LONDON: Kibelloh & Disturbing News!

Lunyungu

JF-Expert Member
Joined
Aug 7, 2006
Messages
8,854
Points
1,250

Lunyungu

JF-Expert Member
Joined Aug 7, 2006
8,854 1,250
Es sasa naona unataka kutuziba kwa kusema hakuiba.

Jibu hoja hapo juu na Luhanjo kaja lini na pe sa zimeibwa lini? Unajua sijui wewe unasema kwamba ni uongo kwa sababu zipi. Gate lipo na bado ni bovu huu ni ushahidi, pia mapicha hayamo kaondoka nayo na jumba ni gofu balozi hajaingia humo ndani unataka upewe ushahidi gani? Huyu Mama Nyoni unaimnba naye watu tunamjua zaidi na wizi kuzuiwa na Luhanjo kwa sasa nitashangaa maana ni CCM ile ile.

JK kaingia kwa rushwa madarakani leo anawezaje kuzuia rushwa kama anawapa wala rushwa muda wa kujirekebisha? Unaongea nini mzee wangu Es. Kibelloh kulindwa ni wazi na halindwi na wewe bali JM kisa cha kumlinda tunakijua na ndiyo maana anavurunda na JM akiondoka Umakamu wa CCM basi wengi wenu watu wa JM ndiyo mwisho wenu wa kutanua.

Kibelloh kaiba 12,000 pounds na nasimamia maandiko yangu.
 

Field Marshall ES

JF-Expert Member
Joined
Apr 27, 2006
Messages
12,659
Points
0

Field Marshall ES

JF-Expert Member
Joined Apr 27, 2006
12,659 0
Mzee naona una maneno mengi ambayo hayahusu the issue, ninasema kwamba mazingara ya ofisi ya ubalozi sasa hivi sio rahisi paundi 12,000 kuibiwa bila serikali kujua,

kwa maoni yangu nitakubali kutokubaliaana, maana pale London kuna watu kibao wa serikali ambao wangeshalifikisha hilo, Mahalu alikuwa akilindwa na Mkapa, lakini akaondolewa, sasa unaponiambia kuwa Kibelloh analindwa na JM, mpaka kuiba paundi 12,000 na JK akamuacha basi hayo kwangu ni makubwa mno,

anyway ninasema nimejaribu kila njia nimeshindwa kupata ukweli wa Kibelloh kuiba hizo hela, na picha, ndio maana ninaomba nikubali kutokubaliana, na hata kama ikibidi kwamba you are right ameiba kweli picha na paundi 12,000!

Hayo maneno yako mengine ya kazi na JM, ni NONESENSE ni njia tu ya kutaka kulazimisha point yako ya Kibbelloh na wizi wa picha na paundi 12,000 tunatakiwa tusiulize maana tukiuliza basi kila mtu ni mwizi, ama kweli siasa na bongo!
 

Lunyungu

JF-Expert Member
Joined
Aug 7, 2006
Messages
8,854
Points
1,250

Lunyungu

JF-Expert Member
Joined Aug 7, 2006
8,854 1,250
Mzee Es naomba tukubaliane kwamba pesa zimeibiwa wakati wa Mkapa na si wakati wa JK.

Uki link sana Mahalu na issue ya Kibelloh kuijenfa hoja yako nitazidi kushangaa maana kuibiwa kwa pesa na Mahalu JK he knew and he did nothing leo ni unafiki kusema kamuondoa na kumwacha mtaani anapeta. Pesa hizo ama JK ama BM ama wote wana chochote walipata ama CCM wakaendesha kampeni na ndiyo maana hutaona Mahalu akifanywa lolote kama vile Mahita maana he did for CCM na nyie wengine ambao mko huko mnazidi kutula sisi.

Na kama kweli Mahalu JK kamuondoa ki aina basi ni kwa kuwa si mtandao maana watu wa mtandao wako wanaingia mikataba na kutoa manenoya uongo kwa mfano Msabaha, Kirimagi nk lakini JK kanywea kama vile hasikii ama hajui.

