RO hawezi kujua kuwa Kibelloh ni mwizi na akamuacha, baada ya bitter vita vyao pale London, no way ninarudia kwamba RO anaweza kumuachia Kibelloh na huo ushahiudi mnaousema, na JK asingeweza na hataweza kumuachia Kibelloh akijua tu kuwa ni mwizi, kweli kuna viongozi ambao Jk anaweza kuangalia lwingine lakni sio Kibelloh, halafu yeye mwenyewe Kibelloh knows better kuwa maadui wote alionao kuanzia serikalini mpaka wananchi, hawawezi kumuachia by now kungekuwa na ushahidi wa kina kule ikulu,
Ni kweli toka tupate uhuru ni kiongozi mmoja tu aliyewahi kuapatikana na hatia mahakamani ya kuiibia serikali yetu, naye ni Dr. Mlingwa peke yake aliyekuwa katibu mkuu wa wizara ya ujenzi, enzi za Mwinyi, basi, nani wa kulaumiwa ni sisi wenyewe wananchi kwa kuwaruhusu viongozi wetu kutuchezea miaka nenda miaka rudi, tulipewa pilau na fulana na kofia basi,
CCM haijawahi kumlazimisha mwananchi yoyote kuipigia kura, tatizo ni sisi wananchi tusiojua lolote, na ni issues kama hizi ndio zinathibitisha zaidi kuwa we have no idea what is going on, balozi wa bongo nje ni hela ngapi anazoweza kuiba mpaka kutufanya tusiwe na umeme? Mpaka tusiwe na madawa hospitali? Juzi hapa Dar, imegunduliwa kuwa imekuwa ni tabia sugu ya wenye maduka ya madawa kuwauzia wananchi dawa zilizo expire, sasa ungetegemea kilio kikubwa cha wananchi, hasa media, guess what NOTHING, wazee wa majuu huko hebu tuambieni hiyo inawezekana huko kwenu majuu?
Ni sisi wananchi tuliolala usingizi ndio tatizo la nji yetu sio viongozi, kuhusu marupurupu ya wabunge mbona wananchi walikuja juu na wabunge wakanywea? Why not kwenye other issues as well, badala yake ni kulilia Kibelloh tu, baada ya utumishi wote alioufanya kwa taifa, all we can say to him ni kwamba umetuibia picha na hela za geti, hizi ni hadithi za mtaani tu,
yaani Kibelloh ameshindwa kuiba utalii, ambako ndiko kwenye dola hasa, halafu akashindwa kuiba kwenye ukatibu wa foreign ambako ndiko kwenye dola hasa, akasubiri kuiba London tena picha na hela za geti,
kwa mwendo huu CCM watatawala milele!, maana sisi wananchi tumeshawahakikishia kuwa we are good for only, fulana, pilau, na kofia za kijani, yes hivi unajua leo matajiri wanapoamua kugombea nmafasi za CCM, huwa wana wasi wasi na viongozi wa CCM sio wananchi hata kidogo, kwa mfano uchaguzi wa ubunge uliopita Kigamboni, ili kumtoa Manji ilibidi kiongozi mmoja wa CCM aje juu kwenye kamati kuu kuwa wakati umefika wa CCM kubinafsishwa, kama Manji si good kuwa mbunge wake lakini tayari wananchi walishamchagua,
wakati umefika wa sisi wananchi wa bongo kujiangalaia usoni, na ku-get serious na real issues ambazo ni muhimu kwa taifa letu, lakini as long as tunakubali unafiki wa kiongozi mmoja dhidi ya mwingine kama huu wa Kibelloh, CCm wataendelea tu kutuchezea!