Loose ends Kifo cha Martha Towo

Loose ends Kifo cha Martha Towo

Hapo wanakaa watu wanne mezani, kila mmoja na karatasi nyeupe na penseli sio kalamu ya wino, then kuna mtu wa tano hua anitwa analyst anakua anaeleza kutokea kwanza shinyanga yule mtu aliishije huko, atakuja analyst wa pili wa kibaha ataeleza wale wanne watandelea kuchora michoro ya penseli kila mtu kivyake, halafu baadae kuna kitu tunaita added information hizi hutoka idara mbalimbali ikiwamo labda TISS , nazo zinachorwa wakati huo wahisiwa wa mwanzo walishakamatwa muda mrefu yaani afisa upelelezi jeshi la polisi wilaya atashirikiana na RCO na RSO wake issue mapema mchana kweupe baadhi ya waliokamatwa watafirwa na kufinywa mapumbu hapo anti robery ndio watahusika na zoezi ay watapigwa shot za matakoni hadi mambo yataisha within 30 days kesi mahakamani tayari upelelezi utaendelea kukamilishwa taratibu kwa kuua mawasiliano ya wahusika mmoja baada ya mwingine hadi wajichuje wenyewe kama kuku wenye mdondo pumbavu zao, wahalifu hao wa huyo binti
Hapo kwenye kubinya pumbu wanakosea sana na kuwapa mateso. Mtu anakiri kwa kuogopa mateso. Hiyo ilitokea wilayani same miaka 3 iliyopita. Mtu alimenywa kucha hadi akakiri mauaji ya x wake. Kumbe muuaji ni fundi. Walikuja kumkamata kupitia simu ya marehemu kutumiwa na baba wa muuaji baada ya mwaka tangia mauaji. Ndo pona pona ya ex wa marehemu
 
Nipo nje ya mada nisamehewe!

Jamiiforums sijui wamebadili nini tena kwa tunaotumia browser imezidi kuchukiza,nipo nasoma main post mtu ana-reply uzi inanipeleka kwenye new post wakati sijamaliza kujua maudhui ya mleta mada.

Hiyo namna ya ku-like sasa,wameweka vijiboksi boksi mtu hata hujui ufanyeje bora ile ya emoj kuliko hii.
Hio kwenye app yako tu
 
Hapo kwenye kubinya pumbu wanakosea sana na kuwapa mateso. Mtu anakiri kwa kuogopa mateso. Hiyo ilitokea wilayani same miaka 3 iliyopita. Mtu alimenywa kucha hadi akakiri mauaji ya x wake. Kumbe muuaji ni fundi. Walikuja kumkamata kupitia simu ya marehemu kutumiwa na baba wa muuaji baada ya mwaka tangia mauaji. Ndo pona pona ya ex wa marehemu

Wasalimie same, sijui uko mjini, ndungu, makanya, au njoro wape salamu
 
Familia iko kwenye msiba mzito. Tunawapa pole. Ni kifo kinachotokana na mauaji hivyo hakiwezi kukosa mijadala na msingi wa hiki kifo cha mauaji lazima kiwe na sababu, kiwe na viashiria.

Kiwe na mhusika/wahusika wakuu
Kiwe na bajeti
Kiwe na watendaji/watimiza lengo. Kwa msingi huu wauaji
Kiwe na mpango kazi
Kiwe na fool proof
Kusiwe na dosari kuanzia kupanga, kutekeleza na hatimaye kutawanyika na kumalizana kama kuna malipo ya mwisho yalikuwa bado

Uchunguzi wa kifo hiki ni rahisi sana na si chini ya watu 20 wanaweza kuhusishwa nacho, ambapo watachujwa mpaka watabaki si chini ya watano .. Na ni uchunguzi rahisi kutokana na makosa mengi waliyofanya wauaji.. Hawakuwa wajuzi maana wajuzi huwa hawaachi alama! Japo kuna kosa moja dogo sana hufanya na kufumua mpango wote.

Uchunguzi wake utaanzia kazini kwake, maisha yake nje ya kazi, marafiki zake, wateja wake, mishe na dili zake, mawasiliano yake pamoja na mahusiano.. Hapa ni kwa ajili ya ku 'establish' Msingi wa kesi na 'motive' ya muuaji/wauaji.