Huu ni ujanja na bado nasema pesa imeibiwa na Kibelloh na even JK na JM knows an wewe unajua ila tumesha kujua kwamba penye maslahi yako utasimama na kuupinda ukweli na unalifanya hili.

Tuendelee ila ukweli ni kwamba Kibelloh kweli ni Kibelloh
 

tafiti then jadili

Senior Member
Joined
Aug 24, 2006
Messages
119
Points
0

tafiti then jadili

Senior Member
Joined Aug 24, 2006
119 0
Naam nimekuwa very bize for the last few days na kwa kweli nimekuta sura mpya ya saga la Kibelloh. Kuna mengi yamefunikwa kuhusu Kibelloh kwa kweli na hakika wale wasiojua au kumjua wataishia humo humo kuweka historia ya vyeo vyake tuu na kuishia kusema hapa na pale kuwa kuwa tunamjua:

Inashangaza baadhi yetu huwa hatutaki kuweka akili zetu huru bali huamua kuweka kufuli kabisa yaani mtu anaamua kusema kabisa hakubali hata kama ikiwa ni kweli! Duh this is ridiculous!!

Naam rumours kuhusu utendaji wa Balozi Kibelloh zimekuwa ni nyingi mno kwa kweli kama tulivyowahi kuandika huko nyuma alikuwa katika hot seat sana habari za manyanyaso ya mtumishi wake wa ndani zilipoanza kuibuka. Mambo ya Kibelloh yapo mengi ya aibu. Naweka baadhi ambayo nayajua from good authority:

1. Balozi huyu alipofika hapa kulikuwa na kijana mhasibu akichapa mzigo kweli kweli basi anaitwa Ally siku makamu wa Rais alipotembelea jengo la ubalozi na ilipobainika kuwa Shein yupo karibu na huyo kijana Balozi kibelloh akamtimua! baada ya hapo kukawa na mahesabu shaghala baghala kiasi ripoti ya mkaguzi wa mahesabu mwaka 2004/5 ripoti ilitoa mapungufu ya 84m za kitanzania zikiwa unaccounted for! Incharge alikuwa Kibelloh inawezekana ni kuzembea kukubwa kulisababisha upotevu wa mamilioni haya lakini ukweli ni kwamba under his captaincy 84m Tanzanian shillings ziliyeyuka!

2. Nyumba ile iliyovamiwa na homeless pale karibu na nyumbani kwake ilitokana na yeye mwenyewe Balozi Kibelloh kukataa ushauri kutoka kwa subordinates wake kwamba ile nyumba kwa vile haikaliki basi iwe sealed off lakini akakataa kulipia £1000.00 ya kuweka fensi na ulinzi badala yake ikambidi alipie thousands of pounds in legal fees na gharama za kuleta viongozi wa kuchunguza kadhia hiyo!

3. Baada ya balozi kuwatimua wapishi wake aliokuja nao kutoka bongo [hii ni mada nzima] akina Bhoke Mgoyo balozi huyu alimuajiri mtu anaitwa Marco Chongwe ambae ndio pia alikaa kwenye nyumba ya pale Deneweood Road kabla hajaondolewa kikazi na nyumbani hapo, huyu nae aliondolewa bila sababu ya msingi, huyu bwana wakati anaondoka alikuwa anamdai Balozi paundi elfu tisa. Hapa inabidi kufafanua kuwa Balozi kisheria ana allowance ya kuajiri mpishi na huwa ana fungu lake katika bajeti ya ubalozi lakini huyu bwana alikuwa hajalipwa wakati kwenye akaunti ya ubalozi pesa zilikuwa zimechukuliwa tayari!

4. Kutokana na muda mrefu kupita baina ya balozi Sharifu kuondoka na balozi kibelloh kuteuliwa na kuja hapa London, nyumba ya balozi, one of the prestigious buildings in the area ilikuwa kidogo katika hali mbaya, nakumbuka kwenda pale na kuona baadhi ya kuta zikiwa na rangi chakavu sana kutokana na nyumba kuvuja na bustani kuwa katika hali mbaya sana, ilibidi ikarabatiwe na bustani kuwekwa sawa, the builder and gardener alikuwa ni kijana wa kibongo ambae mpaka sasa ukitaka mgombane basi mtajie Balozi Kibelloh mbele yake manake balozi alimwambia usiwe na wasi wasi fanya kazi nitakulipa, Balozi Kavuta kwenye kasma ya ubalozi kisha kamlipa jamaa peanut, kwa mujibu wa huyo builder anasema alipunjwa elfu tatu na amezidai mpaka ikawa gharama za kufuatilia haki yake zinalingana na pesa anazodai akaamua kugive up...


