Liverpool FC (The Reds) | Special Thread

Liverpool FC (The Reds) | Special Thread

View attachment 3433176
No Kelleher no problem ๐Ÿ˜Ž๐Ÿ˜Ž๐Ÿ˜Ž๐Ÿ˜Ž๐Ÿ˜Ž๐Ÿ”ฅ๐Ÿ”ฅ๐Ÿ”ฅ๐Ÿ”ฅ๐Ÿ”ฅ๐Ÿ”ฅ๐Ÿ”ฅ๐Ÿ”ฅau unasema aje Saint Anne

YNWA
Sasahivi hamuwezi kuona matatizo maana mnacheza na timu za maporini.

Subiri ligi zenyewe za maana zianze,tutaongea lugha moja.
 
Habari za ndani kutoka Bayern Munchen zinabainisha kwamba usajili wa Luis Dรญaz ulipangwa kabisa kwa masharti ya Liverpool, huku Bayern wakibaki wakifuatilia tu bila ushawishi wowote. Richard Hughes (Mkurugenzi wa Michezo wa Liverpool) ndiye aliyeendesha mazungumzo hayo kuanzia mwanzo hadi mwisho, akiweka mfumo mapema na kutokubali kuachia udhibiti wa mazungumzo hata kidogo.

Kwa upande wa Bayern, mazungumzo yaliongozwa na Jan-Christian Dreesen, lakini hakuwa na mamlaka, ushawishi wala ule ujuzi wa mazungumzo ya hali ya juu wa kuweza kubadili mwelekeo wa makubaliano hayo kwa namna yoyote ile.

Hughes alihakikisha mapema anapata ishara za wazi kutoka kwa watu wa karibu na Dรญaz kuwa mchezaji huyo yuko tayari kuhamia Saudi Arabia katika siku zijazo. Akiwa na uhakika huo, Liverpool walisisitiza kuwepo kwa kipengele cha kuuza tena mchezaji (sell-on clause) ambacho kingewapa faida kubwa endapo Dรญaz atauzwa kwa bei kubwa baadaye. Bayern, ambao walikuwa chini ya shinikizo kubwa la ndani la kusajili mchezaji maarufu na hawakuwa na mbadala madhubuti, walikubali masharti hayo kama yalivyowasilishwa.

Makubaliano ya mwisho yalijumuisha ada ya msingi ya euro milioni 72, na nyongeza ya euro milioni 9 ambazo zinachukuliwa kuwa rahisi sana kutimia, kiasi kwamba jumla ya euro milioni 81 tayari inahesabiwa kama jambo lililokamilika. Kwa kuzingatia kipengele cha kuuza tena, kiasi Liverpool wanaweza kupata kinaweza kufikia euro milioni 95 au hata 100 endapo kutatokea uhamisho wa bei ya juu โ€“ jambo ambalo linaonekana ndani ya klabu kuna uwezekano mkubwa.

Ndani ya Bayern, hakuna aliyekataa jinsi mchakato mzima ulivyokwenda. Ingawa usajili huo unaonyesha hadharani kama hatua kubwa ya mafanikio, wale waliokuwa sehemu ya mazungumzo wanajua vizuri namna mambo yalivyokuwa. Liverpool waliweka masharti, walilinda maslahi yao ya baadaye, na wakapata thamani ya juu zaidi kutoka kwa mchezaji wao. Bayern, kwa upande mwingine, wamelipa kiasi kikubwa, wakakubali mfumo ambao hawakuubuni wao, na wamempata mchezaji ambaye tayari huenda akawa kwenye ramani ya kuuzwa tena.

Kwa kila kipimo, huu ulikuwa usajili uliofanyika kwa masharti ya Liverpool pekee.
 
Kwanini Firmpong na Kerkez mishahara yao ni midogo sana tofauti na vipaji vyao?

Kuna baadhi ya facts

1. Hawa madogo bado wako kwenye hatua za mwanzo za career zao. Klabu kubwa kama Liverpool zinawaona kama "developing players" badala ya "finished products", hivyo mishahara yao huakisi hali hiyo.

2. Walikotoka vilabu vyao havikuwa na financial muscle" kama Leverkusen (Frimpong) au Bournemouth (Kerkez), hana nguvu sana kudai mishahara mikubwa kama ambavyo mchezaji kutoka PSG au Bayern Munich angekuwa nayo.

3. Vijana kama hawa, huwa tayari kupokea mishahara ya chini ili tu wachezee klabu kubwa yenye jina kama Liverpool, wakijua baada ya muda wataongeza kupitia performance-based renewals.

(Hukumuona Kerkez alivyo kuwa anajig selfie kwenye training center ya AXA?) ๐Ÿ˜‚

Frimpong mwenyewe amewahi sema kwenye mahojiano: "I want to keep improving and play at the top level โ€“ the money comes after."

4. Mishahara inaweza kuonekana midogo "kwenye karatasi", lakini mchezaji analipwa vizuri kupitia:

Performance bonuses (appearances, assists, clean sheets)

Loyalty bonuses

Image rights (especially kwa brand kubwa kama Liverpool)
 
Captain Marvelous bhanaaa nimesoma sehemu nyingi sana kumhusu Guรฉhi inaonekana hafai kwenye mfumo wa Slot ๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚

Marc Guรฉhi ni disciplined defender, lakini hana kasi ya kutosha ya ku-recover kwenye high line, na kwenye mechi kadhaa ameonekana kubanwa akiwa kwenye presha (pressed in build-up), hasa dhidi ya high-intensity teams.

Katika mfumo wa Slot, beki wa kushoto (LCB) anatarajiwa kuwa na uwezo wa ku-cover space kubwa nyuma ya attacking left-back kama Kerkez. Kwa hiyo, ukosefu wa top-end speed na elite ball distribution ya Guรฉhi huleta mashaka kwenye compatibility yake na falsafa ya Liverpool ya sasa.

Performance ya mchezaji huwa heavily influenced na system, role, na aina ya kocha aliyonayo.

Liverpool wanahitaji plug and play defenders kwenye mold ya mfumo wa Slot."

Guรฉhi anaweza akakomaa kwenye build-up na akaboresha passing range yake, lakini top-end recovery pace ni attribute ya kiasili ambayo ni ngumu โ€˜kufundishwaโ€™ na hilo ndilo linamfanya asiwe priority kwa system yenye high defensive line kama ya Slot.
 
IMG-20250806-WA0006.jpg

Hivi inakuwaje hawa Newcastle kila mchezaji wanashindwa kusajili?
 
๐Ÿšจ๐Ÿ”ดโšช๏ธ RB Leipzig have started discussing contract terms with Harvey Elliott as priority target to replace Xavi Simons.

Discussions ongoing waiting to understand playerโ€™s decision.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom