LONDON: Kibelloh & Disturbing News!

Nilijua tu hii habari isingefika mbali kwa vile haikufuata maadili ya Tafiti then jadili, busara kwa habari kama hii ilikuwa nadhani ni kutafuta ukweli kwanza na kisha kuweka hapa, au kuomba data kiumakini kabisa kama yule ambae alitaka kujua wasifu wa wateule wa Rais ilikuwa kibusara kabisa lakini hapa mtu kakurupuka uuh sasa unashindwa hata kujua mantiki ilikuwa ni nini.

Data za kuwa balozi Mwanaidi alipita hapa akapitishwa ofisini kisirisiri nazichukua with a pinch of salt kwa vile balozi mteule hajawahi kupita hapa UK tangu ateuliwe! amekuja baada ya muda kadhaa akiwa Dar presumably wizarani for formalities, tangu uteuzi hajapita hapa zaidi ya alivyokuja two fridays ago kuanza majukumu rasmi. tafiti utajua.

Nimemtembelea Balozi Kibelloh ofisini kwake mara mbili akiwa ofisini na nilikwenda kumuaga habari njema za kwenda France zilipokuja na hii ilikuwa very punde before he left, hakuna picha za mabalozi wa zamani ofisini kwake wala kwenye foyers leading to his offices zaidi ya picha yake na Malkia Elizabeth.

Kikubwa kilichopo ni orodha kwake ni picha kuubwa ya rais JK na bendera ikipepea na pia kuna kitabu cha wageni ambacho kina orodha ya mabalozi wetu pale.

Hizi habari muwe mnachunguza, otherwise mtakuwa mnatuletea non-issues hapa, lakini kama alivyosema Mwanakijiji read at your own peril...
 
Hapana,

(1). Mama Mwanaidi, alipita London akiwa njiani kwenda Norway, the matter of fact kuna malalmiko rasmi pale foreign kutoka kwa serikali ya UK, kutokana na hiyo safari na hasa ku-sneack ofisini!

(2). Mzee Kibelloh, kabla ya kuondoka London aliomba picha za mabalozi wote waliowahi kuwa hapo London, yaani wabongo, with understanding kwamba atazibandika somewhere, kama alivyoomba, sasa ameziweka wapi? Sijui, lakini alitumiwa rasmi na foreign,

Ninashaangaa kwamba umeshindwa kuongelea la wizi wa picha at all, lakini umepata muda wa kuongelea the sideshow? WHY?

Here you are kama kawaida yako kutaka kuipindisha issue, issue ni wizi wa picha unaodaiwa kufanywa na balozi Kibelloh, kabla ya kuondoka London, nimetumiwa kwenye PM, na ukienda kule Maoni, org kuna mada kabisaa!, Huo utafiti ulioutoa, labda unaposema ulikwenda kumuona Kibelloh, sasa if that is the case na kuongea naye hata kwa simu ni utafiti basi and if that is your case sitaki kuwa mtafiti na kujadili, maana kama hiyo uliyoisema ndio formula yakre basi ni NONESENSE!

Mzee Kulikoni kumbe angalau your are fair minded,

Mzee Mlalahoi,

Ninaona jazba yako katika kujibu kitu usichoelewa, at one point umeuliza swali, sasa kabla hujajibiwa umeanza kutoa hukumu, sasa let me get things straight,

(1). Issue ya Real sijui aliyeitoa ni nani, ila ninajua kuwa kuna aliyem-crticise rais wetu, mimi ninapingana na hiyo message kwamba rais anayo haki ya kuwa mwanamichezo, akiwa kama rais au mwananchi wa Tanzania, at this point wewe na mimi hatujui alikwenda pale Real under which capacity, rais au mwananchi,

(a). Kama alienda kama rais tatizo ni nini? (b). Na kama alikwenda kama raia, tatizo ni nini?

The rest ya maneno yako samahani sina muda! Ila nitalumbana na wewe at anytime ukijibu hayo maswali mawili, then we can make an issue, unajua one thing about me, huwa siogopi na huwa ninasema asiyeweza kusimamia hoja yake hapa hapaswi kuwa hapa!
 