Kwa hakika nakubali huyu Mzee Kibelloh ameserve katika capacity nyingi lakini nisichoelewa ni kipi kimemuweka madarakani mpaka leo ilhali kila mtu ubalozini analalamika kuhusu yeye, lau mngekuwepo london pale wafanyakazi ubalozini waliposigh kwa relief kubwa waliyopata huyu mzee alipohamishwa....

Hizi za geti sizishangai sana manake ni kawaida yake, ukisoma hadithi ya Bhoke Mgoyo utaona kuwa ingawa ni mkewe ndie alokuwa akidai malipo ya gesi na umeme toka kwa wapishi hao [75 each week] balozi aliratify madai ya mkewake, hivyo hashindwi kutia ndani elfu kumi na mbili...

Kwa kifupi Balozi Kibelloh ni liability!
 

JokaKuu

Platinum Member
Joined
Jul 31, 2006
Messages
17,401
Points
2,000

JokaKuu

Platinum Member
Joined Jul 31, 2006
17,401 2,000
Kibelloh ni swahiba wake JK. Kibelloh alipandishwa cheo kuchukua nafasi ya Balozi Mtango, "mkorofi" aliyesafisha uchafu uliachwa na Diria na Msabaha wizara ya mambo ya nje.

Kuna watu ambao hawakupenda utendaji kazi wa Mtango. Inasemekana hiyo ndiyo sababu ya kupelekwa Japan "kupumzika." Mtango aliwapa taabu sana wazembe wizara ya mambo ya nje kwasababu ya kuwaburuza. Ilifikia kipindi akapachikwa jina Mussollini[Dikteta wa Italy.]
 

Field Marshall ES

JF-Expert Member
Joined
Apr 27, 2006
Messages
12,659
Points
0

Field Marshall ES

JF-Expert Member
Joined Apr 27, 2006
12,659 0
Ilikuwaje ukaenda kumuaga mtu muovu kiasi hiki? Hayo yote ni yale yale ambayo tumeyasikia kwa muda mrefu, yaani majungu ya London yanayowafanya viongozi wakuu wa nchi yetu wapaogope,

yaani hata mtoto mdogo huwezi ukamshawishi kuwa kuna balzoi yoyote duniani anayeweza kumfukuza kazi mtu aliyekaribu na makamu wa rais wa nchi yake, yaani the right word ni NONESENSE!

Labda tuendelee kusubiri majungu mapya!
 

Lunyungu

JF-Expert Member
Joined
Aug 7, 2006
Messages
8,854
Points
1,250

Lunyungu

JF-Expert Member
Joined Aug 7, 2006
8,854 1,250
ndiyo vijana naona moto unawaka na mzee wenu Es sasa hajibu kitu anaita ukweli Nonsense. Juma ndiye aliyefukuzwa yaani Juma ally kama sijakosea naye yuko London hapa na yuko tayari kutoa ushahudi kwamba ni kweli alifukuza. sasa mzee Es kama akija hapa na akasema alifukuzwa uko tayari kuomba msamaha ama utasimama na Kibelloh wako ?

Swala la kufukuzwa na Makamu wa Rais ni rafiki tu ama ana fahamiana inategema Kibelloh kwa kuwa ni bingwa wa kjenga hoja atakuwa alisema nini . Kumbuka Kibelloh halindwi na JM ukweli ni kwamba Kibelloh analindwa na JK na mshikaji wake sana sana ndiyo maana pamoja na mauza uza yote JK anampeleka Paris akatumalize .

