Liverpool FC (The Reds) | Special Thread

Yule barcola nae vile vile ni bench warmers kule PSG. Najiuliza kama barcola ni paund 120+M , je kvara bei yake ni shingap?
Barcola ame deliver wakati akipewa nafasi hivyo ni mwalimu wake tu ameona walio mbele yake wapo kamili zaidi yake na kupelekea Barcola kutamani kusepa na kutua mahala atakua 1st 11. Anataka mahala ambaopo atakua chagua la kwanza.

YNWA
 
PSG wamenunua wachezaji wa Tatu wazuri chini ya combined figure ya £130m yaani wamepata winga wawili na MD mmoja. Huku Hughes akiturisha matango pori.

YNWA
Tatizo management yenu inakurupuka dirisha la usajili linaenda kufungwa walikuwa wapi hapo mwanzo Ndio maana mnaekewa Bei za kukomolewa Kuna possibility ya kufanya panic buying yaani unamruhu vipi Salah anaondoka ukiwa Huna replacement yake hii ni akili au matope
 
Barcola ame deliver wakati akipewa nafasi hivyo ni mwalimu wake tu ameona walio mbele yake wapo kamili zaidi yake na kupelekea Barcola kutamani kusepa na kutua mahala atakua 1st 11. Anataka mahala ambaopo atakua chagua la kwanza.

YNWA
Hana thamani ya hela wanayotaka PSG. Barcola huyu chance 7 anapata 1 mbio nyingi kama bolt sizani kama ataiweza EPL
 
Liverpool ni kama baba aliefanikiwa akapata mahela mengi aafu akafika mahala akajisahau mbinu zilizompa ela akaanza kupoteana,.
Klopp ndio nguzo kuu iliyokuza dhamani ya Liverpool na Leo hii dhamani ya Liverpool tetesi ni zaidi ya £6b wote tunajua kibarua kizito Klopp anachukua klabu alichokutana nacho na mpaka anasepa mafanikio nje ya uwanja na ndani ya uwanja ni dhabiti hakuna shaka aliweza , klabu ikawa sasa ina pesa wakaanza manunuzi ya ajabu ajabu matokeo yake ndio tupo hapa.
Klopp kwa £120m ananunua Mane, Gini, Salah, Tsimikas na chenji inabaki lakini sasa tulipofikia ni pambaya sana sielewi kama idara ya scouting inakwama wapi au wamekua madalali🤓
Yaani PSG wao wanaweza kuwapata wachezaji wazuri kwa chini ya £40m huku sisi tukikomaa na over £100m mchezaji mmoja na tukiwa bado na majeraha ununuzi wa Florian na Isak haujawa na mafanikio mpaka sasa.
Wachezaji wapo wengi muda ulikuwepo mpaka tunafikia hapa kuna uzembe. Tazama dogo Rafael Leao kwa £35m pale Ac Milan ana miaka 27 na jembe haswa winga machachari, kwa hii pesa ya Barcola tungeweza kupata winga mmoja Rafael, beki RB mmoja Munoz wa Crystal Palace na DM mmoja kutoka Ufaransa au Ureno.

Ngoja tuzidi kua wasidikizaji.

YNWA
 
Hana thamani ya hela wanayotaka PSG. Barcola huyu chance 7 anapata 1 mbio nyingi kama bolt sizani kama ataiweza EPL
Dogo ana kipaji bei sio sawa yaani ukumbuke hatujapata replacement ya Salah mpaka sasa maana upande wa kushoto Yupo Rio, Gapko,Chiesa na Victor. Upande wa kulia hatuna direct output ya Salah labda wampe Elliott dakika tuone au na mfumo unakua tofauti kwa kweli muda utasema.

YNWA
 
Ndio umtumie SARR????🤣🤣🤣
🤓🤓🤓Mkuu mbinu zipo nyingi aisee. Pale Crystal Palace wangetua kwa yule beki wao Munoz jembe sanaaa, huyu Sarr ni mzuri lakini sio kwa hio bei. Pale Porto tulipompata Diazi kuna ma winga machachari sanaaa sijui wanachotaka ni kipi maana mfungaji yupo Isak na Hugo hivyo wanasaka watengezaji na hayo magoli hivyo wangetazama na Kule.

YNWA
 
Dirisha linaelekea mwishoni na sioni dalili ya kununua DM kwa maana hio tutegemee maumivu, mechi ya Newcastle ilionyesha bila chenga kwamba pale kati Ryan anapwaya mno kama ailivyopwaya mzunguko wa pili msimu uliopita.
Biashara ilitakiwa ifungwe mapema sana hii nunua Defensive Midfielder, Right Back , Right Winger... kama kuna mauzo ndio wangeanza kuboresha kwingine.

YNWA
 
Poleni sana sio kwakuteseka huko huku kwetu raha kama zote
 
Liverpool's opponents in full:
Mechi za awali UCL ndio hizi.

Liverpool vs Inter Milan (A),
Liverpool vs Atletico Madrid (H),
Liverpool vs FC Porto (H),
Liverpool Club Brugge (A),
Liverpool vs Villarreal (H),
Liverpool vs Fenerbahce (A),
Liverpool vs Lens (H),
Liverpool vs Lask (A).

YNWA
 
Lamine Camara ni mchezaji mzuri?
 

At last katua mwenye namba yake ya kushoto🤓🤓🤓.
Here we go.
Anaelekea Uingereza kwa ajili ya vipimo vya afya.
Miaka mitano anasaini.
Pamoja na nyongeza dili lake halitazidi £123m advance PSG wanalipwa £106m zingine zitalipwa kwa awamu na vipengele kadhaa akiweza kuvitimiza

YNWA
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…