Mzee Es said:
Hapana,


Mzee Mlalahoi,

Ninaona jazba yako katika kujibu kitu usichoelewa, at one point umeuliza swali, sasa kabla hujajibiwa umeanza kutoa hukumu, sasa let me get things straight,

(1). Issue ya Real sijui aliyeitoa ni nani, ila ninajua kuwa kuna aliyem-crticise rais wetu, mimi ninapingana na hiyo message kwamba rais anayo haki ya kuwa mwanamichezo, akiwa kama rais au mwananchi wa Tanzania, at this point wewe na mimi hatujui alikwenda pale Real under which capacity, rais au mwananchi,

(a). Kama alienda kama rais tatizo ni nini? (b). Na kama alikwenda kama raia, tatizo ni nini?

The rest ya maneno yako samahani sina muda! Ila nitalumbana na wewe at anytime ukijibu hayo maswali mawili, then we can make an issue, unajua one thing about me, huwa siogopi na huwa ninasema asiyeweza kusimamia hoja yake hapa hapaswi kuwa hapa!

Kabla sijakujibu,naomba niseme kuwa tatizo lako lipo kwenye forums nyingi tu:watu flani wanaoamini kuwa siku zote wako sahihi,wanajua kila kitu na hawachagui maneno wanapotoa michango inayopingana na mawazo yako.Wapo watu ambao hawaafikiani na baadhi ya hoja zako lakini hawa-conclude kuwa hoja hizo ni NONSENSE.

Majibu ya maswali yako hayo mawili ni kwamba wewe mwenyewe ni mpindishaji mzuri tu wa mada.Reaction yangu ilikuwa juu ya kauli yako kuwa mada ya "JK kuileta Real Madrid Bongo" ni non-issue na NONSENSE.Unasema hukubaliani na aliyem-criticize JK kuhusu ziara yake Barnebau,je hoja nzima imekuwa NONSENSE kwa vile tu hukubaliani na criticism hiyo dhidi ya JK?Excuse me,who on earth are you tell someone alichoandika ni nonsense?Dont be judgemental.Hapa kuna makundi ya watu wa aina tofauti:nyie wenye high connections,mnaojua nini kinaendelea ofisi gani,nk na sie ambao tunaegemea zaidi kwenye world views na upeo wetu mdogo tulionao kiakili.As I said,kwa jinsi navyokuheshimu siwezi kuuita mchango wako NONSENSE.Non-issue,may be.Nonsense,no way.Suala sio huwa huogopi kusema na kwamba asie na hoja asije hapa,bali la muhimu ni kutumia lugha ya kistaarabu hata pale mtu anapotoa mchango ambao kwako hauna maana.Upeo wako wa juu ulio nao wewe sio sawa na upeo wangu mdogo unaonitosheleza mwenyewe.Respect pleeez.
 
Kijana bado sielewi tatizo lako, ambalo linaonekana kuwa personal mimi sina muda wa personal na hayo uliyoyasema ya personal nimeyasikia kwa muda mrefu sana toka BCS, na at this age sina mpango wa kubadilika, I was never raised kwenye kuwa binadamu wa SORRY STATE,

I was raised a man, and I am a big boy na America ikaniimarisha zaidi namna ya kusimamia mawazo yangu, so far kwenye maneno yako sioni issue ya kuwasaidia wengine kwenye hii forum, nitakapoiona we will talk like big boys!
 
Mzee Es said:
Kijana bado sielewi tatizo lako, ambalo linaonekana kuwa personal mimi sina muda wa personal na hayo uliyoyasema ya personal nimeyasikia kwa muda mrefu sana toka BCS, na at this age sina mpango wa kubadilika, I was never raised kwenye kuwa binadamu wa SORRY STATE,

I was raised a man, and I am a big boy na America ikaniimarisha zaidi namna ya kusimamia mawazo yangu, so far kwenye maneno yako sioni issue ya kuwasaidia wengine kwenye hii forum, nitakapoiona we will talk like big boys!