Uchunguzi wa pili ni eneo lilikofanyika tukio.. Pori la Mitamba linalosifika kwa matukio ya mauaji, Mitamba halina tofauti sana na Mabwepande na kama linaweza kuchunguzwa vizuri kuna maiti ngingi mule zinaweza kuwa zimezikwa.

Mitamba liko Kibaha njia ya kwenda Bagamoyo eneo linaitwa Pangani.. Sehemu kubwa ya pori la Mitamba ni eneo la wizara ya mifugo na uvuvi na kuna kipindi matapeli wa viwanja Kibaha walilivamia na kuwauzia watu viwanja mpaka serikali ikaingilia kati.

Marehemu ni mkazi mwenyeji wa Kibaha Kwambonde kakulia hapo, kosoma Tumbi nknk. Wazazi wake wanaishi hapo mpaka sasa na ni watu unaoweza kuwaita maarufu eneo hilo na hata kanisani kwao Tumbi. Kwanini muuaji/wauaji wakachagua kuja kummaliza 'nyumbani kwao'?

Marehemu alisafiri salama salimini toka kituo chake cha kazi Shinyanga mpaka nyumbani Kwambonde Kibaha. Pengine alitumia ndege, usafiri binafsi au wa jumuiya lakini alifika salama.

Je, wauaji walikuwa wanamfuatilia kote huko?
Je, wauaji ndio walimuita aje Kibaha?
Je, lengo lake la kuja nyumbani Kibaha lilikuwa ninini?
Je, mpango wa kummaliza Kibaha pori la Mitamba ulikuwa mpango plan A au B?

Marehemu siku ya tukio alikuwa kanisani na ndugu zake.. Ni wazi alipata wito wa kuitwa nje mara moja ama kwa ishara ya mtu alikuwa ndani ya kanisa ama kwa simu kwakuwa mikoba yake aliacha alipokuwa kaketi. Hakurudi!

Ni wazi walimuita walikuwa nje kabisa ya kanisa barabarani! Kanisa la KKKT Tumbi liko pembezoni mwa barabara ya kuelekea Tumbi hospital. Ni wazi kulikuwa na gari ambalo ama alipanda kwa hiari ama kwa lazima/Kutekwa.

Ni wazi safari ilianza kuelekea Pangani pori la Mitamba.. Macho ya marehemu yata 'reveal' kilichotokea ndani ya gari kwa hicho kipindi chote mpaka kufika Mitamba kumwagiwa Petrol na kuchomwa moto!

Ukurasa wa pili juu ya mpango kazi ambao ninaamini ndio plan A.

Wauaji waliona eneo salama la kummaliza ni eneo la nyumbani alikozaliwa. Wauaji ni wenyeji wa Kibaha wanaofahamu vema jiografia ya Kibaha hasa eneo la Mitamba Pangani ambako hakuna doria za polisi, kuko kimya na mbali na makazi ya watu. Pia ni eneo lenye gate away nzuri kwahiyo ni rahisi kupoteza maboya mtu anayekufuatilia.

Unaweza kutokea Kimara
Unaweza kutokea Baobab
Unaweza kutokea Kibaha maili moja eneo la shell
Unaweza kutokea NIDA
Unaweza kutokea picha ya Ndege
Unaweza kutokea Loliondo nk na kote huko mtu asijue umetokea Mitamba Pangani

Kwa vyovyote mwenye mpango wake alikodi watu wa kumsaidia kuutimiza
  • Dereva
  • Mfuatiliaji aliyekuwa kanisani
  • Mtu aliyempatia sindano ya sumu
  • Backup
  • Hapa kuna watu wa kati hawakosekani
  • Malazi, kama watekeleza mpango walitoka mbali ni wazi walilala gesti za maeneo ya Kibaha ama jirani na Kibaha.
Loose ends/makosa ya kiutendaji yasiyotarajiwa
Wajuzi hufanya rehearsal hata zaidi ya mara tano kutegemeana na mlengwa na bajeti na kila rehearsal hugundua makosa kadhaa na kuyarekrbisha.

Je, makosa makubwa kwenye hili tukio ni yapi?