Hakuna mtu anayepinga uwezo wa Kibelloh wa kuchapa kazi . Ni mchapa kazi hasa na sana sana na kazi yake anaijua ila tabia zake na kushindwa kuishi vyema hata na watu wa chini yake kikazi na kudokoa mali ya watanzania na uharamia mwingine ndiyo issue hapa . Kibelloh ni kichwa sana kwenye kazi no question ila shida yangu ni uharamia na udokoaji . Sasa ninasema aliyefukuzwa yupo na Makamu wa Rais kama si mpenda makuu na mla rushwa na mcha Mungu anaweza kukaa kimya tu na kuangalia maana balozi ana mamlaka na maamuzi .usiwafumbe watu macho kwenye hadithi za Kibelloh maana you are serving your interest hapa na si za Tanzania .

Kwako Murangira nimeona umeneno kweli mzee baadaye akaja Mzee wa kujadili baada ya kutafiti .Nakuweka sawa tu kwama huyu Balozi Sharif alikuwa ni mwizi sana na mbaya sana .Kwanza alipata ubalozi kwa kujuana mwanzoni alikuwa anaishi kule London kwenye a two bedroom flat na mtaa ukitaka utapewa na namba ya nyumba .

Mzee wake yaani Mzee mwinyi akalamba dume akampa ulaji wakati huyu Sharif hakuwa anajua lolote ,kajifunza kazi akiwa hapo hapo UAE ambako ndiko aliko pelekwa kuanzia kazi .Baada ya mabadiliko akapelekwa UK ambako kw amuda mrefu aliendeleza kutuibia pesa zetu kwa kufanya biashara na ndugu yae wa UAE.Shariff alikuwa anaagiza hata stationary toka UAE hebu shangaa zinatoka huko kuja London , kisa mradi wa ndugu yake uendelee na wakawa wanakula pesa zetu .

Shariff alikuwa anatafuta huduma nyepesi ili azike pesa yeye na dereva walitembea kutafuta hata mafundi wa nyumba kwa bei cheap with low quality ya kazi isa pesa aweke mfukoni.

Aliumbuliwa kwa wizi ya pesa za compensation za eneo la Nothern Circula road ama A 406 baada ya kila mtu aliyekuwa na nyumba eneno kupewa malipo hayo kwa kuwa matengenezo aa extension ya barabara ili waathiri. Pesa hizo Shariff alizichukua na baada ya ukahuzi ndugu Kiama akagundua kupotea kw apesa hizo baada ya kuona baadhi ya documents zikiwa na habari hizo . Kiama akakomaa na Shariff akarudisha pesa hiz kimya kimya . Hawa ndiyo mabalozi wetu na London ambao leo mnawatetea kwa nguvu ama kwa makusudi kwa kuwa mna maslahi binafsi ama kwa kutokujua ukweli.

Shatiff na Kibelloh wote ni wale wale
 

Field Marshall ES

JF-Expert Member
Joined
Apr 27, 2006
Messages
12,659
Points
0

Field Marshall ES

JF-Expert Member
Joined Apr 27, 2006
12,659 0
Mzee wa Shughuli,

Heshima yako mzee, sikatai kuwa Kibelloh ana matatizo ya ku-deal na wananchi binafsi, na nilisema huko nyuma kuwa hayo atajitetea mwenyewe, mimi kwangu ni taifa ndilo muhimu,

balozi wa nchi hawezi kumfukuza mtu kazi bila ya kuwepo sababu za kimsingi, na hasa local staff maana huwa ni uamuzi wa kamati ya maofisa na sio balozi peke yake, kwa sababu balozi peke yake hawezi kumuajiri mtu bila maofisa wote kukubaliana,

halafu hizi habari za ndani ya ubalozi huo mbona zinatoka saaa hizi baada ya yeye kuondoka? au? ninarudia kuwa Kibelloh ameshika wadhifa mwingi serikalini na wizi huwa ni tabia, sasa ilikuwaje huko nyuma kote asiibe aje aibe hapa tu London? halafu habari zake za wizi zitolewe tu baada ya yeye kuondoka? akiwepo tumesikia malalamiko mengi ya binafsi ambayo ninarudia kuwa simtetei hayo ya wapikaji wake hayo ni ya kwake, lakini la wizi sio kweli Kibelloh ana matatizo ya binafsi ambayo kula kiongozi na wananchi wanayo,

lakini sio mwizi, maana wizi na udokozi ni tabia ya kuzaliwa nayo angeiba kote alikowahi kufanya kazi, tena ninashukuru sana kwa kuliweka sawa la kuhusu nani anayemlinda, ni JK mwenyewe je Jk analinda wezi? labda kwa wale tusiomfahamu ndio tutaamini hilo la JK kulinda wezi!