Ok Mzee.Nothing personal here.Hoja inajibiwa na hoja.I didnt ask for a "sorry" from you,bcoz I'd be stupid to expect one from you ( though I said sorry to you when I wrongly mentioned you as one of those who attended mkutano wa JK New York but didnt contribute).Nimalize kwa kusema you were right to conclude kwamba mada yangu was Nonsense.Why,bcoz it's your constitutional right to believe,conclude and say anything you like.Let me take it as your compliment.
 
Mzee nikiandika NONESENSE, una all the rights kuiita as it is tena anytime be my guest, lakini I am not amused na maneno ya chooni yale yale kila siku hebu tafuteni mapya yanayoni-describe vizuri, kwamba I am nothing but a big boy, siko hapa kutafuta babysitter, NO! Taifa, taifa and taifa langu that is all!

Wewe ukiomba msamaha na mimi niombe msamaha bila kosa? Is that what you want from me, na hao wengine wote wanaolia lia toka issue ya miezi iliyopita, mpaka leo bado tuuuu wanalia na kuvizia vizia bila ya hoja?

Ok! here Mzee nisamehe sana baba yangu, nimekosa kuiita mada yako NONESENSE!, samahani sana ninaomba radhi baba yangu!

Ok lets get back to the issues,

(1). Rais kwenda Real, je tatizo liko wapi?

(2). Kibelloh kuiba picha, je unajua kitu chochote kuhusu hiyo habari?
 
Mzee Es said:
Mzee nikiandika NONESENSE, una all the rights kuiita as it is tena anytime be my guest, lakini I am not amused na maneno ya chooni yale yale kila siku hebu tafuteni mapya yanayoni-describe vizuri, kwamba I am nothing but a big boy, siko hapa kutafuta babysitter, NO! Taifa, taifa and taifa langu that is all!

Wewe ukiomba msamaha na mimi niombe msamaha bila kosa? Is that what you want from me, na hao wengine wote wanaolia lia toka issue ya miezi iliyopita, mpaka leo bado tuuuu wanalia na kuvizia vizia bila ya hoja?

Ok! here Mzee nisamehe sana baba yangu, nimekosa kuiita mada yako NONESENSE!, samahani sana ninaomba radhi baba yangu!

Ok lets get back to the issues,

(1). Rais kwenda Real, je tatizo liko wapi?

(2). Kibelloh kuiba picha, je unajua kitu chochote kuhusu hiyo habari?

Licha ya "permission" ya mie ku-brand mchango wako NONSENSE,I simply cant do that.Why?coz I believe kwamba utakuwa umetumia akili (sensibility) kabla ya kuposti mada au mchango wako,and I'm in no position whatsoever kuamini otherwise.That's my democratic and constitutional right.

On safari ya JK huko Barnebau and his eventual invitation to the club to visit TZ,hoja yangu was simple:I satarized the visit and invitation as one of his successes ya ziara yake.
On Kibelloh,kwanza sijui kama sheria inamzuia kuhama na picha or not.Pili,sijui kama alichukua hizo picha or not.Tatu,sijui kama hizo picha zilikuwepo in the first place or not.And finally,whether he took them or not,haiwasaidii Watanzania kukabiliana na depreciation of our shilling,it doesnt resolve our umeme crisis,and at the end of the day nadhani JK knows better when he decided to extend Kibelloh's tenure as an ambassador than sending him back home.
 
Man great debate, lakini I respect your boldness, kwa maoni yangu hakuna cha mimi kuendelea kujadili kwa manufaaa ya wanaforum mpaka atakapotokea mtu mwenye data za picha za ubalozi kuibiwa na balozi,

nitasubiri utafiti, ha! ha!
 
Mzee Es said:
Man great debate, lakini I respect your boldness, kwa maoni yangu hakuna cha mimi kuendelea kujadili kwa manufaaa ya wanaforum mpaka atakapotokea mtu mwenye data za picha za ubalozi kuibiwa na balozi,

nitasubiri utafiti, ha! ha!

