maeneo ya Kibaha ama jirani na Kibaha.
Loose ends/makosa ya kiutendaji yasiyotarajiwa
Wajuzi hufanya rehearsal hata zaidi ya mara tano kutegemeana na mlengwa na bajeti na kila rehearsal hugundua makosa kadhaa na kuyarekrbisha.

Je, makosa makubwa kwenye hili tukio ni yapi?

1. Mtandao wa mawasiliano simu na jumbe za sauti na maneno
2. Kuhusisha watu zaidi ya mmoja
3. Kutochagua wajuzi wa kazi
4. Kutofanya rehearsal
5. Kumchoma sindano ambayo haikuwa na sumu kali au ambayo haikuchomwa kwa usahihi
6. Kudhani amekwisha kufa hivyo kutengeneza fool proof ya kumchoma moto uliomzindua
7. Pengine kuondoka eneo la tukio haraka bila kuhakikisha ameungua vizuri
8. Macho kubaki salama, yalirekodi kila kitu

Kwa dondoo hizo hii kesi ni nyepesi kuliko ya bilionea Msuya ana yule mzungu wa tembo. Marehemu alibaki kuwa hai kuanzia tarehe 3 march mpaka 9 alipoaga dunia. Siku sita ni nyingi sana kuweza kupata na kujua mengi

Damu ya mtu ni nzito na inanuka! Harufu hukoma haki ikitendeka
Ila watu wanaroho ngumu jaman.emungu utusadie na hii dunia iliyojaa watu wakatili.
 
Calm down, well planned crime bongo hadakwi hiyo sahau, labda hao wanaoanzia kwa waganga
Ya group mnanaswa labda ya mtu mmoja,hakuna siri ya watu wawili.
Pili labda wahanga waamue tu kupotezea na police ufanya Kazi KWA msukumo na uwezeshaji wa ndugu.
Labda tu ndugu waache sababu haya mambo ni gharama sana kufanya uchunguzi na serikali haiwezi toa pesa za uchunguzi.
Wengi huwa wanaamua kuachia tu ndio pona pona ya wauaji
 
Kiintelenjensia.
Hakuna muhalifu yeyeto Smart ni lazima ataacha tu alama pa kuanzia.
Watu wakiingia mitamboni mbona sekunde tu wauaji udakwa chapu.
Hapo pa kuanzia ni sehemu mbili tu ishu ya mapenzi au kazini. Tap call zake zote kuanzia siku ya tukio rudi nyuma hata miezi 3 ukizisikiliza zitakupa starting point na lazima utampata tu muuaji.
Ipo hivi
Kabla ya mauaji huwa ni lazima mawasiliano ya simu uwepo yakiwa na nia ya urafiki na sio hitimisho la mauaji, mauaji huja baada ya kushindwa kufikiana kwa muafaka.
Kosa kubwa la wauaji ushindwa kutambua back walitumia simu kuongea.
KWA hili unaweza tumia
1.Technologia ya mawasiliano kupitia call recording
2.White magic pia ukupa picha ya tukio zima.
Ukimsikiliza baba yake anaongea codes ni kama kuna kitu anakihisia ambacho kina uelekeo wa ukweli sababu alikuwa karibu na binti yake kuna mambo alishea nae thus hakutaka kufunguka sana.
Kifupi hakuna muhalifu smart popote duniani hata awe na akili au ujanja vipi ni lazima ataacha shaka.
Technology na white magic haziongopi. Labda tu wahanga waamue tu kumuachia Mungu , KARMA
wahalifu wa bongo wengi shule hawana yani mtu anasafiri na simu yake kwenda kufanya uhalifu ila anatumia simu nyingine kuwasiliana hajui kama mtandao unatrace simu bila hata kuwasiliana.... WENGI MAWASILIANO NDO YANAWAPONZA.
 
Hapo kanisani kama pana cctv itabaini aliondoka na nani, ukiipata picha ya aliyeondoka nae. Unapost kwenye media unatangaza dau, lazima anauzwa na watu walio karibu nae au watakaomuoana. Ukimpata tu yeye ndie atawaja wahusika wote.
Na kama aliitwa kwa namba ya SIMU au msg bhasi aliemtumia msg hata kama alitumia kitambulisho feki kujisajili chain nzima inashikwaa so long technology ya simu imehusika HATAPONA MTU labda wahonge mabilion
 
Sasa last image si itakuwa ma Dr wa hospital? Ndiyo maana nikauliza wanatumia technolojia gani ku retriew data za kwenye macho? let say wanavuta image labda za week moja nyuma kutoka kwenye retina.
hii kitu zaman tulikua tunaaminishwa hadi marehemu wanatobolewa macho...ila ilikuja julikana ni uongo
 
