Vien
JF-Expert Member
- Mar 6, 2020
- 8,356
- 14,831
Habari wana JF 👋🏾
Wahenga walituhusia mengi, lakini kadri muda unavyozidi kwenda mambo yanabadilika.
Moja ya misemo maarufu ni:
“Mtegemea cha ndugu hufa masikini.”
Lakini ukija kwenye uhalisia wa leo, picha siyo ile ile kabisa.
Nimekua na nimeona familia nyingi za watu matajiri-wazazi wamejenga mali kubwa, lakini watoto wao hawana ile hustle au uwezo wa kutafuta pesa kama waliowatangulia. Pamoja na hilo, bado wanaishi maisha ya kifahari: magari mazuri, safari za nje, biashara zinaendelea kwa sababu ya msingi uliowekwa na familia.
Hapa ndipo unagundua kuwa dunia imebadilika. Kuna watu wanategemea legacy ya familia na hawaishi maisha ya umasikini hata kidogo.
Mfano halisi:
•Familia ya Paris Hilton - alizaliwa kwenye utajiri wa hoteli (Hilton), na maisha yake yote yameendelea kuwa ya juu hata kabla hajajitengenezea jina kubwa mwenyewe.
•Kim Kardashian - alitoka kwenye familia yenye uwezo mkubwa kupitia baba yake na connections zake, kitu kilichomuweka kwenye nafasi nzuri mapema.
•Watoto wa Bill Gates - hata bila hustle kubwa ya mwanzo, tayari walishazaliwa kwenye mazingira ya kifedha yaliyo stable sana.
•Hata hapa Afrika, watoto wa wafanyabiashara wakubwa au wanasiasa mara nyingi wanaendeleza maisha ya juu kwa sababu ya misingi ya familia zao.
Hii haimaanishi kuwa msemo wa wahenga haukuwa na maana - ulikuwa sahihi kwa wakati wao, ambapo fursa na mifumo ya kurithishana utajiri haikuwa structured kama sasa.
Lakini leo hii, ukweli ni kwamba:
Kuna watu wanategemea cha ndugu - na hawafi masikini