Sawa Mzee, na mie naheshimu sana mchango wako.
 
ni saa 21:21 hapa London na baridi inaanza . Nimeingia juzi hapa kikazi lakini nikaona nitumie muda huu kuyajua yale ya Kibelloh na wizi wa picha .Nime jaribu kufika hapa kule alipokuwa anakaa na sasa ni gofu maana hakuna anaye ishi kwenye hiyo nyumba baada yua Kibelloh kuhamishiwa paris club aendelee kutesa .

Ukweli wa mambo ni kwamba ni kweli Kibelloh kaondoka na picha ukutani si toka ofisini kwa balozi bali nyumbani kwa balozi.Ile nyumba wakati inanunuliwa kwa ajili ya mabalozi wetu hapa london palikuwa na picha nzuri sana za kuchorwa yaani wall paintings ambazo Kibelloh alimua kuziondoa na kuondoka nazo ni kinyume cha utaratibu kabisa na huu unaweza kuwa n wizi maana nyumba ni mali ya serikali na kila kilicho nunuliwa kikiwamo ni mali ya walipa kodi .

Nimeshangaa sana baada ya kufuatilia pia malipo ya matengenezo ya gate nyumbani kwa balozi ambalo yeye alilitolea invoice ya 12,000 pounds si kwa ajili ya kuweka gate jipya hapana bali kulitengeneza tu kwamba limeharibika nalo bado lina hali mbaya na sijaelewa kwa ni i Kibelloh alilipa pesa zote zile kwa ajili ya gate .

Kibaya zaidi hadi ninavyo andika hapa balozi mpya anaishi kwenye apartment baada ya Kibelloh kuingia paris na kuacha nyumba ya balozi Uk ikiwa kama pango na sasa najiuliza kwamba kama huku UK kaharibu namna hii je huko Paris huyu Kibelloh hawezi kutuuuza jamani sisi watanzania ? Ni aibu sana kwamba picha kaondoka nazo pamoja na mshahara na heshima yake nadhani angaliweza kununua picha zake na kuacha heshima yake iwe juu lakini sasa kwa hili sijui kajiweka wapi. Ama ndiyo mchezo wa kila mmoja kuchukua chake mapema ?Naomba kuuliza kwa anaye mtetea Kibelloh aje na maelezo ya kina atujulishe kwa nini 12,000 pounds kwa marekebisho madogo ya gate na kuacha jumba gofu hadi sasa balozi anaishi kwenye apartment nyumba haitamaniki .
 
Mzee Lunyungu,

Heshima yako mkuu, hapa hakuna anyemtetea isipokuwa tulitaka kujua ukweli ya yeye kuiba picha si kweli, ameondoka kwenye nyumba ambayo ni lazima ikarabatiwe kabla ya kuingia balozi mpya, huo ni utaratibu wa serikali na huko majuu kwa ujumla,

Ukifuatilia balozi zote za kwetu nje, utakuta hakuna hata moja ambayo balozi mpya huja na kuingia moja kwa moja, regardless ya hali ya nyumba sasa picha na vitu vyote vya thamani ndani ya hiyo nyumba ambavyo ni mali ya serikali haviwezi kuachwa tu na mtu anayehusika navyo pale ubalozini, huyo mtu huitwa AA, ndiye wajibu wake kuvikusanya vitu vyote vyenye thamani na kuvihifadhi hadi nyumba itakapokuwa imetengemaa na balozi mpya kuingia, na ninaamini that is the case huko London,

Pounds 12,000 za ubalozi haziwezi kuchukuliwa bila ya ofisi kwa ujumla ku-feel maana Bongo hatuna hela kiasi hicho za kutuma ubalozini zikakaaa bila sababu mpaka kuibiwa, unless useme zimeibiwa hela za viza, halafu kuna mama mmoja mshikaji wangu Hazina anaitwa Mama Nyoni, yaani Mkaguzi Mkuu Wa serikali, sasa hizo hela za ubalozi kutengenezwa haziendi bila ya yeye kuziruhusu, na akishaziruhusu, huwa anazifuatilia mwenyewe, ukidokoa senti tano yeye huwa ni mtu wa kwanza kujua kabla ya mtu yoyote, kama humfahamu waulize wanaomfahamu wakwambie moto wake?