na kuhusu utafiti huo ni NONESENSE, maana huyo jamaa ni nothing but mnafiki na mpenda sifa za forum tu, hakuna balozi wa Afrika anayeweza kumfukuza kazi mtu wa karibu na Veeep, haya ndio majungu yenyewe!
 

Lunyungu

JF-Expert Member
Joined
Aug 7, 2006
Messages
8,854
Points
1,250

Lunyungu

JF-Expert Member
Joined Aug 7, 2006
8,854 1,250
Bwana Es ninashindwa kujau huyu Kibelloh alikupa nini. Lakini nimegundua kwamba ni tabia yako sasa kutetea maslahi yako. Kibelloh nadhani ni jamaa yako kama alivyo Charles anaye tuhumiwa kuhonga apate Ubunge na wewe unakataa.

Swali: Je, unaweza ku support maneno yako kwamba Kibelloh si mwizi ? Kupitia nyadhifa Kibao na akaja kuiba hapa ni matter of time and timing. Opportunities na huko pia wizi upo ila hakuna mwenye gutts za kusema hapa ubalozini. Invoice ile ya kutengeneza gate Mzee Es unajua kamuulize Kibelleh akueleze vyema hata yeye anajua alivyo ivurunda na kukimbia na picha ukutani. Ndiye Kibelloh huyu kama aliweza kuwazima hata wapishi pesa zao nk huo unaita nini kama si wizi na uharamia? Kwani kwa akili yako mwizi ni mtu wa aina gani ? Kaiba mishara ya watumishi wake , pia wizi huo.

Kibellhoh ni mwizi na JK anamlinda sasa ukisema JK ni mwizi mimi sijui utajaza mwenyewe lakini tukitaka kuangalia Nchi inavyo endesha kishikaji nk yeah wasi wasi lazima uwepo. Maana Msabaha na wengine wanavurunda kakaa kimya leo tumwelewe vipi? Kama Kibelloh anatupatia hasara kubwa namna na bado anamlinda what do you want us to think?

Hukai na Kibelloh na wewe si PS wa Kibelloh leo unakataa juu ya Uharamia wake, unatushangaza sisi sana. Watu walio kaa na Kibelloh leo wanasema na walishasema hata akiwepo ila Kibelloh mtemi na hana utu na huruma ndiyo maana wanajificha kama wewe unavyo jificha kujulikana kwa wana Jamvi na hata unapotakiwa ujutokeze US ukutane na watu wa Jambo forum bado unajificha why?

Ukiwa na sababu zako basi hata hawa wanaotoa data Kibelloh akiwa Hotelini Paris wana damu kama wewe na wanataka kula na kuishi na watoto wao.
 

Field Marshall ES

JF-Expert Member
Joined
Apr 27, 2006
Messages
12,659
Points
0

Field Marshall ES

JF-Expert Member
Joined Apr 27, 2006
12,659 0
Maneno yako nimeyasikia, ingawa sasa it is getting too personal maana sasa inakuwa ni mimi sio tena Kibelloh, yaani mnategemea kusiwe na the otherside humu wote tuwe side moja? Hapana, somebody has to be on the otherside na kwenye hii mada ni mimi, kazi ya Kibelloh kwa taifa inafahamika,

Haya majungu ya London sasa tumeyazoea, ninajua kuwa kuna adui wake Kibelloh mkubwa aliyebaki hapo na ndiye anayepika haya majungu mapya ya picha, Kibelloh hajaiba picha, wala hela za geti, Kibelloh ana matatizo mengi ya binafsi ya kutoelewana na wapishi, lakini sio mwizi wa hela za umma, na JK ana matatizo mengi lakini hatetei wezi hata siku moja,

kama ni ndugu yangu? Kibelloh ni mtu wa Tanga na Charles ni mtu wa Musoma ambaye according to you ni ndugu yangu pia, je inawezekana? Charles hana hela ya kumpa mtu rushwa na ndio maana ninamwita rafiki yangu masikini, ninasema siku zote kuwa sitetei viongozi wabovu, na ninawatetea viongozi wenye uwezo wa kazi kwa taifa letu, FULL STOP!