Ukumbuke chunguzi ni uwezo wa teknolojia na bajeti, kuna chunguzi huchukua hadi miaka 50 , yaani ukweli unakuja kujulikana hata muhalifu alishafariki muda tu, haya mambo yaache kama yalivo, japo kwa slogan ya kichunguzi ya “ ulipo tupo “ au “ palipo na mtu nasi tupo “ wahalifu uchwara hudakwa kama kuku tu
Kwetu bajeti ya uchunguzi labda ndugu wawawezeshe police tofauti na ulaya wao bajeti ya kutosha kufanya uchunguzi ipo,pia ni sifa kwa chombo pia ni kama homework kwa study za field ya uchunguzi.
Thus bongo mtu akifanya uhalifu anakimbia mkoa mwingine anakaa miaka akirudi hata jalada lake halipo kituo alichokuwepo.
Mfano wale wote wauza mayai wa kitunda wengi walikimbia uhalifu Tarime ya mauaji,wizi,kujeruhi,baada ya miaka hata 10 ndo anarudi kusalimia kwao kesi ilishaisha nguvu.
 
Polisi wetu wakiamua wanaweza kuwakamata wote hao.

Shida ni moja. Huwa wanaweka nguvu kwenye upelelezi wenye interest za Taifa ama watu wenye mahela.

Mfano mzungu wa tembo ule upepelezi ulikuwa mkali sababu ulikuwa na interest za seriakli na pia taasisi za kimataifa zilihitaji kujua matokeo

Pia kwa bilionea msuya. Matajiri wa madini na connections za bilionea msuya kwa wakubwa zilifanya upelelezi uwe mkali.

Mwenzangu na mie ukiuliwa hawapotezi muda
 
Kahama.
Kibaha.
Mhasibu/Afisa mikopo Boa bank.
kuacha kazi mwenzi mmoja nyuma.
Mipango ya ndoa.
Kumiliki mali.
Kuchukuliwa kanisani.

Kwanini alifuatwa kanisani? inamaana huwa hana mizungukuko mingine zaidi ya nyumbani na kanisani? Kwanini ilikuwa rahisi kwa wauwani kumfuata kanisani?

Kwanini wamteke, sindano ya sumu na kumchoma moto, huyu dada hatokagi out? haendagi disco/club nk.

Accounts na transaction za hela za dada ziangaliwe siku za karibuni kulifanyika nini.
 
Nimesoma mahala, hii wanasema Boss wake alimwambia aandike cheque ya 1B.
Halafu aseme ilikosewa, ili hizo hela zisionekane bank. Inaonekana martha hakutaka kulitekeleza.

Akawa anamsumbua, akaomba ruhusu kwenda kwao Kibaha. Inasemekana, boss wake akampigia Baba mzazi wa Martha, akamwambia amwambie mtoto wake, aache kazi ndani ya masaa 24.

Katika yote hayo yaliyokuwa yanaendelea, Martha alikuwa akiwasiliana na Baba yake na mchumba wake.

Wakasema siku ya tukio, alipigiwa simu na wafanyakazi wenzake, wa Shinyanga. Kuwa wanasafiri watapitia hapo Kibaha, wamsalimu mara moja. Alipotoka hakurudi tena.
Inavyosemakana boss anashikiliwa.
*Nimesoma sehemu tu, nikaileta kama ilivyo.
ah ah cheque ya billion moja sio ah ah dah ingekua rahisi hivyo basi wafanyakazi wengi wa bank wangekua mabilionea..eh nani alifanya clearance ya hiyo cheque..halafu kwahiyo mtu unapigiwa tu simu uache kazi ah ah am humbled you know
 
Nilipokuwa vidudu niliambiwa ukimuua mtu ye anaenda mbinguni kustarehe kisha dhambi zake zote zinahamishiwa kwako.Sasa kuanzia miaka hiyo mpk leo suala la kuua naliwekaga mbali sana hata niwe nimekwazika vipi.Ipo sababu nzito sana ya hawa watu kutenda hivi,ila damu itawadai daima.
 
Nilipokuwa vidudu niliambiwa ukimuua mtu ye anaenda mbinguni kustatehe kisha dhambi zake zote zinahamishiwa kwako.Sasa kuanzia miaka hiyo mpk leo suala la kuua naliwekaga mbali sana hata niwe nimekwazika vipi.Ipo sababu nzito sana ya hawa watu kutenda hivi,ila damu itawadai daima.
 
Back
Top Bottom