Halafu kwenye mabalozi yetu yote ya nje, for the last six months Mzee Luanjo alianzisha tabia ya kuwapeleka wahasibu ambao ni wabongo, as opposed to wahasibu wa zamani ambapo wengi walikuwa ni wa-Fillippino, walioajiriwa na mabalozi waliokuwa wanakula nao, huo mchezo uliisha maana hao wahasibu wabongo ni answerable kwa katibu mkuu bongo tu! na sio balozi!

Halafu pia Mzee Luhanjo alianzisha tabia ya maofisa wa ubalozi kukutana na kuamua kama kamati matumizi yoyote ya ubalozi, na pia maofisa hao kuwa na haki ya kupinga matumizi hayo inapobidi, meaning kwamba matumizi ya paundi 12,000 yasingweza kuidhinishwa bila ya hicho kikao, na ufuatiliaji wake pia ni wa kamati hiyo,

Kwa hiuyo ndugu yangu ninakuomba usome kwa makini huu ujumbe wangu halafu uniambie kama bado unasimamia maneno yako, kule France Kibelloh pia sasa hivi anakaaa hotelini je ina maana balozi Juma Mwapachu alikuwa mwizi na ameacha gofu? Mahiga alipofika NY alikaaa hotelini kwa miezi mitatu na kuhamia kwenye aprtment kwa mwaka mzima, je Mwakawago alikuwa mwizi aliyeacha magofu? Je unajua kuwa 3/4, ya mawaziri wetu wanakaa hotelini je ni kwa sababu ya wizi?

Uongozi mbovu ni one thing, na kuwa kiongozi mwizi ni serious charges bro!, I mean respect kwa uchunguzi wako na ndivyo tunavyotaka kwenye hii forum, lakini please!
 
Mama Nyoni ni Accountant General
Mzee Kiama ndiye alikuwa Auditor General kwa sasa ni Mzee Utouh kutoka NBAA alikokuwa mkurugenzi.

Kuweka mambo sawa hakuna kilichoharibika tuendelee...

FD
 
Mzee FD,

My point ni kwamba hakuna hela inayotolewa na kutumika ubalozini bila ya Mama Nyoni kuiruhusu na kujua imetukaje na kwa kawaida yeye huja mwenyewe na kuhakikisha kuwa imetumika ilivyotakiwa,

na huiarifu serikali mara moja kama ana wasi wasi na matumizi ya ile hela, sasa kama Kibelloh ambaye siku zote kuna wanaompiga vita bila sababu, wangepata hicho chambo wangemuacha?

Halafu Tafiti anyekaa hapo London amesema hiyo hadithi ya picha sio kweli, na wewe uliyefika kwa masaa tu unasema ni kweli, je hiyo inawezekana kuwa kweli?

Mzee FD shukrani kwa masahihisho yako, lakini the fact ni kwamba hakuna hela inayotolewa na serikali kwa mabalozi bila ok ya huyo mama, ambaye kutokana na kuijua kazi yake mpaka leo toka enzi za BM, anaendelea nayo na ndiye aliyemripoti Mahalu huyo mama ni motto wa kuotea mbali, na hata bunge zima linamfahamu maana huliweka chini bunge kwa masaa na kutoa darasa kuhusu mahesabu,

kwa hiyo sitegemei kwamba unataka kubadili somo hapo!
 
Mzee Es,

Kuhusu utendaji wa mama Nyoni toka yupo TRA mpaka Hazina wala sina shaka nao maana nimefanya kazi naye!.

Umetoa point nzuri kuhusu hayo matumizi mabaya aliyotuhumiwa nayo Balozi.

Mimi ningependa kuchangia kuwa kama jamaa wanadai hakutengeneza geti na kuna uwizi, so simple, alete mwaka ambao matumizi yalifanyika tukaangalie ripoti ya mkaguzi mkuu wa serikali in the respective year.

Au siyo jamani?

FD
 
Mzee Es,

Heshima yako mkubwa na mimi nasema nasimamia maneno yangu. Naomba kusema yafuatayo baada ya kupata habari mpya toka kwa mtu wa karibu wa Ubalozini pale.