Je viongozi wenye uwezo kwa taifa hawana matatizo ya binafsi? wanayo hata Mwalimu alikuwa nayo, hata Clinton the best ever American president alikuwa nayo matatizo ya binafsi, ndio ubinadamu, lakini hatuwezi kum-disqualify uwezo wake wa kazi kwa taifa, kwa sababu ya wapishi kutokupika vizuri na yeye kuwajia juu,

mimi sio lazima nijitokeze ili kuendelea kuweka vitu hapa, nijitokeze ili iwe nini? Hiyo idea nilishaifuta kwa sababu haiwezi kunisaidia kitu chochote zaidi ya kuniharibia kazi, maana sasa hivi majui kazi yangu lakini kila siku ninasikia mapya hapa, jinsi JK alivyonifukuza, jinsi ambavyo JM akitoka CCM nitakufa, all NONESENSE, badala ya issues, mambo ni hapa hapa tu mawe tu!,

Huko London muache majungu jamani, imetosha tumesikia ya kutosha wewe ukitaka majungu nenda London tu, hata uwe mwananchi wa kawaida tu utakaangiwa majungu na hawa kina tafiti, jamani imetosha fanyeni kazi
 

Lunyungu

JF-Expert Member
Joined
Aug 7, 2006
Messages
8,854
Points
1,250

Lunyungu

JF-Expert Member
Joined Aug 7, 2006
8,854 1,250
Duh!! Bwana Es kama ukweli unaita majungu na ukihojiwa unajilinda kwa kasi kubwa sawa ndugu . Ndiyo JK anawalinda wezi kama unasema hawalindi mbona issues za Mahalu, NSSF nk kanywea na anawalinda wauza Nchi yetu . Yaani hata matapeli wa kariakoo wanapewa mikataba ya aina a IPTL na yeye kakaa kimya ama tuseme kwa kuwa ni kampuni ya waislam wenziwe ? It is Time RO kumwambia Boss wake kwamba mnatupeleka kubaya na watanzania watachoka siku moja .
 

Field Marshall ES

JF-Expert Member
Joined
Apr 27, 2006
Messages
12,659
Points
0

Field Marshall ES

JF-Expert Member
Joined Apr 27, 2006
12,659 0
JK halindi wezi, Mahita ilipodhihirika kuwa ni ukweli ana mambo mengi hakumlinda na ni rafiki yake mpenzi, leo iwe Kibelloh? JK atamwacha Kibelloh akijua kuwa ni mwizi kama Mahalu? Hapo ndipo ninasema kuwa huenda some of us humu hatumjui JK vizuri,

Toka aingie urais nitajie kiongozi ambaye unaamini na una ushahiidi kuwa ameiba hela za umma? Wewe leo kuna wanaolaani kupewa uwaziri maana hakuna kula, nyie mnasema JK mwizi? Jamani msalieni mtume kidogo, hakuna kiongozi anayeweza kuiba hela za umma mbele ya JK, kujua unless ni majungu kama haya ya Kibelloh ambayo hayawezi kuthibitishwa kisheria,

mimi sina nguvu au ubavu wa kumlinda kiongozi yoyote niliyonayo ni sauti kama yako, na kusimamia taifa langu, mabaya ya JK nayajua lakini wizi sio mojawapo, Kibelloh ana madhambi mengi sana, lakini wizi sio mojawapo, viongozi wezi tunawafahamu lakini waliiba enzi za awamu ya kwanza, pili, na tatu, sio leo leo hakuna wizi, ndugu yangu umesikia JK katoa shillingi billioni moja kwa kila mkoa, waulize wanaozisimamia kama inawezekana kuzichota weee, umesikia habari za mkuu mmoja wa wilaya aliyejaribu kuzichota yaliyomkuta?

