Japo Salah sio Messi au Ronaldo(business wise) lakini kibiashara pale Liverpool yupo juu sana anauzika zaidi ya wachezaji wengine hivyo analeta mpunga wa maana kwa timu. Kwa mfano mauzo ya jezi tu Salah peke yake anachangia asilimia 35 ya mauzo yote hivyo ingekua ni uzembe kumwachia Salah kuodoka Liverpool regardless matokeo uwanjani yapo vipi kwa sasa.
Ukifuatilia kwa kina utagundua kwamba mikataba mingi ya wachezaji Liverpool ipo capped kwenye incentives zaidi hivyo inakua win win situation kwa Liverpool na kwa mchezaji husika.. Utakuta kwa mfano Salah kila jezi inayouzika ana asilimia kadhaa pale inayoingia kwenye mshahara wake...
Mwaka 2021 Salah alikua tano bora kwa mauzo ya jezi duniani..
Mkataba wa Liverpool na Nike upo kimslahi sana kwamba kila jezi au merchandise inayouzwa chini ya Nike basi! Liverpool wanapata asilimia 30 au 20 ya mauzo hayo, malipo hayo ni nje ya zile £30m kila msimu Nike wanalipa ina maana kwa msimu Nike wanalipa £70m+ pale Liverpool. Mkataba ule ni based on incentives pia.
Salah anapata anachostahili japo kama mchezaji ana mapungufu yake lakini fursa ya kucheza Liverpool ameitumia vyema kujijenga ki soko na kampuni nyingi tu kama Pepsi, Oppo, Vodafone, Adidas nk zinamtumia kutangaza bidhaa zao.
Huku kupoteana kwa Salah Klopp amesema ni kwa kukosa utulivu wa wachezaji aliozoea pale mbele Firmino na Mane. Lakini pia sikutegmea Salah afunge sana wakati timu kila idara imechuja sana.
YNWA