Kwanza napenda kukueleza haya kwa kupingana nawe juu ya swala la Balozi kukaa Hotel kisa ni matengenezo ya nyumba.Uk alikuja Balonzi Nsekela akaingia moja kwa moja baada ya nyumba kufanyiwa usafi na nyumba ya balozi wa Tanzania iliitwa ana inaitwa tanzania house kwa jinsi ilivyo nzuri nk. badaye akaja Nyaki , Malecela,Mchumo wote hawa waliinga moja kwa moja na hawakungoja matengenezo maana nyumba ilikuwa safi na inatunzwa na wote waliacha hizi picha ambazo Kibelloh kaondoka .

Kwa taarifa yako AA hajachukua hizo picha wala kugusa chochote mle ndani na huu ndiyo ukweli na si zaidi ya hapa unavyo taka watu waamini. Sharif hakuwa mwizi ila mbana matumizi na ndiyo maana kabla ya Kibelloh kuingia ilichukua muda yakafanyika matengenezo.Ila Kibelloh alikuja na roho nzito mno na ukaidi akawa hataki hataki watu kufika kwake na matokeo yake wote wanajua kwamba alikuwa na bado ni Mnyanyasaji hadi sasa. Aibu sana kaondoka na hata picha na kuacha jumba gofu.

Kibelloh kwa mujibu wa vitabu vya Kihasibu vya Serikali Financial Orders 5th Edition ya mwaka 1983 akiwa Balozi ni Accounting Officer na ana maneno ya mwisho ya kusema juu ya pesa za Ubalozi.Ubalozi wa UK haujawahi kuwa na mhasibu Mgeni ila wako hadi sasa pale reception, Visasa, na Upishi lakini si pesa. Sasa hadithi yako kidogo inatuacha hoi hapa mzee.

Ubalozi wa Uk pekee kila 3/4 wanapokea more than 30,000 UKP na hizo zinapelekwa kwa mujibu Funds na leo Kibelloh kula 12,000 kwa ajili ya gate haiwezi kunishangaza mimi. Naongea habari hizi nikiw ana uhakika maana source zangu za karibu zimesema haya na ni ukweli kwamba Kibelloh he did all na wala si allegation.

Unasema kuna Accountability? Ama kwa vile Kibelloh analindwa na Malecela? Balozi zetu kibao zina matatizo makubwa ikiwemo ulaji na sijawahi kusikia haya yako ya leo hii. I am no buying your story kaka kisa uko naye karibu hapana Kibelloh kafanya mbaya. Paintings alizikuta na wote walio mtanguliwa walizikuta na wakaziacha yeye kwa nini?

Leo nyumba inahitaji matengenezo makubwa kisa yeye hakuwa mwangalizi mzuri lakini nimekuonyesha huko kabla yake walio ingia bila kufanya ukarabati wowote ial kufanyiwa usafi.

Kibelloh anakaa Hotel kwa kuwa Mwapachu ilibidi aondoke kwa uharaka kwenda nairobi kwa post yake mpya na sasa familia yake bado iko kwenye nyumba ya balozi na ndiyo sababu pekeee leo Kibelloh anakaa hotel pending the vacation of that family.

Mawaziri kukaa Hotelini TZ nawaachia watu waamue kwa kuwa wanajua kwamba CCM wana mambo yao na maamuzi ya ajabu ya kuuza nyumba za watumishi wa serikali. Sitagusa hili la mawaziri maana majibu yako wazi issue hapa ni Kibelloh na pesa na picha za ukutani. Kumbuka yeye ni Accounting officer na ama maamuzi ya mwisho juu ya matumizi yeyote ya pesa.

Heshima Mbele wazee
 
Mzee Lunyungu,

Sahihisho: Nafikiri ulitaka kusema Mh. J.V. Mwapachi aende Arusha-makao makuu ya EAC-kwenye post yake mpya.

Swali: Ina maana mpaka sasa familia yake (JV) bado iko Ufaransa? Kwa gharama ya nani? Kama ni kwa serikali inatakiwa iwe imeondoka baada ya muda gani? Na yeye huko Arusha bado anakaa hoteli? EAC nao hawana nyumba za viongozi wa juu? Au na zenyewe washauziana kama zile za serikali zilivyouzwa?
 