Kumchukia kiongozi kwa sababu za binafsi ni one thing, lakini kumsingizia tuuu kwa sababu hapendwi na watu fulani sio ustaarabu hata kidogo, tukianza huo mchezo tutafika mahali hapa watattokea viongozi wezi wa kweli, tutashindwa kuwanyooshea vidole,

London nyie kina tafiti muache majungu huko!
 

Ogah

JF-Expert Member
Joined
Mar 10, 2006
Messages
6,233
Points
1,225

Ogah

JF-Expert Member
Joined Mar 10, 2006
6,233 1,225
Kama Kibelloh ni mwizi, taarifa za uhakika zitolewe hapa akina Babu Ubwete wafanye kazi yao.
Mishahara ya akina Bhoke, pesa za Gate na picha kama kweli Kibelloh ameiba basi alikuwa anajifunza wizi, namshauri Kibelloh akamuone Prof. Mahalu, Mary Ndosi et al ili ajue jinsi ya kutafuna pesa zetu sisi wadanganyika.

Well, wizi ni wizi uwe mdogo ama mkubwa still ni wizi, wenye information za uhakika mwageni hapa pumba zitaondolewa, mchele ukibakia watu wapo humu watalifanyia kazi, otherwise Mzee ES has a point, there still no strong points za kumjudge Kibelloh kama ni mwizi au lah (atleast from what i have read here)

Huyo kijana Ally kufukuzwa kazi eti kwa sababu za kujuana na VP are just mere speculations and baseless allegations, kama kweli alifukuzwa kutakuwa na zaidi ya hayo muyasemayo but sio eti kwa sababu aliongea/kujuana na VP, its very absurd.
 

tibwilitibwili

Senior Member
Joined
Sep 12, 2006
Messages
181
Points
0

tibwilitibwili

Senior Member
Joined Sep 12, 2006
181 0
Ogah

Issue hapa ni wizi wa 12,000 pounds pesa za gate na wizi wa picha za ndani yaani wall paints.Hao Ubwete na wengineo humu ndani am sure they know better na mambo ya akina Bhoke nk yako na yalikuwa wazi tangia mwanzo.Point nyingine si kuomba watu wachukue hatua sasa ama la wezi wapo na wizi upo lakini wote hawa ni wana CCM wanajuana wanabebana sisi tunasema hapa wajue lakini hakuna wa kuchukua hatua.

Nipe mfano mmoja wa kiongozi wa CCM ambaye amewahi kushitakiwa kwa kuiba mali ya Umma. Nasema CCM kwa kuwa ndiyo wenye serikali. Mambo ya akina Ally etc yako pia lakini hapa kubwa ni Kibelloha kaiba picha hazipo Ubalozini kaondoka nazo na watu wa Usalama maana wanasoma hapa esp RO knows ukweli zaidi na wizi wa ku forge invoices nk hajaanza leo haya ni machache kati ya mengi.

Sasa kama mnageuka kuwa Mkapa mnataka ushahidi kwanza tena kwenye jukwaa la siasa sawa. Lakini from what I have read here, na tabia za viongozi na hasa Kibelloh naamini kuna ukweli mwingi tu.
 

Field Marshall ES

JF-Expert Member
Joined
Apr 27, 2006
Messages
12,659
Points
0

Field Marshall ES

JF-Expert Member
Joined Apr 27, 2006
12,659 0
RO hawezi kujua kuwa Kibelloh ni mwizi na akamuacha, baada ya bitter vita vyao pale London, no way ninarudia kwamba RO anaweza kumuachia Kibelloh na huo ushahiudi mnaousema, na JK asingeweza na hataweza kumuachia Kibelloh akijua tu kuwa ni mwizi, kweli kuna viongozi ambao Jk anaweza kuangalia lwingine lakni sio Kibelloh, halafu yeye mwenyewe Kibelloh knows better kuwa maadui wote alionao kuanzia serikalini mpaka wananchi, hawawezi kumuachia by now kungekuwa na ushahidi wa kina kule ikulu,