1. Mtandao wa mawasiliano simu na jumbe za sauti na maneno
2. Kuhusisha watu zaidi ya mmoja
3. Kutochagua wajuzi wa kazi
4. Kutofanya rehearsal
5. Kumchoma sindano ambayo haikuwa na sumu kali au ambayo haikuchomwa kwa usahihi
6. Kudhani amekwisha kufa hivyo kutengeneza fool proof ya kumchoma moto uliomzindua
7. Pengine kuondoka eneo la tukio haraka bila kuhakikisha ameungua vizuri
8. Macho kubaki salama, yalirekodi kila kitu

Kwa dondoo hizo hii kesi ni nyepesi kuliko ya bilionea Msuya ana yule mzungu wa tembo. Marehemu alibaki kuwa hai kuanzia tarehe 3 march mpaka 9 alipoaga dunia. Siku sita ni nyingi sana kuweza kupata na kujua mengi

Damu ya mtu ni nzito na inanuka! Harufu hukoma haki ikitendeka
Watu waliweza kumuua waziri mkuu,Sokoine,sembuse huyu lay person!?kuhusu DNA kukutwa kwenye nguo au mwili wa marehemu Hilo,halipo,maana waliutia moto mwili!kazi ya benk alikuwa ameisha acha,
Kama watu walimuua yule mtangazaji wa ITV,aliyekuwa Hana mkono mmoja,na wakabeba mwili wakautupa makumbusho!!na hawajapatikana mpaka leo.
Hata huyo dada,ndugu zake,wazike tu maisha yaendelee,jeshi letu halina hali Wala motisha ya kufatilia vifo vya watu wadogo kama Hawa.
 
Kila unachoona kwenye teknolojia unafahamu kuna njia za kuepuja usijulikane, hizo iphone zina setting za security ambazo hata maongezi yako hayawezi kua recorded popote na watu wakitrace wanakuta nill! Sema wahalifu wetu wa kutegemea matunguli wanadakwa tu kirahisi hawa hata haina shida
Mkuu ngoja nitete na mshana ww ni muhimu sana
 
Kila unachoona kwenye teknolojia unafahamu kuna njia za kuepuja usijulikane, hizo iphone zina setting za security ambazo hata maongezi yako hayawezi kua recorded popote na watu wakitrace wanakuta nill! Sema wahalifu wetu wa kutegemea matunguli wanadakwa tu kirahisi hawa hata haina shida
Kinyume chake: Kila unacho ona kwenye teknolojia kuna njia ya kufanya ili kijulikane.

Teknolojia haina siri asilimia zote
 
Watu waliweza kumuua waziri mkuu,Sokoine,sembuse huyu lay person!?kuhusu DNA kukutwa kwenye nguo au mwili wa marehemu Hilo,halipo,maana waliutia moto mwili!kazi ya benk alikuwa ameisha acha,
Kama watu walimuua yule mtangazaji wa ITV,aliyekuwa Hana mkono mmoja,na wakabeba mwili wakautupa makumbusho!!na hawajapatikana mpaka leo.
Hata huyo dada,ndugu zake,wazike tu maisha yaendelee,jeshi letu halina hali Wala motisha ya kufatilia vifo vya watu wadogo kama Hawa.
Sio udogo ama ukubwa wa mtu bali ni kuhusu uhai
 
Watu waliweza kumuua waziri mkuu,Sokoine,sembuse huyu lay person!?kuhusu DNA kukutwa kwenye nguo au mwili wa marehemu Hilo,halipo,maana waliutia moto mwili!kazi ya benk alikuwa ameisha acha,
Kama watu walimuua yule mtangazaji wa ITV,aliyekuwa Hana mkono mmoja,na wakabeba mwili wakautupa makumbusho!!na hawajapatikana mpaka leo.
Hata huyo dada,ndugu zake,wazike tu maisha yaendelee,jeshi letu halina hali Wala motisha ya kufatilia vifo vya watu wadogo kama Hawa.

Umekosea sana , kwanza upelelezi hufanyika kwa gharama ili kuwabaini wahalifu, halafu faida kubwa kwanza ni kuzuia uhalifu mwingine wa njia hiyo kutokea, lakini serikali ina wajibu wa kulinda raia na mali zake, lakini kwenye uhai hakuna udogo au ukubwa, rejea kesi ya msuya wa arusha na je toka enzi zile umesikia mauaji tena ya watu wa tanzanite kama ilivokua zamani? Au toka akamatwe yule jamaa wa mwanza na kinondoni umesikia tena mtu kuvamiwa akiwa katoka benki kuchukua pesa, uchunguzi hufanyika kubaini wahalifu lakini pia kumaliza mtandao wa uhalifu ule,
 
Back
Top Bottom