Mwanagenzi
Swala la gharama analipa nani kwa familia hiyo sina hakika kwa Paris na wazee kule EA hiii ndiyo Tanzania ila mimi nasema juu ya Kibelloh ambaye yuko Hotel na nimefuatila kujua kwa nini ndiyo vyanzo vyangu vimesema haya ninayo wapa hapa .watakaa muda gani bado sina majibu kwa kweli .Kibelloh kuishi Hotel nadhani anafurahi maana anapenda kuponda maisha na mapesa y walipa kodi sana .Kisa ana God fazer Malecela
 
By the way who is this thief Kibello!!

WHO PROTECTS HIM??!! IS TRUE THAT IT IS MALECELA AS MURANGILA SAID? HOW AND WHY?

JK IS THE ONE WHO GAVE HIM THIS NEW POST. NINAKUMBUKA WANACHI WENGI HUKO NYUMA KABLA YA uchaguzi wanachi wengi walipiga kelele sana kuhusu huyu Mwizi. Hata mimi nimesekia kuhusu hizo hela pound 12000 za matengenezo ya gate na siyo kununua gate jipya!!!

12000*2386.95=28,643,400/Tsh= roughly milioni 29!!!!!!:confused:
Watu wa usalama wa taifa ambao ni wakweli siyo wale wahuni tunaowasikia humu wakitetea wezi fuatilieli haya mambo mtu kama huyu anapaswa kupumzishwa na afunguliwe kesi. Dawa ya mahalu itumike hapa kwa kibello pia. Huku kulindana kutawafikisha pabaya.


Huyo Kibello kuendelea kukaa Hotelini ni kwa kuwa anapenda kura raha tu!!

Hayo mabilioni wanayolipa katika hotel za wazungu kwa mabalozi wote yanaweza hata kuzidi gharama za kununua generator moja ya Umeme wa nguvu hapo UBUNGO!!

WEZI WANA WEZI WENZAO WANAOWATETEA NA KUWALINDA HUMU HUMU!
 
Tatizo ni watu wengi humu mko karibu na ubalozi wa London, na hadithi zenu ni tofauti, halafu hatuko hapa kufuata mkumbo hapana nafikiri mmesema ya kutosha na pia mnaweza kuongeza,

bado ninarudia kuwa hakuna balozi wa bongo, ambaye toka Luhanjo aingie Foreign ambaye angeweza kuiba hela zote hizo bila katibu mkuu kujua,

Halafu bila ya mama nyoni kujua, jana nimeongea naye kwa kirefu kuhusu ukaguzi wake wa mwisho alipoenda pale London, ambapo pia alialikwa dinner na Kibelloh wakiwa na Mwinyi, na Kawawa, kuna matatizo mengi London lakini amesema wizi sio mojawapo,

Ikulu kuna malalamiko mengi dhidi ya Kibelloh, lakini wizi halijawahi kuwemo, mbunge Nyami alipiga sana kelele bungeni against Kibelloh, lakini wizi haikuwa one of the issue,

Kibelloh, amekuwa director wa Utalii, balozi wetu Sweeden, Mkurugenzi wa foreign Europe na US, katibu mkuu foreign, balozi wetu London, na sasa Paris the best he could na tabia yake ya wizi sugu ni kuiba picha na pound 12,000 London basi? huko kote kwingine tabia ilikuwa kimyaaa?

What Jm has to do with this? Hivi JK nyinyi mnamuonaje? Mahalu ameiba imejulikana lakini Kibelloh isijulikane? Mahalu unajua alikuwa analindwa na nani?

Siwezi kuzuia haki ya mjumbe yoyote hapa kusema anayotaka, lakini hiziserious accusations ni lazima tuwe waangalifu, jamani ninarudia kuwa habari zenu sio za ukweli, hakuna anayemlinda mtu hapa kumfahamu mtu sio swala la kumlinda mtu, just facts baby!
 
Back
Top Bottom