Ni kweli toka tupate uhuru ni kiongozi mmoja tu aliyewahi kuapatikana na hatia mahakamani ya kuiibia serikali yetu, naye ni Dr. Mlingwa peke yake aliyekuwa katibu mkuu wa wizara ya ujenzi, enzi za Mwinyi, basi, nani wa kulaumiwa ni sisi wenyewe wananchi kwa kuwaruhusu viongozi wetu kutuchezea miaka nenda miaka rudi, tulipewa pilau na fulana na kofia basi,

CCM haijawahi kumlazimisha mwananchi yoyote kuipigia kura, tatizo ni sisi wananchi tusiojua lolote, na ni issues kama hizi ndio zinathibitisha zaidi kuwa we have no idea what is going on, balozi wa bongo nje ni hela ngapi anazoweza kuiba mpaka kutufanya tusiwe na umeme? Mpaka tusiwe na madawa hospitali? Juzi hapa Dar, imegunduliwa kuwa imekuwa ni tabia sugu ya wenye maduka ya madawa kuwauzia wananchi dawa zilizo expire, sasa ungetegemea kilio kikubwa cha wananchi, hasa media, guess what NOTHING, wazee wa majuu huko hebu tuambieni hiyo inawezekana huko kwenu majuu?

Ni sisi wananchi tuliolala usingizi ndio tatizo la nji yetu sio viongozi, kuhusu marupurupu ya wabunge mbona wananchi walikuja juu na wabunge wakanywea? Why not kwenye other issues as well, badala yake ni kulilia Kibelloh tu, baada ya utumishi wote alioufanya kwa taifa, all we can say to him ni kwamba umetuibia picha na hela za geti, hizi ni hadithi za mtaani tu,

yaani Kibelloh ameshindwa kuiba utalii, ambako ndiko kwenye dola hasa, halafu akashindwa kuiba kwenye ukatibu wa foreign ambako ndiko kwenye dola hasa, akasubiri kuiba London tena picha na hela za geti,

kwa mwendo huu CCM watatawala milele!, maana sisi wananchi tumeshawahakikishia kuwa we are good for only, fulana, pilau, na kofia za kijani, yes hivi unajua leo matajiri wanapoamua kugombea nmafasi za CCM, huwa wana wasi wasi na viongozi wa CCM sio wananchi hata kidogo, kwa mfano uchaguzi wa ubunge uliopita Kigamboni, ili kumtoa Manji ilibidi kiongozi mmoja wa CCM aje juu kwenye kamati kuu kuwa wakati umefika wa CCM kubinafsishwa, kama Manji si good kuwa mbunge wake lakini tayari wananchi walishamchagua,

wakati umefika wa sisi wananchi wa bongo kujiangalaia usoni, na ku-get serious na real issues ambazo ni muhimu kwa taifa letu, lakini as long as tunakubali unafiki wa kiongozi mmoja dhidi ya mwingine kama huu wa Kibelloh, CCm wataendelea tu kutuchezea!
 

Jizaledo

Member
Joined
Sep 5, 2006
Messages
89
Points
0

Jizaledo

Member
Joined Sep 5, 2006
89 0
Hizi taarifa zote ukizichunguza zinaashiria kuwa Kibelloh ni mwizi na utetezi mwengine unashangaza. Kwani ni nani aliyezaliwa akiwa anaiba bali ni wangapi wameshindwa kusihika maadili na kuanza kuiba uzeeni si tunaonywa kuwa vitu huaribikia uzeeni. Mfaransa kama Kibelloh kuzipenda na kuzichukuwa paintings isingeshangaza na tunapoambiwa kuwa amefanya hivyo inabidi tutulie na kutafakari tusirukie kutetea tu.

Mama ABM alipopewa zile bangili kule machimboni si alikana kuwa hajapewa na hatima yake ilikuwaje si aliungama ila akasema alizipokea kwa ajili ya Ikulu sasa na huyu Kibelloh ajitowe kimasomaso aseme alikwenda kupambia ofisi ya kule Paris.
 

Forum statistics

Threads 1,381,621
Members 526,148
Posts 33,806,324
Top